Ukomo wa serikali ya tz kukopa ili isifilisike unakaribia mwisho.....imefahamika..

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Katika hali ambayo tayari inadhihirisha serikali ya tz iko hoi bin taaban na inaelekea kushindwa kujiendesha......imefahamika kuwa sasa serikali (kupitia BOT) inajiendesha kwa kukopa hela toka kwenye taasisi za ndani za kifedha kwa kutumia makaratasi yanayoitwa treasury bonds na treasury bills (T-bonds na T-bills).Makaratasi haya hupewa taasisi hizi (baada ya kuipa serikali pesa)yakiwa kama garantee ya malipo ya madeni (kwa riba) kwa kipindi fulani.....(inaweza kuwa miaka 2 au 7 au 10). Pamoja na kukopa kwa kutumia makaratasi haya pia serikali(BOT) imefikia hatua ya kuyapiga mnada makaratasi haya(T-bonds and T-bills auctions) ili kupata pesa za kujiendesha.Katika hali ambayo inatisha....sasa hivi hata minada ya haya makaratasi hairudishi pesa inayokusudiwa kupatikana kwenye minada. Mfano mmojawapo ni hivi majuzi serikali (BOT) ilifanya mnada wa makaratasi ya T-bills kwa lengo la kukopa sh.bil 100 lakini wakaishia kupata sh.bil.13.56 tu. Pia kesho wametangaza mnada mwingine wa T-bond kwa lengo la kukopa bil.20.(tutafatilia kujua)

  • Wataalam wa uchumi wanasema serikali imefikia hatua hii mbaya ili kujinusuru na kufilisika ambako kunaonekana dhahiri.
  • Inasemekana taasisi nyingi za kifedha zimekuwa na kigugumizi kuikopesha serikali kwa mtindo huu wa makaratasi ya T-bills na T-bonds kwasababu ya anguko kubwa la shilingi linaloendelea(inflation)...pamoja na kwamba huu ndio mtindo unaotumiwa na serikali mara nyingi kukopa
  • Mbaya zaidi.....mpaka sasa hivi ile bajeti iliyopitishwa hivi majuzi(June)....ina upungufu wa sh. bil.780
  • Wataalam wa uchumi na fedha wanasema hii gap ya bajeti haiwezi kufidiwa hata kama TRA watakusanya mapato yao yooote
  • Kwa kipindi cha miezi sita tu ya mwanzo ya bajeti serikali imeshakopa kiasi cha sh.trillion 1.06......kikiwa tayari kinakaribia kufikia kiwango cha mwisho cha kukopa kwa mwaka ambacho ni trillion 1.2.
  • Wataalam wa uchumi wanasema kuwa kukopa kwa namna hii ni kubaya na kunaathiri kwa kiasi kikubwa sekta binafsi ambayo ndiyo inatoa mchango mkubwa kwa sasa kwenye pato la taifa na ajira
  • Mbaya zaidi......wahisani...ambao ndio wanategemewa na utawala huu....wameshatoa asilimia 10 tu ya mchango wao kwenye bajeti (huu tayari ukiwa nusu ya mwaka wa bajeti)
  • ​SOURCE:
  • http://www.thecitizen.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/18334-spending-govt-seeks-to-borrow-sh20-billion.html
My take:
  • Tutafika kwa mtindo huu?..... serikali wajute sasa kwamba ni kwanini wameshindwa kubana vyanzo vya msingi vya mapato kama madini na utalii?....wamebaki kufanya mambo ya kitoto wakidhani watapata hela ya haraka.....mfano mpango waliopitisha wa kutolea mishahara dirishani (eti wanaita national pay day!!!!what a joke eh!!)....eti huu ni mkakati wa kupata hela!!.........kweli tunatawaliwa.......
  • Watawala wamekalia siasa wamesahau kutumikia watu wao....wamebaki kujali matumbo yao..na wengine wanadai posho katika hali hii bila woga kwa mungu............watu wanaiba hizi hizi pesa ambazo serikali hawana alafu hawachukuliwi hatua........watawala wamesahau kuwa matatizo ya kiuchumi pia yamechangia kuanguka kwa dola nyingi na mifano ipo miingi tu.....(refer kuachia ngazi kwa viongozi ulaya)............that sad day for our economy(anguko) is veeeery near yaani...........i can't wait...
 
....Haya ni matokeo ya kuwa na Serikali taahira, na hata siku moja hutamsikia Kikwete, Pinda, Mkulo au Ndulu kutamka hadharani kwamba Serikali imefilisika na hivyo inabidi ipunguze matumizi yake kati ya 60% to 80% ili kuweza kukidhi mahitaji yake muhimu. Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele.
 
Katika hali hii watu wazima wanajiongezea posho! Nanusa harufu ya mada kesi muda si mrefu
 
teh teh tehhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh teh teh ahhhhhhhhhh aiseeeeeeeeeeeeeeeeeee.kufa hatufi ila sasa cha moto ndo tutakiona eeeeeeehhhhhhhhhhhh uuuuuuuuuuuuuiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiihhhhhhhhhhhhh
 
Watu waliopoenda kupiga kura mwaka jana walifikiria wanaenda kumkomoa nani au kuchagua nini?

Hakuna ajuaye kwa hakika JK ndiye alishinda,watu walijitahidi kupiga kura kumchagua wamtakaye

Kama tume ya uchaguzi itabaki kama ilivyo itatutangazia tena rais wao na siye wa watanzania
 
Kikwete chukua hatua hizi kunusuru taifa:-

1. Ondoa manaibu mawaziri wote, na manaibu makatibu wakuu wa wizara.

2. Punguza wizara zibaki wizara muhimu tu.

3. Futa mara moja kuanzishwa kwa mikoa mipya na wilaya mpya

4. Hakikisha magari yote ya serikali yanafanya kazi za serikali peke yake, familia za viongozi watumie magari yao ambayo wamepewa kipaumbele cha kununua kwa pungufu ya kodi.

5. Magari yote ya serikali yaengeshwe nje ya ofisi za serikali muda wa kazi unapoisha. Watumishi wote watumie magari yao binafsi kwenda na kurudi nyumbani.

6. Futa safari za nje, ikilazimu viongozi wasafiri kwa daraja la kawaida.

7. Punguza manunuzi ya silaha kwa jwtz.

8. Simamisha wabunge wa viti maalum.

9. Piga mnada wa magari ya kifahari yote yanayotumiwa na viongozi wa serikali, kwa kuanza na ofisi yako.
 
Back in July niliwahi kuuliza swali kama huu mwaka wa fedha utaisha salama. There are too many promises and "too few" funds sources, ni upuuzi wa serikali ya huyu KAKA mkubwa. In attempting to please everybody, there are losing everything.
 
rais ajaye Baada ya jk atapata shida
Itamlazimu achukue maamuzi magumu sana kama alivyofanya Sata kule Zambia. Mali za Kikwete, Ridhiwani, Lowassa, Rostum, zikamatwe na wote wafilisiwe. Itabidi tuanzishe mahakama maalumu ya wahujumu uchumi na kusimamisha uchimbaji wa madini mpaka tutakapokamilisha mikataba mipya itakayokidhi maslahi ya Watanzania.
 
Kaazi kweli hivi zile ajira za walimu+watu wa wizara ya afya zitakuwepo kweli? Da NEC walitupatia mtu wao huyu tizama sasa nchi imeshamshinda
 
Kusema kweli nimeshangaa sana nilivyosoma article hii. Kweli hii nchi inasikitisha. Haiwezekani nchi inakopa mikopo ya muda mrefu just to facilitate short term spending!! What a shame. Hawa jamaa wanajua kabisa coming 10yrs chama hakitakuwa madarakani hivyo watawala wa kipindi hicho watafanya kazi ya kulipa madeni. Wachumi wa nchi hii wako wapi? Fanya kumsaidia rais huyu maana kila kitu kimekwama. Naona uchaguzi wa rais kabla ya 2013.
 
Back in July niliwahi kuuliza swali kama huu mwaka wa fedha utaisha salama. There are too many promises and "too few" funds sources, ni upuuzi wa serikali ya huyu KAKA mkubwa. In attempting to please everybody, there are losing everything.

hii ni kweli kabisa mkuu,mikataba kibao ya barabara ilitiwa saini kisiasa na macontractor kupewa advance tu,wakati pesa za kuendeleza mradi hazipo hivyo ujenz unasuasua sana na baadhi umesimama kabisa hivyo kuendelea kutia hasara
 
huyu Mh.Alhaj Dr.Dr.Dr.Dr.Kikwete baada ya kuona Mkulo katika kipindi chake cha mwanzo ameshindwa kukusanya kodi Ndullu ameshindwa kurekebisha mfumuko wa bei basi hakika angeweka watu wenye tija unaona sasa nchi ilivyomshinda ,Kukopa nako wanamzingua watoa pesa
Marafiki zake wahisani wanamdengulia kinamna wanamuacha ajikaange mwenyewe kwa mafuta yake hataki kurekebisha mikataba ya madini anazidi kuingia kwenye mikataba mibovu,kodi aikusanywi bado misamaha ya kodi duh nchi haina mwenyewe hii
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom