Shabiby aitaka Serikali isisikilize maneno ya watu kuhusu kukopa kwasababu inao wataalam wa kutosha, adai ingekuwa yeye angekopa dola bilioni

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Ahmed Shabiby ameitaka Serikali kutafuta dola bila kujali watu watasema nini, Shabibi amesema ingekuwa ni yeye angekopa dola bilioni moja kukabiliana na uhaba wa dola nchini na kuziingiza kwenye mzunguko. Shabiby amesema dola bilioni moja ni kitu kidogo sana kwa Serikali kwani inakusanya trilioni 2.

Shabiby amesema Serikali inatakiwa ikiamua kitu imeamua kwasababu inao wataalam wa kutosha na isisikilize maneno ya nje yanayosemwa na watu kuhusu kukopa.

Ushauri serikali kwa sasa izidishe kuweka Vito vya thamani katika reserve ya benki Kuu hii itatusaidia kuwa mbadala wa dola maana ni vitu tunavyo ndani ya nchi yetu japo asilimia kubwa vimeuzwa kwa wageni.
 
ukishapata hiyoo dola ukanunua mafuta dola ikatoka utakopa tena upate dola?

mafuta yananunuliwa kwa dola, yanauzwa kwa tsh. mkopo wenyewe utakao kopa utarejesha kwa dola.
Mafuta yanatumika kufanya uzalishaji ambao unachochea kupata dola. Huo ni mzunguko wa kiuchumi ndio kanuni hiyo.
 
Kuna mambo machache yangefanyika yangesaidia ongezeko la pesa za kigeni, ila wasomi wanaamini katika kukopa na kukopa tena. Kama ingekuwa mikopo ina strength shilling yetu kwa dollar, basi tungekuwa tumepiga hatua kubwa maana tunajua kukopa.
 
Ajaribu Basi kutumia mikopo yake kuboresha Ile stend ya gairo,inatia aibu
Stend vumbi tupu,amwage hata zege pale
Au aiboreshe iwe kama ya chalinze
Mbunge wa miaka Ila Jimbo lake maskin la kutupwa na hakuna miundombinu
 
Ahmed Shabiby ameitaka Serikali kutafuta dola bila kujali watu watasema nini, Shabibi amesema ingekuwa ni yeye angekopa dola bilioni moja kukabiliana na uhaba wa dola nchini na kuziingiza kwenye mzunguko. Shabiby amesema dola bilioni moja ni kitu kidogo sana kwa Serikali kwani inakusanya trilioni 2.

Shabiby amesema Serikali inatakiwa ikiamua kitu imeamua kwasababu inao wataalam wa kutosha na isisikilize maneno ya nje yanayosemwa na watu kuhusu kukopa.

Anadhani kuendesha nchi ni kama kuendesha Basi la Dar to Moro
 
Back
Top Bottom