UKIKUTANA NA MTU MWENYE KAULI HIZI JUA ANA HISTORIA YA KUTAPELIWA KIMAHUSIANO

Mwanasayansi Kalivubha

Senior Member
Feb 4, 2024
104
271
UKIKUTANA NA MTU MWENYE KAULI HIZI JUA ANA HISTORIA YA KUTAPELIWA KIMAHUSIANO 😔

1.Wanaume/wanawake wote hawafai.
2.Dunia ya sasa hakuna waoaji/waolewaji.
3.Nawachukia sana wanaume/wanawake
4.Hata wewe ni wale wale tu.
5.Siwezi kumuanini tena mwanamke/mwanaume.


KUNA KAZI KUBWA SANA KUISHI NA MTU MWENYE KAULI HIZO 😔

1.Hata uwe mwaminifu 100% bado atakuona sawa na aliyemsaliti.
2.Atakuwa mtu wa kujihami sana maana anakuona hata wewe ndio wale wale
3.Atakuwa mwenye hasira za kulipuka mpaka unashangaa kwa sababu hujamkosea chochote.
4.Atakupa masharti mengi mpaka utaanza kufikiria bora umpoteze tu.


KIPI KIFANYIKE?

Ukitapeliwa kwenye mahusiano jitahidi upone jeraha kwa 100% ndio uingie upya la sivyo utawapa watu wakati mgumu wa kuhusiana na wewe kwa sababu utakuwa mtu wa kujihami sana.

#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako.
 
Anakuwa yupo sahihi
Historia inakawaida ya kujirudia unataka apuuzie apigwe tukio lingine?

Atakuwa ameshajifunza na anajua namana ya kudeal na mtu kwenye mahusiano.

Mimi mwenyewe mwanamke naishi naye kimkakati zaidi.
 
Back
Top Bottom