Madhara ya kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na Golikipa ni haya!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
MADHARA YA KUOA MWANAMKE AMBAYE HAJASOMA NA GOLIKIPA NI HAYA!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimeona kuna vijana hapa wanadanganyana na kuwa na mawazo ya kizamani.

Ati wao wataoa wanawake wenye elimu duni na wasiofanya kazi isipokuwa kazi za nyumbani (golikipa).

Sasa kwa ninyi mliofanya maamuzi ninyi sina neno na nyie kwa sababu huo ni uchaguzi wenu.

Wazo hili ni zao la kizamani ambalo msingi wake ulikuwa kwa jamii isiyoamini kama Mwanamke naye ni mtu.

Lakini ujumbe huu nimeandika ni kwa wale ambao bado hawajafanya maamuzi au hawajui wachague kipi kati ya kuoa Mke aliyesoma na anayefanya kazi za taaluma au Mke ambaye hajasoma na ambaye atakuwa mama wa nyumbani.

Yafuatayo ni madhara ya moja kwa moja ambayo utayapata kwa kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na ambaye hana kazi yaani mama wa nyumbani;

1. Atakuwa Mwanamke Cheap na wagharama nafuu Kabisa.
Hakuna kazi rahisi kama kutongoza Mwanamke ambaye hajasoma na hana kazi. Ni rahisi kama kunywa uji wa mgonjwa. Yaani shwaaa!

Moja ya vitu vinavyompa mtu thamani kwa dunia ya leo ni Elimu.

Hata wanaume watakaomtongoza mkeo watakuwa Lundo kama siafu wekundu, hawamuogopi, wamuogope kwa kipi hasa! Lakini mdada shule ipo tena anawazidi mpaka wanaume Unafikiri hapo kuna nini.

Mpeleke mkeo ambaye hajasoma na hana kazi yoyote Kwenu siku ukitokea msiba uone jinsi atakavyotumikishwa kwa kusugua masufuria na makazi yasiyo na hadhi. Wakati huo Wake wa ndugu zao wamekaa mguu juu na hakuna kima yeyote atakayewasogelea isipokuwa wao wenyewe waamue.

Jipe hadhi kijana acha woga wa kijingajinga.

Unataka familia yako iwe cheap? Unataka watoto wako wajisikieje wakimuona mama yao(mkeo) akitumikishwa kwa kazi dhalili?

2. Mwanamke kuwa Mnafiki na kushindwa kusimama katika nafasi yake ya mke na Mama.
Mke wako hana elimu alafu hana kazi. Atawezaje kusimamia majukumu yake kama mke na kama Mama?

Mke lazima awe na elimu ya kiwango fulani angalau Diploma kwa zama hizi. Kisha awe na kijikazi au kazi ya kuingiza mapato.

Mke ni Mama wa watoto wako lakini pia ni Mama yako mlezi wakati mwingine.

Lazima uwe na Mwanamke ambaye ataweza kubeba jukumu la kukutunza na kukulea kimwili na kiroho na wakati mwingine kiakili pale ambapo utakengeuka.

Sasa unachukua Mwanamke shule hana, hana kazi, Mwanamke anakuogopa badala ya kukuheshimu kisa hana kipato.

Umekengeuka kidogo hakuna wakukurudisha kwenye mstari.

Nawajua wanaume wengi ambao wao ndio chanzo cha kuvunja nyumba zao kwa kukengeuka kwao. Aidha kutumia vibaya uanaume na ubaba wao vibaya.

3. Mkeo hataheshimiwa na Watu wa nje.

Raha ya mke aheshimiwe. Sio kila siku mke anakondeana kwa kudharaulika.

Binadamu ni kiumbe mwenye dharau Sana.

Kanisani atadharaulika. Mtaani hivyohivyo. Kisa hana elimu wala hana kazi. Yaani yupo yupo tuu.

4. Kugawa Uroda kirahisi.
Ni kweli wanawake wengi hugawa uroda lakini kuna kugawa Uroda kirahisi.

Fuatilia hata jamii yenye umalaya mwingi wanawake wao hawana elimu wala hawana kazi.

Yaani Mwanamke awe mwalimu au daktari au mwanasheria alafu awe Malaya, hiyo sio rahisi.

Ila mkeo akiwa hana elimu jua kabisa hata bodaboda hawamhofii. Yaani mwanaume yeyote anaweza kuruka naye kwa sababu mkeo ni level ya chini ambaye yeyote anaweza kutunda yake.

Lakini Mwanamke mwenye elimu na kipato ni kama Mnazi. Mpaka umpate lazima jasho likutoke na wapandaji huwa wachache.

Fikiria mkeo ni mkurugenzi Unafikiri ni wafanyakazi wake wangapi wana ujasiri wa kumtongoza? Lazima wawe na hofu.

Alafu fikiria mkeo hana elimu yoyote Unafikiri kuna mtu anamhofia kumfuata?
Hakuna!

Sasa mwanamke Watu wanatakiwa Wamheshimu yeye bila hata ya uwepo wako. Sio mkeo aheshimiwe kisa umemuoa yaani ni mke wa mtu. Hapo umepigwa.

Yaani Watu wanakuheshimu tuu wewe ndio maana hawamfuati mkeo lakini ukiwa haupo Watu wanajigaragaza. Lakini Mwanamke akiwa na kazi nzuri na elimu hata asipokuwa na mume anaheshimika na wanaume hujifikiri mara mbilimbili kumfuata.

Yote kwa yote Maisha ni ubatili. Lakini Watu wanachokazana ni kuepuka ubatili wenye maumivu, dharau, majonzi na taabu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Siku za hivi karibuni huna hoja kabisa kijana wangu, shida nini??

Ni zuwena gani anaekuzuzua huyo??

Bila shaka mpenzi wako ni mwenye elimu ama anafanana na huyo uliemuandika hapo juu.
Huu uzi umeandika kwa hisia zaidi na sio kitibeli kama ambavyo huwa unajinasibu.
 
Haya ni mawazo ya mtu ambaye anaamini kwenye ufeminism.

1.Elimu ya mke itakusaidia nini?
Wangapi wamewatafuta vipanga na waliopanda vidato mpaka vyuo vikuu ila wakija kuishi nao, wanagundua nje ya Ile karatasi hawana lolote.

2.Kibarua Cha Mwanamke hakina msaada kwa Mume au kwa familia.
Naam wengi wa waliooa wanakiri wazi kabisa pesa na marupurupu ya mwanamke hayana msaada kwa familia yao, watoto wao hadi wao wenyewe kifupi matumizi yao hayatambuliki na hayahojiki kabisa.

3.Kutoa uroda bila kujali Ndoa zao?
Hapa ni hatari, hivi viumbe vinanyanduliwa kuliko maelezo huko makazini, vyuoni.
Kumbuka wako radhi kufanya chochote

4. Kipaumbele ni Taaluma zao
Sijui niseme nini? Ila tambua wanawake hawa familia ndio kitu Cha mwisho na Mume ni kama takataka.

5.Malaya kwenye Career zao na kupenda dezo.

Hili linafahamika na sitaki kulieleza sana.

6. Familia kukosa Uangalizi na Malezi ya mama.
Ndio fatilia familia za namna hii uone watoto wanavyolelewa na mahouse girl au kujilea wenyewe.

7.Mmong'onyoko wa Maadili

8.Baba ndevu, Mama Ndevu
Nadhani fatilieni mahakamani aina hii ya muungano na mwisho wake.

Nitaendelea..............
 
Haya ni mawazo ya mtu ambaye anaamini kwenye ufeminism.

1.Elimu ya mke itakusaidia nini?
Wangapi wamewatafuta vipanga na waliopanda vidato mpaka vyuo vikuu ila wakija kuishi nao, wanagundua nje ya Ile karatasi hawana lolote.

2.Kibarua Cha Mwanamke hakina msaada kwa Mume au kwa familia.
Naam wengi wa waliooa wanakiri wazi kabisa pesa na marupurupu ya mwanamke hayana msaada kwa familia yao, watoto wao hadi wao wenyewe kifupi matumizi yao hayatambuliki na hayahojiki kabisa.

3.Kutoa uroda bila kujali Ndoa zao?
Hapa ni hatari, hivi viumbe vinanyanduliwa kuliko maelezo huko makazini, vyuoni.
Kumbuka wako radhi kufanya chochote

4. Kipaumbele ni Taaluma zao
Sijui niseme nini? Ila tambua wanawake hawa familia ndio kitu Cha mwisho na Mume ni kama takataka.

5.Malaya kwenye Career zao na kupenda dezo.

Hili linafahamika na sitaki kulieleza sana.

6. Familia kukosa Uangalizi na Malezi ya mama.
Ndio fatilia familia za namna hii uone watoto wanavyolelewa na mahouse girl au kujilea wenyewe.

7.Mmong'onyoko wa Maadili

8.Baba ndevu, Mama Ndevu
Nadhani fatilieni mahakamani aina hii ya muungano na mwisho wake.

Nitaendelea..............

😄😄
Siku ukipata Stroke au umestaafu au kufukuzwa kazi au kufa alafu umeacha watoto wadogo ndio utajua jinsi ulivyokuwa na mawazo mgando.

Pesa ya Mwanamke inaweza isikusaidie wewe lakini ikasaidia wàtoto wako.
 
Nakubaliana na baadhi ya maandiko yako ya nyuma ila kwa hili la leo nakupinga asilimia mia.
Kusoma na kuwa na akili ni vitu viwili tofauti, oa mwanamke mwenye akili sio mwenye elimu. Wanawake kibao wenye elimu hasa huko maofisini ni wachafu na malaya kupitiliza tunawaona.

Na mwanamke kutongozwa sio kitu Cha ajabu labda ajabu ni kulala na kila anayemtongoza, kinachopelekea mwanamke kutongozwa ni muonekano na mazingira. Mwanamke mkurugenzi ni rahisi kutongozwa na wakurugenzi wenzake au watu wa Kariba yake.
Mwanamke anaweza akawa hajasoma ila akatongozwa hata na profesa na anaweza akawa amesoma ila akatongozwa hata na watu wa hovyo kutokana na muonekano au mazingira aliyokuwepo.

Kuosha masufuria,kupika na kushirikiana shughuli za kijamii hasa misiba na harusi sio utumwa ni utamaduni wetu tu.
 
Back
Top Bottom