Uchakachuaji huu wa kanuni za Bunge uliofanywa na CCM haukubaliki popote

chadema mliamua kubagua sasa mmebaguliwa. mizee mizima hovyo

nimelipenda hilo la waturudi kwenye posho wana madeni benki

Siyo kubagua bali ni kanuni za kuunda kambi ya upinzani zinatoa haki kwa Chadema kuiunda peke yake, soma kanuni.
 
CDM kwa maoni yangu wasikubali huu ushirika maana utakuwa wa mvurugano. Tujivunie kuwa na chama imara tujipange kuwashitaki kwa wananchi kuelekea 2015 tujipange sawasawa kazi bado ni kubwa. Hao wanajivunia mihimili mikuu ya dola, mafisadi na wamejipanga sawasawa, huko fursa zetu ni kidogo lakini tuzitumie itakapojitokeza. Kambi ya upinzani, dowans,katiba nk changa la macho. Nashauri kupambana kufanakupona kupata tume huru ya uchaguzi kuelekea huko vinginevyo itakuwa vigumu kulinda zao letu historia ikajirudia.
Mungu uwe nasi, tusijeaibika mbele ya watesi wetu AMEN.
 
Hivi kama Kambi rasmi ya upinzani inatafsiriwa kuwa ni jumuisho la wabunge wote wa upinzani ni ipi isiyo rasmi? Kuna haja gani ya kuuita rasmi ya upinzani wakati hakuna isiyokuwa rasmi? Nahisi kizunguzungu!
 
Nafikiri bunge letu linatakiwa kuwa kama bunge la majirani zetu kenya kabla ya wabunge wa chadema kuondoka walipaswa kumpa kisago spika mpka kieleweke
 
Tatizo ni kwamba kanuni inachakachuliwa kwa manufaa ya CCM. Haikubaliki tafsiri ipingane na kanuni zingine

Toeni suluhisho wapinzani wengine (TLP, NCCR, CUF, UDP) wafanyeje katika hali hii?
hivi CDM ikipewa madaraka kutakuwapo upinzani kweli nchi hii? maana kwa hili dogo tu wanawatenga wenzao. Siasa za Bongo taabu kweli kweli umdhaniye ndiye siye ili mradi vurugu tupu. Halafu manufaa gani ya CCM? tafadhali fafanua sote tujue maana huenda kuna hidden agenda unayoifahamu.
 
CHADEMA wamejitakia wenyewe wasitafute mchawi, wakati mwingine ujuaji mwingi huwaponza sana. Sasa hayo ndio matokeo yake. Hongera bunge kwa uamuzi wa busara :clap2::clap2::clap2:
 
CHADEMA wamejitakia wenyewe wasitafute mchawi, wakati mwingine ujuaji mwingi huwaponza sana. Sasa hayo ndio matokeo yake. Hongera bunge kwa uamuzi wa busara :clap2::clap2::clap2:
Hiyo yako haina mantiki kwa sababu bunge linaendeshwa kwa sheria na kanuni siyo matakwa ya mtu binafsi. Pale ni sehemu ya heshima si klabu cha pombe ambapo kila mtu hafanya atakalo. Ni kuvunja heshima ya bunge zima kuweka tafsiri ya kanuni inayovunja makusudi kanuni za msingi.
 
Hapa tatizo ni kwamba, tafsiri ya kuchakachua ya CCM inapinga kanuni za msingi zinazoelekeza kuwa chama cha upinzania kinapata haki ya kuunda au kuwa katika kambi rasmi ya upinzani ikiwa kimefikisha asilimia 12.5 ya wabunge wote. Kama vyama vyote havina idadi hiyo ndio vinaungana kupata asilimia 12.5 na kuunda kambi rasmi. Chadema inajitosheleza kuunda kambi rasmi, na vyama vingine kulingana na kanuni havina haki ya kuwemo katika kambi rasmi ya upinzani. Hivyo kulingana na kanuni Chadema yenye wabunge wengi hailazimiki kuingiza wabunge wa vyama vingine kwenye kambi rasmi ya upinzani. Hiyo tafsiri ya kuchakachuwa ya CCM si halali kwa namna yeyote ile na haikubaliki. Inadhalilisha bunge na kuwa kama kilabu cha pombe.

Chadema ishitaki kwenye mahakama ya umma ili umma utoe hukumu kwa sababu mbinu hizi chafu zimepangwa kwa makusudi kati ya cuf na mumewe ccm kwa makusudi ya kuuwa upinzani na hasa chadema. Lakini wakae wakijua kuwa chadema haitakufa kamwe, kila baya walifanyalo ndio linaongezea uhai badala ya kuiua chadema. Peoples power daima.
 
Back
Top Bottom