Ukitumia ARV'S unaweza kusukuma siku adi miaka mingapi?

Katika maisha yangu sitokuja kumshauri mtu aliepima ukimwi akaambiwa anao atumie Arv.kufanya ivyo ni kama kushiriki mauaji ya moja kwa moja ya mhusika.

Hii thread ni sumu sana,wanadanganyana sana lakini wenyewe hawajijui.Eti wanapeana moyo kwa kushauriana jinsi ya kuishi kwa kunywa sumu inayokuua taratibu.Sasa wanaulizana,"eti ukinywa hii sumu inaweza kukuua baada ya muda gani"?Halafu wengine wanajibu,"aah mbona kuna wengine wanahimili madhara yake kwa zaidi ya miaka 30".

He he heeee ujinga bwana!!
 
hivi mkuu unapata faida gani unavyopotosha uma si bora tuu ukae kimia watu kama nyie wafaa mpigwe mawe mpaka mfe
 
Huyu jamaa ni shiiida!!! Tafadhali endeleeni kuamini kuwa VVU vipo.
 
hivi mkuu unapata faida gani unavyopotosha uma si bora tuu ukae kimia watu kama nyie wafaa mpigwe mawe mpaka mfe

Ukishajua ukweli huu ndipo utakapojua kwamba wewe na wengine mnaounga mkono suala hili ndio mlitakiwa mfutwe kwenye uso wa dunia.Lakini sasa hivi sikulaumu wewe bali nalaumu ujinga wako...sina kinyongo na wewe bali niko tayari siku zote kukufundisha pale utakapohitaji.
 
nawafahamu watu Zaidi wa wanne;
mama wa kwanza tokea aanze kutumia hizo dawa ni Zaidi ya miaka ishirini sasa imepita;
mama mwingine naye ni Zaidi ya miaka 13 imepita;
wale watoto 2 nawafahamu mmoja yuko form four mwingine form one;
wote hao wako vizuri; tena huwezi hata kuwafikiria kama wanatumia dawa;

wakati Fulani nilienda hosp moja kubwa hapa nchini nikaenda kitengo cha waathirika
nilikaa tu kwenye benchi kama mgonjwa kwa Zaidi ya masaa matatu; niliona maajabu
watu wanaokuja kuchukua dawa hauwezi kuamini kama ni wagonjwa;

nilijifunza kitu kuwa kupata virusi siyo mwisho wa maisha; pia inatakiwa kufuata
masharti ya daktari.
 
watu wanaishi adi miaka 40 huyu decpection analeta siasa kwenye mambo ya msingi bhana ni wa kumpuuza watu watumie dawa jamani zinasaidia sana
 
Ukishajua ukweli huu ndipo utakapojua kwamba wewe na wengine mnaounga mkono suala hili ndio mlitakiwa mfutwe kwenye uso wa dunia.Lakini sasa hivi sikulaumu wewe bali nalaumu ujinga wako...sina kinyongo na wewe bali niko tayari siku zote kukufundisha pale utakapohitaji.
Nimetoka kupoteza ndugu yangu kizembe sana na haya madawa.najiona mkosaji sana.madhara ya izi dawa yasikie kwa jirani tu.zinaweza kukua ndani ya mwezi tu kama afya sio stable sna.siku nikiwa vizuri nitatoa ushuhuda humu ndani.
 
Ushaur wa kitaalam
1) idadi ya kawaida ya cd4 ni kuanzia around 600 had 1200micromil/l
2.swala la miaka na matumiz ya arvs linategemea na mambo mengi (in general ni ur lyfe style, kama unatumia arvs vizur, unakula chakula bora , unafanya zoez vizru, na unaepuka kufanya unaprotected sex, jnaoata muda wa kupumzika. .unaweza ishi maisha malefu tuu as a normal person
3) unapoanza ku2mia arvs hua kuna maudhi madogomadogo (side effects) ambazo most pple wanazipata for the 1st 2 weeks then wanakua poa, but kama zikiendelea unaweza badilishiwa dawa
ASANTE
Maelezo mazuri sana kiongozi.
 
Izi ndio lugha zenu adi mgonjwa akikata roho utaskia mapenzi ya mungu!!!mtu anaanzishiwa dozi bila ya kupima afya yake kujua damu ikoje,ini,figo,moyo!!yaaan very sad!!tena uko kubadilishiwa dawa ndio kbisaa .mnafanya majaribio kwenye maisha ya watu!!
 
Mnaonekana mna uzoefu mkubwa wa kutumia hizo dozi.
Basi watalaamu wote wa afya watakua wanaumwa magonjwa wanayotibia, kwa inamaanisha anaejua tatizo na tiba yake ni mgonjwa, kweli tunatofautiana uelewa. Unadhani forums hii ni ya mambumbu tupu, aina watu phani zao, kama unaelewa hivyo pole sana, kwa taarifa yako hapa kuna wataalamu wa fani mbalimbali pia wako hapa majukwa mbalimbali ya forums hii.
 
Maafa ya ARV

ZAIDI YA WATU 400,000 WADAIWA KUPEWA DAWA BANDIA NCHINI, MAMLAKA YA MADAWA YAAGIZA ZIONDOLEWE HOSPTALINI

MAELFU ya watu walioathirika kwa ugonjwa wa Ukimwi ambao kwa sasa wanaotumia Dawa za Kurefusha Maisha (ARVs) nchini wapo hatarini kufupisha maisha yao baada ya kubainika kuwa toleo mojawapo la dawa hizo la Machi, 2011 ni bandia. Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa dawa hizo zilizosambaa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mara zilianza kusambazwa tangu Mei mwaka huu na hadi sasa bado zipo sokoni, jambo lililoilazimu Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kuagiza zirudishwe Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Tayari TFDA imetoa waraka ambao umesambazwa kwenda kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuwaagiza kuondoa dawa hizo kwenye mzunguko mara moja.

Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Fatuma Mrisho aliliambia gazeti hili jana kuwa Tanzania kuna zaidi ya watu 900,000 waliojiandikisha kutumia dawa za ARV, lakini asilimia 55 ya watu hao ndiyo walioanza kutumia. Asilimia hiyo ni sawa na watu 495,000. Barua hiyo yenye kumbukumbu namba BD.411/412/01D/58 ya Agosti 23 mwaka 2012, imesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi uliobaini kuwa ni bandia.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Dk Sikubwado Ngendabanka dawa hizo hazipaswi kutumika na zinatakiwa kuondolewa sokoni mara moja.

Barua hiyo ya TFDA iliendelea kufafanua kuwa, “TFDA imefanya uchunguzi na kubaini uwepo wa dawa bandia yenye jina la biashara TT-VIR 30 (yenye mchanganyiko wa viambata hai vya Nevirapine 200mg, Lamivudine 150 mg na Stavudine 30 mg) ya vidonge inayotengenezwa na Kiwanda cha dawa cha Tanzania Pharmaceutical Industries LTD (TPI),” ilisema sehemu ya barua hiyo. Hata hivyo, taarifa za ndani ya TFDA za kiuchunguzi zinasema kwamba TPI wameonyesha kutoitambua dawa hiyo hivyo kuzidi kujenga wasiwasi iliingiaje sokoni kupitia MSD.

Iliendelea kueleza kuwa, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa vidonge vya dawa yenye toleo namba (batch number oc.01.85) iliyotengenezwa Machi 2011 na muda wa matumizi kutarajiwa kuisha Februari 2013 viko tofauti. “Baadhi vikiwa na kiambata hai cha Efavirez pekee na baadhi vikiwa na mchanganyiko wa viambata hai vya Nevirapine, lamivudine na Stavudine.

Aidha, baadhi ya vidonge vya toleo hili havina ubora unaokubalika ikiwa ni pamoja na kubadilika rangi na kuota fangasi,” ilisema barua hiyo. Ilisema kuwa, Mamlaka hiyo inaendelea kufanya uchunguzi zaidi kwa nia ya kubaini mtengenezaji na msambazaji halisi wa dawa hiyo ambayo kwa sasa imepatikana katika baadhi ya hospitali za Serikali katika Mikoa ya Tanga, Mara na Dar es Salaam,” ilisema.

“Kutokana na hali hiyo, TFDA inawaomba muwaeleze Waganga Wakuu wa Wilaya, kusimamisha matumizi ya toleo tajwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati na kurudisha dawa hizo kwa msambazaji (MSD), kwa hatua zaidi za kisheria,” ilisema na kuongeza. “Endapo itabainika kuwapo kwa matoleo mengine yenye ubora wenye mashaka, taarifa zitolewe mara moja ili nayo yaweze kuondolewa kwenye mfumo wa usambazaji wa Serikali na sokoni pia.”

Akizungumzia barua hiyo jana, Mkurugenzi wa TFDA, Dk Hiiti Sillo alisema pamoja na maelekezo hayo, uchunguzi bado unaendelea ili kujua ni nani aliyetengeneza dawa hizo. “Kama kawaida yetu sisi tukipata habari mara moja huwa tunachukua hatua ili kudhibiti madhara zaidi, kwa hiyo kweli hiyo barua ni yetu na kwa sasa wataalamu wetu wanaendelea na uchunguzi zaidi,” alisema Dk Sillo.

Alisema kuwa, suala hilo ni nyeti na linagusa maisha ya watu wengi hivyo uchunguzi lazima ufanyike kwa kina. Dk Sillo alilieleza gazeti hili kuwa, baadhi ya mambo yanayochunguzwa ni endapo kweli dawa hiyo ni bandia na kama tarehe ya kutengeneza na kumalizika kwa matumizi yake ni sahihi.

“Tukibaini kuwa ni bandia kabisa hatua za kisheria zitachukuliwa, ila kwa sasa tunasubiri uchunguzi huo ukamilike kwa sababu pengine yawezekana tu kuwa zipo chini ya kiwango,” alisema Dk Sillo: “Ukitaka kujua zaidi juu ya dawa hizo, hatua iliyofikia katika kuziondoa sokoni na uchunguzi wake juu ya kuwa bandia ama laa, nitafute kesho, sasa hivi niko barabarani.”

Kwa upande wa MSD, ambao ndiyo wanaodaiwa kuwa wasambazaji wa dawa hizo, walisema kuwa kupata taarifa kamili ya kiasi cha dawa kilichosambazwa na kile ambacho kimerudishwa baada ya taarifa ya TFDA, watatoa taarifa rasmi leo. “Siwezi kusema chochote leo, nitumie barua pepe kesho kwenye saa tano nitakuwa nimekujibu,” alisema Msemaji wa MSD, Ety Kuseluka.

Uchunguzi wa ndani ya TFDA ambao hauko katika barua iliyotumwa kwa waganga wa mikoa yote nchini unasema kwamba aina hii ya dawa feki imeanza kusambazwa Mei mwaka huu na idadi kubwa ya watu tayari wametumia na huenda wamepata madhara.

“Kwa jumla, dawa hizo zimesambazwa maeneo mengi na tayari zimesambazwa kwa wagonjwa wengi. Jambo la kusikitisha ni kuwa baadhi ya kopo hizo zina dawa aina ya Efavirenz ambazo hupaswa kutumiwa mara moja tena nyakati za usiku tu . Hivyo wagonjwa waliotumia dawa hizo wamekuwa wakitumia dawa moja (monotherapy) kwa muda mrefu na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa virusi kujenga usugu,” ilisema taarifa hiyo ya uchunguzi. Usikose gazeti la Mwananchi kesho kupata taarifa za kina zaidi kuhusiana na dawa hizi zinazodaiwa za bandia.

chanzo.HABARI NA MATUKIO: Maafa ya ARV
 
Dawa za ARV zabainika kujenga usugu

PIC+DAWA.jpg

By Florence Majani

Dar es Salaam.

Kwa ufupi
Ripoti mpya iliyotolewa jana na jarida la kisayansi la Lancet, imeeleza kuwa usugu wa dawa hizo utasababisha matibabu kwa watu wanaoishi na VVU duniani kuwa magumu.

Tumaini kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) sasa linayeyuka mithili ya barafu kwenye moto baada ya dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo (ARV) kubainika kuwa zinajenga usugu.

Ripoti mpya iliyotolewa jana na jarida la kisayansi la Lancet, imeeleza kuwa usugu wa dawa hizo utasababisha matibabu kwa watu wanaoishi na VVU duniani kuwa magumu.

“Kutokana na hali hiyo, matibabu na usimamizi kwa watu wanaoishi na VVU ni lazima yaboreshwe na wagonjwa wafuatiliwe,” inasema ripoti hiyo.

Kisayansi, dawa za ARV zinapojenga usugu maana yake ni kuwa hazitaweza tena kupambana na VVU hivyo mgonjwa kuendelea kupata magonjwa nyemelezi.

Kadhalika ripoti ya utafiti huo inaeleza kuwa dawa za ARV ambazo zimejenga usugu ni pamoja na Tenovofir efavirenz na lamivudine.

“Kama dawa zinajenga usugu, basi hiyo ni hasara kubwa,” mwandishi wa utafiti huo, Dk Robert Shafer amesema.

Ripoti hiyo inasema watu wenye VVU hujenga usugu wa dawa aina ya Tenovofir kwa namna mbili, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutotimiza masharti ya dawa na hivyo virusi kuzaliana au pengine wamepata maambukizi kwa mtu ambaye tayari ana virusi vilivyojenga usugu.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangala alisema kama kweli dawa hizo zimekuwa sugu, basi lazima mabadiliko ya sera za matibabu yabadilike na mfumo wa usimamiaji wa matibabu ya ARV pia ubadilike.

“Nitakuwa kama mbumbumbu kama nitakuambia chochote sasa. Hizo taarifa ni nzito na zinaweza kubadili chochote katika matibabu kama ni kweli,” alisema Dk Kigwangalla ambaye aliahidi kuzungumzia suala kwa kina atakapojiridhisha kuhusu suala hilo.

Watafiti wa Lancet wanasema walitumia taarifa kutoka kwenye sampuli ya watu 1926 wenye VVU kutoka nchi 36 ambao wanatumia ARV.

Utafiti huo ulibaini kuwa tenovofir ilijenga usugu kwa asilimia 20 ya wenye VVU barani Ulaya na zaidi ya asilimia 50 ya wagonjwa hao kutoka kusini mwa jangwa la Sahara.

Chanzo cha Tenovofir kujenga usugu kunatajwa na watafiti hao kuwa ni pamoja na kuanza dawa wakati kinga ya mwili (CD4) ipo chini na matumizi ya dawa muambata za ARV.

chanzo.Dawa za ARV zabainika kujenga usugu
 
Attachments

  • PIC+DAWA.jpg
    PIC+DAWA.jpg
    11.3 KB · Views: 131
anti ukibishana na mjinga na ww unaweza kuonekana mjinga unajua malipo ni hapa hapa duniani ndiyo maana wanasema hakuna ajuae kesho ata mtunzi wa kalenda wengi wanadhani vvu hutokea kwa ngono but unaweza usifanye ngono ukaupata tuu mungu mwache aitwe mungu tuu tuwe na akiba ya maneno ulimi ni kiungo kidogo ila kinawwza msababishia mtu matatizo na kukufuru kwa mungu
Kwa hapa sio ulimi mkuu ni vidole, hasa dole gumba,ulimi hauusiki kabisa
 
Back
Top Bottom