Ugonjwa wa Tetekuwanga (Chicken Pox): Maambukizi, dalili, madhara na tiba

Niliuguwa nikiwa kidato cha tano, nikarudishwa nyumbani ili nisiambukize wengine shuleni, Nilipata homa kali sana ambayo sijawahi kuumwa tena, niliabukiza watoto wote walio kuwa wadogo kwangu hasa under 13yrs, huo ugonjwa siupendi na nauogopa, sipendi uikumbe familia yangu hasa nikikumbuka unavyoleta homa kali, hadi leo ninamakovu manne ya huu ugonjwa ili hali niliugua miaka 10 iliyopita.

Daah mkuu hadi leo bado vikovu bado unavyo, yaan huu ugonjwa unakereketa vile vipele vyenye maji vinawasha afu unaambiwa usivikune arrrrghhhh tukiwa wadogo bro aliugua akawa anasugua mgongo kwa ukuta ajikune vipele vya mgongo kwa pamoja yaan unatesa sana.
 
Mi niliugua mwaka jana na utu uzima wangu nikiwa nimeshaanza kazi. Bahati nzuri kazini kila mtu alishaumwa kwa hiyo sikupata tabu ya kutengwa. Homa yake ndo inatesa na vidonda vikipigwa na jua utatiririka machozi nakwambia!
 
Hii kitu iliingia shule miaka ya 95 wakati nikiwa boarding school moshi yani nusu ya shule iliugua sasa issue ikaja nimepanda basi siku ya tatu narudi dar yani nilikuwa natengwa live kila anaeniona anatamani anishushe kwa hiyo basi (shabaha)
 
Niliupata mimi nikiwa na takriban miaka 6 shughuri yake si ya mchezo. cha kusikitisha tulikuwa tunaishi karibia na meya wa mji mza maeneo ya kirumba hivyo basi nyumbani kwa meya huyo kulikuwa kuna baiskeli ndogo kwa ajiri ya watoto wake.

Sasa na sisi kama majirani tulikuwa tunaenda kuchezea baiskeli hiyo watoto walikuwa wanakusanyika hapo. Lakini mama mwenye nyumba alinikuta nacheza mchezo ndio umenoga alivyo nicheki tu akaniambia nitoke nje ya geti uku akisema nitawaambukiza wenzangu. sikujuwa kama ugonjwa wa tetekwanga unahambukiza.

Niliondoka huku nikisononeka sana
.
 
Daah mkuu hadi leo bado vikovu bado unavyo, yaan huu ugonjwa unakereketa vile vipele vyenye maji vinawasha afu unaambiwa usivikune arrrrghhhh tukiwa wadogo bro aliugua akawa anasugua mgongo kwa ukuta ajikune vipele vya mgongo kwa pamoja yaan unatesa sana.

Makovu ya huu ugonjwa ni balaa, nawaza dengue ingekuwa inaambukiza kama tetekuwangu sijui tungekuwa wapi sasa, maana inaambukiza haraka sana
 
Mimi niliugua mwaka jana nilikua nina mtoto mchanga wa miezi miwili nilizipata chuo kuna dada alikua anaugua na tulikua kipindi cha mitihani akashindwa kuahirisha. Niliteseka saana maana zilinitoka mwili mzima hadi kwenye chuchu nilikua nasikitika kumnyonyesha mwanangu. Tulikua nyumba nzima na mwisho wa siku akaugua mwanangu nilimuwahisha hospital akapewa dawa ya kunywa na kupaka haxikutoka zaidi ya vipele vitatu tu nikamshukuru mungu. Ila niliteseka saaana usoni nilikua kma nimebandikwa tope. Ila nimebaki na alama chache sana.
 
Makovu ya huu ugonjwa ni balaa, nawaza dengue ingekuwa inaambukiza kama tetekuwangu sijui tungekuwa wapi sasa, maana inaambukiza haraka sana

Kweli aisee hivi dengue ingekua ivo afu nasikia ishafika zbar na mbeya sasa najiuliza ni mbu kasafiri all the way to those places au kuna njia flan mtu unaambukizwa mayb wataalam wali over look
 
Niliupata 2004 nikiwa form 3. Nilipewa ruhusa lkn pia niliambukiza wanafunzi wenzangu wa kidato cha 3 wengi. Nilimaliza dozi bila kupona na nikashauriwa kutumia mwarobaini kwa kuchemsha majani yake kisha naoga na mengine nakunywa.
Hd leo bado baadhi ya makovu yapo.
 
According to bi mkubwa, sijawahi kuugua tetekuwanga. Ingawa nimewahi kuuguza shosti yangu wakati nipo chuo, tena nilimfulia hadi nguo kipondi yupo mgonjwa na haikunipata. Kwa hiyo sidhani kama ile dhana ya kuwa kama hukuwahi kuugua lazima utaipata ni sahihi
 
Mimi niliugua mwaka jana nilikua nina mtoto mchanga wa miezi miwili nilizipata chuo kuna dada alikua anaugua na tulikua kipindi cha mitihani akashindwa kuahirisha. Niliteseka saana maana zilinitoka mwili mzima hadi kwenye chuchu nilikua nasikitika kumnyonyesha mwanangu. Tulikua nyumba nzima na mwisho wa siku akaugua mwanangu nilimuwahisha hospital akapewa dawa ya kunywa na kupaka haxikutoka zaidi ya vipele vitatu tu nikamshukuru mungu. Ila niliteseka saaana usoni nilikua kma nimebandikwa tope. Ila nimebaki na alama chache sana.

Daah pole aisee huu ugonjwa uliupata wakati mbaya sana bora ulimuwahisha mtoto dawa kangepata shida kweli
 
Niliungua mwaka 2008, ulipoanianza sikujua ndio ugonjwa wenyewe ila vipele vilikuwa vinaongezeka kila baada ya muda mfupi, nakumbuka nilitoka vipele hadi kwenye kichwa
 
Jamani naombeni msaada nini dawa ya ugonjwa watete kuwanga hata ya kiasili mana zimenitoka mwili mzima na ugonjwa unasababishwa na nini? na ipi dawa yake? na je unaambukiza?
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom