Kanuni za maduka ya kubadilishia fedha za kigeni za mwaka 2023

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
TAARIFA KWA UMMA

KANUNI ZA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI ZA MWAKA 2023

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kwamba, kwa mamlaka iliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Kigeni (Sura namba 271), imetoa Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za mwaka 2023. Kanuni hizo zilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali namba 729 la tarehe 6 Oktoba 2023.

Pamoja na mambo mengine, Kanuni hizo zimeweka madaraja matatu ya leseni za biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kama ifuatavyo:-

1. Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja A

2. (a) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja A ni duka linalomilikiwa na wageni au wenyeji lililoruhusiwa kufungua matawi sehemu yoyote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(b) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja A linalomilikiwa na wageni litatakiwa kuwa na mtaji usiopungua Shilingi za Tanzania bilioni moja.

(c) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja A linalomilikiwa na wenyeji lilitakiwa kuwa na mtaji usiopungua Shilingi za Tanzania milioni mia tano.

(d) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja A litaruhusiwa kufanya miamala ya papo kwa papo, kutuma fedha na kufanya biashara kama wakala wa benki, taasisi ya fedha, kampuni ya bima, mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu, au huduma nyingine zozote za fedha kama itakavyoidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania.

Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja B

(a) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja B ni duka la kubadilisha fedha za kigeni linalomilikiwa na wenyeji.

(b) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja B halitaruhusiwa kufungua matawi kwa ajili ya kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni.

(c) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja B litatakiwa kuwa na mtaji usiopungua Shilingi za Tanzania milioni mia mbili.

(d) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja B litaruhusiwa kufanya miamala ya papo kwa papo na kufanya biashara kama wakala wa benki, taasisi ya fedha, kampuni ya bima, mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu, au huduma nyingine zozote za fedha kama itakavyoidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania.

3. Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja C

(a) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja C ni duka la kubadilisha fedha za kigeni lililoanzishwa na hoteli (yenye hadhi ya nyota tatu au zaidi) kwa ajili ya kufanya miamala ya papo kwa papo kwa wateja wa hoteli tu.

(b) Leseni ya Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja C itatolewa kwa hoteli au kwa mmiliki wa hoteli.

(c) Duka la Kubadilisha Fedha za Kigeni Daraja C halitatakiwa kuwa na mtaji wa kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni.

Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za mwaka 2023, ambazo zimefuta rasmi Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za mwaka 2019, zinapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania kupitia:


GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA

1697443969868.png

1697443983436.png
 
TAARIFA KWA UMMA

KANUNI ZA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI ZA MWAKA 2023

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kwamba, kwa mamlaka iliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Kigeni
Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba- Governor na Dr . Mwigulu Madelu Mchemba waziri ni magineous sana aisee.....
 
Hapo kwenye duka la daraja C ndipo watu hutakatishia pesa.
 
Mimi ningepiga marufuku dollar kutumika kulipia huduma au bidhaa yeyote ndani ya mipaka ya Tanganyika
Sioni kama itasaidia
sana sana unataka dola zote ziende kwenye Bureau na mabenk ambako huna control nazo kwa 100%
Kama tutazikataa dola inamaana hela zote zitakuwa shilingi; halafu tukiagiza madawa, magari nk tubadilishe tena shilingi iwe dola? mbona naona kama haiko sawa sawa....
 
Back
Top Bottom