Ujue Ugonjwa wa Malaria: Dalili, Madhara, Kinga, Tiba, Malaria kwa Wajawazito na Mpango wa Serikali katika kuzuia Malaria

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kama 'Plasmodium' ambavyo huenezwa na mbu jike aina ya Anofelesi.

Ugonjwa wa Malaria huenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine pale mbu mwenye vimelea vya malaria anapomuuma mtu mwingine na kuacha vimelea mwilini mwake.​

DALILI ZA MALARIA
Dalili za malaria zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni dalili za malaria kali na dalili za malaria isiyo kali​

1. Dalili za Malaria isiyo kali
  • Homa
  • Kuumwa Kichwa
  • Kuumwa viungo
  • Kichefuchefu/Kutapika
  • Kuhara/Kuumwa tumbo
  • Kutetemeka
  • Kutokwa jasho
  • Kukosa hamu ya kula
2. Dalili za Malaria Kali
  • Degedege - viungo vya mwili kukakamaa hasa kwa watoto wadogo
  • Weupe wa viganja unaotokana na upungufu wa damu
  • Kuchanganyikiwa
  • Kupoteza fahamu
  • Uchovu mkubwa kupita kiasi (Mgonjwa hawezi kukaa au kusimama bila kusaidiwa)
  • Kutapika kila kitu, kushindwa kunyonya (Kwa Watoto)
Ukubwa wa Tatizo
Pamoja na takwimu za utafiti kuonesha kupungua kwa maambukizi ya malaria hapa nchini, ugonjwa huu bado umeendelea kuwa tatizo kwa afya za wanajamii, maendeleo na ustawi wa Taifa. Takriban asilimia 94 ya Wazazi wote hapa nchini wanaishi kwenye maeneo ambayo yana maambukizi ya malaria kwa kipindi cha mwaka mzima.​

Madhara ya Ungonjwa wa Malaria
Ugonjwa wa malaria ni hatari kwa jamii nzima lakini zaidi kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. Madhara ya malaria ni pamoja na;​
  • Kusababisha kuugua na vifo hususani kwa matoto chini ya miaka mitano​
  • Upungufu wa damu hasa kwa wajawazito, kuharibika kwa mimba na wajawazito kujifungua watoto wenye uzito pungufu au njiti​
  • Kupunguza nguvu kazi ya Taifa pale watu wanaposhindwa kufanya kazi kwa kuugua au kuuguza​
  • Kupunguza mahudhurio ya Wanafunzi darasani​
  • Kutumia gharama kubwa katika matibabu (hasa pale mgonjwa anapolazwa) badala ya kutumia fedha hizo kwa maendeleo ya familia​
  • Matumizi makubwa ya Serikali katika manunuzi ya dawa na vifaa tiba​
1702366873846.png


KINGA DHIDI YA MALARIA
Kinga dhidi ya Ugonjwa wa Malaria ni muhimu ili kupunguza matukio ya ugonjwa na vifo vinavyotokana na Malaria. Afua (Interventions) za udhibiti wa Ugonjwa wa Malaria ni zenye ufanisi mkubwa endapo zitatumiwa vizuri kwa ufanisi uliokusudiwa.

Udhibiti wa Mtu Waenezao Malaria kwa Njia za Utangamano
Lengo Kuu la Udhibiti wa Mbu waenezao Malaria ni kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria na hivyo kupungua kwa idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na malaria. Udhibiti wa mbu wa malaria unatakiwa ufanyike kwa ufanisi na uwe endelevu.

Afua (Interventions) Kuu za Udhibiti wa Mbu Waenezao Malaria kwa Njia za Utangamano ni;
  • Matumizi ya Vyandarua vyenye dawa​
  • Upuliziaji wa viuatilifu ukoko kwenye kuta ndani ya nyumba​
  • Udhibiti wa mazalia ya mbu;​
    • Kuangamiza viluwiluwi vya mbu kwenye mazalia kwa kutumia viuadudu vya kibaolojia (Biolarviciding)​
    • Usimamizi wa mazingira kwa kuondoa mazalia ya mbu​
Mafanikio ya utekelezaji wa udhibiti wa mbu waenezao Malaria kwa njia za Utangamano yanatengemea ushirikiano imara na endelevu kati ya Wizara ya Afya na Wizara/Sekta nyingine kama vile TAMISEMI, Kilimo, Mifugo, Ujenzi, Elimu na Ushirikiano wa sekta binafsi pamoja na jamii kwa ujumla.

Ufanisi wa mkakati wa udhibiti wa Mbu waenezao Malaria kwa njia za Utungamano. Mkakati huu unajikita katika;​
  • Kuhakikisha upatikanaji wa vyanadarua vyenye dawa kwa watu wote walio katika maeneo mbalimbali yenye maambukizi na katika hatua zote za udhibiti​
  • Kuimarisha na kuongeza wigo wa upuliziaji wa viuatilifu ukoko ndani ya nyumba katika maeneo yenye maambukizi makubwa​
  • Kudhibiti mazalia ya mbu kwa kuangamiza viluwiluwi vya mbu hususani kutumia viuadudu vya kibaiolojia​
  • Kuhamasisha usimamizi wa mazingira katika jamii husika ili jamii ishiriki katika kuharibu mazalia ya mbu​
  • Kufanya tathmini ya mara kwa mara kuhusu udhibiti wa mbu kwa njia ya utangamano na kutumia mbinu mpya za kupambana na usugu wa mbu dhidi ya viuatilifu na mabadiliko ya tabia zake​
1702372907050.png
1702372945367.png


UCHUNGUZI, TIBA NA TIBA KINGA YA MALARIA
Hatua muhimu ya kwanza kwa jamii ni kutambua dalili za Malaria mapema na kuwahi kwenda katika Vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata huduma za uchunguzi na tiba sahihi ya Malaria.

Utoaji wa huduma kwa watu wenye dalili za Malaria hujikita katika upatikanaji wa huduma bora za vipimo na matibabu sahihi kwa wakati.

Uchunguzi wa Ugonjwa na Tiba Sahihi ya Malaria
Lengo Kuu la mkakati wa Uchunguzi na Tiba ya Malaria ni kuhakikisha kwamba dalili za Malaria zinatambuliwa na jamii mapema na matibabu sahihi yanapatikana kwa haraka. Aidha, wagonjwa wote wanaodhaniwa kuwa na malaria watapata huduma bora za utambuzi/vipimo ili kubaini uwepo wa vimelea vya malaria kabla ya kupatiwa dawa.

Kipengele cha Utoaji wa Huduma na Matibabu Sahihi ya Malaria kuna Afua za Kimkakati zifuatazo;​
  • Kutoa huduma bora za Uchunguzi wa vimelea vya Malaria zinazo wafikia watu wote​
  • Kutoa huduma bora za matibabu dhidi ya malaria kwa watu wote​
  • Kupunguza hatari ya maambukizi ya malaria katika makundi ambayo yanaathirika zaidi kwa kuwapa kipaumbele katika upatikanaji wa afua za kudhibiti malaria​
  • Kuwa na mipago mizuri ya uagizaji, ugomboaji, utunzaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba vya matibabu vyenye ubora​
  • Kupunguza athari za kuugua Malaria na vifo wakati wa matukio ya dharura​
Ufanisi wa mkakati wa Uchunguzi na Tiba ya Malaria. Malengo Mahsusi yafuatayo yakifikiwa yatawezesha kupata ufanisi wa Mkakati wa Uchunguzi na Tiba ya Malaria;​
  • Watu wote wenye dalili za malaria wataweza kupata huduma ya vipimo kwa wakati​
  • Watu wote waliothibitika kuwa na malaria watapatiwa matibabu sahihi kwa wakati​
  • Makundi ya watu ambayo yanaathirika zaidi na malaria kibailojia, kijamii na kiuchumi tayafikiwa kwa urahisi kupatiwa huduma za kupunguza maambukizi ya malaria na madhara yake​
  • Vifaa na vifaatiba vinavyotumika katika kinga na tiba dhidi ya malaria vibnapatikana wakati wote ana vitakuwa na ubora uliohakikiwa​
1702375365885.png


Pia Soma:

 
Ningeshauri Wizara ya Afya ifanye mpango wa magari ya kuulia mbu yawe yanazunguka mitaani kila baada ya wiki moja yaani kila jumapili kumwaga dawa mitaani haswa wakati wa usiku ili kusaidia kuuwa mbu na kuwasaidia Wananchi Wasiokuwa na vyandura vya kuweza kuwazuia mbu wasiweze kuwatafuna na kupatwa na maradhi ya Malaria. Jambo la pili Wizara Ya Afya ifanye mpango mkakati wa Dawa ya kuuwa vyanzo vya kuzaliana wadudu Mbu katika mabawa, mito na sehemu ya maji yaliyo tulia ili kuweza kutokomeza kuzaliana kwa wingi mbu.Kuliko Wizara Ya Afya kuzungumza tu katika mitandao pasipo na kufanya kwa vitendo halisi, haisaidii kitu . Ushauri wangu.
 
Back
Top Bottom