Escardo-bird
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 622
- 220
Niliuguwa nikiwa kidato cha tano, nikarudishwa nyumbani ili nisiambukize wengine shuleni, Nilipata homa kali sana ambayo sijawahi kuumwa tena, niliabukiza watoto wote walio kuwa wadogo kwangu hasa under 13yrs, huo ugonjwa siupendi na nauogopa, sipendi uikumbe familia yangu hasa nikikumbuka unavyoleta homa kali, hadi leo ninamakovu manne ya huu ugonjwa ili hali niliugua miaka 10 iliyopita.
Daah mkuu hadi leo bado vikovu bado unavyo, yaan huu ugonjwa unakereketa vile vipele vyenye maji vinawasha afu unaambiwa usivikune arrrrghhhh tukiwa wadogo bro aliugua akawa anasugua mgongo kwa ukuta ajikune vipele vya mgongo kwa pamoja yaan unatesa sana.