Ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya wadau wa elimu kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne-2013

Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
2,089
829

[h=3][/h][h=3]BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA[/h]











UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013


[h=2][/h][h=2][/h][h=2][/h][h=2][/h]


[h=2]Imetolewa Na:[/h][h=2]KAIMU KATIBU MTENDAJI[/h]25 Februari, 2014


UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013

Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo: 1. Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012. Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1. Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.
Kundi
Gredi
Alama
Idadi ya Pointi
1
A
75 - 100
1
2
B+
60 - 74
2
3
B
50 - 59
3
4
C
40 - 49
4
5
D
30 - 39
5
6
E
20 - 29
6
7
F
0 - 19
7
Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili (12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa. 2. Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika. 3. Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katikaDaraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2. Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013
Daraja
Pointi
I
7 – 17
II
18 – 24
III
25 – 31
IV
1. Ufaulu katika somo moja kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C au 2. Ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili katika Gredi D
0
Alama chini ya D mbili
4. Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa "Credit" na Gredi D itahesabika kuwa ni "pass". Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli. 5. Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.


Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
 
mbona mashuleni huu mfumo hautumiki.ni lini walimu walipewa semina ya jinsi ya kitumia hizi alama mpya ili wanafunzi wazizoee.walimu nao hawaelewi ila baraza na wizara ndio wanaojua huu mfumo mpya.
 
NECTA wametupa maelezo kuwa nchi nyingine pia zina makundi hadi 12 ya ufaulu, maswali ya msingi ni kuwa ili mtahiniwa ahesabiwe kuwa amefaulu katika nchi hizo anahitaji alama ngapi na je utaratibu wa kulinganisha haya makundi mapya ya ufaulu (7) na yale matano ya zamani ukoje. Tunaomba mfafanue kwa ujumla badala ya kila siku kutupa ufafanuzi nusu nusu. Kumbukeni kuwa hilo ni elimu nyeti kwa hiyo yale yote yanayoweza kuleta jakamoyo kwa watu myaeleze kinaga ubwaga
 
Xo mfano mwanafunzi atakaepata.B ya bios. B ya Geograph na D ya Chemistry atakuwa amepata kombi ya CBG au??
naombeni ufafanuz wadau
 
Naunga mkono hoja ufafanuzi haijajitosheleza
NECTA wametupa maelezo kuwa nchi nyingine pia zina makundi hadi 12 ya ufaulu, maswali ya msingi ni kuwa ili mtahiniwa ahesabiwe kuwa amefaulu katika nchi hizo anahitaji alama ngapi na je utaratibu wa kulinganisha haya makundi mapya ya ufaulu (7) na yale matano ya zamani ukoje. Tunaomba mfafanue kwa ujumla badala ya kila siku kutupa ufafanuzi nusu nusu. Kumbukeni kuwa hilo ni elimu nyeti kwa hiyo yale yote yanayoweza kuleta jakamoyo kwa watu myaeleze kinaga ubwaga
 
Angalau tumeelewa sasa! Ila maelezo haya yalitakiwa kutolewa mapema kabisa wakati ule ndg mchome anatangaza viwango vipya vya ufaulu na madaraja!
 
Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo: 1. Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika.



Kwa sababu ambazo ziko wazi kabisa (tunazijua), Baraza limekiuka kanuni zilizowekwa.
Kanuni iliyokiukwa ni hiyo hapo kwenye nyekundu.

Hapo awali, "A" ilikuwa: 81 - 100
Imepanuliwa kuwa: 75 - 100

Baraza halikuishia hapo; wameondoa penalti kwa watakaofeli hesabu. Hii imefanywa makusudi ili watahiniwa wengi waingie kwenye kundi la alama "A". Kwa maana nyingine, hii ni sawa na kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo usiofanana.

Moja ya madhara ya madudu haya ya CCM (chini ya kivuli cha Baraza) ni kushusha bidii ya wale waliokuwa wakipata "A" kwa kutoka jasho.
 
Tuangalie takwimu.

ZAMANI: Tofauti ya 81 na 100 = 19
SASA: Tofauti ya 75 na 100 = 25
Hivi sasa, kundi la wenye "A" limefanywa kuwa kubwa zaidi.


ZAMANI: Tofauti ya range ya failures ilikuwa: 34 - 0 = 34
SASA: Tofauti ya range ya waliofeli (E na F): 29 - 0 = 29
Hivi sasa, range ya waliofeli imefanywa kuwa ndogo kwa makusudi.

(EDIT: Hiyo 34 ni viwango vya zamani kabla ya mfumo uliopita.)
 
History E. Literature D. Math F. Civics D. Biology D. Kiswahili B. English C. Geography C. Chemistry D Samahanini jamani je kwa matokeo yangu haya naweza nikasoma combination yenye history????? Plzzzzz
 
History E. Literature D. Math F. Civics D. Biology D. Kiswahili B. English C. Geography C. Chemistry D Samahanini jamani je kwa matokeo yangu haya naweza nikasoma combination yenye history????? Plzzzzz

subiri utaratibu mpya.
 
History E. Literature D. Math F. Civics D. Biology D. Kiswahili B. English C. Geography C. Chemistry D Samahanini jamani je kwa matokeo yangu haya naweza nikasoma combination yenye history????? Plzzzzz

ndiyo unaweza kusoma kombi zenye somo la History ila katika shule za binafsi.
 
History E. Literature D. Math F. Civics D. Biology D. Kiswahili B. English C. Geography C. Chemistry D Samahanini jamani je kwa matokeo yangu haya naweza nikasoma combination yenye history????? Plzzzzz

.
Huwezi kabisa mkuu history yaaani umepata madudu kabisa
.
E= amefanya vibaya katika somo husika
D = anahesabiwa kapita
 
Kitu ambacho sijaelewa hapa inakuwaje E na F zote zina hadhisawa yaani Fail. Kama E ina hadhi sawa na F, kulikuwa na sababu gani ya kuianzisha mpaka imesababisha mkanganyiko wa madaraja watu wanaopata pointi sawa kuanzia 41-45. Hii inachanganya watu bila sababu ya msingi. Yaani NECTA wameifa tu kuwa nchi nyingine zina makundi mengi bila kutueleza ndani ya hayo makundi kuna nini. Tusifanye kazi kwa mazoea na kuiga tuangalie inaongeza thamani gani katika elimu ya taifa letu
 
Back
Top Bottom