UHURU: CHADEMA yapasuka

Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?

Hivi hili nalo ni gazeti?
 
Yaani hata kama ni kweli Dr Slaa akigombana na Mbowe hili lina uhusiano gani na CDM kupasuka??? Eti mwandishi ana habari za kikao cha siri. Aisee! Jamaaa ana haribu wino na karatasi za bure kuandika upuuzi huu. Adhabu kubwa anayopaswa kupewa na kumpuuzia
 
uhuru na habari leo
ccm ikifa sijui wataandika nini tena
wahariri vilza wachumia tumbo.
ni wa kutemea mate kwa kuandika upuuzi badala
ya kujikita kuadika habari za maendeleo.
 
Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?

Wapika majungu hawa tushawazoea.... Wafa maji hawaachi kutapatapa
 
Slaa hatakiwi kugombea Urais na Mzee Mtei kwa sababu za kutokuwa na maadili.
 
Gazeti la udaku@work now! Wajinga ndio waliwao! Sisi tulishaamka zamani! Amkeni mliolala kumekucha!
 
Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?

source: toilet paper
 
Mie siamini kama habari hii ni habari kwani gazeti hili bado lipo ?Nani mhariri wake ?
 
Ziara ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mikoa ya Kanda ya Kusini, imehitimishwa kwa viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.
Willbroad Slaa kutofautiana.

Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.

Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.

Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.

Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.

Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.

CHANZO: NIPASHE
 
utapeli wa maneno hayo tunawahua nyie ni ccm amkosi cha kuongea lengo ni kuchafua
 
Source: Uhuru mnapoteza muda kwenye mambo ambayo siyo ya msingi baadala ya kushughulika na matatizo ya wapiga kura wenu.
time will tell!
 
Huo ni utumbo. Kuna idadi gani ya wananchi hadi Slaa atake kuwaona watu wengi?Huo mji una watu milioni?Acha ujinga wewe na chanzo chako cha habari hizi.
 
Chama hai lazima kuvutana juu ya mitazamo kadhaa wa kadhaa, Slaa yuko sawa, Mbowe pia yuko sawa, ni uhai wa chama unaowafanya wawaze kitofauti tofauti. Yote juu ya yote kikao (wajumbe) ndo kinaamua nini bora kufanyika. Tunasuguana mawazo lakini hatugombani.
 
Back
Top Bottom