Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

Status
Not open for further replies.

Ina maana huko Tanzania vyama vya Kisiasa vinajiingiza na Mambo ya Udini ndani yake? ikiwa ni chama cha Chadema ni chama cha Wakristo je CCM ni chama cha watu wenye Dini gani? Nauliza Swali nifunguwe macho Mkuu mkigoma

MziziMkavu CCM ni chama cha watanzania toka kikwete aingie madarakani amefanya mapinduzi mazuri sana ndani ya chama udini alioacha mkapa ameufutilia mbali ... chadema ni anti Muslims wala haitaki torch -

1) mzee mtei kupinga tume ya katiba akidai waislam wengi "islamophobia"

2)Mchungaji msingwa kusimama bungeni kuhoji kwanini mwezi wa ramadhan zanzibar watu hawali mchana "chuki waziwazi"

3) wana ushirikiano na chama cha kikristo cha ujerumani CDU .. kwney mkutano jangwani walikuwepo ...

... ETCL

hili la kufanyia mkutano bar tena mida ya iftar .. inaonesha walivyo wabinafsi ..
 
Lazima tukubalia makosa haya kama kweli imefanyika hivyo. Ni makosa makubwa kwa wtayarishaji ambao hawakutazama pande zote mbili na hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ambao hauwezi kupotea kichwani unapopanga hafla kubwa kama hii..
Wakati mwingine tuwe wadogo kukubali makosa badala ya kuonyesha jeuri wkaati makosa kweli yamefanyika, haiwezekkani kabisa mtu upange mkutano BAR halafu muda wa kufutur kisha kuna watu mnataka kutetea ujinga huu..
 
Naomba nisema yafuatayo:

1. Mtoa hoja alikuwa na hoja nzuri sana kama angeiweka kwa msingi ambao alitaka hasa kuusemea ambao naamini ni 'sensitivity'. Yaani, kuonesha kujali hisia na mahitaji ya wengine. Kwa wale ambao tumekulia kwenye mazingira ya Waislamu (wawe wengi au wachache haijalishi) mojawapo ya vitu ambavyo tumevizoea ni kuwa Mkristu akitaka kuchinja kuku au mnyama mwingine anatafuta Muislamu kuja kumchinjia. Sababu ni moja tu yaani kutaka mnyama yule ahalalishwe. Hii itaondoa uwezekano wa Muislamu kula haram. Sasa huwa inafanywa hivi hata kama walaji wanaotarajiwa ni Wakristu.

Bahati mbaya hili kwenye baadhi ya maeneo limeanza kutoweka kwa sababu ya udini wa watawala wetu. Kwamba sasa wapo Wakristu ambao hawajali kabisa kama mgeni anayekuja ni Muislamu au la yeye anachinja tu "akitaka kula ale asipotaka lwake". Huku ni kukosa hekima na kumjali "jirani yako". Binafsi naamini point ya mwandishi ilitakiwa kujikita kwenye hili.

2. Waandaaji wa mkutano huo kwa kutumia hekima walipaswa kufikiria hili na kuonesha sensitivity. Siyo tu kuhusiana na suala la ukumbi bali pia suala la muda. Kama lengo ni kuwakaribisha Watanzania wote wanaotaka kuunga mkono Chadema kwenye eneo hili basi swali la msingi lililotakiwa kujibiwa ni: Sehemu gani na muda gani ungefaa kuweza kuleta watu wengi zaidi? Na katika hilo bila ya shaka suala la mfumo wa Ramadhani lingekuwepo. Suala la Bar peke yake haliwahusu Waislamu tu. Wapo Wakristu ambao hawanywi na wanachukulia mazingira ya pombe kuwa ni mazingira ya dhambi. Hata hivyo kusema kitu kinafnayika "bar" tu haimaanishi moja kwa moja inafanyika kwenye ukumbi wa baa. Kama ukumbi unaomilikiwa na bar tu haufai (hata kama siyo ndani ya semu ya kunywea) tunaweza kuelezea vipi mikutano mbalimbali ambayo inafanyika hata leo hii sehemu mbalimbali ambazo ni mahoteli yenye baa? Je ukumbi kuwepo eneo la bar ni sababu tosha ya watu wenye pingamizi la kiimani kuweza kukataa? Mbona tayari tunaona mikutano na hata baadhi ya sehemu futari zimeandaliwa kwenye mahoteli ambayo twaweza kusema nayo yana baa?

Kitu pekee ambacho naamini ni tosha ni kama mkutano unafanyika kwenye ukumbi wa baa wenyewe. Katika mazingira hayo hoja ya 1 inasimama. Waandaji walipaswa kufikiria eneo ambalo ni neutral.

3. Mwandishi anapotoka sana (na anajipinga) kwa kudai kuwa eneo neutral ni lazima lisiwe la bar. Anasema (na kugundua makosa yake) kuwa "Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam."

Sasa hapa si tatizo kwa kweli kufanyia kwenye ukumbi wa msikiti. Ni tatizo kwa mtu ambaye anaona udini kwenye kila kitu. Kwa wale tunaoishi hapa maeneo ya Detroit tunafahamu mojawpo ya kumbi zinazotumiwa sana na Waafrika ni ule wa "St Mary Hall". Ni ukumbi wa kanisa lakini siyo kanisa. Watu wanalipia na kwenda kufanya burudani au shughuli mbalimbali pale. Wanaoshiriki ni watu wa dini na rangi mbalimbali. Hivyo hata kama wangeweza kufanyia kwenye ukumbi wa msikiti haina maana ni kuwatenga wasio Waislamu isipokuwa kama wale wanaoenda kwenye ukumbi wa msikiti wanatakiwa kwanza kusema Shahda na kuswali kwanza! Hapo utakuwa ni ubaguzi. Sidhani kama hilo linafanyika.

4. Si vyema hata kidogo kuangalia kila kitu kwa msingi wa "sisi against wao". Kwamba likifanywa jambo na kiongozi Mkristu basi ni lazima liwe ni udini na likifanywa na Muislamu basi pia ni udini. Katika yote niliyosoma hapo juu hakuna kitu chochote kilichowekwa wazi kuwa uamuzi wa kufanyia mkutano huko ulifanywa kwa ajili ya kuwatenda Waislamu. Ninachoona mimi ni kukosekana kwa hekima na sensitivity tu. Mtu yeyote angeweza kufuatilia na kujua kwanini hawakutafuta ukumbi mwingine na kuleta hoja hizi pale pale kwa uongozi unaoandaa na kusikia majibu yao. Nina uhakika kuchagua ukumbi huo kulikuwa na sababu na kama haikuwa sababu ya kutosha basi wanachama na mashabiki wangeweza kufikiria namna ya kufanya bila kusababisha kikwazo kwa mtu yeyote.

5. Pamoja na yote hapo juu 1-4 bado uamuzi ulitakiwa kufanyika na mahali pa mkutano kuchaguliwa. NI dhahiri kuwa siyo wakati wote mtu anaweza kuridhisha watu wote kwa kiwango sawasawa. Ni jukumu la kiongozi au viongozi wakati wote kuwa na akili ya kufikiria matokeo ya maamuzi yao na kupunguza hisia hasi za matokeo hayo. Je kulikuwa na ulazima wa kufanya mkutano huo mahali hapo na muda huo? Je kulikuwa na uchaguzi mwingine wowote ambao waandaji hawakuuangalia? Kama uamuzi wa kufanya mkutano huo mahali hapo haukujali kabisa suala la muda na mfungo wa Ramadhani na hivyo ulifanywa kiholela (arbitrarirly) basi waandaji wanapaswa kuwaomba Watanzania wengine msamaha. Jamani juzi baada ya Gabby Douglas kufanya vizuri NBC ilirusha tangazo la biashara likionesha nyani akicheza gymnastics na watu wakaona kuwa haikuwa sensitive na kulazimisha NBC kuomba radhi. Wakati mwingine maamuzi ambayo hayana hatia yanaonekana kuwa ni ya makosa.

6. Pamoja na yote hayo naamini kosa kubwa zaidi la mwandishi na ni la makusudi ni kumwandikia Dr. Slaa "kama mtendaji" mkuu na kuleta tuhuma za udini wa CDM kuhusiana na suala la London. Kwa wale tunaofuatilia kwa karibu masuala haya tunaweza kuona jaribio jingine la kutaka kumfanya Dr. Slaa aonekane kama ndiye aliyebariki uamuzi huu na kwa vile wapo ambao wamekuwa wakieneza tuhuma za udini wa CDM basi ionekane Dr. Slaa ndiye anawajibika. Lakini zaidi tunatambua kuwa lipo kundi la watu ambao wanamchukia Dr. Slaa kwa sababu aliwahi kuwa Padre na alitaka kugombea Urais na hivyo kuonekana kama Ukristu wake ni tatizo na hivyo hata hili lihusishwe naye.

Mwandishi anasema hivi: "Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam. muda ulipo wa masaa haya saba unatosha au si vibaya hata kulifanya zoezi hili kwa weekend." Sasa kwa vile mkutano haukuhamishwa na umefanyika ulipopangwa ni Dr. Slaa ambaye watu hawa watambebesha mzigo huu wakitaka ionekane kuwa "licha ya kumwandikia Dr. Slaa na viongozi wengine" lakini CDM walifanya mkutano wao kwenye bar tena muda wa kufuturu wakionesha kutokujali hisia za Waislamu!

Ninaamini suala hili lingeweza kushughulikiwa na viongozi wa huko Uingereza ambao waliamua kuanzisha tawi la CDM hapo. Huyo aliyeandika barua alihitaji kuandika barua kwa viongozi hao wa CDM huko na siyo Dr. Slaa. Na zaidi kama kweli angetaka mwitiko wa mara moja angeweza kumtafuta Bw. Lema ambaye alitakiwa kufungua tawi hilo na kumueleza hisia zao ili ahamasishe kuhamisha eneo la mkutano. Hili halikuwa suala la Dr. Slaa. Kama tutakubali Dr. Slaa kuingilia kila kitu kinachofanyika kwenye kila tawi (ndani na nje ya nchi) na kuwa mambo madogo kama uamuzi wa wapi kikao kifanyike tutakuwa siyo tu tunashusha hadhi yake lakini zaidi tutakuwa tunawadhalilisha viongozi wa chini wa chama! Iweje Katibu Mkuu wa Chama kinachojiandaa kutawala ahangaike kuamua mkutano wa tawi ufanyike wapi?

Kimsingi barua hii haikupaswa kuandikwa wala kutumwa kwa mtu yeyote. Waliokuwa na manung'uniko (kwa msingi wowote ule) walipaswa kuyamaliza kwa kuzungumza na waandaaji. Hili halikuwa jambo kubwa la kuandika barua makao makuu na kutuma hadi kwa balozi na bloggers mbalimbali. Barua inaonesha tu udhaifu wa baadhi ya watu kuweza kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo isipokuwa kwa kuanzisha shari.

MMM
 
Mwanakijiji,

Naomba kutofautiana na wewe ktk hili. Labda nitangulize kusema makosa nayoyaona ni kuwepo kwa waraka huu hapa JF wakati ni ombi ambalo limepelekwa kabla ya janga halijatokea. Kama ingefanyika hivyo na barua hii ingeonyesha malalamiko ya maandalizi kwa wale walioshindwa kwenda ningeelewa lakini sii Kabla.. Makosa yamefanya na watu ambao sii wanaChadema isipokuwa wapenzi wa Chadema kama huyu jamaa yetu.

Kuhusu BARA mkuu wangu swala hili usilifananishe na Waislaam ktk mfungo wa ramadhan kwa sababu huu ni wakati wa kuyashindwa majaribo na haikuanza na Muhammad bali Nabii Issa AS (YESU) nasi tunafuata kwa maagizo yake kwamba asiyefunga sii rahisi kuiona pepo. Kwa hiyo hata wewe mwenye kuamini Ukristu wa kweli unatakiwa kufunga, japokuwa mambo haya yalikuja geuzwa baadaye na kuonekana sii lazima kihivyo..

Na sababu kubwa ni utukufu wake kiimani ktk kumshinda sheitan, yaani yale matamanio yote ya dunia unajaribu kushindana nayo kiroho hivyo kuingia Bar inayouza Pombe wakati wa Ramadhan inaweza kutokea ukashindwa kuvumilia ukiona zile bubble za rangi ya gold zikipanda juu ya povu zito jeupeee!. Kwa hiyo waelewe jamaa zako wako ktk mtihani mkubwa wakati huu japokuwa sii lazima kwako..
 
Nashauri tu na Ikulu kiundwe kitengo cha mshauri wa mambo ya Kiislamu, maana inaonekana nchi hii unapopanga jambo lolote ukimamliza inabidi sasa umpate sasa Islamic adviser akushauri kabla ya kuamuwa.
Ila akitokea Mkristo kuhoji zile pesa za Ikulu kufuturisha watu kila siku zinatoka kwenye mfuko gani basi hapo wewe utaitwa mdini?

Mleta mada si Mwanachadema bali ni MwanaCUF for sure na hawa ndio waliotusababishia Tanzania kufutiwa Entry Viza na UK kwa kujifanya wakimbizi wa CUF. hawa wamejaa UK na ni fitina tu zilizowajaa, wewe utashindwaje kuwasiliana na kiongozi ambaye yupo London halafu upate muda wa kuwatumia email blogers na Dr Slaa? huyu ni pimbi tu.
 
Too much from this society world wide hata sijui tatizo ni nini!!?? Haya soma hapa uone:

Spreading The Truth Of Islam wrote:

They are competing in the Olympics for Gold;
We are competing in Ramadaan for Paradise.

The world is watching them;
Allah is watching us..
 
Mimi nilifikiri mwezi mtukufu ni pamoja na kupunguza UNAFIKI kama sio kuacha kabisa, Kwanini unaona ya CDM kufanya mkutano wao Bar lakini huoni ya Serkali yako kuwaruhusu dada zako kuogelea nusu uchi huku wakiangaliwa duniani kote tena mwezi huu huu wa Ramadhani! ama kweli MNAFIKI hawezi kuiona PEPO... yaani hilo la mkutano bar limekukera saaaaaana mpaka umepoteza muda wako (MAPOVU YANAKUTOKA) kuandika PUMBA eti Lema alivuliwa Ubunge kwasababu ya ubaguzi wa kidini kule Arusha... that's b...l sh!!!t and ****. next time u better F***k your sh...t up! Kwassisi Watanzania tulio huku ambao hatujawahi kufika huko tulifikiri mtu ukiwa ulaya basi Umbeya, Unafiki na Majungu unaviacha kumbe bado mnaendeleza hata huko!!!! a bit shock!
 
Mwanakijiji

Hebu tueleweshe vizuri, ni kuwa

1. waandaaji mkutano inawezekana walizingatia Ramadhan na muda wa iftar lakini maamuzi yao yameoneka kuwa na makosa kinyume na dhamira njema

2. Waandaji labda wanaweza kuwa na kosa la ukosefu wa hekima kutozingatia "sensitivity" kwa Waislam na Ramadhan yao

3. Muandishi wa barua ana makosa mengi ila kosa kubwa na la kusudi ni kumwamdikia Dr.Slaa

Yaani hao waandaaji unawapa benefit of doubt lakini mwandishi umejua moja kwa moja kuwa kafanya kosa la kusudi!!
Hakuna hata mjadala kuwa amekosea kibinaadamu, ni kusudi.

Hii double standard unaweza kuitolea maelezo?
 
Mwanakijiji

Hebu tueleweshe vizuri, ni kuwa

1. waandaaji mkutano inawezekana walizingatia Ramadhan na muda wa iftar lakini maamuzi yao yameoneka kuwa na makosa kinyume na dhamira njema

2. Waandaji labda wanaweza kuwa na kosa la ukosefu wa hekima kutozingatia "sensitivity" kwa Waislam na Ramadhan yao

3. Muandishi wa barua ana makosa mengi ila kosa kubwa na la kusudi ni kumwamdikia Dr.Slaa

Yaani hao waandaaji unawapa benefit of doubt lakini mwandishi umejua moja kwa moja kuwa kafanya kosa la kusudi!!
Hakuna hata mjadala kuwa amekosea kibinaadamu, ni kusudi.

Hii double standard unaweza kuitolea maelezo?
Spreading The Truth Of Islam wrote:

They are competing in the Olympics for Gold;
We are competing in Ramadaan for Paradise.

The world is watching them;
Allah is watching us..
 
...Kama haiwahusu mnawashwa nn au mnataka kujipeleka ili mfanye nini !! Mnajulikana nyie wanafik tu hamna lolote....subirini mkutano na magamba au akija yule mnafik mwingine Hamad mtaitwa hotelini na mtapewa na vyumba vya kulala kabisa alivyolipia Kameron !! Na ni ushamba tuu, kwani pubs ni baa tuu hakuna zenye sehemu ya kula au hata conference rooms ?

Unataka usababishie watu ban,huna tofauti na wabunge wa bunge la jioni,ndo maana unafurahia event ya grocery,lema aangalie asifanywe kama ulimboka si unajua mambo ya bar.
 
Ndugu Zangu kujiamini ni kitu cha msingi sana utaona watu wasio na uwezo wa kujibu hoja wanavyokurupuka na maneno ya kukejeli badala ya kuandika vitu vya msingi.

Ieleweke waislam ndio waliosimama kidete kugombea uhuru wa nchi hii, kihistoria imefichwa ila inajulikana wazi ndio watu waliokuwa na ujasiri wakisaidiana na Mwalimu JK.

Ieleweke kwa miaka sasa waislam wamekuwa wanapigania haki zao ambazo imani zingine wamekuwa wakizibeza....sasa basi CHADEMA Inatakiwa ikae chini na iwafikirie waislam mapema maana hao ndio wapambanaji wa kweli.

Najua imani nyingine zina mapungufu na hazipo tayari kuambiwa ukweli ila hilo tusiliweke sana kisiasa.....M4C bila waislam nchi hii mtaisikia.

" Historia imefichwa waislamu ndo waliopigania uhuru" So what? Jamani mwezi wa toba huu tupunguze unafiki najua hatuwezi kuacha uko kwenye damu..
 
Spreading The Truth Of Islam wrote:

They are competing in the Olympics for Gold;
We are competing in Ramadaan for Paradise.

The world is watching them;
Allah is watching us..

Huyo Spreading The Truth Of Islam ni nani?
 
Lazima tukubalia makosa haya kama kweli imefanyika hivyo. Ni makosa makubwa kwa wtayarishaji ambao hawakutazama pande zote mbili na hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ambao hauwezi kupotea kichwani unapopanga hafla kubwa kama hii..
Wakati mwingine tuwe wadogo kukubali makosa badala ya kuonyesha jeuri wkaati makosa kweli yamefanyika, haiwezekkani kabisa mtu upange mkutano BAR halafu muda wa kufutur kisha kuna watu mnataka kutetea ujinga huu..

Mkandara,

..hao ni wa-Znz wanaotaka kuwaletea vurugu tu CDM.

..tuache kudanyana kwamba ipo siku CDM watakuwa na support ya wa-ZNZ.

..kama suala la Ramadhani halikuwa considered, maana yake ni kwamba kwenye kamati ya maandalizi hakukuwa na Muislamu aliye-raise objection ya shughuli hiyo kufanyika kwenye baa, na kabla ya watu kufuturu.

..pia suala la baa au POMBE siyo kitu haramu kwa jamii mbalimbali za watu wa bara. tena kuna jamii huku bara huwezi kufanya jambo lolote lile kubwa bila kuhusisha POMBE.

..binafsi sidhani kama Muislamu analazimika kwenda kwenye shughuli ya CDM na kuvuruga taratibu zake wakati wa mfungo wa Ramadhani.

..CDM itakuwepo hata baada ya mfungo wa Ramadhani, na wakati huo hakutakuwa na kitu chochote kile cha kuwakwaza Waislamu kushiriki shughuli za ufunguzi wa matawi.
 
MziziMkavu CCM ni chama cha watanzania toka kikwete aingie madarakani amefanya mapinduzi mazuri sana ndani ya chama udini alioacha mkapa ameufutilia mbali ... chadema ni anti Muslims wala haitaki torch -

1) mzee mtei kupinga tume ya katiba akidai waislam wengi "islamophobia"

2)Mchungaji msingwa kusimama bungeni kuhoji kwanini mwezi wa ramadhan zanzibar watu hawali mchana "chuki waziwazi"

3) wana ushirikiano na chama cha kikristo cha ujerumani CDU .. kwney mkutano jangwani walikuwepo ...

... ETCL

hili la kufanyia mkutano bar tena mida ya iftar .. inaonesha walivyo wabinafsi ..

Kwakuwa CDM wanashirikiana na chama cha CDU moja kwa moja kinakuwa nichakidini... this is another ****!
Mwezi wa TOBA tupunguze unafiki na majungu.
 
Mkandara,

..hao ni wa-Znz wanaotaka kuwaletea vurugu tu CDM.

..tuache kudanyana kwamba ipo siku CDM watakuwa na support ya wa-ZNZ.

..kama suala la Ramadhani halikuwa considered, maana yake ni kwamba kwenye kamati ya maandalizi hakukuwa na Muislamu aliye-raise objection ya shughuli hiyo kufanyika kwenye baa, na kabla ya watu kufuturu.

..pia suala la baa au POMBE siyo kitu haramu kwa jamii mbalimbali za watu wa bara. tena kuna jamii huku bara huwezi kufanya jambo lolote lile kubwa bila kuhusisha POMBE.

..binafsi sidhani kama Muislamu analazimika kwenda kwenye shughuli ya CDM na kuvuruga taratibu zake wakati wa mfungo wa Ramadhani.

..CDM itakuwepo hata baada ya mfungo wa Ramadhani, na wakati huo hakutakuwa na kitu chochote kile cha kuwakwaza Waislamu kushiriki shughuli za ufunguzi wa matawi.

Kwanza walifanikiwa kutuharibia kwa Serikali ya UK na tukafutiwa Entry Viza, sasa na masuala ya Watanganyika wanataka kutuingilia wakati wao wana nchi yao na hawahitaji Muungano, hao ni wanafki watupu hakuna anayefunga hapo bali wanashinda na njaa tu. Phweeeeeeeeeeeeeew!!
 
Kwakuwa CDM wanashirikiana na chama cha CDU moja kwa moja kinakuwa nichakidini... this is another ****!
Mwezi wa TOBA tupunguze unafiki na majungu.
Wakimaliza single hiyo ikianza kuchuja utawasikia Vatican ni nchi ya kanisa, halafu wanasahau kwamba Iran, Saudi Arabia na Pakistan zote hizi ni Jamhuri za Kiislamu na zote zina balozi zao hapa Tanzania, lakini Ubalozi wa Vatican ndio unaonekana tatizo. This people puuuuuuuuuuuuuhhhhh!!!
 
Kwanza walifanikiwa kutuharibia kwa Serikali ya UK na tukafutiwa Entry Viza, sasa na masuala ya Watanganyika wanataka kutuingilia wakati wao wana nchi yao na hawahitaji Muungano, hao ni wanafki watupu hakuna anayefunga hapo bali wanashinda na njaa tu. Phweeeeeeeeeeeeeew!!

Matola,

..CDM wangeamua kufanya shughuli yao kwenye ukumbi wa kanisa kungekuwa na kelele kubwa zaidi.

..lakini mwandishi anapendekeza CDM wakakodi ukumbi wa msikiti, kwasababu hiyo ni sehemu "neutral."

..kwa watu hawa hakuna jema linaloweza kufanywa na CDM. wangekuwa wanaipenda CDM kwa dhati basi wangekuwepo ktk kamati ya maandalizi, na mapendekezo yao yangefanyiwa kazi.

NB:

..huu ni mwezi MTUKUFU kwa ndugu zetu WAISLAMU, sasa siyo vizuri kudai kwamba wanashinda njaa.
 
Matola,

..CDM wangeamua kufanya shughuli yao kwenye ukumbi wa kanisa kungekuwa na kelele kubwa zaidi.

..lakini mwandishi anapendekeza CDM wakakodi ukumbi wa msikiti, kwasababu hiyo ni sehemu "neutral."

..kwa watu hawa hakuna jema linaloweza kufanywa na CDM. wangekuwa wanaipenda CDM kwa dhati basi wangekuwepo ktk kamati ya maandalizi, na mapendekezo yao yangefanyiwa kazi.

NB:

..huu ni mwezi MTUKUFU kwa ndugu zetu WAISLAMU, sasa siyo vizuri kudai kwamba wanashinda njaa
.

Haya maneno na ya simame kama yalivyo, kuna ndugu zetu wengi wa Kiislamu wanashinda njaa tu pengine bila wao wenyewe kujuwa. Funga na mnafki ni vitu viwili tofauti. wapo wanaofunga na funga yao inapokelewa kwa Mungu, lakini wanafki waongo na wafitini hawa bora wawe wanakula tu maana wanashinda njaa hakuna funga yoyote.
 
Lazima tukubalia makosa haya kama kweli imefanyika hivyo. Ni makosa makubwa kwa wtayarishaji ambao hawakutazama pande zote mbili na hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ambao hauwezi kupotea kichwani unapopanga hafla kubwa kama hii..
Wakati mwingine tuwe wadogo kukubali makosa badala ya kuonyesha jeuri wkaati makosa kweli yamefanyika, haiwezekkani kabisa mtu upange mkutano BAR halafu muda wa kufutur kisha kuna watu mnataka kutetea ujinga huu..

Kimsingi hii ilikua ni big mistake ktk swala zima la kiufundi na limetriger vitu vingi sana kwa uchache kabisa ni wasiwasi wa Chadema kuongoza nchi kwa uadilifu. Kuna vitu ambavyo vinawezekana njia moja tu, umeshafanya makosa kubali na jaribu kurekibisha makosa na baadae uombe msamaha. Kimsingi kama Chadema watashindwa kuandaa mkutano mwengine ambao utawajumuisha wananchi wote watakosea sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom