UDASA Wagomea JAKAYA Kutunukiwa PHD ya HESHIMA

Jamani tusilaumu sana, inawezekana wanataka kumpa PhD <em><strong>ya safari nyingi nje ya Nchi zisizokuwa na maslahi kwa watanzania!!!!</strong></em>! Inadhihirisha dhahiri ya kwamba tumkichukua yeye (JMK), Nyerere, Mwinyi na Mnzee wa mikataba feki (BWM) &nbsp;huyu wa saizi ndiye aliyeongoza kusafiri mara nyingi nje ya Nchi, kwa hiyo kama UDSM wanataka kumpa <strong>PhD wampe ya kuwa na safari nyingi nje ya Nchi bali sio ya heshima!!!! &nbsp;<br><br></strong>MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI UDASA
 
Hii ni kweli kabisa. Angalau Bakhressa amewapa watu kazi

Hata mimi naunga mkono jamaa huyu ni jasiriamali wa mfano hapa Tanzania na hata wafanyabiashara wa nje wanamgwaya. Na kama jamaa nalipa kodi zote basi anastahili sana kwa mchango wake mkubwa wa kutengeneza ajira na bidhaa nafuu kwa ajili ya walalahoi.
 
UDASA mko juu; hapati mtu PhD ya mezani hapo bila ya kupitishwa kwenye tanuri lilelile walimopitia akina Hassy Kitine na ile thesis yake ya kufa mtu. Halafu leo hii wajanja fulani tu kwa ukada wao tu kwenye chama fulani waanze eti kuzawadia wanasiasa viji-digrii uchwara hapo kiholela holela hivo na watu tukubali tu???????????

Hilo likitokea basi ni sharti nyinyi wenyewe mturidhishe kwamba ni tangu lini mmegeuza taalum kuendeshwa kisiasa badala kujitahidi kutusaidia walau siasa zetu za nchi ndio zikaendeshwa kitaaluma kwa manufaa ya wengi, na kwamba katika tafiti zenu mliesoma sana wenzetu mtakua mmegundua tija gani humu katika hili la kukirimia watu PhD za hisani kisiasa??

Naona aliyebikiri utaratibu huo mpya nchini ni yule Prof Idris Kikula na sasa ni zamu ya Mkandara na kitchen cabinet na keshokutwa tutasikia CBE na mwisho Tambaza High school nao wameunga tera. Mwenye kuja kulaumiwa hadi hapo ...???????????

Nasema hilo likitokea basi moja kwa moja ni jukumu la UDASA kuridhisha walipakodi wamiliki wa chuo hicho hapo Milimani kwamba tangu sasa ni utaratibu rasmi yeyote anapobahatika tu kupata mkataba wa upangaji wa jumba letu tu pale Magogoni basi hadi hapo anayo haki yake ya PhD hapo UDSM inamsubiri tu kuja kukaokota.

Lakini, huko mbele ya safari, wanataalum msije mkalaumu kwamba wanasiasa hawawathaminini nyinyi na kwamba hata malipo yenu ni kiduchu kuliko yale ya kwao kwa kuwa ni nyinyi wenyewe mmejichagulia kwa ari zaidi na kasi zaidi kujirahishisha kiasi hicho.

Nasema kwa mtindo huo wenzet mtakua mmetutangazia sisi kama umma wa nchi hii ili tunapowaona tuamini tu kwamba PhD Vitumbua pengine ndio vingi zaidi nchini hata ikatufikisha kweye janga nyingine la 'LITERARY BARRENESS OF THE 'GLASSY' SECTIONS OF THE ACADEMIC COMMUNITY' ndani ya taifa hili ambao hivi sasa wanaingia kwa kasi kwenye jukwaa kuu la usomi kupitia mlango wa nyuma.
 
Mimi naungana na hao wanaotakata asipewe,maani wanazuoni hufanya makubwa hadi kufikia hadhi.Wanazuoni msimezwe na wanasiasa.
 
Kwa mwanasisa yeyote, ukimuondoa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere, huo msamiati 'TOSHA' hata siku moja haujawahi kufahamika kwenye hulka zao the mean ego of 'go for everything' ever rules their actions and behaviour.

Si tayari anayo PHD???Haitoshi?
 
Jamani maswala ya kitaaluma siyo maswala ya siasa. nasema hivyo kwa kuwa kwanza hatujui tofauti ya PhD na Honoris causa na hatujui nani anayestahili kupewa PhD na anayestahili kupewa Honoris Causa. Tufanye utafiti kwanza kuhusu hili. najua hata huyo uliyemuuliza hajui hiyo tofauti bila kujali yeye ni mhadhiri kweli au umemua kuweka hivyo ili uonekane umetafiti. PhD lazima uisotee kwa kuandika na kufanya tafiti za kina kuhusu namna ya kutatua kero au suluhu ya jambo fulani katika jamii bila kujalisha umefanyiwa au umefanya mwenyewe na prof. wako. Honoris causa ni heshima hivyo haijalishi mtazamo wa kundi fulani, dini fulani au siasa fulani.

Tusiwasingizie UDASA eti wamgomea hilo swala ilihali hakuna statement iliyotolewa on that matter. mi naijua executive committee ya UDASA ilivyo strong lazima wangetoa statement.

Kingine lazima tujue ni mchakato upi unatumika mpaka mtu kupata Honoris Causa. Nasema hivi maana Hivi karibuni nilifika Norway kuhudhuria maadhimisho ya miaka 200 ya chuo fulani kule na kilito Honoris Causa 12 na mojawapo ilikwenda kwa somebody from Cameroon na huyu bwana alikua hajawahi kufika Norway hiyo ndiyo first time, nilishangaa sana.

Tuache politic za chuki tujenge nchi
 
leader should be soft but hader in standard,lakini tz ni kujipendekeza na viongozi walioko madarakani aiming to hold the status,hatufiki mbali:fish:
 
Tena wasimpe huyo bwana, katika uongozi wake na katika kipindi chote cha usomaji wangu/uanafunzi wangu huyo bwana hajawahi hata kutia mguu pale. Amekuwa akieneza uvumi mbaya juu ya udsm na amekitenga ktk maendeleo, jitihada zake zipo UDOM kwake Udsm nikama kambi ya upinzani. Kifupi NAWAUNGA MKONO UDASA KWA MSIMAMO WAKE, HIYO PHD HAITAKUWA NA MAANA, NI KAMA VIONGOZI WA UDSM WANAJIPENDEKEZA!

Mumshauri Mukandara asimsahau Rostam kwa PhD kwa kujivua gamba mwenyewe na kuweka mfano-wengine wameshindwa kama akinaJK, EL na AC!!!!!!!!!!
 
...huyu jamaa akipewa Phd nina wasiwasi iko siku wazee wanaocheza bao pale Msoga watapewa u-Dr.
 
Back
Top Bottom