Utafiti uliodumu kwa Miaka 22 kuhusu Mungu yupi ana nguvu katika Ulimwengu wa Rohoni. Hakika Mungu wa Walokole ana nguvu

Uyu hapa

JF-Expert Member
Oct 14, 2021
348
401
Mtafiti Huyo ni :Nelson Jacob lushasi .

Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.

Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.

Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.

Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.

Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.

Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.

Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".

Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.

Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.

Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.

Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?

Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?

Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?

Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?

Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.

Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.

Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.

ITAENDELEA


INAENDELEA........
Basi udadisi wangu ulianzia kwa dadangu wa kuzaliwa tumbo moja,ilikua kila jioni wakati nipo mdogo miaka ya shule ya msingi,kila ikifika jioni mamangu ambae alikua mlokole alikua anawaita wamama majirani zake kusali jioni baada ya kula na wanasalia uani kwenye nyumba.Wakiwa wanasali na sisi kama watoto tunaenda kukaa chini pale tunasali nao ila sio serious,basi dadangu ananiambia angalia ukutani kuna "Malaika"wamekuja.Mimi natoa macho sioni na kumbe kuna baadhi ya wale walokole wanawaona pia ila hawasemi.Dada baadae anaenda kumsimulia mamangu na mamangu anaenda kuwasimulia waumini wenzake kua mwanangu jana kaona malaika.Basi wale wamama wakiongozwa na mama mmoja hivi anaitwa "Mama Samueli"ndio kama wamemwagiwa maji ya moto maana kesho wakija ni maombi pale uani masaa saba au sita kila jioni na kila siku nachungulia nitawaona hao malaika au sitowaona, nikaambulia patupu ila dadangu siku moja moja anawaona na kunielezea.

Ndipo udadisi wangu ukaanzia hapo kutaka kujua viumbe hawa wa kiroho na jinsi walivyo na utararibu wao wa maisha na wanakaa wapi na madhumuni yao kushuka duniani kuja kukaa na walokole wanapokua wanasali.

Miaka ikaenda na nikasahau hayo mambo ila kuna vitu vikawa.Kuna siku nilikua msibani nikajiuliza sana kwanini binadamu wanakufa na wakifa wanaenda wapi,nikaanza upya udadisi wangu kuhusu ulimwengu usioonekana.Kuna wakati nilisafiri mkoani kigoma nikakutana na mzee mmoja nikamuelezea kuhusu udadisi wangu wa haya mambo ya ulimwengu usionekana.

Mosi:Akaniambia nje ya ulimwengu huu wa kawaida kuna ulimwengu mwengine na kuna jamii mbili ambazo ni jamii za watu wanaofanana na binadamu na wanaakisi mwanga wa jua na makazi yao ni anga za mbali nje kabisa na mfumo kani wa ulimwengu karibia maili trion zisizohesabika kwa hesabu za kibinadamu.Na pia jamii ya watu wanaofanana na binadamu ambao wanakaa katikati ya dunia ila wanazurura kwenye sayari zote za mfumo wa jua ila hawawezi kwenda nje ya mfumo kani wa ulimwengu sababu sio eneo lao la kiutawala.

Pili: Hizo jamii zote zina imani zao na zimeleta imani hizo kwa binadamu na kuwafundisha na nikitaka anaweza kunifundisha pia,lakini ni imani kinzani.
Tatu:Nikitaka kujua haya mambo nichague upande mmoja wa jamii zile mbili niwe mfuasi wake lakini kuna miiko na utaratibu wake wa kuzingatia katika hilo.

Akaniuliza yule mzee ""Wewe unataka kujua nini""nikamjibu kua mimi nataka kujua na kuwaona wale viumbe waliokua wanamtokea dadangu utotoni ikiwezekana niwahoji baadhi ya vitu kuhusu wao.Nakumbuka yule mzee akachekaa akaniita kwa kucheka""Mulashani""nani alikupa jina hilo na mimi nikamjibu ni babu yangu mzaa baba,akacheka akasema unajua maana yake hilo jina.Nikamjibu sijui,akasema maana yake ni mtu mpiganaji na wapiganaji waga wadadisi na wadadisi hupatwa na majanga sababu ya udadisi wao.Lakini akaniambia nitakupa njia rahisi ya wewe kuwaona hao viumbe,ila akauliza ni nani aliyekuelekeza kwangu.

Nikamjibu kua wewe mzee............ ni mnajimu na una elimu ya anga nilielekezwa kwako na flani........nikamtajia jina la mtu aliyenielekeza kwake.
Akasema wewe shida yako tu ni kuwaona hao viumbe wanaokwenda kwa walokole kila mara??????Nikamjibu ndio,akaniuliza ukiwaona hautoweza kuzungumza nao sababu haujapitia njia yao kwenye ulimwengu wa ndani,kwanini usiende kwa walokole wakufundishe jinsi ya kuwaona.Nikamjibu kua shida yangu ni kuwaona na kuamini kama wapo hao viumbe.Akaniuliza tena unajua wanaitwaje,nikamjibu kwa kusema wanaitwa"Malaika au makerubi""akaniambia wanaitwa watu wa jamii ya jua na mkuu wao hana upinzani katika ulimwengu zoote saba.Nikaanza udadisi na maswali kwanini wanajihusisha na walokole.
Mzee akanijibu wanajihusisha na walokole sababu walokole wana usharika nao kupitia""Mwana wa mmliki""ambae walokole wanamwita Mungu wao na wanatumia jina lake ila hawezi kulitaja hapo sio mahali pake.

Akasema wao hao watu wa jamii zenye kuakisi mwanga wa jua wana makazi yao nje kabisa ya mfumo wa sayari za ulimwengu na wana miaka sawa na mwanga wa mfumo wa sayari za ulimwengu mara trioni.Akimaanisha kua walikuepo miaka trioni kabla ya mfumo wa sayari za ulimwengu kuwepo.

Nikamuuliza vipi kuhuusu ile jamii nyingine ya wale watu alioniambia wanakaa katikati ya dunia kupitia chini ya maji,akanijibu shida yangu ni kuwajua viumbe marafiki wa walokole basi hayo mengine niachane nayo kwanza.Akaniambia tayari washajua nia yangu ya kutaka kuwaona hivyo nikwaona nijue ni kwamba wao wameamua niwaone na nisipowaona nijue ni wao wameamua nisiwaone.
Akaniuliza nia yako ni kuwaona tu hakuna jingine lolote,nikamjibu ndio.Basi akasema atanielekeza nimuone mkuu wao ambae ni nyota ya mashariki wao wanajimu wanamuita hivyo.
Akasema ikifika jioni twende karibia na kanisa lolote la kilokole au mkusanyiko wowote wa kilokole hasa wakiwa katika maombi yao.Yeye hawezi kusogea ila mimi naweza kuwasogelea wale walokole na wakianza kusali nifumbe macho pia ni ishara ya heshima kwa mkuu wao(Mungu wao)..Afu nitakachokiona iwe siri yangu ili nisiwashitue wale walokole wanaosali pale

Basi ile wilaya niliyokuwepo kuna makanisa mengi ya walokole hasa pale mjini,nikaona ndio kitovu cha utafiti wangu kuwatafiti walokole kisayansi nijiridhishe dukuduku zangu kuhusu matukio ya utotoni.Basi kufikia jioni tukaenda kwenye kanisa alilonielekeza tukawadadisi walokole tuwapeleleze.Mimi na akili zangu za kisayansi afu mzee wangu mnajimu na akili zake za uganga na utaalamu wa nyota na anga wanaita unajimu.

Tulipokua njiani akawa ananiambia wewe kijana mdadisi ila na mimi udadisi wako umenivutia na mimi ngoja nikupeleke afu mimi nakaa mbali maana walokole nawajua na imani zao nazijua na kwa mbali tunasikia miziki ya vyombo inatoa sauti watu wanaimba kwaya maana kanisa halikua mbali sana ni kilimani tu unapandisha,mimi mbele na mzee wangu nyuma tunapandisha kilima.

Cha ajabu sasa nipo njiani yule mzee wangu mnajimu tunapiga story mara nahisi ukimya ile kugeuka eeeh kanikimbia kimiujiza nimebaki peke yangu njiani.Nageuka kushoto simuoni nageuka nyuma simuoni,nageuka kulia simuoni.Lakini nilipoangalia mbele tena"""Eeeeh"""Nakutana na mtu mrefu kama wale wachezaji wa mpira wa kikapu ananitazama,na anaakisi mwanga wa jua,amevaa kanzu bwanga na miguu yake haifiki chini ila imefunikwa na ile kanzu.Uso wake ulikua wa kirafiki sababu alikua anatabasamu ila hauonekani vizuri hata nywele sababu ya kuakisi mwanga wa jua na ngozi yake kama rangi za sarafu ya mia mbili au sarafu za shilingi hamsini,kwa haraka haraka ni kama mtu wa shaba ila mrefu kuliko binadamu wa kawaida.Lakini sasa anatembea kuja barabarani nilipo,na sio kwa kutembea kule bali kuelea wimawima hewani.Hayo yote ni ndani ya nusu dakika,na mzee kashakimbia simuoni.Ile nataka nianguke kwa hofu yule mtu akapotea ila sasa mimi nipo nimeganda kama sanamu hofu yoote imetoweka limebaki bumbuwazi natoa macho tu.

Baadae kidogo ndio akili inarudi ila cha ajabu hofu sina naona kawaida tu,yule mzee wangu simuoni sijui alipoteaje bila kunitaarifu.Safari ya kwenda kanisani kwa wale walokole ikaishia hapo nikaanza kurudi chini kilimani kumtafuta mzee wangu na nilipomkosa nikarudi mpaka nyumbani kwake namkuta kakaa ananisubiri huku kanuna ila mimi nikaanza kucheka.Akaniuliza unacheka nini afu yeye akaanza kucheka ila ananicheka mimi""Wewe si mdadisi mbona ulikimbia mjukuu

wangu"""nikamwambia sikukimbia ila niliganda kwa hofu na yule kiumbe alitokea na kupotea ndani ya nusu dakika.Akaniambia yule sio kiumbe bali ni wale watu wa jamii ya jua walinzi wa walokole.

Akasema mpango wa kuwadadisi wale walokole tutaufanyia tukiwa mbali ila sio karibu na makanisa yao na akanitaka ninuie kua mimi shida yangu ni udadisi tu na sio kitu kingine chochote.Nikanuia pale na akaniapiza na tukapanga tutaendelea na udadisi wetu siku nyingine kwa siku ile nilichokiona kinatosha,ila sasa nikitaks kuendelea na udadisi lazima niwe msiri nisitangaze kwa watu,afu niwe nakariri maombi ya walokole maana waga wanaongea moja kwa moja na mkuu wao ambae anaitwa""Mwana wa mmliki"'ikiwezekana niombe kibali cha kufanya udadisi wangu sababu sina nia mbaya na walokole bali nachofanya ni udadisi wa kujiridhisha utafiti wangu.Cha ajabu japo yule kiumbe alikua ametokea ghafla ila sikua na uoga kabisa moyoni baada ya yeye kutoweka.

Akili yangu na hamu ya udadisi kwenye ubongo wangu ikaendelea kuongezeka wakati ule nipo mkoani kigoma kwenye wilaya moja inayopakana na nchi jirani.Mzee wangu akaniambia kila alhamisi ndio siku atakazokua na nafasi kunifundisha kidogo kidogo na kunielezea kwa undani hao walokole ni watu wa aina gani na hiyo alhamisi atanieleza kwanini alinikimbia siku ile pale kilimani wakati tunaenda kuwapeleleza walokole kwenye kanisa lao
ITAENDELEA............!!!

INAENDELEA:
Basi alhamisi ikafika na kama kawaida mimi na mzee Matata tukaendelea na utafiti wetu.Mzee matata akaniambia kijana wangu unajua siku ile pale kilimani sikukimbia,bali kile kilikua kivuli changu tu.Mimi nilikaa nyumbani na kukuacha wewe uende kwenye utafiti hatua ya kwanza.Ulipotoka tu hapa wale watu warefu walikua pembeni yako wanayasoma mawazo yako na wakaamua kukusindikiza ila wewe ulikua huwaoni mpaka pale mmoja wao alipoamua kujionyesha kwako kwa sekunde chache mbele yako.Na mimi nisingeweza kuja kuongozana na wewe sababu mimi ni mganga na mnajimu,vitu ambavyo kwa wale watu warefu ni makufuru.Na huu unajimu sikuutoa kwao bali nilipata hii elimu kwa wapinzani wao.Sasa mimi pamoja na unajimu wangu kuna vitu siwezi kama kusoma mawazo yote ya binadamu"""Elimu yetu ya unajimu na uganga ina kikomo""sababu kumjua tu binadamu ni elimu pana sana na tumefundishwa tu kiduchu na viumbe wasio binadamu wa kawaida ola hilo sio la muhimu sana wewe kujua,wewe shida yako ni kuwadadisi walokole na wale watu warefu ili kuwajua.

Lakini kuwajua wale watu warefu wenye miili ya shaba na wanaoakisi mwanga wa jua ni ngumu zaidi,sababu maarifa yao ni mara trion elfu za maarifa ya unajimu.Historia yao kwa elimu ya kibinadamu ya uganga na unajimu inasema kua hawa watu warefu wanaoakisi mwanga na wenye mabawa kama ya ndege, na wengine hawana mabawa ni jamii moja na wale watu warefu wasioakisi mwanga wa jua ambao hawana mabawa na wanakaa katikati ya dunia kupitia chini ya zuio lolote la maji juu ya dunia,kama bahari au ziwa au mto au maporomoko ya maji.
Walipokua jamii moja miaka trion elfu za nyota kwa hesabu ya kinajimu.

Waligombana na sababu kuu ya kugombana haijulikani ila inaonyesha ilikua ni kugombea madaraka na udhibiti wa anga lote la juu nje ya mfumo kani wa ulimwengu wa sayari.Jamii moja ikaja duniani na jamii nyingine ikabaki angani,na kila jamii ina kiongozi wake mkuu.Tokea hapo hizo jamii mbili hazijawahi kupatana na ile jamii ya angani ina nguvu kubwa kuliko ile jamii ya baharini.Jamii ya angani ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani na jamii ya baharini ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani,namaanisha wafuasi ambao ni binadamu.Hakuna binadamu au jamii yoyote ya wale watu warefu wa baharini ambayo inaweza kuvuka mpaka uliowekwa na mkuu wa wale watu wa angani kuelekea kwenye makao yao ya mwanga wa jua.Nchi yao inaitwa"Mwanga wa jua""sababu hakuna usiku huko ni mchana tu,na kwa hesabu za unajimu huwezi kufika huko ila unaweza kukadiria uwepo wake kupitia wale watu wa angani wakiwa wanakuja na kuondoka duniani kuwatembelea walokole unaotaka kuwadadisi.

Mzee matata akaniambia hakuna kitu kizuri duniani kama udadisi wenye manufaa.Nikamuuliza sasa wewe mzee wangu hizi habari zote umezipataje? Akanijibu kwa kusema na mimi nilikua mdadisi kama wewe ila kwa kupitia uganga na unajimu.Akaniambia kuna vitu hatonieleza sababu mimi sio mnajimu na kuna vitu atanieleza kuhusu udadisi wangu.Hiyo ilikua alhamisi mchana na ilipofika jioni akaniambia nenda kwa jirani zako wale walokole ukae nao na uwaambie wakufundishe kuhusu imani yao na dini yao na jinsi wanavyosali kwa mkuu wao.Wakishakujibu na kukufundisha imani yao basi utakuja hapa alhamisi inayofuatia tuendelee na utafiti wetu taratibu wala hatuna haraka.

Nikaondoka pale nyumbani kwa mzee Matata moja kwa moja mpaka nyumbani,nikapanga jumamosi nitaenda kwa jirani yangu mzee Karugala anifundishe kuhusu dini yake ya kilokole na anijuze zaidi imani yao na utaratibu wao wa maisha na nitamuuliza pia kuhusu wale watu warefu wa angani wanaoakisi mwanga wa jua na kuelea angani kama manyoya ya kuku au ndege.
Kichwani ile picha ya mtu mrefu anayeelea angani kama unyoya haikunitoka na jinsi alivyovaa na uangavu wake na sura yake ya shaba za kumetemeta haikua rahisi kuisahau japo ilikua ni kwa sekunde thelathini tu.Nikajipa moyo nitaendelea na utafiti wangi hata ipite miaka kumi taratibu bila haraka yoyote ile.

Basi jumamosi ikafika nikaenda nyumbani kwa mzee Karugala na nikamkuta,baada ya salaamu nikamueleza yafuatayo.

MIMI:Mzee wangu leo nimekuja kusali nyumbani kwako na unihubirie kidogo
MZEE KARUGALA:Akichekaa"""umekuja mwanangu kunisalimia na kusali pamoja na mimi?

MIMI:Ndio mzee wangu na ninataka unifundishe kuhusu nguvu ya imani yako ya kuokoka na unifundishe kuhusu Yesu na roho mtakatifu.Na unifundishe kuomba kama nyinyi walokole mnavyoomba.
MZEE KARUGALA:Inabidi baada ya mafundisho nikuongoze sala ya toba kijana wangu.

MIMI:Sawa mzee wangu
MZEE KARUGALA:Simama tuombe kwanza ulinzi wa roho ya Mungu kabla ya yote maana naamini ni roho wa Mungu wangu kakuleta hapa.
Tuliposimama tu ile mzee anaanza kusali tukiwa tumefumba macho,nikahisi uwepo wa wale watu warefu,kuwaona siwaoni ila nahisi wapo pembeni yetu kama wananigusa begani.Mzee karugala akamaliza kuomba huku mimi begani kuna mkono wa moto umenigusa maana nilikua nahisi vidole kabisa ila cha ajabu lile joto haliniunguzi.

Mzee Karugala akaanza mahubiri yake huku mimi simuelewi hata neno moja akili yangu yoote ipo kwenye ule mkono ulionigusa begani.Nilikua nimekaa kwenye kiti sebuleni kwa mzee Karugala na pembeni yake alikuja kukaa mkewe na binti zao wawili kuendelea na ile ibada.Mzee ananihubiria ila mimi nachokumbuka ni maneno ya ""Ameen""tu basi.Akili yote ipo kwenye ule mkono ulionishika kirafiki begani.

Nikahesabu kimoyomoyo mpaka tatu,afu nikageuka ghafla nimuone yule mtu alienishika mkono.
Si nikakutana uso kwa uso na yule mtu wa siku ile ila safari hii amesimama pembeni yangu kwa nyuma huku akitabasamu kunielekea na sura yake ile ile ya rangi ya shaba,nikajikuta naropoka"""Wewe tena"".Kumbe ile sauti yangu hakuna aliyeisikia wao wanaendelea tu na ibada kiongozi akiwa mzee wa familia Karugala na hawaoni kama nimegeuka bali wanaona nimetulia nawasikiliza""Hayo maelezo walinipa baadae"".

Yule mtu mrefu akaniambia kwa kiswahili ila kwa mtindo wa kuniuliza swali""UNATUPENDA KAMA TUNAVYOKUPENDA??? akacheka na kupotea tena.Yote hayo yalifanyika ndani ya sekunde ishirini hivi pale kwa mzee wangu Karugala.Basi tukaendelea na ibada iliyotuchukua masaa mawili na alipomaliza maombi ya kufunga ibada akaniambia nipige magoti anisalie toba.Ile napiga magoti ule mkono ukanishika tena begani ila safari hii sikufumbua macho nikatulia tuli.Mzee Karugala akasali maneno yake akaniambia nimfuatishe kusema na alipomaliza akaniambia nisimame.Ule mkono ukaacha kunishika bega pia niliposimama.Nikala chakula cha jioni pale kwa Mzee wangu Karugala afu nikaaga kurudi nyumbani na baiskeli yangu.

Sikumwambia chochote mzee Karugala wala Babu Matata nikagonja mpaka alhamisi tukiendelea na utafiti wetu ndio nitamwambia tukio lile.
Lakini cha ajabu sikua na uoga bali moyo wa udadisi ndio ukaongezeka na nikaamua mengine nitakua simuambii Mzee Matata bali nitakua nayaweka moyoni ili yanisaidie kwenye utafiti wangu wa viumbe wale warefu wasiokua wa kawaida ila ni marafiki wa walokole.Nikarudi nyumbani kuendelea na maisha mengine nikisubiria Alhamisi inayokuja niendelee na utafiti wangu wa kiudadisi na kisomi kuhusu walokole nikiwa na Mzee Matata mganga bingwa na mnajimu wa nyota na mambo ya Anga.
ITAENDELEA

INAENDELEA...........
Tulikutana na mzee Matata na tukaendelea na utafiti wetu kuhusu walokole,ila sikumuambia kuhusu yule mtu mrefu aliyenishika bega na kunitamkia yale maneno ya kirafiki.Ila kuna siku moja mzee Matata akaniambia""Kijana wangu wale watu warefu walikugusa"""nikamwambia ndio.Akaniambia mbona hukuniambia? Basi nikamuelezea tukio lile la siku ile pale nyumbani kwa mzee Karugala nilipoenda kufanya ibada.Akaniambia wale watu warefu wamekuachia alama kwenye bega lako haifutiki,lakini nikamwambia ni kitendo cha sekunde ishirini tu yote hayo yalitokea Akajibu akasema wale watu warefu wameshakuweka alama yao ila hakuna madhara.

Bas tukaendelea na utafiti wetu kwa kutumia elimu ya unajimu kuwadadisi hao watu warefu na walokole.Akanipa mtihani nisome kitabu cha sala cha walokole kinaitwa biblia na humo ndani akaniambia nisome kitabu kinaitwa isaya na kitabu kinaitwa ufunuo.Pia nisome kitabu cha kinajimu kinaitwa Al azif na nisome humo ndani sura inaitwa miliki ya anga, nikimaliza tutaendelea na utafiti wetu wa kinajimu.Basi ilikua kila jioni tunakaa na kuanza kusoma kitabu kimoja baada ya kingine na tunaunganisha doti kwenye utafiti wetu.Kuna kitu mzee wangu alinionyesha,ilikua ikifika ijumaa usiku walokole wengi wanakua kwenye mikesha na wakiwa wanasali anga inafunguka unaona wale watu warefu wanashuka kuwaendea.Mimi nakua nimekaa mkekani nje uwani kaniacha pale mzee wangu nashangaa maajabu ya anga na viumbe vyake namaanisha wale watu warefu.

Ikifika asubuhi tunaingia darasani kuwachambua ni akina nani na asili yao ni wapi na ni kwanini wana mahusiano ya moja kwa moja na walokole..Vile vitabu ndio vilikua muongozo,maana mzee alisema ukitaka kuwajua walokole na hawa watu warefu wa angani basi tumia vitabu vyao

UTAFITI WETU UKAIBUA MAMBO 3
MOSI: Ikatuonyesha katika vitabu vya walokole hasa kitabu cha isaya kuna ibara imetaja kwa upana zaidi kuhusu hizi jamii mbili za watu warefu (Wale wa kutokea angani na wale wa kutokea baharini) na ikazungumzia vita yao ya miaka trion elfu kugombea anga.Pili kitabu cha Al azif kuna sura inasema wale watu warefu wa baharini ni ndugu na wale watu warefu wa angani ila walifanyiana fitina wakatawanyika na kuja duniani kabla ya binadamu kuanzisha makazi.Tukapata jibu kua wale watu warefu wote wa angani na baharini wametokana na mionzi ya nguvu kani za jua kuu nje ya ulimwengu wa nyota kwenye ule mduara wenye uhai wa moto ndani ya pumzi za moto zenye uhai zinazowazunguka walokole.
PILI:Kupitia hivi vitabu tukagundua kua hawa walokole wana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu warefu wa angani sababu wanazungumza lugha moja yenye herufi zisizotamkika kibinadamu ila wao walokole wakiwa wanasali ni kama wanazungumza na wale watu warefu.Na hii ndio maana inaleta uhusiano wa moja kwa moja kati yao.

TATU:Jinsi tunavyowachunguza ndio kama tunajikuta tunavutiwa nao ili tuwachunguze zaidi kwa namna yoyote ile.Tujue je wanakula,je wana familia,je wanakufa,je wanazaliwa?????
Kitabu cha Al azif kinawataja kama wana wa angani na kitabu cha biblia kinawataja kama wana wa Mungu(Mungu wa walokole).

Nikamuuliza mzee Matata mbona nikiwa nawatazama mkekani anakimbia????Yeye akanijibu kua ananipa mda mzuri wa kutulia na kutafakari peke yangu.Bas tuliendelea na utafiti wetu na lengo likiwa baada ya kuwasoma kwenye vitabu basi twende kwenye makazi yao kuwapeleleza mimi na mnajimu mzee Matata.Lakini sasa ili kuwafikia inabidi tujenge urafiki nao namaanisha tuwe walokole au tuwavizie wakiwa wanatoka kwa walokole tuwafuatie kwa nyuma nyuma.Nilipotoa hayo mawazo mzee matata akachekaaa akasema wao ukisema uwafuatie kwa nyuma hutowapata wanatembea kwa kasi ya zaidi ya umeme utapotea angani ila kujenga urafiki nao unaweza ukiwa mlokole.

Bas tukaendelea na udadisi wetu huku vitu vipya vya kustaabisha na kushangaza vinatokea kila siku.Unaweza kuuliza nilipataje uwezo wa kuwaona hao watu warefu,nitaelezea hapo mbele
ITAENDELEA.

INAENDELEA............
Sasa Mzee Matata akaja na mbinu zake za kinajimu za kunifundisha jinsi ya kukariri majira ya anga kama wanavyofanya wale watu warefu kuweza kupaa.Akaendelea na somo lake kua kinachowapaisha sio mabawa au mazingaombwe bali kusoma na kuelewa na kukariri majira ya anga.Lengo letu ni kupeleleza na kupata majibu ya udadisi wangu,sasa ikabidi tuanze kujifunza mbinu mpya nje ya ulimwengu na cha kwanza kabisa kujifunza kupaa.
Siku hiyo mchana kweupe mwalimu na mkufunzi wangu mzee matata akanichukua mpaka barabarani ambayo watu wanapita kama kawaida.Akanipa kombe nikanywa na yeye akanywa afu akasema hapa sasa hatuonekani.Akakaa chini aanze kutoa vifaa kazi anifunze kupaa kwa hesabu za kinajimu,mara tukasikia sauti""Hivi nyie mna akili kweli""alafu kikafuatia kicheko.Yaani mnaloga mpaka kwenye kikao chetu wajinga nyie.Eeeh kuangalia kumbe lile eneo ni eneo la kikao cha wazee wa jadi,nao walikua na mambo yao mchana ule.Mzee matata akageuka ndipo nikaona wazee kumi na saba wakiwa wamevaa lubega zao za kahawia na nyeusi walikua eneo lile wanazindika mambo yao.Wakahoji nyinyi wakurungwa mnafanya nini hapo?????,Mzee matata akawasalimia kwa heshima na kusema nipo na kijana wangu tunapata darasa la elimu anga.Wakamuuliza nani kawapa ruhusa na yeye mzee matata kabla hajawajibu nikasikia kishindo""Puu"na wale wazee kila mtu mbio barabara nzima ikabaki nyeupeee🤣🤣.

Nikabaki mimi na mzee matata nae kakimbia🤣🤣.Kumbe bhana alikua anapita mlokole barabarani mda ule yupo na mtu mrefu pembeni yake,sababu pale palikua ni barabarani afu mchana tu watu wanapita.Bas bwana wale wazee wa vilinge wakatimua kona kidogo nibaki kucheka.Mm nipo pale nashangaa shangaa mara mzee matata huyo katokea na kuniambia""Kijana wangu wale wazee wa tambiko wasingetuingilia tungekua hewani mda huu"""Nikamuuliza kwanini walikimbia,akanijibu kua walikua wanamkimbia yule mlokole na kampani yake ya mtu mrefu.Akasema zoezi limeshaingia gundu tuhairishe mpaka siku nyingine.

Mda ukasogea na utafiti wetu ukaendelea ila suala kujaribu kupaa halikufanyika tena.Kuna kipindi nilikua mkoa wa pwani nikakutana na mzee mmoja na yeye pia ni mnajimu nikamdokeza dokeza ila sio moja kwa moja issues hizi naye akanielezea mengi nitafunguka huko mbele.
Bas mzee matata akaniambia unajua kufanya utafiti wako kwa vitendo ni hatari zaidi sababu unaingilia himaya za watu,,kwanini usichague upande mmoja?

Maaana duniani kuna himaya mbili kubwa.Haya maoni ya mzee Matata ndio kama yakanifungulia udadisi zaidi.Kwanini wale wazeee walimkimbia mtu mrefu na kwanini mzee matata anamkimbia pia mtu mrefu.Maswali juu ya maswali nikapambana niyatafutie ufumbuzi. Unajua haya mambo ya udadisi wa mazingaombwe yapo hivi,jinsi unavyojua zaidi ndio jinsi unavyokua na hamu ya kujua zaidi ya pale ulipokomea.
NITAENDELEA

NAENDELEA....!!!
Duniani ukipatizama kwa ulimwengu wa kinajimu unaona dunia mbili.Kuna dunia inayoonekana na dunia isiyoonekana.Kwenye dunia inayoonekana kila Mtu anaijua ila kwenye dunia isiyoonekana ni wachache wanaijua.
Mzee matata aliponiambia nichague himaya,basi nikaanza kumdadisi yeye yupo himaya ipi na akaniambia yafuatayo

MAMBO MATATU MAKUU
MOJA: Kuna mkuu wa ulimwengu akimaanisha mfumo wote wa sayari zinazojulikana na zisizojulikana.Na kuna mkuu wa wakuu nje ya mfumo wa ulimwengu.Mpaka sasa wanajimu wameshindwa kumchambua mkuu wa wakuu sababu yupo mbali ya mfumo huu wa nyota.Na himaya zipo mbili za mkuu wa mfumo wa ulimwengu na mkuu wa wakuu.Akasema wale watu warefu wanapoenda nje ya mfumo wa sayari za ulimwengu waga wanaenda kuripoti kwa huyo mkuu wa wakuu.
MBILI:Binadamu kiasili wamefanana kiumbo na aliyewatengeneza kuanzia sura na mpangilio wa mwili kasoro tu vimo na akili.Lakini binadamu ni zao la mawazo ya kiumbe mwenye nguvu na akili kuliko binadamu,hivyo basi binadamu hawakutokea kwa bahati mbaya.Ndio maana wale watu warefu wana muonekano kama binadamu kwa asilimia 90%.Sasa aliyewatengeneza either ni mkuu wa ulimwengu au mkuu wa wakuu nje ya mfumo wa ulimwengu.

TATU:Kuna ukweli na uongo na kuna uzuri na ubaya na kuna kujua na kutokujua na kuna kupatia na kukosea.Yote haya yanaheshimika sana katika unajimu.

Mzee matata akaniambia kama wewe shida yako ni kuwajua wale watu warefu basi nakushauri ujiunge na himaya yao.Unadhani kwanini mimi nawakimbia??? Jibu ni jepesi sipo katika himaya yao na hawanitambui ndio maana hawaji kwangu.Wewe unataka kuwajua ila ili uwajue zaidi lazima ujiunge katika himaya yao.Na ukijiunga katika himaya yao basi ujue watakua hawaonekani bali utaishi kwa imani""Wale walokole wanaishi kwa imani"""na sisi wanajimu tunaishi kwa kuona.Hiyo ndiyo tofauti yetu kwenye ulimwengu usioonekana kwa macho ya kawaida.

Akaendelea kusema himaya ya wale watu warefu wa anga za mbali ina nguvu sana kuliko himaya za watu warefu wa baharini au kwenye sayari ya Pluto,Jupter na Uranus.Hata vitabu nilivyokupa uvisome kuhusu wale watu warefu kila kitabu kina nguvu yake.Kitabu cha walokole kina nguvu na kitabu cha wanajimu kina nguvu.Lakini usiniulize swali lolote kwa sasa wewe endelea na utafiti wako na mimi nitakua nakusaidia pale unapokwama kimawazo na kielimu,na suala la kukufundisha kupaa lifute maana wazee wamenikatalia hivyo hakuna tena hicho kipengele tujifunze mengine.Akaniambia tujifunze mambi yafuatayo hapa chini
MOSI:Walokole ni akina nani kiroho
PILI:Wachawi ni akina nani kiroho
TATU:Wanajimu na waganga ni watu gani kiroho

NNE:Wale watu warefu na jamii zote mbili ni viumbe gani kiroho
TANO:Hii tunaita dini ni nini kiroho
SITA:Mungu ni nini kiroho na nguvu ya imani ni nini kiroho
SABA:Kifo ni nini kiroho
NANE:Siasa na utawala wa binadamu ni nini kiroho
TISA:Elimu ni nini kiroho
KUMI:Nini hitimisho la haya yoote.
Basi mzee wangu Matata akasema tutajifunza moja baada ya lingine
NB :Nilijua dunia hii ipo tofauti na wengi mnavyoiona kwa nje.Asilimia tisini ya vitu vinavyoonekana havipo kama vinavyoonekana kwa nje.Na katika ulimwengu wa roho binadamu wote ni sawa hakuna mbantu au mchina au mhindi au mzungu au mwarabu na nk.....!!!Wote ni sawa
NITAENDELEA

INAENDELEA...........!!!!!
WALOKOLE : Watu wanawaita binadamu wenzao wa madhehebu ya kipentekoste kua walokole sababu wanasali kwa kukulia.Lakini katika ulimwengu wa kiroho walokole ni watu wa viduara vya miale ya moto vichwani mwao.Ni watu wabaya na waharibu mipango ya wanajimu,watu wa ngome za vimbunga vya moto na washirika wao ni watu warefu wa moto na kelele zao(Maombi) ni moto.Kuimba kwao ni moto na wanaripoti moja kwa moja kwa mkuu wao ambae ni moto mkuu nje ya mfumo wa sayari ya dunia.Lakini kwa muonekano wa kibinadamu ni wanyonge na kipato cha wastani au kusema ni watu wa maisha ya kawaida kwa asilimia kubwa sababu hawajishughulishi 100%na ubinadamu ,wapo kiroho zaidi.Wakiamka wanasali,wakitembea wanasali,wakilala wanasali,wakifanya kazi zao wanasali na ni watu wa ajabu sana kwenye ulimwengu wa kiroho.Kinachowatofautisha na binadamu wengine ni kwamba wao kimoyomoyo wanamshukuru Mungu wao hata kwenye shida.Basi wanapomshukuru Mungu wao hasa nyakati za shida bila kunungunika katika ulimwengu wa roho wanakua kama binadamu wenye ngozi za moto, wanazungukwa na wale watu warefu wenye panga za moto.

Lakini hatari zaidi ni pale wanapomlilia mungu wao aliye kule nje ya mfumo wa ulimwengu na sayarï (Vilio vyao ni kama radu za umeme zinapaa kumwendea mungu wao) .Wale watu warefu wanashuka kwa wingi na kuwazunguka na kuwalinda dhidi ya wabaya wao na wale watu warefu wa jamii ya baharinii.Kiroho walokole wanaitwa ""Wana wa mwangaza""sababu ya vile viduara vya moto vichwani mwao.
Mzee Matata akaniambia katika ulimwengu wa roho basi hao walokole hawashikiki.

WACHAWI :Binadamu hawa wanaoitwa wachawi kiroho wanaitwa""Wasumbufu""ni watu wanaopenda kusumbua wenzao kwa kila hali.Wanaroga na kuharibu nyota za watu,wanajihusisha na elimu ya giza na hawamtambui mkuu wa walokole sababu ameulaani uchawi.Kwa muonekano wa nje wachawi ni binadamu kama binadamu wengine na wana vipato vya ngazi zote,kuanzia umasikini mpaka utajiri.Kwenye ulimwengu wa kiroho ni washirika wa ile jamii ya watu warefu wanaotoka baharini.Na wakitembea basi wanatembea na wale watu warefu wa kutoka baharini.Kwenye ulimwengu wa kiroho hawana mwanga wa kuakisi jua,na hawana nguvu kama walokole sababu wamejaa damu za watu.Wao huua ili wapate nguvu na wana mengi mabaya kwa muonekano wa kibinadamu.Pia waoga sana wanapowaona walokole au wale watu warefu wa kuakisi mwanga wa jua.Wana mkuu wao na mungu wao tofauti kabisa na mungu wa walokole.Wao wana moto ila sio mkali kama moto wa walokole maana walokole wakianza kusali tu basi ule moto wao unazima.

Na ndio maana hwapatani kabisa na walokole katika ulimwengu wa kiroho.Wana nguvu ila sio kama za walokole,sababu nguvu za wachawi sio za asili bali makafara lakini walokole nguvu zao ni za asili tena ya moto.Hapo kwa kidogo tu nimechambua jamii hizi mbili katika ulimwengu wa kiroho
NITAENDELEA

NINAENDELEA.......!!!!
WANAJIMU NA WAGANGA :Wanajimu na waganga hawana usharika na walokole katika lolote lile.Wao ni washirika wa wale watu warefu wa baharini.Unajimu haufundishwi kwenye mikusanyiko ya kilokole sababu una makufuru na hatua zake nyingi zina ushirikiano na uganga.Wanajimu wanachukua nyota za wangu na kuzitumia kwa manufaa yao.Wanajimu wanafanya tafukuri ambayo ni laana kiroho.Wanajimu hawana utii kwa mkuu wa mamlaka aliye mkuu wa wote,bali wao wanatii uganga wako na miungu ya kwenye sayari za ndani ya mfumo ww jua wa ulimwengu.

Wanajimu wanashirikiana na wale viumbe wa baharini kumuhujumu mwanadamu aliepo duniani.Wanajimu wanatafuta elimu ya anga kwa njia za uchawi wa kale wa kiarabu na kiajemi.Wanajimu hawana maombi ya kubariki bali wana maombi ya kulaani,kwani kwao laana ni sehemu ya matambiko yao.Hivyo wanajimu ndani ya ulimwengu wa kiroho sio watu wema.

WALE VIUMBE WAREFU :Kama nilivyosema pale mwanzo kua,kuna aina mbili za wale viumbe warefu
MOJA :Watu warefu wa angani wanaoakisi mwanga
MBILI :Watu warefu wa baharini wasioakisi mwanga.
WATU WAREFU WA ANGANI WANAOAKISI MWANGA :Wale watu warefu wazuri kwa muonekano,wanaoshika panga na kulinda walokole ni watu wa ajabu sababu ya tabasamu zao na upendo wao.Akikusogelea kwa karibu utatamani ulie kwa furaha maana unapata amani ya moyo iliyopitiliza.Wana upendo mkuu sababu ukiona jinsi wanavyowahudumia walokole lazima upendezwe nao.Walokole ni kama vitoto vidogo mbele ya hawa walinzi wao ""Watu warefu""..Upenda na ulinzi ndio sifa yao kuu.Wao ni moto ndani ya moto wa shaba,wana nguvu kama umeme wa radi.Kimuonekano wengine wana mabawa na wengine hawana mabawa ila wote warefu kwa vimo.

WATU WAREFU WA BAHARINI WASIOAKISI MWANGA :Hawa ni washirika wa waganga na wanajimu na wachawi.Kimuonekano ni watu wa kubadilika badilika.Hawana muonekano mzuri wa kudumu bali wanachukua sura halisi za binadamu,hasa binadamu wa bara hindi na uajemi.Hawana usharika na walokole sababu walokole wanaharibu kazi zao wanazofanya na wanajimu na wachawi.Hawana upendo wala amani ya moyo wakikusogelea,zaidi zaidi utasisimka na kuogopa.Ni washirika wa mkuu wa ulimwengu mwenye vita vya kudumu na walokole.Tusiwazungumzie sana hapa maana lengo sio kuwazungumzia wao bali Mungu wa walokole.

Kwa binadamu wa kawaida unakua na amani ukikutana na hawa watu warefu wa angani ambao ni walinzi wa walokole,maana wanalinda watoto,wanalinda wagonjwa,wanalinda walokole na wasiokua walokole na wanazuia majanga ya kutengenezwa na wale watu warefu wa baharini na washirika wao ambao ni wachawi na wanajimu na waganga na washirikina wa kibinadamu.Popote pale duniani kwenye ulimwengu wa kiroho utawaona wanaruka huko na huko.
Afu mungu wa walokole ambae ni mkuu wa mfumo wa anga kuu nje ya mfumo wa sayari za ulimwengu kaficha siri ya mfumo wa ulimwengu nje ya mfumo wa anga na sayari zote,,maana angani ni kama mfumo wa anga na sayari unaelea ila huwezi jua umejishikiza wapi.

Hesabu za kinajimu zina kikomo ila hesabu za unajimu wa nje ya mfumo wa ulimwengu hazina kikomo na zinaongozwa na mwana wa mmliki.Na ndio maaana huyo mwana wa mmliki na wale watu warefu weupe wanaishi milele toka dahari ya kwanza mpaka dahari isiyo na ukomo kwa kingereza wanaita""Eternity's""".
Walokole wanaposali ndio mda mzuri wa kua nao sababu mungu wao anashuka kwa njia kuu tatu(3)
MOJA :Kama njiwa mweupe wa dhahabu

MBILI :Kama moto wa mataji ya viduara na kukaa vichwani mwa walokole

TATU :Kama wingu za moto unafunika eneo zima.
Sasa kama walokole wakiwa wanasali na wewe upo karibu basi baraka zao kiroho zinakufikia mpaka wewe.Mungu wa walokole hana ubaguzi katika kutoa baraka kwa binadamu,ni kama anatusubiri tumjue atubariki.Lakini pamoja na upole wake,huyu mungu wa walokole ana mzaha pale unapotaka kudhuru walokole wake na haoni hasara kukuua kwa pumzi yake ya moto.Anawapenda walokole wake kuliko kitu kingine chochote.
NITAENDELEA..... ....!!!!



NINAENDELEA......!!!
Mungu wa walokole ambae ndio mkuu wao anawajua watu au washirika wake kiroho na kimwili.Kiroho kila pumzi wanayotoa walokole ni uhai na wanaongozwa na utulivu wa akili na mioyo mnaita(Upendo)......!!!!
Walokole wanaposali basi mambo haya hutokea wakiyatamka.
NAFUNGA:Basi kunatokea vizuizi vya kingo za moto na wanafunga njia.
NAKEMEA:Basi kunatokea radi za moto na kuelekea kule kuliko kemewa.
NABARIKI:Basi kunatokea wingu jeupe linafunika kulikobarikiwa.
KWA JINA LA""YESU"": Hapa tusikilizane kidogo maaana ndipo penye kiini cha walokole wenyewe.Huyo yesu ni nani na kwanini walokole wanapomtaja ni kama kunatokea mtetemo wa aridhi na anga katika ulimwengu wa kiroho.Huyo yesu ni mlinzi mkuu wa walokole ambae jina lake halitajwi hovyo na walokole mpaka wawe kwenye matatizo.Ni kamanda wa wale watu warefu na anaakisi mwanga mara trioni kuliko mwanga wa jua.Ulimwengu wa kinajimu ndio yule wanamuita mwana wa mmliki au nyota ya mashariki au Issa.Hawawezi kutamka jina lake sababu halipo katika herufi za kibinadamu kiroho,ila linasomeka kwa kilatini kama""Alfa na Omega""maana yake mmliki wa wamiliki asiye na mwisho.
SIFA ZA HUYU YESU WA WALOKOLE
MOJA: Anao usharika na wale watu warefu ambao wana usharika na walokole.Yeye ndio kamanda wao
MBILI: Yeye na mungu wa walokole ni kitu kimoja na katika ulimwengu wa kinajimu waga hawatenganishwi.
TATU: Ni mkuu wa dini na imani ya walokole na ndie anaewalinda dhidi ya wanajimu na wachawi na washirika wao wa baharini.
Ninamzungumzia huyu yesu sababu walokole wana mihuri ya jina lake usoni mwao.Na jina lake ndio mwongozo wao,wakilitamka tu ulimwengu wote wa kiroho unatikisika.
NNE: Huyu yesu wa walokole ndie aliewafukuza wale watu warefu wa baharini kutoka angani za nje ya mfumo wa jua baada ya wao kupingana nae baadhi ya vitu miaka trioni elfu iliyopita.Wanajimu wanasema kua kimondo kilichoanguka duniani miaka bilioni sita hivi iliyopita kua kilikua ni rundo la wale watu warefu waliofukuzwa na huyu yesu wa walokole kutoka anga za mbali.
TANO: Sifa ya tano ya huyu yesu wa walokole ni kua ni marufuku,hapa nasisitiza NI MARUFUKU KWA WANAJIMU NA WAGANGA NA WACHAWI NA WASHIRIKA WAO WA BAHARINI KUMTAJA KWA JINA LAKE HILI LA ""YESU"".Wanaweza kumuita majina yoyote yale ila sio kwa jina hili.Sababu lina upinzani nao kiroho.Na hizi ndio sifa za yesu wa
walokole.....TUENDELEE.........!!!!!!
Kuwaelewa walokole lazima kwanza uelewe muonekano wao kiroho upoje,ngoja nifafanue kidogo.
Walokole sio watu dhaifu kiroho kama watu wanavyodhani.Utasemaje watu dhaifu wakati wakiwa njiani kiroho wanaongoza vikundi vikundi vya walinzi wa kiungu.Utasemaje watu mafukara wakati kiroho zile taji zao ni za madini ya Lulu.Utasemaje hawana akili wakati kwenye ulimwengu wa kiroho sayansi yao imeshindikana kuigwa.Tofauti yao na binadamu wa kawaida ni kwamba wao walokole wamekaa sana kiroho kuliko kimwili.

Wale watu warefu wanatembea na walokole popote pale iwe barabarani au kwenye daladala au bafuni au chooni au kitandani au shambani au ofisini au kwenye mikusanyiko ya ibada na ni kama mapacha wa wa wale watu warefu wenye kushika panga za moto kuwalinda.Mungu wa walokole kawapa upendeleo wa ajabu walokole.Ukiwachunguza kinajimu unajikuta unaanza kuvutiwa nao.Mzee matata aliniambia ukiendelea kuwadadisi basi ipo siku na wewe utakua mlokole na utajikuta unakua kama wao kiroho.Basi nikamuuliza mzee matata wewe upo upande upi kiroho????? Akanijibu na kusema,"""Mjukuu wangu endelea na utafiti wako usinihoji""...Kuna vitu nikawa najiuliza na nikapanga nikawaulize walokole wa kanisani mambo yafuatayo:

MOJA: Je wanajua wanalindwa na watu warefu?????
MBILI: Je wanajua nguvu za hilo jina la""Yesu""????
TATU: Je wanajua kua wao ndio wanaongoza kwa sayansi ya kiroho kuliko makundi mengine????
NNE: Je wanawajua wapinzani wao kwenye ulimwengu wa kiroho??????
TANO: Je wanajua kua wao kiroho ni kama watu wa ulimwengu mwingine na sio dunia hii ya kimwili toka siku walipoamua kua walokole na kuamua kufanya usharika na mkuu wa wakuu na mwanae aitwae""Nyota ya mashariki au Mwana wa mmliki????
SITA: Je wanajua kua yale matunda yao ya rohoni waga yanaonekana mwilini mwao kiroho wakitembea?????
SABA: Je wanajua miili yao ni kama mahekalu ya moto na ni makazi ya wale watu warefu mda wote???!!!
NANE: Je wanajua kua wakiwa na huzuni na Yesu wao anahuzunika pia na wakiwa na furaha na Yesu wao anafurahi pia na wakiomba anaomba nao na wakiimba anaimba nao
TISA: Je wanajua wao ndio muhimili wa dunia dhidi ya mashambulizi ya wale watu wa baharini na wachawi na waganga na wanajimu??????
KUMI: Je wanajua maana halisi ya neno ulokole ni mnyambuliko wa maneno mawili ya kiroho ambayo ni UPENDO USIO NA MIPAKA NA UTAKATIFU ULIOKAMILIKA?


Maswali yote hayo nikapanga nitayatafutia majibu ya kiudadisi zaidi ili nijiridhishe na utafiti wangu kuhusu nguvu za mungu wa walokole...
NITAENDELEA.....


NINAENDELEA..............!!!!!!!
Mzee matata pmoja na unajimu wake wote na utaalamu wake wa uganga hakatizi wanapokuwepo walokole na anawaogopa.Wanajimu ni wachawi waliojificha na wana usharika na viumbe wa baharini.Jiulize vitu vichache tu kuhusu wanajimu
MOSI: Mbona wana usiri sana katika mambo yao na ufundishaji wa hii fani kuna sehemu maalummaalumuu katika hii pande ya dunia wanaenda.
PILI: Ukitazama vitabu vyao vya kujifunzia kama Al Azif na vyenginevyo vimejaa mafunzo ya kufuru na waandishi wake wa hivi vitabu ni jamii ya watu warefu wa baharini wanaitwa""WANEFILI""hawa nao jamii ya wale watu warefu wa angani ambao wakifukuzwa kutoka anga za mbali na mkuu wa wakuu.Vitabu vyote vya unajimu vinamtukuza AZAZELI"""na ndio muasisi wa taaluma hiyo kwa wanadamu na lengo likiwa ni wamsaidie katika kazi zake za makufuru.Kwahiyo hiyo ni ishara tosha kua wanajimu wamefundishwa na BABA WA UCHAWI ""AZAZELI""
Mzee Matata anasema mtu yoyote yule anaejihusisha na wanajimu ni mshirikina pia.

Basi mzee matata akaniambia unajua watu wengi wana uelewa mdogo kuhusu mungu wa walokole,lakini ukiwafuatilia walokole basi utamjua mungu wao.Akasema kua ukiwafuatilia wale watu warefu wanaoakisi mwanga kwenye makazi yao kuna anga zaidi ya saba na kila anga kuivuka ni miaka ya kuakisi mwanga trioni na trioni.Hakuna aliyewahi kufika huko mpaka wao wenyewe watu warefu wampeleke huko.Huko wana mji mkubwa na wana utawala mkuu ambao unaongozwa na yule mwana wa mmliki mlinzi wa walokole.

Akasema wao wanajimu wameyajua hayo sababu wana uwezo wa kuelewa ulimwengu wa siri.
Nikamuuliza kwanini sasa na yeye asijiunge na walokole afaidi hayo mambo.Akasema pale tu binadamu anapokua mlokole haya mambo hayaoni bali anaishi kwa imani na imani ndio kipimo cha ulokole wao,labda mungu hawaruhusu waone mambo yanayowazunguka kiroho.Lakini mtu anapokua mchawi haitaji vipimo vya imani ili kuona ulimwengu wa kiroho,hivyo yeye inamuwia ngumu kua mlokole sababu ya hayo na pili ameshakula viapo vya kua mnajimu.

Ukishakula viapo vya kua mnajimu inakua vigumu kutoka nje,ila akasema anauhusudu sana uwezo wa walokole nje ya mwili yaani kiroho.Akasema waganga na wanajimu wanaishi kwa masharti na utaratibu ambao wakiugeuka wanapata adhabu ila walokole wanaishi kwa imani tu na sio lazima waone,bali imani tu na wakigeuka wanapata nafsi ya pili (TOBA) maana mungu wao ni muanzilishi wa tendo hilo la toba katika ulimwengu wa roho.Akasena watu wengi wanashindwa kua walokole sababu ya imani haba na wanataka kila kitu mpaka waone ndio wasadiki.
Akasema mpaka leo hii kuna walokole ukiwaambia kua wanalindwa na watu warefu hawatokuamini ila mpaka waone kwa macho yao ndio wataamini,wakati ulokole haupo hivyo.Imani hata katika mambo yasiyoonekana na yanayoonekana ndio msingi wa ujenzi wa imani ya kilokole kiroho.

NITAENDELEA............!!!!!!!
 
FB_IMG_1689244373343.jpg
 
Mkuu Hebu angusha data hapa, hopefully Ilikuwa ni quantitative follow up study, miaka 22 sio mchezo naamini una database ya kutosha kuprove hypothesis yako! Sisi kama third parties tunapenda kujua facts na quantity zake tujiridhishe na research yako, karibu sana boss…
 
Chanzo,

Ukiangalia bandiko hili na la Uyu hapa nikama linashabiana
 
Duniani hakuna Mungu wawalokole jamaa Mungu ni wawote sema hujaamini ukamwita mwite na wewe atakusikia

Mungu anawalio wake humuhumu duniani ,Hilo ni fungu lake,

Linalobski ni fungu la shetani.

Sasa walio WA Mungu
Hao ni wale walio kidhi vigezo vyake.

Kuna viumbe vyake na Kuna walio wake ,ni maneno mawili tofauti.

Mungu kukujibu haimaanishi ni MIONGONI MWA walio wake ,atakujibu kama sehemu tu ya walio viumbe vyake.
 
Tatizo lililopo ni kuwa DELUSION za wanadini zimemuingiza MUUMBA NCHI NA MBINGU katika mifuko ya suruali zao....hakika hii ni KUFURU.....

Elimu ya Mwenyezi Mungu ni kubwa zaidi kuliko aliyowafunulia wanadamu na mitume....

Yaani wanadamu wanaoishi katika sayari 1 tu wazijue SIRI zote za MWENYEZI MUNGU aliyeumba bilions of galaxies?!!!

Hakika huu nao ni UTAAHIRA......

#YetzerHatov
 
Mungu anawalio wake humuhumu duniani ,Hilo ni fungu lake,

Linalobski ni fungu la shetani.

Sasa walio WA Mungu
Hao ni wale walio kidhi vigezo vyake.

Kuna viumbe vyake na Kuna walio wake ,ni maneno mawili tofauti.

Mungu kukujibu haimaanishi ni MIONGONI MWA walio wake ,atakujibu kama sehemu tu ya walio viumbe vyake.
Kumbe hujui kitu eh Mungu hachagui mtu Mungu ni wawote ndio maana mashoga wanaishi ili wamrudie Mungu malaya ,wanafiki, mafisadi, wale waovu wote ili wamrudie Mungu nawajue Mungu ni kwa ajili yao Yesu alikifa kwa ajili yao wabadilike na kumwabudu yeye so nadhani unamenielewa
 
Kumbe hujui kitu eh Mungu hachagui mtu Mungu ni wawote ndio maana mashoga wanaishi ili wamrudie Mungu malaya ,wanafiki, mafisadi, wale waovu wote ili wamrudie Mungu nawajue Mungu ni kwa ajili yao Yesu alikifa kwa ajili yao wabadilike na kumwabudu yeye so nadhani unamenielewa
Ina MAANA mpaka MTU ametubu amefanyika kuwa wake Mungu,

Ni hivi , hukuelewa walio WA Mungu ni watu Gani,

Walio WA Mungu ni wale walio kubari kutubu na kuishi katika njia yake alioichagua ya utakatifu tu.

Hao ndio Walio wake,
 
Ina MAANA mpaka MTU ametubu amefanyika kuwa wake Mungu,

Ni hivi , hukuelewa walio WA Mungu ni watu Gani,

Walio WA Mungu ni wale walio kubari kutubu na kuishi katika njia yake alioichagua ya utakatifu tu.

Hao ndio Walio wake,
Hujanielewa unahitaji nikueleweshe Yesu hakuja kuwakomboa wale wanaomfahamu tu bali alikuja kuokoa dunia yote ili waliobaki ambao bado hawamwamini wamepewa chance yakumuamini Mungu nawanamuda wakumuamini leo kesho na hata mbeleni . Hakuna limit ya watu Mungu alioweka eti hawa ni wangu hapana anytime mtu akihitaji kuwa wake atakuwa wake elewa hivyo aliumbA dunia na inawatu wengi sana . Na wote anajua watakuwa wake tu ni muda wata mwamini
 
Hii sio research mkuu, sema umekaa miaka 22 kutunga stori ya page chache na sasa umeipublish JF, research ina principles zake na hamna hata moja umeonyesha uliyotumia, huna tofauti na mashimo wa Yanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom