Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 60
- 1,237
1. Bunge linapaswa kuundwa na wabunge wasiozidi 300. Kwamba muundo wa majimbo uliopo ufutwe na badala yake wilaya ndio zinapaswa kuwa majimbo ya uchaguzi kwa kuwa na wabunge wawili wa kuchaguliwa mmoja akiwa mwakilishi wa wanawake jimbo husika.
Bunge hilo litaundwa na wabunge wa aina tatu kama ifuatavyo;
a). Wabunge wa kuchaguliwa majimboni watakuwa 139 sawa sawa na idadi ya wilaya nchini. NB Mbunge katika jimbo ndio atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli zote za maendeleo na pia atakuwa mwenyekiti wa kamati ya nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa serikali katika halmashauri ndani ya jimbo lake. Hivyo kupunguza gharama kwa serikali hahitajiki wakuu wa wilaya kuwepo.
b). Wabunge wanaowakilisha wanawake watakuwa 139 sawa sawa na idadi ya wilaya nchini. NB Wabunge hawa watapigiwa kura na wanawake wote wenye sifa za kupiga kura katika jimbo husika kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni za tume Huru ya uchaguzi.
c.) Wabunge wanaotokana na kura za Urais. Kwamba wagombea urais ambao hawakushinda uchaguzi lakini walipata kura zaidi ya asilimia 1 ya kura zote moja kwa moja watateuliwa na tume ya uchaguzi kuwa wabunge.
Mgombea wa Urais aliyeshika nafasi ya pili baada ya majumuisho ya kura
zote moja kwa moja ndiye atakuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani.
Kwa undani zaidi unaweza kupakua pdf hapa chini.
Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.View attachment MUUNDO WA BUNGE- Mdude's Dreams.pdf