Ukatiri na unyanyasaji wa mbowe wadhihirika

Status
Not open for further replies.
Mtoa mada ni kada maarufu wa magamba,mwenyekiti wa willaya fulani,jina linahifadhiwa
 
Madaya haya yote umejitakia mwenyewe! Wewe unaleta pumba zako kwa watu wenye muono mkubwa.Sasa nakushauri uombe msamaha kwa kuleta post isiyo na mbele wala nyuma.
 
Kweli kuna haja ya kumjibu Nape hapa? I don't think so...let ignorant fly by itself.

Mnamo mwaka 1958 ni mwaka wa kihistoriakatika Nchi hii ya Tanzania.Mjadala wa kura tatu ni miongoni mwa matukio hayo ya kihistoria ambapo Mwl.Nyerere alikuwa mzungumzaji mkuu katika mjadala huo.Kutokana na huruma, busara,mvuto na ushawishi mkubwa aliokawanao Mwalimu huo;viongozi wa TANU na watu wengine waTabora walipanga mkakati wa kumnyanyua mwalimu huyo wakati atakapowasili kwenye mjadala huo.
Na tazama jinsi Nyerere alivyoongozwa na busara na huruma kubwa pale alipokataa kunyanyuliwa huku akisisitiza kuwa, hali hiyo ni sawa na ukatiri,unyanyasaji,ubinafsi na utumwa uliopea.Hali ni tofauti kwa Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe,ambaye kutokana na ukatiri, unyanyasaji na ubinafsi wake alionekana kujawa na furaha mithili ya mtu aliyefanikisha kupiga chafya pale aliponyanyuliwa na wafuasi wake wa CHADEMAkule Arusha baada ya kupata dhamana ambao kwa bahati mbaya hawajui kama wamelishwa unga wa ndere na chama hicho na hivyo kushindwa kung'amua baya lolote la viongozi wao wadhalimu.Wafuasi hao walionaswa na sumaku kali ya CHADEMA na hivyo kudumaa kimawazo, wanaonekana kuwaona wajinga wataalamu wa saikolojia ya binadamu wanaozifahamu tabia za binadamu kulingana na muktadha mahsusi huku wakijikakamua kutoa hoja zao zilizoathirika na unga huo wa ndere kama watakavyojitokeza katika hoja hii.
Nilishangawza sana kuona kiongozi huo akifurahia kunyanyuliwa na wafuasi wake ambao kwa bahati mbaya hawakusoma historia ya utumwa nakwamba hiyo waliyoifanya ni 'aspect' yake.
 
Madaya,
Pole sana wewe ni shujaa wa cinema za kihindi usivunjike moyo kama ungekuwa kibaka basi kipigo ulichokipata ni cha kariakoo, karibu sana jamvini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom