nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,281
- 3,243
Katika hali ambayo tayari inadhihirisha serikali ya tz iko hoi bin taaban na inaelekea kushindwa kujiendesha......imefahamika kuwa sasa serikali (kupitia BOT) inajiendesha kwa kukopa hela toka kwenye taasisi za ndani za kifedha kwa kutumia makaratasi yanayoitwa treasury bonds na treasury bills (T-bonds na T-bills).Makaratasi haya hupewa taasisi hizi (baada ya kuipa serikali pesa)yakiwa kama garantee ya malipo ya madeni (kwa riba) kwa kipindi fulani.....(inaweza kuwa miaka 2 au 7 au 10). Pamoja na kukopa kwa kutumia makaratasi haya pia serikali(BOT) imefikia hatua ya kuyapiga mnada makaratasi haya(T-bonds and T-bills auctions) ili kupata pesa za kujiendesha.Katika hali ambayo inatisha....sasa hivi hata minada ya haya makaratasi hairudishi pesa inayokusudiwa kupatikana kwenye minada. Mfano mmojawapo ni hivi majuzi serikali (BOT) ilifanya mnada wa makaratasi ya T-bills kwa lengo la kukopa sh.bil 100 lakini wakaishia kupata sh.bil.13.56 tu. Pia kesho wametangaza mnada mwingine wa T-bond kwa lengo la kukopa bil.20.(tutafatilia kujua)
- Wataalam wa uchumi wanasema serikali imefikia hatua hii mbaya ili kujinusuru na kufilisika ambako kunaonekana dhahiri.
- Inasemekana taasisi nyingi za kifedha zimekuwa na kigugumizi kuikopesha serikali kwa mtindo huu wa makaratasi ya T-bills na T-bonds kwasababu ya anguko kubwa la shilingi linaloendelea(inflation)...pamoja na kwamba huu ndio mtindo unaotumiwa na serikali mara nyingi kukopa
- Mbaya zaidi.....mpaka sasa hivi ile bajeti iliyopitishwa hivi majuzi(June)....ina upungufu wa sh. bil.780
- Wataalam wa uchumi na fedha wanasema hii gap ya bajeti haiwezi kufidiwa hata kama TRA watakusanya mapato yao yooote
- Kwa kipindi cha miezi sita tu ya mwanzo ya bajeti serikali imeshakopa kiasi cha sh.trillion 1.06......kikiwa tayari kinakaribia kufikia kiwango cha mwisho cha kukopa kwa mwaka ambacho ni trillion 1.2.
- Wataalam wa uchumi wanasema kuwa kukopa kwa namna hii ni kubaya na kunaathiri kwa kiasi kikubwa sekta binafsi ambayo ndiyo inatoa mchango mkubwa kwa sasa kwenye pato la taifa na ajira
- Mbaya zaidi......wahisani...ambao ndio wanategemewa na utawala huu....wameshatoa asilimia 10 tu ya mchango wao kwenye bajeti (huu tayari ukiwa nusu ya mwaka wa bajeti)
- ​SOURCE:
- http://www.thecitizen.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/18334-spending-govt-seeks-to-borrow-sh20-billion.html
- Tutafika kwa mtindo huu?..... serikali wajute sasa kwamba ni kwanini wameshindwa kubana vyanzo vya msingi vya mapato kama madini na utalii?....wamebaki kufanya mambo ya kitoto wakidhani watapata hela ya haraka.....mfano mpango waliopitisha wa kutolea mishahara dirishani (eti wanaita national pay day!!!!what a joke eh!!)....eti huu ni mkakati wa kupata hela!!.........kweli tunatawaliwa.......
- Watawala wamekalia siasa wamesahau kutumikia watu wao....wamebaki kujali matumbo yao..na wengine wanadai posho katika hali hii bila woga kwa mungu............watu wanaiba hizi hizi pesa ambazo serikali hawana alafu hawachukuliwi hatua........watawala wamesahau kuwa matatizo ya kiuchumi pia yamechangia kuanguka kwa dola nyingi na mifano ipo miingi tu.....(refer kuachia ngazi kwa viongozi ulaya)............that sad day for our economy(anguko) is veeeery near yaani...........i can't wait...