Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,591
- 4,278
Nchi yetu imekuwa na nia njema sana ya kuendeleza Vijana katika fani mbalimbali hasa za ufundi na ujasiriamali.
Kimsingi vijana wenye uelewa wa somo la hesabu wanaweza kufanya vizuri sana katika fani hizo za ufundi na ujasiriamali.
Hata hivyo kutokana na upungufu/ ukosefu wa waalimu wa hesabu katika Shule za msingi na upungufu mkubwa katika shule za Sekondari, wanafunzi wengi wanaotarajiwa kujiunga na fani hizo humaliza wakiwa wamepata alama sifuri.
Napendekeza Vijana wa Kidato cha sita wenye Ufaulu wa C na kuendelea katika somo la Hesabu waruhusiwe kufundisha somo la Hesabu shule za Sekondari na Vijana wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa C katika somo la hesabu na kuendelea waruhusiwe kufundisha shule za msingi.
Hii itasaidia kupunguza pengo wakati tunajipanga.