Umeme wakatika tena sehemu kubwa ya nchi?

Tanesco wamesema kuwa umeme unaozalishwa mtera utakuwa unatolewa kidogokidogo ili angalau utusukume hadi msimu ujao wa mvua za masika.Kinachozalishwa sasa ni MW30 tu....SOURCE TBC taifa.
 
Tanesco wamesema kuwa umeme unaozalishwa mtera utakuwa unatolewa kidogokidogo ili angalau utusukume hadi msimu ujao wa mvua za masika.Kinachozalishwa sasa ni MW30 tu....SOURCE TBC taifa.

Hapo kwenye red:
Mkuu umeme siyo sukari kusema ukishaizalisha unaiweka godown. Ni bidhaa ambayo unapoizalisha ni lazima uitumie papo hapo.
 
Na hivi tunavyoongea umekatika tena nchi nzima kwa wale waliounganishwa katika gridi ya taifa.
"Tumejaribu, tumeweza, tunasonga mbele".
 
Washenzi jana wameturudishia umeme saa saba usiku, wakaukata saa sita mchana. Yaani wiki nzima sijarudi nyumbani toka work nikakuta umeme hadi naanza kujiuliza kama umeme wa Tanesco ndo tuufanye uwe back up alaf jenereta ndo liwe linatuzalishia umeme wa matumizi ya kawaida.I HATE TANESCO.
I love TANESCO but i hate ccm.
 
Hapo kwenye red:Mkuu umeme siyo sukari kusema ukishaizalisha unaiweka godown. Ni bidhaa ambayo unapoizalisha ni lazima uitumie papo hapo.
Una uhakika na hilo kuwa once umeme ukiwa generated hauwezi kuhifadhiwa?Ebu rejea tena madaftari yako mkuu.Watakuwa wanaingiza kwenye grid kidogo kidogo!
 
Una uhakika na hilo kuwa once umeme ukiwa generated hauwezi kuhifadhiwa?Ebu rejea tena madaftari yako mkuu.Watakuwa wanaingiza kwenye grid kidogo kidogo!

Mh! Mkuu hapo...!
Sijui labda kwa kuwa tafiti zinafanyika kila siku huenda imeshagundulika hivyo....lakini mi sina hiyo habari.
Labda wataalam wenye fani zenu mtusaidie kwa hili.

Sitaki kubadili maudhui ya sredi hii lakini nijuavyo mimi umeme huu tunaotumia (wa Tanesco) huwezi kuuzalisha ukauhifadhi, ni lazima utumike wakati huo huo unapozalishwa.
Zipo aina za umeme unaoweza kuzalishwa na kuhifadhiwa, lakini sio huu wa Tanesco tunaotumia. Kwa Tanesco, kinachoweza kuhifadhiwa ni nishati ya kuzalishia huo umeme sio umeme wenyewe.
Kama una uelewa tofauti nimwagie hiyo shule mkuu.
 
Hawa jamaa uwezowao umefika mwisho na mgao utaendelea kuwa mkali jinsi muda unavyozidi kwenda.tatizo sio tanesco bali ni serikali.viva tanesco.
 
Ishu hapa siyo CCM! Tatizo ni utendaji mbovu wa mgt ya Tanesco! Hamna Mkurugenzi yeyote wa Tanesco anayeripot CCM! Wote wako chini ya Bodi!Tutenganishe haya mambo!
@Nyamizi,Inakuwaje Mke umtafute wewe umpende wewe Ufungenae Ndoa wewe,Kisha Umpe Mwenzako Aishinae na Atoe huduma utakazo wewe?HIYO NDIO SELIKALI NA TANESCO ZINAVYO ISHI.
 
@Nyamizi,Inakuwaje Mke umtafute wewe umpende wewe Ufungenae Ndoa wewe,Kisha Umpe Mwenzako Aishinae na Atoe huduma utakazo wewe?HIYO NDIO SELIKALI NA TANESCO ZINAVYO ISHI.

Hapa ndipo mkuu Rejao anaponiacha hoi,linapokuja swala la utendaji mbovu wa serikali ya CCM,gafla anakuwa kipofu,yaleyale ya mapacha watatu ni Magamba yanakichafua chama,lkn aliyewekwa Ikulu na hayo magamba (RACHEL) yeye si gamba.
 
We unaye ng'ang'ana arusha kuna umeme (power on) unamaana arusha hamjawaconnected kwenye grid ya taifa??ishawekwa Wazi hili ni janga la taifa, kukatikakatika Kwa umeme Kwa jumla wake ni ubabaishaji. Tunatakiwa Kama wananchi tuwe na msimamo wa pamoja ktk kumaliza suala huko..mi nadhan kuna maslahi fulan ktk hili suala mana hata Richmond ilichomekwa ktk mazingira Kama Haya haya. Ona Sasa had waziri mkuu aNafkiria kubadiri sheria ya manunuz ili tuingize nchini mitambo chakavu , ni wiiiiiiz mtupu
 
Tinymonster. Hili la "washa zima, washa zima. Mimi nadhani kuna kikosi cha wanataesco wameajiriwa hivi karibun wapo on job training ya kuzima na kuwasha. Yaani, wanajifunza kuwasha na kuzima.... Mana c kawaida, ratiba sasa haieleweki, wanaijua tanesco wenyewe,
 
Na mwisho wa siku kwenye kuunga mkono bajeti ya nishati na madini utasikia: "Ndiooooooo".
 
Yaani watu wanadiriki hadi kuhonga ili bajeti ipite...? Hii sasa ni hatari, na ni ishara tosha kuwa tukiwa na ccm hii tusitarajie miujiza.
 
Back
Top Bottom