Ugonjwa wa Tetekuwanga (Chicken Pox): Maambukizi, dalili, madhara na tiba

Gigo

JF-Expert Member
Aug 6, 2006
456
46
Kuna jamaa yangu ameugua ugonjwa wa tete kuwanga.Na yeye ni zaidi Ya miaka 14 sasa naona ameshamuambukiza kaka yake mwenye umri wa zaidi ya miaka 24. Nimepata wasiwasi huenda anayefuatia kuugua ni mimi,lakini nilishawahi kuugua kabla.

Je, naweza kuugua tena kwa mara ya pili?

Je, nini kinga na tiba ya ugonjwa wa tetekuwanga?

2. mama fulani anauliza..
Habari za mida hii wakuu! ndugu zangu naugua tetekuwanga kwa siku ya pili leo nimeenda hospital nimepewa dawa ya vidonge ambayo ni AMPICLOX na ya kuogea POTASIUM PEMANGANET zinanisaidia kiasi fulani maana muasho umepungua japo vipele vinaongezeka.

Sasa tatizo ninasikia zinaambukiza haraka sana na mimi nina mtoto wa miezi sita nanyonyesha.

Je, naweza kujikingaje ili nisiambukize wengine hasa huyu mtoto wangu mdogo maana nina homa kali sana naogopa sana yakimpata mtoto.

Kuwanga.png

=========
Maoni na ushauri wa wadau

Pole sana,
Fuatilia maelezo ya mimi49, pia kuna dawa ya 'Calamine Lotion' hutumika kutibu tetekuwanga na vilevile hutumika kama anti pruritic na anti sptic.

Kuna baadhi ya magonjwa yasababishwayo na virus (tetekuwanga, surua, etc) yakishampata mwanadamu na akafanikiwa kupona, basi mwili hujenga kinga ya asili na magonjwa hayo huwa ni nadra kurejelea tena.

Namna ya kujikinga:
Kwa kuwa ugonjwa huu huambukizwa kwa mfumo wa hewa, ni vyema kuhakikisha unakaa mbali na wale ambao hawajaambukizwa. Epuka kugusana ndani ya siku 3 hadi 4 tangia ulipoanza kutoka vipele.
Kwa kawaida virusi wa tetekuwanga "VZV" ni wepesi mno kuuawa, hakikisha unafua nguo zako na sabuni zile za majimaji zenye kemikali ya 'Sodium Hypochlorite', pia unaweza kutumia hata sabuni za unga na kuanika nguo zako juani na sio kivulini.

Chanjo:
Kwa kuwa umepata maambukizi ya tetekuwanga, washauri wa afya hupendekeza chanjo kwa watu wa karibu ya mgonjwa wenye hatari ya kukumbwa na maambukizi hayo.
Jaribu kutafuta chanjo ya ugonjwa huu kwa hospitali kubwa za mkoa au wilaya. Kwa kawaida chanjo hii sio miongoni mwa zile chanjo ambazo watoto wadogo huwa wanapewa kwa ajili ya kinga ya magonjwa kadha wa kadha.

attachment.php


Tete kuwanga ni ugonjwa ambao unaombukiza nakusababishwa na virusi vinavyojulikana kama Varicella zoster virus.Maambukizi ya tete kuwanga huonekana sana kwa watoto wadogo ingawa hata watu wakubwa pia hupata maambukizi ya ugonjwa huu. Tete kuwanga hupatikana duniani kote.Katika nchi zenye kupata majira ya baridi, maambukizi ya ugonjwa huu huonekana sana wakati wa kipindi cha majira ya baridi na kipindi cha masika.

Watoto walio na umri wa miaka 4-6 wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya tete kuwanga na ndio katika umri huu ambapo maambukizi ya ugonjwa huu yapo kwenye kiwango cha juu sana.Inakadiriwa ya kwamba, tete kuwanga huambukiza kwa kiwango cha asilimia 90.

Watoto wengi hupata maambukizi ya tete kuwanga kabla ya kufikia umri wa kubaleghe ingawa asilimia 10 ya vijana bado wanakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi ya tete kuwanga.

Katika nchi za tropiki,maambukizi ya tete kuwanga huonekana kwa watu wakubwa na huenda yakawa maambukizi ya hatari sana.

Maambukizi ya tete kuwanga hupatikana vipi?
Tete kuwanga huambukizwa kupitia njia ya hewa au endapo mtu atagusana mwili na mgonjwa wa tete kuwanga(kupitia majimaji yanayotoka kwenye vipele vya mgonjwa).Mtu yoyote yule anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kutoka kwa mgonjwa wa tete kuwanga kwa njia ya kucheka, kupiga chafya, kukohoa.

Hii inatokana na kusambazwa kwa virusi ya Varicella zoster kwa njia ya hewa pindi mgonjwa anapocheka,kupiga chafya au anapokohoa.

Nini hutokea kipindi cha maambukizi (Pathofiziolojia)
Maambukizi ya tete kuwanga kwa mtoto husababisha mtoto kutoa kinga aina ya Immunoglobulin G (IgG), Immunoglobulin M, (IgM) na Immunoglobulin A,(IgA). Kinga hizi pamoja na kinga zinazosaidiwa na chembechembe za mwili (Cell mediated responses)husaidia kupunguza.

Madhara na urefu wa maambukizi haya ya awali ya tete kuwanga.Immunoglobulin G hubakia kipindi chote cha maisha na huweka kumbukumbu ya maambukizi ya tete kuwanga na hivyo kuwa chanjo dhidhi ya ugonjwa huu hapo baadae maishani.Baada ya kupata maambukizi ya Varicella zoster virus, virusi hivi husambaa hadi kwenye tishu za ngozi, kamasi (mucosal) na hata kwenye mishipa ya fahamu (sensory nerves).

Virusi hivi baada ya muda huwa kimya (dormant) {‘’ambapo ndio tunasema mgonjwa amepona’’} kwenye kifundo cha mishipa ya fahamu vinavyojulikana kama dorsal ganglion of sensory nerves.Kuchepuka tena kwa virusi hivi ambavyo awali vilikuwa vimekaa kimya ndio husababisha ugonjwa wa ukanda wa jeshi (herpes zoster),postherpetic neuralgia, na Ramsay Hunt Syndrome Type II.

Ramsay Hunt Syndrome type II inaambatana na dalili za kupooza sehemu mbalimbali za uso,maumivu kwenye sikio/masikio, kupoteza ladha ya ulimi (taste loss),mdomo kukauka, macho kuwa makavu na vipele kwenye mwili.

​
attachment.php



Dalili na viashiria vya Tete kuwanga

Dalili za kwanza ni;
• Kichefuchefu
• Kupungua kwa hamu ya kula
• Maumivu ya kichwa
• Maumivu ya misuli
• Kuumwa tumbo

Dalili hizi baadae hufuatiwa na hatua ya mgonjwa kutoka vipele, uchovu na homa ambayo sio kali sana, hatua hii ndio huonyesha kuwepo kwa ugonjwa wa tete kuwanga.

Vipele hivi mwanzo huonekana kama alama nyekundu ndogo kwenye uso, kichwa, tumbo,kifua, sehemu za juu za kwenye mikono na miguu ambapo baada ya masaa 10-12 alama zile nyekundu hugeuka kuwa uvimbe, uvimbe huu kisha hujaa maji na kupasuka.

Baadae vipele vipya (blisters) huanza kuchipuka kwa makundi kwenye sehemu za tupu ya mwanamke (vagina), kope (eyelids) na mdomoni ambavyo hupasuka na kuwa vidonda vidogo vidogo kwenye sehemu hizi.

Hatua hii ya kutokea vipele huanza kuonekana kuanzia siku ya 10-21 baada ya mtu kupata maambukizi ya Varicella zoster virus na huambatana na kuwashwa sana mwili.Vipele vinaweza kutokea kwenye viganja vya mkono, nyayo na hata kwenye pua, lips, masikio, njia ya haja kubwa.

Vipele venye majimaji (blisters) hutokea siku ya 4-7 baada ya hatua ya kutoka vipele kuanza na hupotea kuanzia siku ya 5 na kuendelea.

Mtu ambaye ana maambukizi ya tete kuwanga huweza kuambukiza watu wengine siku moja au mbili kabla ya kuanza kutoka vipele na kuendelea kuwa na uwezo wa kuambukiza wengine kwa siku 4-5 baada ya vipele kutokea.

Dalili ya kwanza ya tete kuwanga kwa watoto ni vipele kabla ya dalili nyingine nilizotaja awali hapo juu kufuata.Kwa watu wakubwa, vipele husambaa katika maeneo mengi mwilini kwa wingi na homa huwa ya muda mrefu sana na pia huweza kupata homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Varicella zoster virus.

Baadhi ya watoto ambao walipata chanjo ya ugonjwa huu hapo awali huweza kupata tena maambukizi ya tete kuwanga ingawa yanakuwa sio makali sana(hutoka vipele 30 kwa wastani) lakini watoto hawa bado wana uwezo wa kuambukiza wengine ugonjwa huu.Kwa kawaida mtoto hutokea wastani wa vipele 250 hadi 500 wakati wa maambukizi ya ugonjwa wa tete kuwanga.

Ugonjwa huu ni nadra sana kuwa na madhara makubwa ingawa madhara huweza kuonekana kwa wagonjwa walio na upungufu wa kinga mwilini, wenye kuugua magonjwa sugu au wanawake wajawazito ambao hawakupata chanjo ya ugonjwa huu.

Vipimo vya uchunguzi
I. Utambuzi wa ugonjwa huu hufanywa kwa kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa huu(Kichefuchefu, kupungua kwa hamu ya kula,maumivu ya kichwa,maumivu ya misuli, kuumwa tumbo na vipele)

II. Kupima majimaji ya ndani ya vipele kwa kutumia direct immunoflorescent test

III. Kipimo cha damu kuangalia wingi wa Immunglobin M (IgM), ambapo kiwango chake huongezeka panapotokea maambukizi mapya au kuangalia uwepo wa Immunoglobulin G (IgG) ili kuthibitisha kuwepo kwa maambukizi hapo awali.

IV. Kipimo cha ultrasound kwa wanawake wajawazito ili kuangalia dalili za kuwepo kwa maambukizi ya ugonjwa huu kwa kiumbe kilichomo tumboni (Fetal Varicella Infection).Inashauriwa kuchelewesha kipimo hiki kwa wiki 5 toka mama apate maambukizi ya tete kuwanga ili kuweza kutambua kama mtoto ameathirika au la.

V. Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya virusi vya Varicella zoster virus kwa mama wajawazito kwa kuchukua maji kwenye chupa ya uzazi ya mama (amniotic fluid). Kipimo hiki kina madhara kama kusababisha mimba kutoka au mtoto kupata Fetal Varicella Syndrome
Tete%20kuwanga%20mgongoni.jpg


Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yanalenga kupunguza athari za dalili na viashiria vya ugonjwa huu na si kuua virusi vinavyosababisha ugonjwa huu.

Matibabu ya tete kuwanga yanahusisha;
a) Kuwakata watoto kucha ili kuepusha kujikuna na hatimaye kukata vipele hivyo kuongeza kutokea kwa vipele mwilini

b) Dawa za maumivu kama paracetamol n.k

c) Antihistamines-Dawa za kupunguza kuwashwa mwili

d) Calamine lotion ingawa hakuna tafiti zilizofanyika kuthibitisha ubora wa matumizi yake dhidhi ya ugonjwa huu.Dawa hii ni salama

e) Kuongeza kiwango cha usafi wa mwili, kuosha mwili kwa maji ya uvuguvugu

f) Kukaa sehemu zenye baridi ili kupunguza kuwashwa mwili

g) Kuepuka kujikuna vipele

h) Dawa dhidhi ya virusi (antiviral medication) kama acyclovir au valacyclovir ambazo hutolewa saa 24-48 baada ya vipele kuanza,dawa hizi hupunguza kusambaa kwa virusi lakini haziui virusi hao.Dawa hizi hutolewa kwa wale ambao wana upungufu wa kinga mwilini na kwa wanawake wajawazito.

Watoto chini ya miaka 12 au wale wenye umri wa zaidi ya mwezi mmoja hawaruhusiwi kutumia dawa hizi kama hawana tatizo la upungufu wa kinga mwilini ili kuwaepusha na madhara wanayoweza kupata kutokana na matumizi ya madawa haya.

Madhara ya tete kuwanga kwa wajawazito
Maambukizi ya tete kuwanga wakati wa ujauzito yanaweza kuathiri mtoto hasa kama mama atapata maambukizi haya wiki 28 baada ya kushika mimba.Wanawake ambao wana kinga dhidhi ya ugonjwa huu hawawezi kupata tete kuwanga kipindi cha ujauzito na wasiwe na wasiwasi kuhusu

mtoto wao kupata madhara.Madhara ya tete kuwanga kwa mtoto ni kutokana na uwezo wa Varicella zoster virus kuwa na uwezo wa kuvuka kondo la uzazi (placenta) kutoka kwa mama mwenye tete kuwanga na hivyo kumuathiri mtoto.

Maambukizi ya tete kuwanga kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kipindi cha ujauzito hujulikana kama fetal varicella syndrome au congenital varicella syndrome na huambatana na;

I. Madhara kwenye ubongo wa mtoto-Kichwa maji (hydrocephalus), kichwa kuwa kidogo, maambukizi ya ubongo (encephalitis),aplasia of brain.

II. Madhara ya macho kama mtoto wa jicho (cataract), optic cup, optic stalk,microphthalmia, cataracts, chorioretinitis, optic atrophy n.k.

III. Madhara ya mishipa ya fahamu

IV. Madhara ya kibofu cha mkojo, miguu, njia ya haja kubwa,vidole kutoota vizuri n.k.

V. Matatizo ya ngozi kama hypopigmentation na n.k.

Watoto wenye umri wa mwezi mmoja au watoto wachanga wanatakiwa kulindwa wasipate tete kuwanga kwa kuweka mbali na wagonjwa wa tete kuwanga kwa siku 10-21.

Uwezekano wa mtoto kupata tete kuwanga ni mkubwa iwapo mama atapata maambukizi ya tete kuwanga siku saba kabla ya kujifungua au wiki moja baada ya mtoto kuzaliwa.


Tetekuwanga kwa Watoto


Ikiwa aikloviri itaanzishwa kwa masaa ya mwanzo wa vipele itapunguza dalili lakini haina athari kwa kiwango cha kutatiza. Kwa sasa basi, matumizi ya asikloviri haipendekezwi kwa watu wenye kingaimara (yaani, watu wenye siha bora wasio na upungufu wa kinga kwa sasa au wanaotumia tiba za udhibitikinga).


Matibabu ya tetekuwanga kwa watoto hulenga dalili wakati ambapo mfumo wa kinga hukabiliana na virusi. Huku watoto wadogo zaidi ya miaka 12 wakikata kucha na kuziweka safi ni sehemu muhimu ya matibabu kwa

vile wao huwa hatarini zaidi ya kukuna malengelenge yao. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 12 lakini kuzidi mwezi mmoja hawafai kupata dawa za kuzuia virusi iwapo hawaugui ugonjwa wowote mwingine ambao unaweza kuwaweka katika hatari ya kupatwa na matatizo.


Ili kuepuka kuishiwa na maji mwilini ,unywaji wa kiasi kikubwa cha maji unashauriwa hasa iwapo mtoto atapatwa na homa. Homa au maumivu ya kichwa yanaweza kupunguzwa kwa dawa za kupunguza maumivu

kama vile parasetamoli au ibuprofeni. Watoto ambao ni wakubwa kuzidi mwaka mmoja wanaweza kupewa vidonge vya antihistamini au dawa za maji ambazo kusaidia wakati ambapo mtoto hawezi kupata usingizi kwa sababu ya kuwashwa.


Asikloviri au kingaglobulini kwa jumla huagizwa kwa watoto walio katika hatari ya kukumbwa na matatizo yatokanayo na tetekuwanga . Wao hupokea matibabu sawa na iliyotajwa hapo juu kuongezea na dawa dhidi

ya virusi. Kategoria za watoto wanaoonekana kuwa katika hatari ya kupatwa na matatizo ni pamoja na watoto wachanga wa chini ya umri wa mwezi mmoja, walio na mfumo wa kinga hafifu, wale ambao hutumia steroidi au

dawa za kudhibiti kinga au watoto walio na magonjwa sugu ya moyo, mapafuna ngozi. Aidha, watu wazima na vijana huchukluliwa kuwa katika hatari ya kupata matatizo na kwa kawaida hupewa dawa ya kuzuia virusi.


Aspirini haikubaliki sana kwa watoto wadogo wa chini ya miaka 16 kwa vile imekuwa ikihusiana na uwezekano wa hali mbaya na hatari ijulikanayo kama dalili za Reye.
 
Chicken pox, is a highly contagious viral infection.

Chicken pox is acquired by direct contact with infected blister fluid or by inhalation of respiratory droplets.

In addition to affecting the skin, chicken pox can also cause lesions on the mucous membranes in the eyes, mouth, and ******.

Mara nyingi huwa ni kwa watoto under 14, japokuwa kama hujawahi kuugua utotoni chance ya kuugua ukubwani is high.
 
Kwani wewe ni mara ya kwanza kuwa exposed na chicken pox? kama hujawahi kuwa exposed wala kuugua, yes may be, lakini pia inategemea na immunity yako.

Severity ya disease pia ni individual, wengine wanaweza kuugua sana na wengine just one rash n.k

Surua na tetekuwanga zote ni viral diseases.
 
Wakuu naomba kufahamu kati ya calamine lotion na elyvate betamethazone valerate ointment,ipi nzuri kwa mgonjwa wa tetekuwanga?ipi inapönyesha haraka?inachukua muda gani kupona?maana hapa mwili unawasha
 
Wakuu naomba kufahamu kati ya calamine lotion na elyvate betamethazone valerate ointment,ipi nzuri kwa mgonjwa wa tetekuwanga?ipi inapönyesha haraka?inachukua muda gani kupona?maana hapa mwili unawasha

Mkuu, kwanza pole kwa kuwashwa na mwili. Lakini napenda kukuuliza maswali machache kabla ya kukufahamisha dawa sahihi ya tatizo lako.
1: Je diagnosis yako 'tetekuwanga' ni sahihi?
2: Umejuaje tatizo lako la kuwashwa mwili ni tetekuwanga?
3: Je, tatizo lako limeanza lini?
4: Mbali na kuwashwa mwili , Je kuna tatizo lingine limejitokeza?
 
Mkuu, kwanza pole kwa kuwashwa na mwili. Lakini napenda kukuuliza maswali machache kabla ya kukufahamisha dawa sahihi ya tatizo lako.
1: Je diagnosis yako 'tetekuwanga' ni sahihi?
2: Umejuaje tatizo lako la kuwashwa mwili ni tetekuwanga?
3: Je, tatizo lako limeanza lini?
4: Mbali na kuwashwa mwili , Je kuna tatizo lingine limejitokeza?
1. Ndyo tetekuwanga mkuu.
2. Nimeenda hospitali ndyo Wameniambia hvyo.
3. Siku tatu zilizopita.
4.vipele fulan hv kama malengelenge,ndyo vinawasha.
N.b
hospital jana waliniambia dawa hamna ila nikanunue moja wapo kati ya hzo
 
1. Ndyo tetekuwanga mkuu.
2. Nimeenda hospitali ndyo Wameniambia hvyo.
3. Siku tatu zilizopita.
4.vipele fulan hv kama malengelenge,ndyo vinawasha.
N.b
hospital jana waliniambia dawa hamna ila nikanunue moja wapo kati ya hzo

Chickenpox (tetekuwanga) ni ugonjwa unaosababishwa na virus. Self limiting. Mara nyingi inasumbua watoto. Inapotokea kwa mtu mzima au immunocompromised, Mara nyingi ugonjwa unakuwa mkali (severe). Kwahiyo kutokana na swali lako, tumia Calamine Lotion. Re-apply the lotion 12 hourly . Utapona
 
Shukrani mkubwa,maana nilikuwa napaka zote,ngoja niache h moja
Chickenpox (tetekuwanga) ni ugonjwa unaosababishwa na virus. Self limiting. Mara nyingi inasumbua watoto. Inapotokea kwa mtu mzima au immunocompromised, Mara nyingi ugonjwa unakuwa mkali (severe). Kwahiyo kutokana na swali lako, tumia Calamine Lotion. Re-apply the lotion 12 hourly . Utapona
 
Nakubaliana na wewe Mkuu,
Lakini pia unaweza kunywa, antihistamine kama Piriton(R), kupunguza makali ya kuwasha!



Chickenpox (tetekuwanga) ni ugonjwa unaosababishwa na virus. Self limiting. Mara nyingi inasumbua watoto. Inapotokea kwa mtu mzima au immunocompromised, Mara nyingi ugonjwa unakuwa mkali (severe). Kwahiyo kutokana na swali lako, tumia Calamine Lotion. Re-apply the lotion 12 hourly . Utapona
 
Mdogo wangu ametokwa na vipele viduchuviduchu yan kama vya joto sio hata maaana vimeabza juz bt leo mwili mzima anawashwa anajikuna amevimba hadi uson, miguun yan mwili mzima analia tuu sa jana alipelekwa dispensary eti wakamwambia kuwa ni dalili za surua vt then wakasema sio na wakampatia dawa ya mebendazole n alerid-d sijuihata if ni sahihi au laah jamn mwenye upeo maana icant stand seeing him anlia nakujikuna hivoo
 
jf doctor pliz nisaidien mdogo wangu ametokwa na vipele viduchuviduchu yan kama vya joto sio hata maaana vimeabza juz bt leo mwili mzima anawashwa anajikuna amevimba hadi uson, miguun yan mwili mzima analia tuu sa jana alipelekwa dispensary eti wakamwambia kuwa ni dalili za surua vt then wakasema sio na wakampatia dawa ya mebendazole n alerid-d sijuihata if ni sahihi au laah jamn mwenye upeo maana icant stand seeing him anlia nakujikuna hivoo
Mkuu hiyo ni alergy kuna kitu atakuwa amekula,mimi mtoto wangu vilimtokea Ijumaa iliopita mara baada ya kula samaki yaani ndani ya masaa mawili vilitokea mwili mzima na vikawa vinamuwasha mpaka akawa analia nika muwahisha hopitali wakampiga sindano ya mkononi,akapewa vidonge vya alergry jina nimesahau,erythromycin,calamine lotion na mimi mwenyewe nikamnunulia piriton ndio ikwa nafuu yake na mpaka juzi akawa amepona kabisa,nijulishe unaishi maeneo ya wapi inawezekana tunaishi eneo moja ili nikuelekeze hiyo hospitali.
 
Mkuu hiyo ni alergy kuna kitu atakuwa amekula,mimi mtoto wangu vilimtokea Ijumaa iliopita mara baada ya kula samaki yaani ndani ya masaa mawili vilitokea mwili mzima na vikawa vinamuwasha mpaka akawa analia nika muwahisha hopitali wakampiga sindano ya mkononi,akapewa vidonge vya alergry jina nimesahau,erythromycin,calamine lotion na mimi mwenyewe nikamnunulia piriton ndio ikwa nafuu yake na mpaka juzi akawa amepona kabisa,nijulishe unaishi maeneo ya wapi inawezekana tunaishi eneo moja ili nikuelekeze hiyo hospitali.

Nipo hapa airpot dear kuvuka reli dar
 
Huyo mdogo wako ana umri gani? Kwa sababu surua huwapata watoto ila tetekuwanga kama hukuugua utotoni basi hata ukubwani unaweza kupata. Je macho yake ni mekundu?
 
Kama utaweza nenda pale Mbezi mwisho(Morogoro road) kuna Hospitali inaitwa Kipasika otherwise nenda pale ukonga Hospitali ya karibu na recreation centre-Bar ya Magereza jina limenitoka iko barabarani ulizia madereva Tax watakuelekeza.
 
Huyo mdogo wako ana umri gani? Kwa sababu surua huwapata watoto ila tetekuwanga kama hukuugua utotoni basi hata ukubwani unaweza kupata. Je macho yake ni mekundu?

Yupo std 5 n yan kaharibika sidhan kama tetekuwanga coz ni vipele vidogoooooooo sana
 
kama utaweza nenda pale Mbezi mwisho(Morogoro road) kuna Hospitali inaitwa Kipasika otherwise nenda pale ukonga Hospitali ya karibu na recreation centre-Bar ya Magereza jina limenitoka iko barabarani ulizia madereva Tax watakuelekeza.

Iliopo ukonga madafu ile ya kanisani kipenzi? Mana maskin alitaka kusafiri mwenyewe akapumzike likizo hii bt ndo ivo yabid asiende basi ntafanya hivo my dear mana sion any improvement na hizi dawa waliompatia
 
Iliopo ukonga madafu ile ya kanisani kipenzi? Mana maskin alitaka kusafiri mwenyewe akapumzike likizo hii bt ndo ivo yabid asiende basi ntafanya hivo my dear mana sion any improvement na hizi dawa waliompatia

Ndio hiyo,wahi ikiwezekana nenda leo vinatesa sana,nimekuhurumia kwani vilinifanya siku mbili nikae nyumbani bila kwenda kazini nikimliwaza kwani alikuwa almost kachanganyikiwa.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom