Ndugu umenikumbusha mbali sana, Enzi za kuvaa mtumba toka Burundi unaonekana mhujumu wa uchumi,kuogea Sabuni ya Magwanji na kuvaa Batiki.
Mwl,alijaribu kwa kiasi chake aka prove filure ktk sera za ujamaa na sasa utandawazi.
Enzi za kusikiliza praye(santuri) na mwenye cassete memory Q tajiri?.
Ahsante kaka,
Ninakumbuka ila nilikuwa bado mdogo, enzi hizo kuna ndugu yetu alitokea malawi alituletea Sabuni na sukari, mzee alikuwa anashauri tuvifiche maana ile product tungeulizwa imetoka wapi in case ikionekana. Lakini binafsi ninamkubali sana Nyerere amekaa madarakani kwa miaka 23 lakini Mwinyi miaka10+, Mkapa10, na sasa Kikwete miaka5 halali na Mmoja wa usio halali. Lakini mpaka sasa ukiangalia vitu tangible vilivyofanyika enzi za Nyerere ni vingi kuliko vilivyofanyika ndani ya Tawala hizi tatu.
Ukibahatika ukawa na ndugu yako akaenda Ulaya lazima umuagize viatu aina ya raba wakati huo tukuviita RABA MTONI. Kama huyo nduguyo alikuwa anakaa sana Ulaya basi akikutumia RABA MTONI lazima kwanza atume kiatu cha mguu mmoja, ukishakipata ndio anatuma tena kiatu cha mguu wa pili. Akifanya makosa akatuma viatu vya miguu yote miwili kwa pamoja, LAZIMA VIIBIWE POSTA. Pia jamaa yako akienda Kenya lazima umtume akuletea dawa ya meno ya COLGATE na sabuni ya IMPERIAL. Siku ukiogea sabuni ya imperial unajipaka pia mwilini kama mafuta ili kila utakapokwenda watu wajue kwamba umeogea sabuni ya IMPERIAL. Ndiyo maana tangia wakati huo mindset yangu ni kwamba the best tooth paste and washing soap is Colgate and imperial respectively!
Na mwisho akakimbia kwa staili ya kung'atuka.Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Duh unanikumbusha raba za pua ya ng'ombe. Mgambo wakikukuta na raba za mtumba wanakuvua.National Radio Cassette Memory Q, Viatu ilikuwa ni Bora peke yake tena kwa mgao. Jamaa wa RTC walikuwa kama Miungu watu miaka hiyo. Mitumba ilikuwa ikiiitwa kafa ulaya.
Mimi nakumbuka mgao wa bia, ambapo bia zilikuwa zinapatikana mwisho wa mwezi. Kila mtu alipangiwa kunywa bia 3 tu. wakati unakunywa bia USALAMA WA TAIFA wanaokata vizibo vya bia ulizokunywa. Ukimaliza magao wako wa bia 3 unakwenda nyumbani kulala. Ukijifanya mjanja ukahamia baa nyingine kuongeza, ukifika baa mhudumu anakunusa mdomo akikuta unanuka bia unakufukuzwa kwasababu atajua kwamba ulikotoka tayari utakuwa umeshakunywa mgao wako wa bia 3. Pia ninakumbuka MARUFUKU ya kutembeza gari la binafsi siku ya JUMAPILI baaada ya saa 7 mchana. Siku ya Jumapili mwisho wa kuendesha gari la binafsi ilikuwa saa 7 mchana, baada ya mda huo gari la binafsi likionekana barabarani linakamatwa na traffic na kupigwa heavy penalty. Mambo niliyoyaona kipindi hicho yalinifanya NIUCHUKUE UJAMAA HADI LEO, mimi huniambii kitu kuhusu SIASA YA UJAMAA!
Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Hspo ni Dar. Kwa wakazi WA Dodoma tunamkumbuka Shekifu. Na huo ndo ulikuwa mwanzo wake kung'ara hadi alipo sasa.[FONT=comic sans
Kila mtu alikuwa lazima amjue Mkurugenzi mkuu wa NMC mzee Mollel au Mkurugenzi wake wa utawala Mz Uwesu msumi
FONT]
Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Ninakumbuka ila nilikuwa bado mdogo, enzi hizo kuna ndugu yetu alitokea malawi alituletea Sabuni na sukari, mzee alikuwa anashauri tuvifiche maana ile product tungeulizwa imetoka wapi in case ikionekana. Lakini binafsi ninamkubali sana Nyerere amekaa madarakani kwa miaka 23 lakini Mwinyi miaka10+, Mkapa10, na sasa Kikwete miaka5 halali na Mmoja wa usio halali. Lakini mpaka sasa ukiangalia vitu tangible vilivyofanyika enzi za Nyerere ni vingi kuliko vilivyofanyika ndani ya Tawala hizi tatu.
Kikwete na familia yake wameteseka vipi? Wanatajirika kwa kuuza madini na ardhi yetu kwa wazungu. Kawaulize.
Kikwete na mkapa nani kauza madini? Na nyerere na mwadui hebu tueleze ilikuaje?. Wee ni mtu mzima hebu weka ukatoliki wako kando useme ukweli
Soma hotuba aliyoitoa Kikwete Afrika Kusini 2007 kuhusu vile alivyokata mbuga kuwatafuta akina Sinclair ndio uulize swali lako. Mwadui ilikuwepo enzi za ukoloni na usitake kuniambia kuwa Nyerere ndiye aliyeleta ukoloni.
Mimi si Mkatoliki. Ni Methodist.
Khaaa wewe nakukubali,yote hayo na bado unamkubali mwalimu!!?,we mwenzangu japo mi sikula hiyo Yanga wala BurgaWewe unadhani mimi namlaumu Mwalimu? Mimi kati ya watu ambao ni watetezi wakubwa wa Mwalimu lakini sikuleta hii mada ili kumhukumu Mwalimu.
Mimi nilishiriki kuiishi hali hii, nilikula unga wa YANGA, nikabugia BURGA, nikaogea MAJANI YA MPAPAI,nimekunywa chai kwa kuchemsha sukari kwa ukosefu wa majani ya chai, nimeogea sabuni ya MAGADI. Huu ni uzowefu wangu wala sina uchungu na sera za Mwalimu!!