Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

Status
Not open for further replies.
Kwa kuwa kasema ni waislamu nilidhani kutakuwa walau na waislamu wawili watatu hata kwa majina
pili Lema amealikwa na si mwandaaji wa shughuli hii, anasema hawezi ongea naye je huu si ubaguzi?
anakisifia CUF ila amesahau vitendo vya ubaguzi anavyofanya Jsa kwa wakristo
Tatu kama barua inaenda Chadema ni kwa nini awacopy watu wasi chadema? wote tunajua Michuzi ni mwanachama wa ccm iweje ampe nakala ya barua hii?
Hivi ukikodi ukumbi katika bar unamaanisha watu walewe pombe? Ni mara ngapi walokole na wasabato wanafanya harusi zao bar bila kuwepo pombe?
Nadhani haya yote yameandaliwa na akina Nape, tena kwa vile wana ufinyu mdogo wa kuelewa wameshindwa kuutengeneza uongo wao vizuri
lakini pia hilo tangazo limewekwa siku nyingi alikua wapi kupeleka malalamiko yake kabla
HUU NI UNAFIKI
 
Kwa hiyo mnataka kusema hafla hii imeandaliwa makusudi kwenye Bar na mwezi wa Ramadhan, muda wa kufutur kwa sababu Chadema inawaalika Wakristu tu?.. maana sielewi watu mnabishana nini hapa. Mijitu mnatetea vitu ambavyo viko wazi kabisa?.. Mwandiushi kasema karibu na msikiti wao kuna Ukumbi ambao unagharimu kidogo kabisa.. Nimekaa East London kuna wabongo Mmojawapo ni Pailonga (Abubakr) ana duka lake la nguo pale East London, tena wengine watu wangu kwa kuipenda Chadema leo mnakuja na utetezi usiokuwa na kichwa.

Alichokisema mwandishi ni ushauri wake yeye kama mpenzi tu wa chama lakini isiwe sababu kabisa ya kuhalalisha mkutano huo muhimu kwa kuwavuta wanachama wapya ufanyike BAR na mwezi mtukufu wa Ramadhan tena saa za futur..Hii ni sawa na maneno ya Mwanakijiji, yaani mkristu ananyonga mnyama kwa maandalizi ya chakula, halafu anasema hata kama tungechinja ingeleta matatizo mengine kwa waislaam maana walalamishi.. kwa nini mlimnyonga? huwana jibu ila kwa nini hamkushiriki Kwani mliwaalika kushiriki maandalizi wakakataa?..
- A very stupid move waandalizi wamelifanya na UPUMBAVU zaidi kulitetea..Mtanisamehe kwa lugha - but I said so na imewafikia..
 
Udini Hauna Nafasi!! Tuwasamehe Waleta Hoja hawajui watendalo!! Imani na Matendo yako ndio Yatakufikisha kwa Muumba!! Ni sio Haya mambo ya Kupita!!
 
Naomba nisema yafuatayo:

1. Mtoa hoja alikuwa na hoja nzuri sana kama angeiweka kwa msingi ambao alitaka hasa kuusemea ambao naamini ni 'sensitivity'. Yaani, kuonesha kujali hisia na mahitaji ya wengine. Kwa wale ambao tumekulia kwenye mazingira ya Waislamu (wawe wengi au wachache haijalishi) mojawapo ya vitu ambavyo tumevizoea ni kuwa Mkristu akitaka kuchinja kuku au mnyama mwingine anatafuta Muislamu kuja kumchinjia. Sababu ni moja tu yaani kutaka mnyama yule ahalalishwe. Hii itaondoa uwezekano wa Muislamu kula haram. Sasa huwa inafanywa hivi hata kama walaji wanaotarajiwa ni Wakristu.

Bahati mbaya hili kwenye baadhi ya maeneo limeanza kutoweka kwa sababu ya udini wa watawala wetu. Kwamba sasa wapo Wakristu ambao hawajali kabisa kama mgeni anayekuja ni Muislamu au la yeye anachinja tu "akitaka kula ale asipotaka lwake". Huku ni kukosa hekima na kumjali "jirani yako". Binafsi naamini point ya mwandishi ilitakiwa kujikita kwenye hili.

2. Waandaaji wa mkutano huo kwa kutumia hekima walipaswa kufikiria hili na kuonesha sensitivity. Siyo tu kuhusiana na suala la ukumbi bali pia suala la muda. Kama lengo ni kuwakaribisha Watanzania wote wanaotaka kuunga mkono Chadema kwenye eneo hili basi swali la msingi lililotakiwa kujibiwa ni: Sehemu gani na muda gani ungefaa kuweza kuleta watu wengi zaidi? Na katika hilo bila ya shaka suala la mfumo wa Ramadhani lingekuwepo. Suala la Bar peke yake haliwahusu Waislamu tu. Wapo Wakristu ambao hawanywi na wanachukulia mazingira ya pombe kuwa ni mazingira ya dhambi. Hata hivyo kusema kitu kinafnayika "bar" tu haimaanishi moja kwa moja inafanyika kwenye ukumbi wa baa. Kama ukumbi unaomilikiwa na bar tu haufai (hata kama siyo ndani ya semu ya kunywea) tunaweza kuelezea vipi mikutano mbalimbali ambayo inafanyika hata leo hii sehemu mbalimbali ambazo ni mahoteli yenye baa? Je ukumbi kuwepo eneo la bar ni sababu tosha ya watu wenye pingamizi la kiimani kuweza kukataa? Mbona tayari tunaona mikutano na hata baadhi ya sehemu futari zimeandaliwa kwenye mahoteli ambayo twaweza kusema nayo yana baa?

Kitu pekee ambacho naamini ni tosha ni kama mkutano unafanyika kwenye ukumbi wa baa wenyewe. Katika mazingira hayo hoja ya 1 inasimama. Waandaji walipaswa kufikiria eneo ambalo ni neutral.

3. Mwandishi anapotoka sana (na anajipinga) kwa kudai kuwa eneo neutral ni lazima lisiwe la bar. Anasema (na kugundua makosa yake) kuwa "Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam."

Sasa hapa si tatizo kwa kweli kufanyia kwenye ukumbi wa msikiti. Ni tatizo kwa mtu ambaye anaona udini kwenye kila kitu. Kwa wale tunaoishi hapa maeneo ya Detroit tunafahamu mojawpo ya kumbi zinazotumiwa sana na Waafrika ni ule wa "St Mary Hall". Ni ukumbi wa kanisa lakini siyo kanisa. Watu wanalipia na kwenda kufanya burudani au shughuli mbalimbali pale. Wanaoshiriki ni watu wa dini na rangi mbalimbali. Hivyo hata kama wangeweza kufanyia kwenye ukumbi wa msikiti haina maana ni kuwatenga wasio Waislamu isipokuwa kama wale wanaoenda kwenye ukumbi wa msikiti wanatakiwa kwanza kusema Shahda na kuswali kwanza! Hapo utakuwa ni ubaguzi. Sidhani kama hilo linafanyika.

4. Si vyema hata kidogo kuangalia kila kitu kwa msingi wa "sisi against wao". Kwamba likifanywa jambo na kiongozi Mkristu basi ni lazima liwe ni udini na likifanywa na Muislamu basi pia ni udini. Katika yote niliyosoma hapo juu hakuna kitu chochote kilichowekwa wazi kuwa uamuzi wa kufanyia mkutano huko ulifanywa kwa ajili ya kuwatenda Waislamu. Ninachoona mimi ni kukosekana kwa hekima na sensitivity tu. Mtu yeyote angeweza kufuatilia na kujua kwanini hawakutafuta ukumbi mwingine na kuleta hoja hizi pale pale kwa uongozi unaoandaa na kusikia majibu yao. Nina uhakika kuchagua ukumbi huo kulikuwa na sababu na kama haikuwa sababu ya kutosha basi wanachama na mashabiki wangeweza kufikiria namna ya kufanya bila kusababisha kikwazo kwa mtu yeyote.

5. Pamoja na yote hapo juu 1-4 bado uamuzi ulitakiwa kufanyika na mahali pa mkutano kuchaguliwa. NI dhahiri kuwa siyo wakati wote mtu anaweza kuridhisha watu wote kwa kiwango sawasawa. Ni jukumu la kiongozi au viongozi wakati wote kuwa na akili ya kufikiria matokeo ya maamuzi yao na kupunguza hisia hasi za matokeo hayo. Je kulikuwa na ulazima wa kufanya mkutano huo mahali hapo na muda huo? Je kulikuwa na uchaguzi mwingine wowote ambao waandaji hawakuuangalia? Kama uamuzi wa kufanya mkutano huo mahali hapo haukujali kabisa suala la muda na mfungo wa Ramadhani na hivyo ulifanywa kiholela (arbitrarirly) basi waandaji wanapaswa kuwaomba Watanzania wengine msamaha. Jamani juzi baada ya Gabby Douglas kufanya vizuri NBC ilirusha tangazo la biashara likionesha nyani akicheza gymnastics na watu wakaona kuwa haikuwa sensitive na kulazimisha NBC kuomba radhi. Wakati mwingine maamuzi ambayo hayana hatia yanaonekana kuwa ni ya makosa.

6. Pamoja na yote hayo naamini kosa kubwa zaidi la mwandishi na ni la makusudi ni kumwandikia Dr. Slaa "kama mtendaji" mkuu na kuleta tuhuma za udini wa CDM kuhusiana na suala la London. Kwa wale tunaofuatilia kwa karibu masuala haya tunaweza kuona jaribio jingine la kutaka kumfanya Dr. Slaa aonekane kama ndiye aliyebariki uamuzi huu na kwa vile wapo ambao wamekuwa wakieneza tuhuma za udini wa CDM basi ionekane Dr. Slaa ndiye anawajibika. Lakini zaidi tunatambua kuwa lipo kundi la watu ambao wanamchukia Dr. Slaa kwa sababu aliwahi kuwa Padre na alitaka kugombea Urais na hivyo kuonekana kama Ukristu wake ni tatizo na hivyo hata hili lihusishwe naye.

Mwandishi anasema hivi: "Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam. muda ulipo wa masaa haya saba unatosha au si vibaya hata kulifanya zoezi hili kwa weekend." Sasa kwa vile mkutano haukuhamishwa na umefanyika ulipopangwa ni Dr. Slaa ambaye watu hawa watambebesha mzigo huu wakitaka ionekane kuwa "licha ya kumwandikia Dr. Slaa na viongozi wengine" lakini CDM walifanya mkutano wao kwenye bar tena muda wa kufuturu wakionesha kutokujali hisia za Waislamu!

Ninaamini suala hili lingeweza kushughulikiwa na viongozi wa huko Uingereza ambao waliamua kuanzisha tawi la CDM hapo. Huyo aliyeandika barua alihitaji kuandika barua kwa viongozi hao wa CDM huko na siyo Dr. Slaa. Na zaidi kama kweli angetaka mwitiko wa mara moja angeweza kumtafuta Bw. Lema ambaye alitakiwa kufungua tawi hilo na kumueleza hisia zao ili ahamasishe kuhamisha eneo la mkutano. Hili halikuwa suala la Dr. Slaa. Kama tutakubali Dr. Slaa kuingilia kila kitu kinachofanyika kwenye kila tawi (ndani na nje ya nchi) na kuwa mambo madogo kama uamuzi wa wapi kikao kifanyike tutakuwa siyo tu tunashusha hadhi yake lakini zaidi tutakuwa tunawadhalilisha viongozi wa chini wa chama! Iweje Katibu Mkuu wa Chama kinachojiandaa kutawala ahangaike kuamua mkutano wa tawi ufanyike wapi?

Kimsingi barua hii haikupaswa kuandikwa wala kutumwa kwa mtu yeyote. Waliokuwa na manung'uniko (kwa msingi wowote ule) walipaswa kuyamaliza kwa kuzungumza na waandaaji. Hili halikuwa jambo kubwa la kuandika barua makao makuu na kutuma hadi kwa balozi na bloggers mbalimbali. Barua inaonesha tu udhaifu wa baadhi ya watu kuweza kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo isipokuwa kwa kuanzisha shari.

MMM

Baada ya kupitia michango mingi iliyotolewa na wadu mbali mbali hasa yale majibu aliyotoa mwanakijiji akionesha kutetea kitendo hiki na kuigeuza tafsiri yake na kufanya lionekana juwa ni mpango wa watu fulani wa chama funani hasa CCM wanaoshirikiana na wengine katika CUF na Hasa Chadema katika ku-propagate dhana ya udini na kuipigia upatu katika vichwa vya walio wengi katika kizazi cha sasa.

Kwa mtazamo wangu ni kuwa mwanakijiji hakufikri sawasawa katika hili wala hakuandika akiwa balanced kwani katika aliyoyaandika yamebeba alot of double standards descriptions on the particular subject; Nitaeleza kwa kuchambua kila aya aliypoiandika na kubainisha upotofu uliopo kwa kila aya kwa hoja zilizo bayana;

1) Katika aya ya kwanza mwanakijiji anaanza moja kwa moja na kumjadili mtoa mada na kuacha msingi wa alichokiandika, mwanakijiji ametoa msingi mbovu wa hoja zake ambazo zinashindwa kujipambanua katika vichwa vya watu wanaowaza sawasawa. Ameelezea kwa uchache mazingira ya ushirikiano na kulindiana heshima na imani baina ya watu wa dini tofauti wanaopatikana Tanzania lakini mwanakijiji amepotea pale alipotaja na kudai kuwa mabadiliko hasi ya kuondoka ustaarabu wa kutunziana heshima na kuthamini imani ya wengine imesababishwa na Udini wa watawala. na kudai kuwa wakristo sasa kutokana na udini huo wa watawala wamekata shauri kuwa hakuna haja ya kuendeleza ustaarabu na heshima kwa dini ya wengine katika kuchinja na kula. Tuhuma hii inataka kuonyesha kuwa wapo waislamu katika utawala ambao wamewakandamiza wakristo kiasi cha wakristo kukata shauri juu ya kuendeleza heshima na utii walionao kwa kufuata uhalali wa chakula wanachokula pamoja na waislamu. Katika hili mwanakijiji amepotoka, hakufikiri sawasawa.

2) katika aya hii mwanakijiji anaonekana kukubali matokeo na kupinga kile kiletacho mabadiliko hayo, mwanakijiji amekubali kuwa sehemu ya vilevi si barabara kwa waislamu hasa kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu lakini anajikanganya pale anapodai kuwa ikiwa bar inayosehemu ambayo haiuzi vinywaji ni sawa kwa waislamu kuhudhuria, nasema hapana, hata kama sehemu ambayo mkutano huo umefanyika haikuwa ikiuzwa pombe lakini bado kama bar ipo sehemu nyingine ambapo bar inafanya kazi kama kawaida hili pia si sawa kwa waislamu kuwepo mahala hapo.

3) Lakini mwanakijiji anapotoa claims kuwa mwandishi amejipinga kwa kutoa mifano eti kuwa sehemu inaweza kuwa ni ukumbi wa kanisa lakini si kanisa, inaonyesha kwa kiasi gani mwanakijiji hakuielewa mantiki ya mwandishi wa barua hii, mwandishi apingi kitendo cha kuuzwa kwa bia katika eneo la bar hiyo bali anapinga huwepo wa mkutano wenyewe katika eneo la bar. hii ni tofauti kidogo, kwa maana hata kama siku hiyo ya uzinduzi bar ilikuwa imefungwa na haiuzi vinywaji, malalamiko yangekuja tu. Hii ndio tafsir sahihi ya malalamiko haya.

4) Aya ya 4,5 na 6 zote kwa pamoja zinamtaja mwandishi kama mtu aliyepotoka, zikitaja kuwa mwandishi ameandika katika msingi wa "sisi against wao" na kwamba hakuwa balanced, lakini mwanakijiji ameenda mbali zaidi na kuliunganisha suala hili na vita ya udini iliyopo katika chama cha maendeleo na demokrasia chadema ambayo inamuhusisha moja kwa moja Dr Slaa na Mtei, Mbowe kwa upande mmoja na Zitto kwa upande mwingine, na akalipa suala hili mtazamo kuwa linabeba dhana hiyo na limepewa nguvu na makundi hayo. Jambo ambalo si sahihi hata kidogo. Mwanakijiji ameandika katika Aya ya sita (6) kuwa ninamnukuu " Lakini zaidi tunatambua kuwa lipo kundi la watu ambao wanamchukia Dr. Slaa kwa sababu aliwahi kuwa Padre na alitaka kugombea Urais na hivyo kuonekana kama Ukristu wake ni tatizo na hivyo hata hili lihusishwe naye." katika hili mwanakijiji amejitia upofu na kwamba AMEPOTEA LAKINI KIBAYA NI KUWA AMEPOTEZA WENGINE ambao watachukua uelewa huu na kuufanya ndio tafsiri ya malalamiko haya ya waislamu wa London. Suala la kugombea Urais wa Dr Slaa hauna mahusiano kabisa na suala hili, wala hakutajwa Slaa kwa kigezo hiko cha kutaka hausishwe na Udini kwa kuwa yeye ni Padri..,bali mwandishi amekuwa muwazi kubainisha ni ipi sababu ya msingi iliyomfanya kumwandikia Dr Slaa.,ninamnukuu " Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground" ni sababu ya nafasi ya Dr Slaa katika Chadema na Nguvu yake ama uwezo wake kimaamuzi..,Mwanakijiji amejitia upofu wa kutoliona hili na kutaka watu waamini katika hisia na tafsir yake potofu juu ya suala hili.

Mwanakijiji anamtaja mwandishi wa barua kama mshari aliyekusudia kupigia upatu udini kwa watanzania na hanawatoa na
kutowawekea shaka yeyote waandaaji wa mkutano huo kuwa walifanya hivyo kwa msukumo wa hisia zao na Udini walionao.,hii ni kudhihirisha uwepo wa double standard katika mawazo ya mwanakijiji ambapo kwa upande mmoja anamtuhumu moja kwa moja mwandishi kuwa mshari na mdini bila kuweka doubt ya kuwepo kwa makosa ya ubinadamu kama ule anaoudhani kuwa umekuwepo kwa waandaaji."Hili halikuwa jambo kubwa la kuandika barua makao makuu na kutuma hadi kwa balozi na bloggers mbalimbali. Barua inaonesha tu udhaifu wa baadhi ya watu kuweza kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo isipokuwa kwa kuanzisha shari."_mwanakijiji.

Namheshimu sana mwanakijiji lakini kwa hili namtaja kuwa ni "MPOTEVU ANAYEPOTEZA'' nawataka opinion takers hili wamwachie mwenyewe, ni lake.
 
Kweli cdm imekosea. Sielewi kwanini wanachama wengi wapo upande mmoja[ukristo] haileti picha nzuri. Pengine ule msemo wa padri unaukweli ndani yake WAISLAM AMKEN HAMNA CHENU APO

Kila chama kina watu wengi wa dini fulani kama ukitaka number. Ndiyo maana waislam wanataka sensa ya dini.

Anyway, wakati Mtei anaanzisha chama hakuna mtu aliyedai ni cha kidini au cha wachaga. Nakumbuka alikuja SUA na siasa zake za Kibepari tukawa tunamzomea kwa sababu ya propaganda tulizokuwa tumepewa JKT wakati ule. Sasa leo chama kimepata nguvu CCM wamekuja na propaganda ya dini naona kuna watu imewateka kiasi kwamba wanaamini. Lakini ukijiuliza mwenyewe, siku zile miaka ya 80s au 90s dini ilikuwa ni issue TZ?? Binafsi wakati nakua dini haikuwa issue. Tukiwa na sherehe tulikuwa tunaita mwislam kuja kutuchinji mpaka kuku. Tulikuwa tunaalikwa na majirani kufuturu..................... kaka yangu ameoa mwislam, binamu yangu kaolewa na mwislam. Kuoana makabila tofauti nafikiri hata humu ni atleast 60 %. Sasa hizi propaganda za CCM ndizo ninawavuruga watu akili sijui zinaingiaje akilini. Nafikiri Rwanda walianza hivi hivi mpaka wakaanza kuuana mtu na mkewe.
 
Halafu huyu magamba anamkopi Michuzi,Mjengwa na ubalozi anamwacha Mbowe.Kweli M4C imewashika
kweli mjinga ni mjinga sasa hapo alikuwa anajaribu kutaka kupanda mbegu chafu ya udini waisilamu wenyewe siku hizi wameelevuka hawachuji nafaka na kumeza ngamia hilo lake huyo huyo na chama chake cha mabwepande
 
Mwandishi wa barua anachuki dhidi ya CHADEMA, kamwe hawezi kutoa ushauri wala kuwaza vyema dhidi ya CHADEMA.

Kajitahidi kuandika mengi, lakini ni *****.

Mwandishi, ni mwanachama wa Chama kile kilichoolewa na CCM 2010, kisha mwaka 2012 kikajifungua ADC.
 
Tatizo liko wapi kufungua tawi la CHADEMA London wakati wa Ramadhani? Au mnatumiwa na Wanamagamba? Nawaheshimu sana. Mna mambo mengi ya kufanya juu ya ustawi wa dini yenu na nchi kwa ujumla. CC
M inawapoteza. Achaneni nao hata kwa hili tu
Acha kutoa Povu mkuu!! Hebu soma vizuri hizo email mtoa mada kasema, kufungua tawi mwezi wa Ramadhani sio vibaya ila tatizo ni kufungua tawi ktk bar wakati kuna maukumbi mengi ambayo sio bar tena ya Bei nafuu!!tena mkutano unafanyika mda wa kufuturu kwahio inakua ni vigumu kwa waisilamu kuhudhuria? Hebu rudia kuisoma hio email uckurupuke na jazba za kijinga hapa!!
 
Ndugu Zangu kujiamini ni kitu cha msingi sana utaona watu wasio na uwezo wa kujibu hoja wanavyokurupuka na maneno ya kukejeli badala ya kuandika vitu vya msingi.

Ieleweke waislam ndio waliosimama kidete kugombea uhuru wa nchi hii, kihistoria imefichwa ila inajulikana wazi ndio watu waliokuwa na ujasiri wakisaidiana na Mwalimu JK.

Ieleweke kwa miaka sasa waislam wamekuwa wanapigania haki zao ambazo imani zingine wamekuwa wakizibeza....sasa basi CHADEMA Inatakiwa ikae chini na iwafikirie waislam mapema maana hao ndio wapambanaji wa kweli.

Najua imani nyingine zina mapungufu na hazipo tayari kuambiwa ukweli ila hilo tusiliweke sana kisiasa.....M4C bila waislam nchi hii mtaisikia.

Ni kweli waislam ndio walioichangia kwa kiasi kikubwa uhuru wa nchi hii na vilevile ni ukweli usiopingika kuwa waislam wa nchi hii ndio hasa mbeleko inayoifanya CCM na serikali yake kuendelea na kuwa na uhakika wa kuitawala Tanzania milele,kwahiyo basi kwa haya madhila wayapatayo Watanzania (waislam) wakiwemo ambayo yamesababishwa na utawala mbovu,husiojali haki na maslahi ya watu wake WAISLAM hawakwepi lawama hii kwa kukikumbatia CCM na serikali yake toka uhuru hadi sasa.So tunaweza sema kwa kupaza sauti kubwa kwamba WAISLAM wanahujum jamii nyingine nchini kwa kushirikiana na CCM na serikali yake.
 
TANDALE ONE NI ID YA ZITTO ZUBERI KABWE HII NDIYO SHUKRANI YA MTAJI CHADEMA WALIOWEKA JUU YAKE,HUYU NDIYE RAISI MTARAJIWA ANAVYOkIPONDA CHAMA KILICHOMLEA NA KUMPA NAFASI

SHAME ON U

Jilazimishe kufikiri hata kama unafikia kikomo cha fikra zako, ukizoea kusadiki bila kudadisi utapotezwa...!
 
Ni kweli waislam ndio walioichangia kwa kiasi kikubwa uhuru wa nchi hii na vilevile ni ukweli usiopingika kuwa waislam wa nchi hii ndio hasa mbeleko inayoifanya CCM na serikali yake kuendelea na kuwa na uhakika wa kuitawala Tanzania milele,kwahiyo basi kwa haya madhila wayapatayo Watanzania (waislam) wakiwemo ambayo yamesababishwa na utawala mbovu,husiojali haki na maslahi ya watu wake WAISLAM hawakwepi lawama hii kwa kukikumbatia CCM na serikali yake toka uhuru hadi sasa.So tunaweza sema kwa kupaza sauti kubwa kwamba WAISLAM wanahujum jamii nyingine nchini kwa kushirikiana na CCM na serikali yake.
Haujafikiri sawasawa, jaribu kufikiri sawasawa...!
 
1.
mwezi huu situkani nipo kwenye mfungo, najua nakujua wewe ni katonta ndio maana inakuuma.

2.
Chadema ni chama cha wakristo, waislam fumbueni macho, mtaangamiza imani yenu, mimi ni mkristo nayaona haya kanisani.

Mkigoma, Wewe huyo huyo ni mwislamu hapo kwenye 1. na ni mkristo hapo kwenye 2?

Huo ni uongo na unafiki! Ni mambo ambayo Dini ya Kiislamu inayapinga. Tena ni mbaya zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani.
 
Dini na siasahaviendani kabisa. Uislam ni iman tu ambayo ukiwa umeelimika huwezi hangaika sababu hiyo ni iman yako wala hausiani na mambo ya siasa. jitaidi dini yako isiwe kikwazo kwa wengine. USIPENDE KULALAMIKA KWANINI KILA MARA KULALAMA NYIE TU!
 
nijuavyo mimi mzee wetu dkt Slaa nimwelewa sana wa mambo. sitaki kuamini kama hili lilifanywa pasipo kujali matokeo yake yatakuwaje, nadhani pengine wahusika wakuu wa maandalizi ya hafla hii ya ufunguzi wa hapo Londoni walipitiwa tu. ila ngoja tusikilize ujumbe kutoka kwa katibu wetu mkuu dkt.Slaa atasema nini. lakini hili kosa moja tuombe kuvumiliana kwani changamoto zilizo mbele yetu zinatuhitaji kuwa wamoja katika misingi ya kuheshimiana na kuvumiliana kulingana na tofauti zetu za kiimani.

nakupa big up kwa busara zako
 
CDM Haina dini ila wanachama wake ndio wana dini zao tofauti wanazoamini. kwahiyo ni makosa makubwa kusema ufunguzi kufanyikia bar eti waislamu wamelalamika! kwani bar ni eneo rafiki kwa wakristo? hii dhana sio sahihi coz hata ukristo haushabikii pombe mtu anahudhuria kwa maslahi ya chama si dini.
MFANO MZURI: CCM Wanamiliki BAR Kubwa sana kule dodoma inaitwa KILIMANI CLUB na mara zote wanatumia ukumbi wa bar hiyo kufanyia chaguzi zao zote za jumuiya za ccm, na waislamu wa ccm akiwemo alhaj mwinyi, jk, bashe, alhaj kinana na makamba nk, wanaudhuria bila malalamiko!( Iweje leo kwa cdm ndio iwe nongwa?)
utakuwa una ajenda yako ya siri au unatumika!
 
Wewe ulitoa habari hapo juu ulishafika Washington DC,au unaandika haya maneno ukiwa hapo Rumumba makao mkuu ya kifisadi africa.Kwanza nakuuliza kwanini Kikwete ataki kuongea na wananchi waishio Washington DC????????????????????.aLAFU MUULIZE SIKU YA KWANZA KUJA HAPA DC TULIMFANYA NINI????????.SISI HATUMNYENYEKEI MTU HAPA.ALIPEWA UKWELI WAKE HAPA HAPA.ALAFU MUULIZE NAPE MNAUYE NAE ALAFU MUULIZE BALOZI WENU AMEKUJA HAPA KUFUA MATAWI AMEFIKIA WAPIIIIIII,JARIBU KUPATA DATA KAMILI ,SIO KUKAA HUKO NAKULETA PROPAGANDA.TUNAWASIHI WANA CCM WAENDE SHULE ,KWANI WALISOMEA PROPAGANDA [EAST EUROPA].NDIO MAANA UCHUMI UMEDIDIMIA KWA AJILI YAO HAO.WMEKWENDA KUSOMEA KUONGEA UWONGO.SASA MAJI YAMEWAFIKA SHINGONI.
 
Mwanakijiji

Hebu tueleweshe vizuri, ni kuwa

1. waandaaji mkutano inawezekana walizingatia Ramadhan na muda wa iftar lakini maamuzi yao yameoneka kuwa na makosa kinyume na dhamira njema

2. Waandaji labda wanaweza kuwa na kosa la ukosefu wa hekima kutozingatia "sensitivity" kwa Waislam na Ramadhan yao

3. Muandishi wa barua ana makosa mengi ila kosa kubwa na la kusudi ni kumwamdikia Dr.Slaa

Yaani hao waandaaji unawapa benefit of doubt lakini mwandishi umejua moja kwa moja kuwa kafanya kosa la kusudi!!
Hakuna hata mjadala kuwa amekosea kibinaadamu, ni kusudi.

Hii double standard unaweza kuitolea maelezo?

Naam, kosa la mleta hoja ni kutowashawishi waandaji wa mkutano huo na hata Mfunguzi wa tawi hilo Bw. Lema kusitisha au kuhamisha sehemu ya mkutano ikizingatia sensitivity ya Waislamu wa eneo hilo ambao wangependa kuhudhuria. Suala hili si la Katibu Mkuu wa chama bali la waandaji - it is as simple as that. Ni lazima watu tujifunze kufuata chain of command na protocol. Kuna mtu anaweza kuelezea ulazima wa kuwaruka waandaji au hata kugomea kwenda (kama wengine inavyodaiwa walifanya) ili kutuma ujumbe kwa waandaji wengine?

Kumuingiza Dr. Slaa ni kutengeneza mazingira ya kumlaumu baadaye. Itakuwa hivi: Watakuja watu na kusema Dr. Slaa kwa kuendekeza udini aliruhusu tawi la CDM London lifunguliwe sehemu ya bar huku akijua wazi kuwa Waislamu walikuwa wanafunga na licha ya kuandikiwa barua hakuzuia jambo hilo. Na wapo ambao wataamini hilo.

Hili ndilo kosa kubwa la mleta hoja na labda wale ambao walitaka mkutano usifanyike ulipofanyika.

Kwa upande wa waandaji kosa lao kubwa ni kutokuwa sensitive kwa mahitaji ya Waislamu na labda hata watu wengine wa imani ambao wasingependa kufanya mambo yao kwenye eneo la bar (iwe wanauza pombe au hawauzi pombe).

Siyo kusudio langu kabisa kumsema "mwandishi" na inaonekana ananisoma vibaya kuwa nimemlenga "mwandishi". Kauli zangu nilizoziwekea namba kama sijamtaja mtu moja kwa moja ni za jumla na hazina sababu ya kusomeka kuwa namlenga mwandishi kama mtu binafsi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom