UHURU: CHADEMA yapasuka

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.

Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

attachment.php

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.

Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.

Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?
 
Uhuru haliuzi,wanafoji habari za Chama kiongozi CDM,ili walau wapate wateja hawajui wao ni sawa na mwehu.MTAANI HATULITAKI TENA LABDA WATUPE BURE TUSOKOTEE TUMBAKU.
 
Tena kama ni kweli ningeomba hata makonde wapigane,ili kumkomboa mtanzania...sio akina JK kwenye vikao vyao kuchekeanachekeana tu, linchi linzidi kuzama tu...!! Go on CDM
 
Yaani nitoke hela yangu mfukoni ninunue gazati la Uhuru! Halina hata kitu cha maana, tunaliweka kwenye categori ya magazeti ya udaku.
 
Uhuru haliuzi,wanafoji habari za Chama kiongozi CDM,ili walau wapate wateja hawajui wao ni sawa na mwehu.MTAANI HATULITAKI TENA LABDA WATUPE BURE TUSOKOTEE TUMBAKU.

Huo ndio ukweli. Kwa muda mrefu sana sijaona watu wakiichangamkia hii toilet paper. Magazeti bora bongo ni Mwananchi, Nipashe na Tz Daima.
 
alafu wamekosa cha kudanganya dr slaa na mbowe ni ndoto kugombana.
 
Gazeti la mipasho na dhani mhariri wake ni wassira kama si nape.
 
mkubwa!ukisikia mtu anakuambia yafuatayo
  • Mfa maji haishi kutapatapa
  • Sikio la kufa halisikii dawa
Kaa vizuri katika mkao wa kungojea matoke ndio utajua nani MFA MAJI na nani SIKIO LA KUFA.kumbuka nyuma walisha sema eti
  • Chadema ni chama cha ukanda-walipoenda Lindi na mtwara wamebaki wanaumbuka wao
  • Wakasema chadema inaogopa Dsm-walikaja jangwani aibu ikawashika
  • Wakasema chadema ni chama cha msimu-M4C inawaumbua
  • Wakajalibu kuiga jangwani-wameishia kupata aibu
 
Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?

Haya ndo madhara ya waandishi wanaosoma shule za kata na vyuo vya kata.Hivi kweli unaweza kusema mikutano ya CHADEMA imesusiwa na imekosa wahudhuriaji?
Au walimaanisha mkutano wa Nape Njombe, Makambako na ule wa Jangwani?

Mfa maji; haachi kutapatapa
 
huo ndio ukweli. Kwa muda mrefu sana sijaona watu wakiichangamkia hii toilet paper. Magazeti bora bongo ni mwananchi, nipashe na tz daima.

chema chajiuza, kibaya chajitembeza;
hizo toilet paper arusha huwa hata hazionekani; mwananchi wako juu balaa.
 
gazeti la Uhuru siku hizi hata wanaccm wenyewe hawalinunui. Ukiangalia viongozi wa juu hutakuta hata mmoja akisoma gazeti la Uhuru. Utakuta wanasoma mwanahalisi, nipashe, tanzania daima n.k lakini sio Uhuru. Mia
 
Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?

Uhuru ni gazeti la CCM; sasa kama CCM yenyewe ni muflisi unatarajia gazeti lao liweje? hata uwezo wa kuajiri waandishi mahiri hawana unategemea waandike nini kama sio CDM, chama Dume, of course their nemesis!
 
Naona sasa hata magazeti ya udaku,yanayomilikiwa na shigongo kwa udaku hayalifikii hili gazeti la magamba
 
Back
Top Bottom