Yaliyojiri miaka 10 ya Mkutano wa Uhuru wa Mtandao Barani Afrika, Septemba 29, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989

Mkutano wa Uhuru wa Mtandao wa Afrika mwaka 2023 (Forum for Internet Freedom in Africa 2023 – FIFAfrica23) unaoashiria muongo mmoja wa mkusanyiko mkubwa zaidi kuhusu uhuru wa mtandao barani Afrika, unaendelea leo tarehe 29 Septemba ikiwa ni siku ya mwisho ya mkutano huo.

Tanzania ni Mwenyeji wa Miaka 10 ya Mkutano wa Uhuru wa Mtandao Barani Afrika (ulioandaliwa na taasisi ya CIPESA kutoka Uganda.

FIFAfrica23 unaendelea kufanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro, Jijini Dar es Salaam tangu Septemba 27, 2023.

Soma hapa kufahamu yaliyojiri kwenye miaka 10 ya Mkutano wa Uhuru wa Mtandao Barani Afrika, Septemba 28, 2023

Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa zaidi.

NERIMA WAKO-OJIWA, MKURUGENZI - SIASA PLACE
Serikali zimekuwa zikihamasisha vijana kuchangamkia fursa za kidigitali, lakini kuna changamoto. Ili kuelewa kwa undani zaidi, msimamizi wa maudhui (content moderator) kimsingi ni polisi wa mtandaoni. Wao ndio wanaosimamia kuhakikisha kuwa hauoni maudhui mabaya na yenye madhara.

Ninajua labda mtu amewahi kuona kitu kibaya mtandaoni, labda ajali au mtu akujiua. Baadhi yetu tumeshuhudia maudhui yenye taswira za kutisha. Msimamia maudhui anatazama maudhui haya mara nyingine kwa masaa manane, tisa kwa siku - kila siku. Hii ni kazi yao. Na kazi yao ni kujaribu kufanya uamuzi ndani ya sekunde chaxhe kuamua iwapo maudhui fulani yanaweza kuonekana kwa umma au la.

Tunapaswa kuelewa kwamba Kenya tulikuwa na mamia yao wakifanya kazi, lakini tunapaswa kuelewa jinsi walivyovutwa katika nafasi hizi. Nafasi hizo zilivyotangazwa zililenga watu maskini kutoka jamii maskini na kutangazwa kama "mustakabali bora" na "fursa bora". Hivyo, mtu anadhani amepata kazi ya maisha yake. Labda alidhani ni jukumu la huduma kwa wateja, kufanya kazi na kampuni na kusema bidhaa hii ni nzuri.

Mpaka wakati unapofika, anagundua anafanya kazi na kampuni kubwa ya teknolojia. Anaposaini mkataba wa kazi, anakubaliana na Mkataba wa Kutotangaza (NDA). Hawezi kushirikisha wanafamilia wake anafanya nini au unafanya kazi na kampuni gani. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ndani ya mikataba - unatendewa kama vile hufanyi kazi na kampuni niyo. Na zaidi ya hayo, kampuni nyingi hizi haziko nchini Kenya.

Sasa unafanya kazi kama mgeni katika nchi ambayo hutambuliwi kama raia na kampuni haishughuliki nawe sana, na hapa unakabiliana na maudhui haya na unalipwa kidogo, ikilinganishwa na mtu mwingine anayefanya kazi katika nafasi ile ile, kwa mfano, Ulaya. Tunazungumzia masuala ya kiakili hapa. Huwezi kufikiria majeraha ya kiakili wanayoyapata; hawana upatikanaji wa tiba. Unaelezwa tu kuwa furahi kwamba una fursa - kwamba mbali na kuwa Afrika ni maskini, angalau una mshahara.

Wasimamizi wa maudhui wanatendewa kana kwamba hawapo. Watu wengi hawajui kwamba watu wa namna hii wapo. La kutisha zaidi tunapozungumzia eneo letu (la Afrika) - idadi ya lugha tunazozungumza ni nyingi. Tunazungumza lugha nyingi lakini unakuta mtu mmoja anatafsiri lugha zote. Nilikutana na msimamia maudhui mmoja aliyekuwa akifanya tafsiri kwa ajili ya nchi nzima ya Namibia. Hii inawezekanaje?

Tunapozungumzia wafanyakazi wa kusimamia maudhui, wanahitaji kutambuliwa kama wafanyakazi. Jambo la pili ni kujumuisha ustawi wao katika mikataba yao. Kuna suala la kufikia upatikanaji wa tiba, kwa mfano. Nchini Marekani, wafanyakazi wa kutunza maudhui wanapata hiyo aina ya sapoti. Lakini siyo hivyo barani Afrika. Hii ni aina ya unyonyaji wa kisasa. Sheria zilizopo katika nchi zetu zinapaswa kuwalinda.

INNOCENT TSUMBU, UNI GLOBAL AFRICA
Kama muungano wa kimataifa wa vyama vya wafanyakazi, tunachofanya kukuza majadiliano ya kijamii yenye nguvu kupitia vyama vyetu washirika kutoka ngazi ya chini, ni kuwawezesha vyama vyetu washirika kuanzia ngazi ya kijamii, kuwapa mafunzo ili waweze kuunda mtandao katika ngazi ya kikanda, na tunaiita Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi.

Kupitia mashirika yetu, sasa wanaweza kuandaa makubaliano ya kimataifa... Lakini jambo muhimu zaidi ni kwa wasimamizi wa maudhui au wafanyakazi wa sekta ya teknolojia kutambuliwa kama wafanyakazi. Na kama wenzangu walivyosema, wengi wao ni wafanyakazi wahamiaji na mara nyingine inaweza kuwa ngumu kwao kujiunga na chama cha wafanyakazi katika nchi waliopo, lakini kama muungano wa vyama vya wafanyakazi wa kimataifa tunajua kuna Mkataba wa ILO unaohusiana na wafanyakazi wahamiaji. Tunaweza kutumia huu na pia kutumia Azimio la ILO kuhusu makampuni makubwa ya kimataifa.

Tunajaribu kufanya ndoto ya kuwa na kazi zenye heshima/hadhi kuwa halisi barani Afrika, kwa sababu mnaweza kuona wenyewe, kulingana na uchambuzi uliofanywa na watangulizi wangu, kazi zinazoundwa na makampuni makubwa ya teknolojia, je, ni za heshima au la? Na jibu ni rahisi; kazi hizo si za heshima. Na tunahitaji kurekebisha mambo hayo.

Kuyarekebisha, tunahitaji kuhakikisha uhuru wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi unaheshimiwa Afrika kwa sababu wafanyakazi wa teknolojia nchini Tanzania, Kenya wanafanya majukumu sawa na wenzao nchini Argentina na Colombia, kwa nini tusirekebishe viwango ili wote wawe na mishahara stahiki, ulinzi wa kijamii, na afya na usalama kazini? Iwapo hatutafanya kazi kwa njia hiyo, itakuwa ni kama ubaguzi kati ya wanaofanya kazi katika sekta hiyo.

NERIMA WAKO-OJIWA, MKURUGENZI - SIASA PLACE
Tumeshuhudia mapinduzi ya kijeshi nane, na unapoangalia watu wanaochukua madaraka ni wanaume walio chini ya umri wa miaka 40. Kwa hivyo, unapokuwa na watu wanaoishangilia mapinduzi ya kijeshi, basi tunashangaa. Kwa sababu tumeshuhudia maadhimisho kwenye mitandao ya kijamii.

Na unaposikiliza rais wa zamani wa Gabon akizungumza kuhusu "kelele," ilikuwa ni utani. Na hii ni kitu ambacho tunahitaji kuwa makini nacho. Ni utani kwa sababu vijana wengi wanafurahi kuhusu mabadiliko. Kwa hivyo, hata tunapokaa hapa na kuzungumza kuhusu ushiriki wa vijana - ushiriki wao unahama mtandaoni.

Tunaona kupungua tunapozungumzia idadi ya wapiga kura, lakini tunapoongelea uhusiano unaotokea mtandaoni tunaona kuongezeka hasa linapokuja suala la kujadili masuala ya kidemokrasia. Bado kuna vijana wengi wanaofanya kazi mtandaoni lakini hawana sauti kubwa. Tunahitaji algorithm ambazo zinachochea mabadiliko chanya na sio vinginevyo.

CATHERINE
Nakubaliana na hoja kwamba mtandao ni moja ya zana kubwa zilizowahi kuundwa katika uhuru wa kimataifa wa kutoa maoni na kupata habari. Hivyo, haki ya kutafuta, kupokea, na kutoa habari chini ya mfumo wa sheria bila kujali mipaka. Tupo hapa Tanzania lakini tunaweza kutumia mtandao - kupokea habari na kujieleza bila kujali mipaka.

Kuna waandishi wa habari naweza kuwaona katika chumba hiki. Swali ni: bado wanatumia njia za kimwili kueneza habari au wanachukua fursa ya mtandao kueneza habari?

Kwa mtandao na mitandao ya kijamii, kuna utata. Mataifa mengi hawajui cha kufanya kwa sababu kila mtu anawasiliana mtandaoni. Je, tunaona usimamizi au udhibiti? Hilo ndilo swali kubwa. Je, mataifa yanaweza kusimamia mtandao au tunashuhudia udhibiti zaidi?

Pamoja na ukuaji wa mtandao, tunaona wasimamizi wa kati - majukwaa ya mitandao ya kijamii na majukwaa ya habari. Wako katika nafasi ngumu; Wanafanya nini? Ikiwa ninachapisha makala yangu ya habari, je, nawajibika kwa maoni ya wasomaji wangu? Kwa hivyo, jinsi gani unaweza kupunguza madhara mtandaoni na wakati huo huo kuhakikisha uhuru wa kujieleza haukatwi.

Na kisha swali la jinsi wasimamizi wa kati wanavyodhibiti maudhui mtandaoni. Kwa mfano, je, Facebook inazingatia sheria za kitaifa wakati wa kudhibiti maudhui mtandaoni? Ikiwa ndivyo, je, sheria hizo za kitaifa zinaendana na viwango vya kimataifa vya uhuru wa kujieleza?
 
Back
Top Bottom