UDASA Wagomea JAKAYA Kutunukiwa PHD ya HESHIMA

Kumbe mwapachu nae alitunukiwa ya Heshima..ila wote hao wapo tite,kweli udsm wanatisha ni 18,afu ndio wanataka kumpa na jk
..Hawa wafuatao ndio so far wamewahi kutunukiwa Shahada za Heshima za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam





S/NNAMEDEGREEDATE/YEAR
Degrees of the University E. A (Dar es salaam)
1Prof. Karl Worth BigelowDoctor of Literature(honoris causa)1970
2Hon. Solomon Nkya EliufooDoctor of Laws(honoris causa)1970
3Edward Walter RussellDoctor of Science(honoris causa)1970
Degrees Awarded by UDSM
4Hon. Justine Philip TelfordDoctor of Laws(LL.D)1973
5Hon. Abdulkarim Yusufali Alibair KarimjeeDoctor of Laws(LL.D)1973
6Hon. Aboud Jumbe MwinyiDoctor of Laws(LL.D)1976
7Hon. Adam Sapi MkwawaDoctor of Laws(LL.D)1980
8Hon. Amir H JamalDoctor of Literature(D. Litt)1980
9Dr. W K ChagulaDoctor of Science(honoris causa)1981
10Dr. Basil Risbridger DavidsonDoctor of Literature(D. Litt)1985
11Mwalimu Julius Kambarage NyerereDoctor of Literature(D. Litt)1986
12Dr. G .L MonekossoHonorary Doctor Of Science(honoris causa)1989
13Prof. Tormod ForlandHonorary Doctor Of Science(honoris causa)1990
14Ambassador Amon James NsekelaDoctor of Literature(D. Litt)1990
15Professor Dr. Ir.Godfried D.VogelsHonorary Doctor Of Science(honoris causa)1998
16 Ambassador J.V MwapachuDoctor of Literature(honoris causa)2005
17Hon B.W MkapaDoctor of Literature(honoris causa)2006
18Prof. Sven Erick JorgensenDoctor of Science(honoris causa)2007
 
Kama ni kugawa Ph.D kwa mchango wa mtu kwa taifa si mara mia apewe Bakhressa kuliko huyo.

Kwa mtaji huu mimi naona hata Profesa Maji Marefu anatakiwa kupewa Phd ya heshima na UDSM.Tatizo la nchi hii kuna utamaduni wa kijinga wa kulamba viatu vya wakubwa ili kutafuta vijinafasi vya uongozi. Huu utamaduni wa kijinga umewaathiri hata wale tunaodhani ni watu walioelimika kwenye jamii yaani wenye Phd. za kusomea na Maprofesa.
 
ulishawai kusikia anajiita Dr Mkapa????? au Dr Nyerere???
Hata JK hajiiti. Anaitwa na vyombo vyetu vya habari ITV ikiongoza. Wengine wanaomwita ni wanaojikomba kwake kwa sababu mbalimbali. Hata hivyo, kwani hastahili? Vyuo vikuu vilivyompa heshima havitambuliki? Au hatumpendi tu 24/7?
 
Naungana na mchangiaji mwenzako hapo juu,wampe na uprofessor itakuwa safi,mkandala ni mnafiki kweli kaleta fitina mpaka Prof Luanga(Member) kaondolewa ndio shida kuwapa mangwini waendeshe chuo;;Hon Dr. Prof Jakaya Mrisho Kikwete,UDASA KAZENI UZI KAMA NI HESHIMA MPENI PIA SABODO,BAKHRESSA,ZAKARIA,MENGI,MO,wakimpa JK Phd pia wampe na rostam

wapewe pia LACAIRO,nyambari(amechangia kuzalisha madesa mengi ya sekondari) pia spika ana makinda kwa busara pale mjengoni bila kumsaau TAMBWE IZA NA ABOOD.
 
Kwani UDOM hawatoi ph.D.? Hata kama hawajaanza si wafanye remakable ya miaka 50 ya uhuru kumtunuku ndugu yao Jk digrii ya uzamivu ya kwanza?? Kwanini baba wa taifa mpaka kesho anaitwa mwalimu?? Hawa vilaza wa siku hizi ndio wanashobokea vyeo na title zinazowapwaya..shame on them all. Siungi mkono jk kutunukima ph.D nyingne, kama shida yake ni udokta si tayari alizawadiwa na wakenya?? Hapa tz hana cha maana kinachomfanya astahili heshima hiyo.!
 
Napinga wote wanaokataa JMK asitunukiwe hii PhD, tena nasema wasikomee kwa huyu tu, wawape na kina Nape, Rage na Nchemba hawa wanastahili kwa sababu ni wana ccm wazuri, PhD oyee au sijui maana ya hii kitu.

Kwanini wasimkumbuke mtu kama Mwaibula, kwa kazi nzuri kwa taifa, mpango wake aliouanzisha wa kurahisisha usafiri wa daladala sasa unatekelezwa nchi nzima, mabasi yanatambulishwa kwa rangi, makonda wana suti, khah, basi mpeni hata cheti cha PhD
 
Vilaza wanapewa uongozi na kupewa heshida za juu matokeo yake ni kuharibu mfumo mzima wa elimu na uongozi wa nchi.kama udasa wanapinga jay50 kupewa phd inamaana jamaa hana vigezo so nikilaza.pamoja.
 
Katika kuadhimisha miaka 50 Ya Uhuru wa Tanganyika , utawala na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam umepanga kumtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, mzaliwa wa Msoga Mkoa wa Pwani Shahada ya Uzamivu/PHD ya Heshima.

Sasa katika hali isiyotabilrika wasomi wa chuo hicho kupitia UDASA wamekua wakigomea kutunukiwa kwa huyu bwana kwa madai kuwa hastahili kupewa Heshima hiyo kwakua hakuna la maana alilolifanya kustahili Tuzo na hakika wametoa wito kwa Utawala wa chuo kujitenga na propaganda za ajabu ili tu kuupumbaza Umma kuwa anakubalika na kuheshimika sana miongoni mwa wasomi katika Tanzania hii.


(.Note..................................habari hii nimeipata pale ofisi za UDASA kwa Mkufunzi aliegoma kunitajia jina.)
Hapa UDASA mnacomplicate bure,mpeni hizo PHD tena zikizidi muiteni Prof.Kikwete acheke chekeeee hadi basi.Huyu rais ni kituko tu.
Tena Maaskofu jiandaeni kumtangaza Baba Mtakatifu!!!Maadhimisho yenyewe si "Miaka Hamsini Ya UHUNI"
 
Hili ni tatizo la watu wanaopenda kujipendekeza na kupendwa kubebwa. Mtu wa kijipendekeza hata akivaa suti ya namna gani bado ni wa hatari. Yuko radhi aupoteze utu wake akichekacheka ili tu apate shati au kushikana mkono na muheshimiwa au aitwe jina lake na mkuu huyo ama apige picha pamoja. Aibu!!Nimekutana na wazee kadhaa waliokuwa vijana nyakati za ukoloni, walikataa kuwa vibaraka na mafundi wa kujipendekeza hadi uzee wao, jamii inawaheshimu.Alianza Prof Kikula na wenzake (UDOM), akaja Prof Palangyo na wenzake (MUHAS) na sasa anataka kuja Prof Mukandala na wenzake. What a kind of shame is this to academicians?Nilwahi wauliza wahadhiri wawili wa UDOM ambao ni senior(formerly were at UDSM) kitu gani kikubwa alichafanya JK hata kumpa hiyo honorary Phd they fail at all to give a resoanable cause. I ask also three from MUHAS, two of them replied to me head-on, AIBU. the other one akasema ni ujinga wa kisiasa na kujipendekeza ilihali unadharilisha chuo na wanataaluma. Akanyanyuka akaenda ukutani akaifungua Kalenda ya ukuta ya MUHAS 2011, akanionyesha picha iliyowekwa kwa miezi ya Oktoba na Novemba. "Wanasema amepewa Phd ya heshima kutokana na kuutambua mchango wake katika afya. Mchango gani huo? Hivi ana-NGO iliyofanya lolote kwa watanzania japo wa jimbo moja tu kama si mkoa? Tunajua Wizara ya Afya inaendeshwa kwa misaada ya wahisani, yeye kafanya nini? Wengine wanasema vyandarua, upuuzi!Kapeleze uone katika vyandarua hivyo serikali imetia asilimia ngapi? Aaagh! vitu vingine vinauzi....(akalitaja jina langu).UDASA tafadhalini wekeni msimamo kulikataa hili ili kulinda heshima yenu na ya chuo kwa ujumla.
 
Prof,Mkandala unatutia aibu Bukoba,angalia Wasomi wenzako wa pande za kwenu,je unafananao??Acha kujipendekezapendekeza kama Bana.
 
yes aliwahi!!!

alipewa nyingi, kwa Tanzania alipewa mwaka 1998 kama sikosei na SUA , PhD (Rural Development).

kazi karibu zote alizowahi kuzifanya zilikuwa kwa ajili ya maendeleo vijijini...tena kwa dhati..tuanze Azimio la Arusha, Azimio la Musoma, Madaraka mikoani, opeshesheni vijiji vya ujamaa, kilimo cha kufa na kupona, siasa ya uijamaa na kujitegemea yenyewe....vyama vya ushirika...e.tc. e.t.c.....

ilisomwa speech almost 1 hr ikionyesha maeneo haya aliyoyafanuia kazi kwa dhati.......mzee wa watu alisimama kimya wala hakutetereka......akaipokea kwa unyenyekevu.....

alipewa PhD hii miaka mingi baada ya watu kukiri na kuopna impact ya filosofia zake....

Enyi Mukandara na wenzio, lazima muone aibu....munajustify vipi hii phd mnayotaka kumzawadia huyu mheshimiwa ukizingatia huu ndio mwaka wa sita madarakani??? subirini amalize ngwe yake ndio tufanye impact analysis
 
Back
Top Bottom