AL SHARPTON
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 2,797
- 952
Nakumbuka duka letu lilikuwa pale Undali St
Duh umenikumbusha mbali nakumbuka enzi hizo nilikuwa mdogo natumwa kukaa nje kusubiri gari la sukari likisimama niwastue ndani gari ina mlango nyuma ina mifuko ya kilo moja moja ya kaki na huruhusiwi kununia zaidi ya mfuko mmoja.
Acha uongo basi. 1986 hata shilingi yenyewe usingeweza kununua kitu. Eti senti tano? Bongo flevamkuu mimi niliambulia kuona hayo maduka ya RTC sukari, vyombo kwa foleni, kijijini huko naenda na mama kupanga foleni ya kununua robo kilo ya sukari, daftari niliwahi kununua kwa senti 5 1986,
Mwadui ilikuwepo Toka enzi za ukoloni kwa hiyo nyerere asingeweza kufanya kitu.asingeweza kufanya kitu?..hustuki?..we unashtushwa na hotuba ya 2007?...Hii suppott yenu hata kwenye upuuzi uliofanywa na nyerere na mkapa ndio unaotufanya tuamini kuwa chuki dhidi ya kikwete inaanzia kanisani
So???
Nyerere alijaribu kufanya alichofanya kwa kiasi chake, wewe unafanya nini?
Siamini katika kucheza 'mwathirika" (don't play victim)
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Kumbe wewe ni muislam?Kweli watu wametoka mbali. Nakumbuka kaka yangu alivunjika mkono wakti akigombea katika foleni kutaka kununua sababu ya mbuni pale mtaa wa Aggrey kariakoo.
Nakumbuka ilikuwa mkiwa mnakwenda kuswali alfajr tunaweka mawe katika duka la kaya pale Aggrey na ukitoka msikitini tunapangiana zamu kulinda jiwe letu maana mkiondoka tu watu wanalitupa. Na gari la Ugawaji linakuja saa sabaa au nane alasiri.
Kila mtu alikuwa lazima amjue Mkurugenzi mkuu wa NMC mzee Mollel au Mkurugenzi wake wa utawala Mz Uwesu msumi kwa ajili ya kupata kibali cha kununua vitu kwa wingi.
Kweli kila watu na zama zao.
Weka mfano wa hivyo vitu kuandika tu vitu "tangible" ni so vague.
Nilikuwepo wakati huo, kabla ya huo na Alhamdulillah nipo sasa. Tusiandikie mate na wino upo.
Penye nyekundu hapo sijakuelewa weka sawa ili nielewe unataka nini.
Acha uongo basi. 1986 hata shilingi yenyewe usingeweza kununua kitu. Eti senti tano? Bongo fleva
Duh! Mkuu unajua kutia chumvi kama mahindi ya kuchoma ya kileo? Pombe watu walikua wanapiga ila wanawahi kama sanduku mbili mnanunua mnaweka chini ya meza mkiogopa zisiishe. Na pia magari ya Serikali yalikua siku za Jumapili kutembea mwisho saa 8 na hii ilifanywa ili watu wasitumie magari ya serikali kwa starehe zao na ilikua gari la Serikali halitakiwi kuonekana limepaki Bar ukionekana unakamatwa na Polisi ilikua ni suala la maadili sio kama sasa .
NAdhani wewe ndio unatia chumvi! Binafsi baba yangu alikuwa na gari miaka hiyo ya 1960s mpaka 1980s, tukitaka kwenda mahali siku ya Jumapili NI LAZIMA UOMBE KIBALI MAALUM... sijui kuhusu bia, ila ya kuendesha gari siku ya Jumapili ni ukweli ulio wazi na mimi kama shahidi! labda kama familia yako haikuwa ikimiliki gari miaka hiyo huwezi litambua hilo.
Ilikuwa shauri ya kuchunga matumizi ya mafuta hali ilikuwa mbaya sana na hata mashindano ya magari E.African rally yalipigwa marufuku nchiniMkuu ahsante kwa kumjibu huyo jamaa limbogamboga. Mimi mwenyewe ni shahidi kwamba tuliwahi kukamatwa na Traffic na baba yangu tukitoka kanisani baada ya saa saba mchana na gari la baba yangu likapelekwa kituo cha kati. Nilishangaa sana huyo jamaa kunibishia kwamba magari ya BINAFSI yalikuwa hayazuiliwi kutembea siku ya jumapili.
Nakumbuka Nyerere alinusurika kupinduliwa mara 5 shauri ya kuchokwa.Swali lako hapa ni rahisi sana; lakini labda uliulize kivingine... unakumbuka ni Watanzania wangapi walikufa kwa baa la njaa wakati wa duka la kaya? Kule mtaani kwenu au kijijini unakumbuka kuwaona watu wanatembea mbavu nje kwa njaa; au hata kama unakumbuka watu waliokuwa wanakula mizizi yenye sumu ili kupata angalau chochote mdomoni...?? Labda kama kuna mtu mwingine anaweza kutusaidia katika haya...
Unachoita "uzembe" wengine tunakiona "the genius of Mwalimu". Hivi unajua leo hii kuna Watanzania wanatatizo la njaa na hii imekuwa ni kila mwaka licha ya kwamba hakuna tena "duka la kaya"?
Ukisoma wote "wanaokumbuka" kwenda kupanga foleni, kupewa mgao wao utaona kuwa hakuna hata mmoja ambaye anasimama na kusema kuwa kwenye familia yao kuna mtu alikufa kwa njaa...!!
Think about it.. je bila ya duka la kaya tungekuwaje?
mkuu sikumbuki ila sent zilikuwa nyingi wakati huo, sikumbuki lilikuwa linauzwa senti ngapi,Acha uongo basi. 1986 hata shilingi yenyewe usingeweza kununua kitu. Eti senti tano? Bongo fleva
Swali lako hapa ni rahisi sana; lakini labda uliulize kivingine... unakumbuka ni Watanzania wangapi walikufa kwa baa la njaa wakati wa duka la kaya? Kule mtaani kwenu au kijijini unakumbuka kuwaona watu wanatembea mbavu nje kwa njaa; au hata kama unakumbuka watu waliokuwa wanakula mizizi yenye sumu ili kupata angalau chochote mdomoni...?? Labda kama kuna mtu mwingine anaweza kutusaidia katika haya...
Unachoita "uzembe" wengine tunakiona "the genius of Mwalimu". Hivi unajua leo hii kuna Watanzania wanatatizo la njaa na hii imekuwa ni kila mwaka licha ya kwamba hakuna tena "duka la kaya"?
Ukisoma wote "wanaokumbuka" kwenda kupanga foleni, kupewa mgao wao utaona kuwa hakuna hata mmoja ambaye anasimama na kusema kuwa kwenye familia yao kuna mtu alikufa kwa njaa...!!
Think about it.. je bila ya duka la kaya tungekuwaje?