Ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA??

Maelezo ya kwenye Red ndiyo maelezo ya Nyerere ninayemfahamu!!

Kigarama,
Hata mimi. Nilikuwa namjibu Ribosome ambaye alitaka kutuaminisha kuwa Nyerere alikubali yaishe kimya kimya.
Siku hizi za mtandao huwezi hata kumdanganya mtoto mdogo. Utaumbulika.
 
Kigarama,
Hata mimi. Nilikuwa namjibu Ribosome ambaye alitaka kutuaminisha kuwa Nyerere alikubali yaishe kimya kimya.
Siku hizi za mtandao huwezi hata kumdanganya mtoto mdogo. Utaumbulika.
Achana na Ribosome yeye tangu enzi zilee akiitwa vilee akisikia jina la Nyerere anaweweseka. Sisi wengine tumefikia mbali zaidi kuamini kwama Mandela umaarufu wake unakuzwa sana na watu wa Magharibi kwa malengo yao mahsusi baada ya kuwaona watu kama Kwame Nkumah na Nyerere walikuwa ni vikwazo kwao. Mandela hakuwa mwanafalsafa kama Nyerere.

Sifa za Mandelea ni kufungwa tu!!
 
Duka la kaya lilikuwa noma. Kabla vita vya nduli mambo yalikuwa mazuri. Wauzaji tulikuwa tunawaita mameneja. Baada ya vita ilibidi mtu uamke alfajiri kwenda kupanga jiwe au kiroba cha mchanga. La kwetu pale Nyakato sokoni tulikuwa tunapaita Iloganzala. Kila nikipîta pale huwa pananikumbusha sana ile foleni ya kipindi hicho, siku hizi pamevunjwa wakati wa ujenzi wa barabara ya mza-msm. Nyerere ulijaribu R.I.P!
 
Siku moja nakumbuka nilikimbizana na gari la ugawaji mchana wa jua kali kwa zaidi ya maduka kumi. Kufikia duka ambalo sukari ilikuwa inashushwa nikaambulia kilo moja,lakini kurudi nyumbani nilionekana bonge la shujaa!!
 
Wewe unadhani mimi namlaumu Mwalimu? Mimi kati ya watu ambao ni watetezi wakubwa wa Mwalimu lakini sikuleta hii mada ili kumhukumu Mwalimu.

Mimi nilishiriki kuiishi hali hii, nilikula unga wa YANGA, nikabugia BURGA, nikaogea MAJANI YA MPAPAI,nimekunywa chai kwa kuchemsha sukari kwa ukosefu wa majani ya chai, nimeogea sabuni ya MAGADI. Huu ni uzowefu wangu wala sina uchungu na sera za Mwalimu!!

Umenikumbusha sabuni za Kamanyola na Uniform za Marudufu, Jinja na Marekani. Nadhani vitambaa vilitengenezwa na Kiwanda cha Urafiki kabla hakijafa. Angalau wakati ule viwanda vilikuwa vinafanya kazi, japo chini ya kiwango kuliko alivyofanya Mkapa, kuviuza na kuvigeuza maghala.
 
Waliomfuatia Mwalimu afadhali ya Mzee Ally Hassan Mwinyi. Yeye alikuwa dhaifu lakini hakuwa mhalifu kama wenziwe wawili waliomfuatia. Ingawa kuna lile doa la Mama Sitti Mwinyi la kuuza "Stella Atois". Biashara za Ikulu ni mama Maria Nyerere peke yake ndiye aliyesalimika!!
 
Umaskini aliotutumbukiza Nyerere hauna mfano. Mpaka leo wengi wa Watanzania wanateseka kwa ajili yake.

Nyerere hakukutia umaskini wewe !!! Baba na Babu yako ndo walikutia kwenye Umaskini !! alichokifanya Nyerere ni kujaribu kupunguza tofauti ya Nguvu ya Manunuzi kwa watu wote iwe sawa !! ndo maana hata kama Baba yako au Wewe ulikuwa na Mamilioni ulikuwa sawa tu na sisi akina Kapuku tulikuwa na Sh 100 Mchagoni !!!! tukienda dukani tunanunua kulingana na idadi ya Familia zetu na si sababu unapesa unanunua Duka zima na Wasionazo wafanyaje au wangepata wapi ? au wewe ndo ulikuwa mmoja wapo wa walanguzi ?
Tafuta historia ya kwenu kwanza Kisha uje Utwambie hapa Kama Mngeweza kusurvive ile harsh time kama ingekuwa mwenye nacho ndo anapata !!!!! Fikiri kabla ya Kuropoka bana !!! do a research kwanza !!!
 
Usisahau ili kadi ambayo mjumbe wa shina anajaza resho yako. Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa single basi baba mwenye nyumba akawa nampa share yangu.
mkuu mimi niliambulia kuona hayo maduka ya RTC sukari, vyombo kwa foleni, kijijini huko naenda na mama kupanga foleni ya kununua robo kilo ya sukari, daftari niliwahi kununua kwa senti 5 1986,
 
Mie nikiwa kitoto nilimkuta jirani mmoja anafukia mabati mapayaaaa ardhini. Nikawa namshangaa tuu. Akanipiga mkwara mzito nikimwonyesha mtu yoyote hapo nitakiona. Ila uji wa yanga ulikuwa mtamu acheni masihara. Ulikuwa ukikamulia malimao dah mtamu balaa. Wee acheni tuu.
kwakuwa wee shabiki wa YANGA lazima uusifie, wenzio sik hizi wanasifia maandazi ya AZAM, ila bulga bana, na uji wa ngano ambayo haijasagwa, nakumbuka baba aliwahi kuja na maziwa ya unga tulitesa mtaani balaa,
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mimi nakumbuka mgao wa bia, ambapo bia zilikuwa zinapatikana mwisho wa mwezi. Kila mtu alipangiwa kunywa bia 3 tu. wakati unakunywa bia USALAMA WA TAIFA wanaokata vizibo vya bia ulizokunywa. Ukimaliza magao wako wa bia 3 unakwenda nyumbani kulala. Ukijifanya mjanja ukahamia baa nyingine kuongeza, ukifika baa mhudumu anakunusa mdomo akikuta unanuka bia unakufukuzwa kwasababu atajua kwamba ulikotoka tayari utakuwa umeshakunywa mgao wako wa bia 3. Pia ninakumbuka MARUFUKU ya kutembeza gari la binafsi siku ya JUMAPILI baaada ya saa 7 mchana. Siku ya Jumapili mwisho wa kuendesha gari la binafsi ilikuwa saa 7 mchana, baada ya mda huo gari la binafsi likionekana barabarani linakamatwa na traffic na kupigwa heavy penalty. Mambo niliyoyaona kipindi hicho yalinifanya NIUCHUKUE UJAMAA HADI LEO, mimi huniambii kitu kuhusu SIASA YA UJAMAA!
 
duh! hilo la bia ni kali, ingekuwa asaiv ningeshafungwa,
 
duh! hilo la bia ni kali, ingekuwa asaiv ningeshafungwa,

Mzee inaonekana wewe ni mtu wa KIU KALI. Lakini kama ungekuwepo kipindi hicho kiu yako hiyo ingekatika yenyewe. Lakini pia hata pesa ya kununua hizo bia nayo ilikuwa haipo. Uzalishaji wa bia kipindi hicho ulikuwa mdogo sana. Na kwa kuwa UJAMAA ni kugawana UMASIKINI tulionao, ndio maana ukawekwa mgao wa bia angalau kila mtanzania aliyetaka kunywa bia anywe japo kidogo. Kwa wale wavutaji wa sigara, ilifika wakati sigara zikauzwa kwa pafu/fundo. Yaani wavutaji sigara wanajipanga foleni, halafu sigara inawashwa watu wanauziwa kwa pafu/fundo la moshi unaovuta. Wakati mvutaji anapiga pafu/fundo, muuzaji anakuwa amemshika koo, akizidisha pafu/fundo la moshi anamkaba koo.
 
Naukubali ujamaa ingaje ccm wameuchakachua na sasa hawajui wako wapi,
ujamaa ni utu, ubepari ni unyama,
hakuna cha ndugu kwenye ubepari
 
Nakumbuka sisi tulipokuwa tunaishi bahati mbaya hatukupangiwa duka la kaya ilibidi tufanye urafiki na Wapemba waliokuwa na maduka ili angalau akuuzie nusu kilo ya sukari. Siku moja mimi namwenzangu rafiki yetu aliyekuwa anafanya kazi Game reserve alitutumia kopo la mafuta ya kula Supaghee kilo 2 kila mmoja, njiani watu walitushangaa sana tumeyapata wapi.
 
Ukipangiwa redio au kanga au sukari unalazimishwa ununue na bidhaa Ambayo haitoki dukani kama chumvi
 
Hakika zilikuwa zama za aina yake; baba yangu alikuwa mchungaji wakati huo maeneo fulani ya Arusha. Wahujumu uchumi walipotangazwa kuna muumini wake mmoja akaleta gunia la pesa na kumuomba mzee ahifadhi. Tulipata shida sana kwani chumba ambacho gunia la pesa liliwekwa uvunguni mwa kitanda hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia. Mzee aligeuka kichaa, waumini wakija ile tabia ya kuwasindikiza ikafa kabisa, kila wakati ilikuwa ni kuchungulia gunia la pesa. Muda ukaisha, muumini akaja kudai mzigo wake na mzee akamkabidhi. Mategemeo ilikuwa naye apate mgao baada ya kufanya kazi ya ulinzi kwa muda wa miezi 8. Ajabu muumini alichukua mzigo wake na kumpa mzee asante ya mdomo. Kila mtu nyumbani alihuzunika sana kwani mategemeo ya kupata share tena kubwa yalikuwa makubwa! Ohhh! tukaambulia asante ya maneno! Hizo ndo enzi hizo na hakika kisa hiki hunifanya niikumbuke sana miaka ya themanini hasa nikimuona mzee wangu alivyo leo!
 
Mzee inaonekana wewe ni mtu wa KIU KALI. Lakini kama ungekuwepo kipindi hicho kiu yako hiyo ingekatika yenyewe. Lakini pia hata pesa ya kununua hizo bia nayo ilikuwa haipo. Uzalishaji wa bia kipindi hicho ulikuwa mdogo sana. Na kwa kuwa UJAMAA ni kugawana UMASIKINI tulionao, ndio maana ukawekwa mgao wa bia angalau kila mtanzania aliyetaka kunywa bia anywe japo kidogo. Kwa wale wavutaji wa sigara, ilifika wakati sigara zikauzwa kwa pafu/fundo. Yaani wavutaji sigara wanajipanga foleni, halafu sigara inawashwa watu wanauziwa kwa pafu/fundo la moshi unaovuta. Wakati mvutaji anapiga pafu/fundo, muuzaji anakuwa amemshika koo, akizidisha pafu/fundo la moshi anamkaba koo.

hiyo kali kabali la fundo la sigara duuu... bora ubepari
 
Yah! Duuuh! Umenikumbusha Mbali Sanaa Chief!! Ilikuwa Majanga Tupu!! Mgao Kwa Zamu, Tenaa Na Daftari La Family!! Idadi Na Mjumbe Wenu!! Sukari 1/2, Sembe 1 Na Chumvi 1/2 Kg. Tenaa Chumvi Lazima!! Week Mara 2 Tu!! Mwaenda Panga Mawe Ya Foleni Alfjiri!! Mwakimbizana Na Magari Ya Iliyokuwa Ugawaji!!! Wajumbe Wa Nyumba 10 Kuwa Wafalme Na Malikia Wa Mitaa!!! Haupati Shea Yenu, Hadi Mjumbe Awepo Na Kusaini Daftari Lenu!!! Nakumbuka Nilitapelewa Sh. 20 Na Kindoo Cha Kubebea Sembe, Kwa Msela Kuingia Ndani, Ili Akanipatie Kg 5 Za Sembe Ya Magendo Badala Yake Akatokea Mlango Wa Nyuma, Na Kutokomea Na Kila Kitu!! Nilishinda Njaa! Na Home Kulikuwa Hakuna Kitu!!! Asante Sana Maze Ruksa, Kwa Kututoa Hapo!! Mungu Akupe Maisha Marefu Baba!! Je, Waikumbuka Sembe Ya Njano!!?
 
Nakumbuka sisi tulipokuwa tunaishi bahati mbaya hatukupangiwa duka la kaya ilibidi tufanye urafiki na Wapemba waliokuwa na maduka ili angalau akuuzie nusu kilo ya sukari. Siku moja mimi namwenzangu rafiki yetu aliyekuwa anafanya kazi Game reserve alitutumia kopo la mafuta ya kula Supaghee kilo 2 kila mmoja, njiani watu walitushangaa sana tumeyapata wapi.

Ukibahatika ukawa na ndugu yako akaenda Ulaya lazima umuagize viatu aina ya raba wakati huo tukuviita RABA MTONI. Kama huyo nduguyo alikuwa anakaa sana Ulaya basi akikutumia RABA MTONI lazima kwanza atume kiatu cha mguu mmoja, ukishakipata ndio anatuma tena kiatu cha mguu wa pili. Akifanya makosa akatuma viatu vya miguu yote miwili kwa pamoja, LAZIMA VIIBIWE POSTA. Pia jamaa yako akienda Kenya lazima umtume akuletea dawa ya meno ya COLGATE na sabuni ya IMPERIAL. Siku ukiogea sabuni ya imperial unajipaka pia mwilini kama mafuta ili kila utakapokwenda watu wajue kwamba umeogea sabuni ya IMPERIAL. Ndiyo maana tangia wakati huo mindset yangu ni kwamba the best tooth paste and washing soap is Colgate and imperial respectively!
 
Back
Top Bottom