Ugonjwa wa Tetekuwanga (Chicken Pox): Maambukizi, dalili, madhara na tiba

Nimewahi ugua ni hatari sana, sikujua kama ni ugonjwa gani hadi mwanafunzi mwenzangu akaniambia niende hospitali unaumwa tetekuwanga.

Sikuingia darasani siku kadhaa maana nilikua na vidonda kichwani na sehemu zingine za mwili. Uzuri wake matibabu ni rahisi kupata.
 
Niliugua mwaka 2004 nikiwa first year UDSM. Ugonjwa noma sana ule, unatoka vipele kila sehemu ya mwili mpaka ulimi! Ila ukiishaugua unakuwa na kinga so huugui tena!
 
Daaah!. Nikikumbuka aiseee, ni 2010 nipo form5 term ya2 Dom Sec. Nilikaa ndani wiki mbili mfulizo na homa kali, nilikua napakwa machicha ya pombe ya kienyejia alikua anapika jirani yetu Msandawe pia nilikua nafukizwa na kunywa Muarobaini. Alama mpaka leo zipo mgongoni ila usoni hakuna sababu baada ya hapo nilituia cream mbali mbali hadi alama zikapote.
 
Nilikuwa sijawahi kuambukizwa hadi nilipomuona mdogo wangu anaumwa, nikawa nakaa nae nikijua umri umepita sitaumwa tena.

Cha ajabu ameniambukiza juzi baada ya kumaliza chuo
 
nimewahi ugua ni hatari sana, sikujua kama ni ugonjwa gani hadi mwanafunzi mwenzangu akaniambia niende hospitali unaumwa tetekuwanga.sikuingia darasani siku kadhaa maana nilikua na vidonda kichwani na sehemu zingine za mwili. Uzuri wake matibabu ni rahisi kupata.

Na Ukiugua Huji Kuugua Tena Maisha Yako Yote
 
Hii mikitu niliugua nikiwa na miaka mitano au sita niliambukizwa na watoto wa jirani...Nursery ndio ikawa hamna kwenda, nguo zote niliambiwa nisivae nikawa mtu wa kuvaa Shuka nyepesi... Dawa tuliyokuwa tunatumia ni nyeupe kama chokaa.. nakumbuka nilikuwa nakaa ghorofani nachungulia chini huku nimeshika Nondo za Dirisha watoto wenzangu wakicheza nilikuwa naona Dunia chungu.... Nikiona wakicheza TAMPO,Komborela,Sarakasi kwenye Mchanga, Mpira, Mbata, Kidari Po, Kuendesha Matairi na Fimbo, Magari ya Miti ndio ikawa Basi... sie kwetu ikawa ni kucheza Mchezo wa Nyoka Ludo,Monopoly,Karata, na Draft tu... ndio kipoozeo chetu
 
Nlikuwa katoto of 12 by then,nlifurahia tu kutoenda shule mana nlikaa kupakwa calamine lotion,
haikuwa severe navokumbuka,sina makovu
 
Mkuu Makovu Huwa Hayapotei Yale Yanakuwa Tokea Ndani Kwa Hiyo Huwa Hayatoki Sema Kadri Unavyokuwa Ndio Yanavyopungua


Me niliugua nikiwa first year chuoni enzi hizo.. sijabaki na kovu hata mojaaa...ila kuna rafiki yangu nilimuambukiza mpk leo ana vidoa usoni.

Tena mpaka naingia second year kovu hazipo..zilipotea kipindi cha mwaka huo huo mmoja
 
Mi bahati nzuri niliugua mwaka 2012 kwenye likizo ya chuo ya mwaka wa pili kuingia wa tatu nikiwa ubungo dsr.Aliniambukiza mdogo wangu, ila ajabu wazazi na mtoto wetu hawakupata.

Nilikua field, nakumbuka niliwaambukiza wafanyakaz na wanafunzi hadi nikaambiwa nikae hom had npone.

Ila bahati nzuri usoni haikufika ila kuanzia kifuani had chini kwenye pu...u vilikuwepo vipele na sasa makovu, ilikuwa shida had kutembea ilibidi nitembee kama nina busha.

Nilichekwaje.
 
Sikuwahi kuugua huo ugonjwa japokuwa wadogo zangu wote waliugua! Sielewi hata ilikuwaje.
 
Mi Nashkuru zilinipata mdogo nikiwa na 7 or 8 yrs. Alianza kaka yangu mkubwa. Nakumbuka tulikua tunashinda na khanga za shingo tu. Kheri uugue mdg kuliko zikikupata ukubwani.

Mana eti naskia lazim zikupate
 
Sikuwahi kuugua huo ugonjwa japokuwa wadogo zangu wote waliugua! Sielewi hata ilikuwaje.

Una bahati hukupata coz ukianza kwa mmoja lazima mwingine upate unless ushaupata lakini kama hujawahi ugua nasikia lazima uupate hata ukiwa mkubwa kuna friend yangu aliupata tukiwa third year.
 
Back
Top Bottom