Tuwe na umeme wa gridi ya taifa, lakini pia tusisahau kuwa na vyanzo vya kikanda, kwa sasa shida ikitokea sehemu moja, nchi nzima inaathirika

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,684
Nadhani sasa ni muda muafaka kuwa na gridi za kikanda. Kalemani alikuwq ananichekesha alipokuwq anakaza fuvu kufunga mitambo ya mafuta kwa badhi ya mikoa.

Usalama wa umeme ni usalama wa taifa. Hatuwezi kuuweka usalama wa nchi nzima kwenye njia moja bila ya kuwa na njia mbalimbali. Inatokea shida kidatu, watu wanalia mpaka sirari,ngara, na kila mahali.

Ni muda muafaka kuwa na gridi ya taifa, lakini pia za kikanda. Kanda ya ziwa ikae na chanzo cha Rusumo na Uganda, uwepo mfumo utakaoharakisha hilo, hasa pale gridi ya taifa inapoyumba.

Singida na mikoa jirani kama Manyara na Dodoma itembee na umeme wa upepo, hasa pale umeme wa gridi ya taifa unapoyumba.

Nyanda za juu kusini itembee na vyanzo vya huko pale umeme unapoyumba.

DSM na Pwani iwe Kanda Maalum ya umeme, wawe na laini maalum ya uhakika kwa kuwa ni mkoa wa kiuchumi kwa taifa hilo.

Arusha Tanga, kuna bwawa la umeme Tanga.

Kila kanda iwe na uwezeshaji wa kusimamia masuala ya umeme kwa ngazi yake lakini chini ya usimamizi wa Tanesco..

Tusione aibu kununua umeme uganda, wana umeme mwingi, kiasi kwamba kukatika umeme mkoa wa kagera ni ngumu. Kalemani alichekesha watu alipojisemesha eti hatutaki umeme wa uganda,ambo ya hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom