Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,605
Angalizo kwa Wanabodi na Mode

Bandiko hili ni C&P kutoka kwa mwana JF fulani.
Kwasababu mwandishi ni member wetu humu na humu hajaileta, naomba ikitokea ameileta humu, then futa hili bandiko langu.

Nime C&P kwasababu mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kuandika humu kuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 could be Dr. Hussein Mwinyi, kupitia bandiko hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Wanabodi

Lakini kama ataisikia hii sauti, sio vibaya kama atajiandaa na kumuandaa mtu wa kumpokea, kwa maoni yangu, Dr. Hussein Mwinyi atatufaa sana, hivyo namuomba Rais Samia akiisikia sauti, amuombe Dr. Hussein Mwinyi, kwa uchaguzi wa urais wa 2025 aje kugombea urais wa JMT, kuimalizia awamu ya pili ya Mama Samia kwa yeye kukubali kuwa rais wa JMT kwa awamu moja tuu.

Na kipindi hicho cha 2025- 2030 ndipo sasa sasa tufanye grooming ya Mwanamke atakaye kuja kugombea urais wa JMT kwa 2030, na kwa maoni yangu, Mwanamke huyu sii mwingine yeyote zaidi ya Dr. Tulia Akson Mwansasu, Spika wa sasa wa Bunge la JMT.

kama hii sauti ni yake YEYE kweli, then inamaanisha kwa uchaguzi wa 2025, Tanzania tuna mgombea mmoja tuu Mwanamke, yaani the one and only ambaye ama anatakiwa na YEYE apumzike ampishe mgombea mwanaume, ama ...

Unaweza kuta aliyepangiwa na YEYE kuwa rais wetu 2025 ni Mama Samia mwenyew, baada ya kuingia by default kuwa rais wa JMT kwa awamu hii ya kwanza, sasa anajipanga kuendelea awamu ya pili, properly kwa kuchaguliwa na jura za Watanzania, ila kugombea kwake ni kupitia ule mserereko wa CCM , huku Dr. Mwinyi akiji set for his second term in Zanzibar kwa mserereko wa CCM na wala hajui kuwa kuna sauti inamtaka yeye ndiye aje awe rais wa JMT, 2025!, hivyo maono kama haya, yanasaidia sana kuwaandaa watu kisaikolojia!.

Hili la Mwinyi kuja huku, sio la sauti, hili ni langu tuu, maana usikute pia ni mpango ya YEYE, kumfanya huyu jamaa Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii maana
wakati nikiandika hayo, Dr. Shein alikuwa hajui, hivyo hata saa hizi ninapoandika hapa, usikute huyu jamaa wala hajajijua kuwa yeye ndiye anapaswa aje awe rais ajaye wa Zanzibar!. Hii nibkufuatia dhulma kubwa iliyokuwa ikifanyika Zanzibar kwa miaka na miaka, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda lakini sasa kwavile Samia ni mpenda haki, msema haki na mtenda haki, for the first time in Zanzibar tangu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964, uchaguzi wa 2025 unaweza kuwatendea haki!.
Hivyo hoja kama hii inapotolewa na mwajeiefu mwenzetu, mwandamizi kama huyu, hivyo nimejikuta ni muhimu kuisambaza.

Paskali.

(Mwanzo wa kunukuu Barua ya...)

Kwa kiasi kikubwa, siasa za Tanzania zimejikita zaidi kwenye chaguzi, hususan uchaguzi mkuu. Kwamba vyama vya siasa hutumia muda mwingi kujiandaa na chaguzi kiasi kwamba kuna dhana kwamba haviwatumikii wananchi vya kutosha kutokana na hilo.

Lakini lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Na katika nchi za kidemokrasia, kushika dola kunawezekana kwa njia moja tu, yaani uchaguzi mkuu. Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kwa vyama vya siasa kujipanga vema kwa ajili ya chaguzi.

Na kwa chama tawala, kisipofanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya chaguzi zijazo, nafasi yake kama chama kinachoshika dola inakuwa hatarini.

Ni katika mazingira hayo ndio maana kumekuwa na maongezi mengi kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 japo bado miaka miwili hivi kabla ya uchaguzi huo. Na japo kuna chaguzi za serikali za mitaa mwakani, maongezi mengi ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kwamba kuna jitihada zinafanyika huko Zanzibar kumwezesha Dkt Hussein Mwinyi kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2025.

Si tayari CCM “ina mgombea wake” 2025?
Naam. kwa mujibu wa utaratibu usio rasmi huko CCM, rais aliyepo madarakani anakuwa automatically mgombea pekee wa urais mwaka katika uchaguzi utakaomuingiza awamu ya pili ya urais wake.

Ilikuwa hivyo kwa Mkapa mwaka 2000, Jk 2010 na Magufuli 2020. Na inatarajiwa iwe hivyo kwa Mama Samia 2025.

Hadi wakati makala hii inaandikwa haijafahamika rasmi kwanini kuna mpango huo amba sio tu utapelekea “kuukoroga utaratibu huo usio rasmi wa Rais aliyepo madarakani kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo ili akamilishe ngwe zote mbili” bali pia utakuwa upinzani baina ya wanasiasa wawili kutoka Zanzibar.

Maandalizi yameanza
Taarifa zinaeleza kwamba tangu Zanzibar ijiunge na Tanganyika mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna kipindi ambapo upande huo wa Muungano umepokea fedha nyingi kutoka serikali ya Muungano kama kipindi hiki cha utawala wa Mama Samia.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa sehemu ya fedha hizo zimekuwa zikitumiwa na wanamkakati wa mpango huo wa kumwezesha Dkt Mwinyi kuwa mgombea mwaka 2025.

Licha ya ukweli kuwa maandalizi ya uchaguzi wowote hule huhitaji fedha za kutosha, yaaminika kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 utatawaliwa na matumizi makubwa ya fedha hasa kutokana na ukweli kwamba wanasiasa wengi wamepoteza mvuto machoni mwa wananchi na njia pekee ya “kupendeka” ni kumwaga fedha.

Mama Samia anawarahisishia kazi wapinzani wake ikiwa ni pamoja na mwanasiasa huyo wa Zanzibar
Kuna matukio mawili makubwa ambayo yanatarajiwa “kumsumbua” Mama Samia kati ya sasa na uchaguzi mwaka 2025. La kwanza ni suala la mkataba wa bandari ambalo japo “kwa nje ya CCM” linaonekana kama lilikuwa lina mwafaka miongoni mwa wana-CCM, ukweli ni kwamba sio tu lilizua mgawanyiko wakati wa mjadala bali pia limeacha makovu ambayo yanaweza “kukwanguliwa” pindi kampeni za urais zitaposhika kasi.

La pili ni hili la “Mama Samia kujichoma msumari mwenyewe” kwa kumteua Bashite kuwa katika mwenezi wa chama hicho, huku akifahamu fika kuwa kada huyo anachukiwa na wengi ndani na nje ya chama hicho.

Japo Mama Samia anatarajia kuwa Bashite atamsaidia kukabiliana na “wapinzani wake”, nguvu za kada huyo huko nyuma zilitegemea zaidi staili ya uongozi wa kibabe wa marehemu Magufuli, ambayo ni tofauti na satili ya uongozi wa Mama Samia, unless aamue kubadilika.

Hitimisho
Kuna msemo kuwa kwenye siasa, wiki moja ni sawa na uhai mzima (lifetime). Na kwa hakika, kati ya sasa Novemba 2023 hadi Oktoba 2025 ni takriban miaka miwili, na mengi yanaweza kutokea aidha kuimarisha dhamira ya mwanasiasa yeyote mwenye ndoto za kumpiku Mama Samia au urais wa Mama Samia ukaimarika zaidi kiasi kwamba yeyote mwenye ndoto za kum-challenge atakuwa anapoteza muda wake. (mwisho wa kunukuu)

Mwana if fulani.
C&P by Paskali
Update 1
Mchango very objective
Mnatuharibia nchi kwa ramli zenu hizi.
Hizi sio ramli, ni trends readings, kusoma mielekeo, karibu ujifunze kusoma mielekeo uone ni mielekeo gani watu kama sisi tuliwawekea humu na ikaja kutokea.
SSH kakwambieni hatogombea 2025?
SSH hahitaji kumwambia mtu yoyote kuwa atagombea au hagombei 2025, kwasababu hata akipoupata urais, hakumwambia mtu yoyote kuwa anautaka urais wa JMT, ni imetokea tuu SSH akawa rais wetu ile March 17, 2021 lakini trends za SSH atakuwa rais wetu, watu wa trends, tuliziweka humu toka 2017!. Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020
Huyu Mwinyi ana tofauti gani, ukizingatia kule Zanzibar kwanza ndio ajamaliza vipindi vyake viwili kama ilivyo ada ya CCM.
Ni kweli utaratibu wa CCM ni rais kushika madaraka vipindi viwili, ila it's not fast and hard rules, no utaratibu tuu wa CCM, kipindi cha urais kwa mujibu wa katiba zote mbili ya JMT na ya ZNZ, urais ni miaka 5, anaweza kugombea kipindi cha pili lakini sio lazima, Ali Hasan Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kimoja tuu, akafuatiwa na Idris Abdul Wakil alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kimoja!, hivyo urais wa vipindi viwili sio lazima!.

Hata JPM, angekuwa anasoma jf na kuufuata ushauri wa humu, saa hizi angekuwepo!, watu tulimshauri humu asigombee kipindi cha pili na badala yake ampishe Samia, ni mwaka 2017 kwenye bandiko hili Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.
Kisha 2020 kwenye bandiko hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?. Hili mnalionaje?.
Hivyo usiite hizi ni ramli hizi sio ramli na kwa taarifa yako mabandiko kama haya ndio mabandiko ya kusaidia nchi, na kuwasaidia viongozi wetu kujiandaa kisaikolojia kwa yajayo. Huwezi jua kama JPM angeusikiliza ushauri wa humu ile 2020 kuwa ampishe tuu Samia, you never know labda saa hizi angekuwepo!. Ndio maana nilipo isikia sauti hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke nikaileta ili kumsikilizisha mtu ili...

Siku zote nasisitiza humu kuwa kauli zinaumba!. Karibu utembelee hapa kuangalia baadhi ya hizi kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

P
 
Hili jambo la Dokta Mwinyi kuna mtu ndani ya Chama alinieleza Februari, 2022.

Kama nawe umelipata huenda litakuwa na Ukweli fulani.

Kwenye Siasa huwa wanasema hakuna "Adui wa Kudumu wala rafiki wa Kudumu"

Ndiyo maana hata lile bomu la DP World taarifa ilipenyezwa na mtu wa ndani ya system kwenda CHADEMA ili kumwambia Mama safari yake ni mwisho 2025.
 
Hili bandiko sio bure, nadhani limekuja kimkakati zaidi, JF ni jukwaa Pana Sana, wanaoingia humu hawasemeki, hawachangii wala kuanzisha Uzi wowote, Ila wana nguvu kubwa, sasa kwa huu ujio wa mleta taarifa nadhani hao wakaa kimya wamekuja kivingine.
NINAONAVYO MIMI : MAMA KAINGIA CHAKA KUMRUDISHA BASHITE, bila Shaka hili linaweza kumtafuna, tusubiri tuone.
 
Kwa hiyo ndio huyo humble, patriotic, Truthfully, visionary and intelligent atakaefanikisha next stage sio!!?

Bado mapema mnyukano utamuibua mwingine kabisa wakuu!!

Kwasasa ngoja tuone hizi karata za Mama kumteua kina mwegelo uwt na makonda zitamfikisha wapi!!

Bahati mbaya sana ndani ya CCM kadri jinsi unavoupigania urais ndio unavozidi kuukosa kabisa!!

Tunasubiri haya,

Halafu we Pascal si ulituambia Mpango ndio Mpango mzima!au amekua sio Mpango!!?
 
Msichokijua ni kuwa kile kiti kina addiction sio rahisi kama mnavyodhani mama samia kampita mbali sana mwinyi kwenye uongozi kwa sasa.
Hawezi kubali hilo kila mtu anapenda kuacha legacy ya kipekee na ndio samia anachotaka kufanya kwa upande wake.

Ushauri kwa team Mwinyi kuna mambo sio ya ya kulazimisha na sio kila mtu ameandikiwa au ana haki ya kuwa rais wa jamhuri jifunzeni kwa kwa mhe. Lowasa na mkubali yapite..
 
Kwa hiyo ndio huyo humble, patriotic, Truthfully, visionary and intelligent atakaefanikisha next stage sio!!?

Bado mapema mnyukano utamuibua mwingine kabisa wakuu!!

Kwasasa ngoja tuone hizi karata za Mama kumteua kina mwegelo uwt na makonda zitamfikisha wapi!!

Bahati mbaya sana ndani ya CCM kadri jinsi unavoupigania urais ndio unavozidi kuukosa kabisa!!

Tunasubiri haya,

Halafu we Pascal si ulituambia Mpango ndio Mpango mzima!au amekua sio Mpango!!?
Huu Uzi umeletwa na watu wa propaganda kupima upepo. Inakuwaje Mwinyi ampinge Dada yake? Mwinyi ni Rais mzuri Sana ila siungi mkono njia anayotaka kuitumia. Amalizie Kwanza Zanzibar aje na kwa Muungano Kama afya inaruhusu.

Lingine bandiko hili halimhusu Mwinyi bali Kuna mwanasiasa antaka kumfanyia Shambulizi la kushutukiza Rais Samia. Yaonekana hali sio shwari chamani na serikalini.
 
Samia amepwaya, hili halina mjadala, na kabla hata hayo mambo mawili hayajatokea, la bandari na Makonda kuwa Mwenezi wa CCM, tayari palishakuwepo na minon'gono kuwa Samia hatagombea 2025.

Kwa sasa kusema nani atagombea au vipi, hili sioni kama lina uzito sana, ila Mwinyi kupewa hiyo nafasi labda ndio watampa ili kurekebisha namba, kwani atakuwa tayari ameshatumikia kipindi kimoja Znz, ili cha pili aje kumalizia Bara.
 
Back
Top Bottom