trachomatis
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 3,758
- 736
Leo ofisini kwangu nimeshuhudia tukio la kushangaza..Katibu muhtasi wangu[P/S] alimkimbia mgeni wake na kwenda kujificha.Mgeni baada ya kuona hapewi ushirikiano aliamua kuaga na kuondoka.
Cha ajabu P/S alirudi huku akilia na kuwalaani wote[anaowajua na asiowajua] waliomwelekeza ''mpenzi'' wake huyo mahali aliko. Alianza kupiga simu nyingi kama kachanganyikiwa,akiomba ushauri kwa ndugu na rafiki zake wanaomfahamu ''mpenzi'' wake huyo wa zamani.Tulipomhoji alifunguka hivi: alikuwa mpenzi wake tangu mwaka 2000.Walipishana umri kiasi cha miaka 10.''Akamfac ilitate'' akasoma kozi ndogo ya uuguzi ya mwaka mmoja. Hakupata kazi zaidi ya kuuza kwenye maduka ya dawa.Ilipofika 2007,bwana yule alihamishwa kikazi.Katika kipindi chote hicho walikuwa wakiishi pamoja.Na bwana alipata kudhamiria kumuoa dada huyo,kigezo kilichomdisqualify kilikuwa ''dini''. Wakati binti alikuwa radhi kubadili,wazazi wake hawakumruhusu. Binti aliamua kuondoka na kurudi kwao kwa sababu ambazo hajaniambia[ nafikiri huduma hazi kuwa hafifu. Aliendelea kuwa na mahusiano mengine,ila alikosa amani yule bwana alipokuwa akirudi kwani yue bwana alijihesabu kuwa ndiye MMILIKI wa mwili wa yule dada.. Kivipi? Hata apotee miezi 9,miezi mi3 inayobaki yulew dada anakuwa ndiyo mke.Imekuwa ikimnyima raha sana hali hiyo.
Kwa hiyo nikamuuliza maswali mawili,je alikuwa mwanaume wako wa kwanza kabisa maishani mwako?,akajibu ndiyo.Nikamwuliza je, ulipokuwa naye kulikuwa na shida ya huduma? Akajibu,hapana. Nikaongezea hapohapo,je mbali na kazi yake[udereva],ana mradi wowote wa nje? Akasema ana gari 2 zenye kufanya biashara ya usafirishaji. Je mtu wa aina hii unapomuuliza kwa nini ana chuki ya kiasi hicho anakwambia ''mi simtaki tu'' inawezekana?