Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,101
- 2,345
1. Tatizo lilianza seriously wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete (2005 - 2015). Alijaribu kulitatua lakini serikali yake haikuwa na nia ya kutatua bali viongozi wa serikali kutumia tatizo hilo kufanya ufisadi ili kuiba pesa ya umma tu. Rejea kashfa ya Richmond.
2. Tatizo hili limedumu kwa miongo mitatu na ushee sasa. Lugha na staili ya kulitatua ni ileile ambayo mtu makini akichunguza hataona nia ya kweli ya kutatua zaidi ya viongozi wa serikali kutumia tatizo hilo kama fursa ya kupiga pesa (kufanya ufisadi) huku nchi na wananchi wakitaabika Kwa uchumi wao mdogo kujeruhiwa na wengine kufa kabisa..
Haiwezekani tatizo dogo kama hili la umeme lidumu kwa zaidi ya miaka 35 huku serikali kongwe ya CCM ikiwa madarakani kwa miaka 63+ tangu 1961 ikiwa imeshindwa kupata ufumbuzi wa kudumu kiasi cha watu kujiuliza wanafanya nini ofisini kama hawatumii vichwa vyao vyema kufikiri?
Swali kuu la kujiuliza ni; Je, ina maana nchi hii haina watu wenye akili wanaoweza kufikiri vyema na kuja na Suluhu ya kudumu kuondoa tatizo hili? Kama wapo, kikwazo ni nini?
Hebu nyie chawa wa mama, wana CCM kindandaki kina Lucas mwashambwa, Paul Makonda, ChoiceVariable chiembe, FaizaFoxy, MamaSamia2025, Tlaatlaah Pascal Mayalla na wengine hebu tupeni maelezo tuwaelewe..!!
3. Wakati wa utawala John P. Magufuli (2015 - mwanzoni mwa 2021), kulikuwa na mwanga kidogo wa uelekeo kutatuliwa kwa changamoto hii. Huyu Mzee alianzisha mradi mkubwa wa kujenga bwawa la kuzalisha umeme ktk maporomoko ya Stigler Gorge yaliyopo katika mto Rufiji mkoa wa Pwani. Mradi huo umepewa jina Julius Kambarage Nyerere Hydro Electric Power Station (JKNHP)..
4. Pamoja na kuanzishwa kwa mradi huu, wakati wote wa u - Rais wa John P. Magufuli (2015 - 2021), hakukuwa na mgawo wa umeme kabisa ulio rasmi nchi nzima na kiasi cha kudumu kwa muda mrefu. Kama kulikuwa na kukatika umeme, basi ilikuwa ni kwa sbb za kiufundi na kwa muda mfupi tu..
John P. Magufuli alikuwa na ubaya wake. Lakini ktk eneo hili pamoja uchumi alifanya vyema sana. Mimi nampa maua yake🌹🌹🌹huko alikohifadhiwa...
5. Cha kushangaza, Mara baada ya kifo Cha Magufuli na nchi kutwaliwa na Makamu wake kikatiba, ghafla everything turned upside down. Maisha yakawa magumu. Thamani ya shilingi ikaporomoka kwa kasi. Mafuta ya petrol yakapaa kupita kiasi ktk muda mfupi sana ikiwemo kuadimika. Ghafla tatizo la umeme likaanza na linadumu hadi sasa..
Tunajiuliza kulikoni? Mbona lilishatatuliwa na Rais Magufuli imekuwaje ghafla linaanza tena? Bila shaka huu ni mchezo mbaya wa serikali kuhujumu wananchi wake wenyewe..!
Cha kushangaza ni kuwa huyu Rais anaonesha wazi kuwa hajali na hajui taabu wanayokumbana nayo wananchi. Yuko bize kukata mitaa huko duniani. Ameshindwa kabisa kuonesha uongozi katika haya. Madume aliyoyateua mwenyewe yanatumia udhaifu wake wa kuwa mwanamke kumhujumu. Yakitaka kuiba, yanampangia safari kwenda ughaibuni kutembea. Kuna siku yatampangia ziara kwenda Somalia kuomba msaada🙄🤔 ili mradi tu yapate mwanya wa kupiga..!
Tunataka serikali ituambie shida ya hii kitu iko wapi? Mbona tatizo ni la miongo zaidi ya mitatu? Kama CCM mmeshindwa kutatua, mnafanya nini kwenye ikulu yetu???