UHURU: CHADEMA yapasuka

Tatizo ni moja tu, CCM ni Kikwete na Kamati kuu, hivyo wanadhani CDM ni Chair and Katibu, kumbe ukweli ni kwamba CDM ni Wananchi wa TZ, Chair na Katibu au Baraza Kuu wakigombana CDM inakwenda mbele (concept ya misuguano wa hoja ni lazima kwa vipanga). Wakipatana, mmoja anakaa ikulu mmoja wizarani, Tanzania inakombolewa.
 
mfamaji haishi kutapatapa,ccm haina mvuto na mtaji wao ni wajinga.nasema wajinga ni mtaji wa kwa sababu ndio wanaweza kuwadanganya,tunaona kabisa mikutano ya chadema watu wanakuja wenyewe na wanchangia chama ushahidi ni mkutano wa jangwani hivi majuzi,wao wanawaleta watu, wanawalipa na wanawapatia usafiri lakini bado hawakuti chadema poleni sana
 
CCM lazima wakumbwe na ukuta kwa sababu ya kufadhili miradi ya kipuuzi kama hili gazeti ya Uhuru. Gazeti halina wasomaji zaidi ya mt wa Lumumba na walivyo vichwa team ya Lumumba inaweza kusimama mbele ya umma na kurudia huu upuuzi wa Uhuru.

Uhuru, badala ya kukaa chini na kutunga nani anaongea na nani, pengine mmengejikita kujua kwa nini bajeti za baadhi ya wizara mwaka jana zilipata 30% ya bajeti iliyopitishwa na bunge? Hela zimeenda wapi?
 
Gazeti la CCM Uhuru linaongoza kwa habari kwamba CDM imepasuka na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa wamerushiana maneno makali katika kikao cha siri mwandishi anachodai amenasa habari zake zote.Pia gazeti limeendelea kudai kwamba mikutano ya CDM mikoa ya kusini imekosa wahudhuriaji na wazee wamekikataa chama hicho kwa madai ya ukabila uliokithiri.

My Take:
Mimi ninadhani ni bora CCM ikahangaika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kuliko kupika propaganda ambazo hazina mashiko tena kwa Watanzania.Pia wanapaswa kujua kwamba watanzania wanakiamini CDM kama chama na sio kwa ajili ya Personalities za watu.Hivi utamdanganya nani kwamba mikutano ya CDM inasusiwa wakati kila siku watu wanaona umati wa watu kwenye mikutano yake kupitia taarifa za habari ITV?

Uhuru ni gazeti la propanganda la CCM (ieleweke sio la kibiashara) kwa maana hiyo usitarajie liandike chochote chema kwa CHADEMA na viongozi au wafuasi wake. Waandishi wake ni wale wanaosubiri fadhila za kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na vinafasi vingine serikalini na kwenye chama chao!
 
My Take:
Jacqueline Liana achana na UDC. Rudi Lumumba kaokoe gazeti lako.... hebu ona sasa. Inavyoelekea kuna mrithi wako anatafuta sifa kwa nguvu pale. Sifa, sifa, sifa zinamsumbua...sijui anataka nayeye apate UDC? Watakuuliua gazeti kabisa sasa.... rudi.
 
CCM ungetekeleza ahadi zako ulizokuwa unahaidi watanzania za maisha bora kwa kila mtanzania usingekuwa unahangaika na propaganda za kijinga.

Tafuteni njia za kutatua matatizo yanayo wakabili wanachi na sii kupambana na CDM inayofanya jitihada za kushika dola na kuwajali watu wake.

Kusema ukweli watanzania walio wengi bado baadhi yao wanaipenda CCM,Ila CCM haiwapendi ndiyo maana kwa sasa wanaanza kutafuta anaye wapenda.

Kama mngekuwa mnatekeleza mnayo yasema kwa kweli kusini na Pwani ingekuwa ngome yenu kwa miaka 50 ijayo,ila kwakuwa hamkuwajali na hamkutaka kuwa karibu nao,CDM imekuwa karibu nao nataratibu baada ya muda kutakuwa kama mikoa ya kaskazini na kanda ya ziwa.Tena mkumbuke mnavyo kaa na kupika propaganda za uongo mnazidi kukipa jina CDM.
 
mkubwa!ukisikia mtu anakuambia yafuatayo
  • Mfa maji haishi kutapatapa
  • Sikio la kufa halisikii dawa
Kaa vizuri katika mkao wa kungojea matoke ndio utajua nani MFA MAJI na nani SIKIO LA KUFA.kumbuka nyuma walisha sema eti
  • Chadema ni chama cha ukanda-walipoenda Lindi na mtwara wamebaki wanaumbuka wao
  • Wakasema chadema inaogopa Dsm-walikaja jangwani aibu ikawashika
  • Wakasema chadema ni chama cha msimu-M4C inawaumbua
  • Wakajalibu kuiga jangwani-wameishia kupata aibu

Msikini CCM kwa heri maana una dalili zote wa marehemu mtarajiwa,Gaazet lako limedhihilisha hili na Comrade Ruhazwe amekumaliza kabisa looooo
 
Nani asiyejua kua UHURU Ni Gazeti la Nape na magamba wenzake hilo gazeti hivi bado lipogo linakufa na chama chao CCM
 
Ni aibu kwa gazeti kongwe kama uhuru ambalo kwa kiasi kikubwa na kwa miaka mingi limekuwa likinufaika na kodi zetu kuandika habari isiyo na chanzo cha kuaminika.

Hivi viongozi wa CCM wakisoma habari hii watafurahia au watatoa karipia kwa mhariri wa gazeti hili kuandika udaku!
 
Uhuru haliuzi,wanafoji habari za Chama kiongozi CDM,ili walau wapate wateja hawajui wao ni sawa na mwehu.MTAANI HATULITAKI TENA LABDA WATUPE BURE TUSOKOTEE TUMBAKU.

Haliuzi una uhakika ? hebu tupe takwimu hapa tujue yapi yanayo uza ? IF NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK HERE IN JF
 
Hivi hilo gazeti la umbea uliokubuhu lipo?
Hata sikumbuki mara ya mwisho nililigusa lini.
Mhariri mkuu wa hilo gazet ni wasira,
huwa anafanya kazi usingizini.
 
Hilo ni dua la kukuu...Huyu Nepi ndiye atakayepasuka siyo CDM. kijana anapata shida sana huyu utafikiri kuku anayetafuta mahali pa kutagia mayai. Hata Headline sasa anatengeneza yeye na kuamuru iandikiwe...Peoplessssssss!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi kwenye mahusiano mke na mme wakipigizana kelele ndani ya chumba ndio kiashiria kuna mpasuko? Just trying to think outside the box
 
Nlishawahi kmuuliza muuzaji mmoja wa magazeti kama gazeti la uhuru linapata wateja akanijbu kuwa haliuziki huwa anachukua kopi moja tu kila siku na wakati mwingine hachukui kabisa.Hilo lishajifia siku nyingi na nduguze Mzalendo, Burudani, na Jambo Leo ...
 
Ninachoipendea CCM,
Wanacheza ngoma ya CDM.
Lakini hawajaweza kubadilika kabisa na kuacha UDAKU!
Wamelazimika kubadilisha jezi zao!.
Na sasa wamelazimika kuwatembelea wananchi kupitia Nape! na kufanya mikutano.
Tuwavumilie walikuwa wamezoea. Wakijajua watakuwa wamechelewa!.
 
Back
Top Bottom