Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru chamtunuku Rais Samia Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), leo Oktoba 10, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya kitaifa nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.

View: https://www.youtube.com/live/VuNUt9YAn8Q?si=JkkkUnFuBzu6q8PP

3f9be868-e713-4e8f-8133-5a1c2c4c94e9.jpeg

68f33c4f-4dd0-4689-9a42-52d4233b01fb.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023. Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho Nchini India.

Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe.

===
Rais Samia ameshukuru kwa heshima hii aliyopewa ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) kutoka chuo cha Jawaharlal Nehru, India, na amesema hii ni mara ya kwanza kwake kupatiwa heshima hii nje ya nchi baada ya kupatiwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Amewashukuru wazazi wake kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwa mtoto wa kike, CCM, ndugu zake pamoja na watu wote waliomshika mkono kuhakikisha anafikia sehemu alipo hivi leo.
c7a99983-f59f-4af1-9146-05bc39aac89e.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
Tuzo hii ameitoa kwa watoto wa kike wa kitanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu, amewatia moyo kuwa hakuna kisichowezekana.

Kwa Tanzania, India sio nchi tu bali ni sehemu ya familia iliyotenganishwa na mwambao wa bahari, pia ni rafiki wa majira yote. Urafiki huu ulianza zamani, tangu enzi za ukoloni ambapo wananchi wengi wa India wapo nchini Tanzania, hata baadhi ya vyakula vya kihindi vinapatikana Tanzania.

Sherehe ya diwali husherekewa pia Tanzania, pia mahekalu ya Kihindu yapo Tanzania na hata kwenye ziara hii imejumlisha Watanzania wenye asili ya Kihindi.

Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (Javāharalala Neharū Viśvavidyālaya) ni chuo kikuu cha utafiti wa umma kilichoko Kusini Magharibi mwa Delhi , India. Kilianzishwa mwaka 1969 na kupewa jina la Jawaharlal Nehru, Waziri Mkuu wa kwanza wa India.
36da961e-b579-4461-8dfa-d9b34d59ea78.jpeg

1b0ae186-24a8-4559-8099-528d199be3a5.jpeg

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini humo tarehe 10 Oktoba, 2023.

90ede436-12e7-47e3-8641-7e99ed31700e.jpeg

3bcf1f78-d841-4674-b6e9-a8f7d7d48e55.jpeg

874d9670-15f8-4caf-bcc3-8e02e1b625de.jpeg

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.
PIA SOMA:
- Mama Samia Atunukiwa Udaktari wa Uchumi (Doctorate of Economics Degree) Uturuki

- Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi ya Utalii na Masoko ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), leo Desemba 28, 2023

- Rais Samia ashiriki Mahafali ya 52 Duru ya 5 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Atunukiwa Shahada ya Heshima

- Dkt. Jakaya Kikwete amtunuku Rais Samia Shahada ya Udaktari wa Heshima UDSM. Sasa ni Dkt. Samia
 
Jawaharlal Nehru was an Indian anti-colonial nationalist, secular humanist, social democrat, and author who was a central figure in India during the middle of the 20th century. Nehru was a principal leader of the Indian nationalist movement in the 1930s and 1940s. Wikipedia

Huyu bwana historia yake alikuwa mzalendo, mwana demokrasia na mpingaji wa ukoloni, inasikitisha chuo chenye jina lake kutumika vizuri kwa kutambua mchango wa Rais wetu kipenzi, hakika mama anaupiga mwingi kuanzia Dubai hadi India ..
 
... hivi huwa ni vigezo gani vinatumika? Mwenye andiko lenye hoja zilizopendekeza hiyo award aliweke humu tulidadavue tafadhali. I think it should be public document!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya kitaifa nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.

Rais Samia ameshukuru kwa heshima hii aliyopewa ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) kutoka chuo cha Jawaharlal Nehru, India, na amesema hii ni mara ya kwanza kwake kupatiwa heshima hii nje ya nchi baada ya kupatiwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Amewashukuru wazazi wake kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwa mtoto wa kike, CCM, ndugu zake pamoja na watu wote waliomshika mkono kuhakikisha anafikia sehemu alipo hivi leo.

Tuzo hii ameitoa kwa watoto wa kike wa kitanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu, amewatia moyo kuwa hakuna kisichowezekana.

Kwa Tanzania, India sio nchi tu bali ni sehe,u ya familia iliyotenganishwa na mwambao wa bahari, pia ni rafiki wa majira yote. Urafiki huu ulianza zamani, tangu enzi za ukoloni ambapo wananchi wengi wa India wapo nchini Tanzania, hata baadhi ya vyakula vya kihindi vinapatikana Tanzania.

Sherehe ya diwali husherekewa pia Tanzania, pia mahekalu ya Kihindu yapo Tanzania na hata kwenye ziara hii imejumlisha Watanzania wenye asili ya Kihindi.

Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (Javāharalala Neharū Viśvavidyālaya ni chuo kikuu cha utafiti wa umma kilichoko Kusini Magharibi mwa Delhi , India. Kilianzishwa mwaka 1969 na kupewa jina la Jawaharlal Nehru, Waziri Mkuu wa kwanza wa India. Kilianzishwa kwa Sheria ya Bunge mnamo mwaka 1969.

Nikiangalia hicho chuo vs vyuo vya Tanzania kwenye miundombinu
 
Chuo Kikuu maarufu nchini India cha Jawaharlal Nehru, leo Oktoba 10, 2023 kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa shahada hiyo na chuo hicho.

Rais Samia anapokea shahada hiyo ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kumtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari kutambua mchango wake katika kuboresha sekta ya elimu, uchumi, demokrasia, na usawa wa kijinsia nchini.

Chuo hicho kilianzishwa Aprili 22, 1969 na kupewa jina la Waziri Mkuu wa kwanza wa India, Jawaharlal Nehru, na kuwa moja ya vyuo vikuu bora nchini India na duniani kwa ujumla kikijivunia kuwa taasisi ya elimu ya juu ambapo watu maarufu wa India walipata elimu yao ya juu.

Baadhi ya majina maarufu yaliyoandikishwa katika chuo hicho ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Bw. Subrahmanyam Jaishankar, na Waziri wa Fedha, Bi. Nirmala Sitharaman, huku kikitoa Shahada ya Heshima kwa viongozi wawili pekee akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Hayati Shinzo Abe.

Shahada hiyo ya heshima imetolewa kwa kutambua juhudi za Rais Samia katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na India, kutokana na mafanikio yake katika uwanja wa kidiplomasia, haswa diplomasia ya kiuchumi, na mafanikio katika kuchochea maendeleo yanayojikita kwa watu nchini Tanzania.

Aidha, sababu nyingine ni kutokana na mafanikio yake katika kuendeleza ushirikiano wa kikanda, kuimarisha mahusiano ya kimataifa, na kuendeleza utaratibu wa kushirikiana kimataifa katika Umoja wa Mataifa.

IMG_8533.jpg
 
View attachment 2777560
"kuendeleza utaratibu wa kushirikiana kimataifa katika Umoja wa Mataifa"! Sifa hii siielewi naona imekaa kichawa zaidi, naomba iondoe.
 
Back
Top Bottom