Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?