Elections 2010 Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza?

Katiba iundwe upya pale ambapo hatutakuwa na Chama kimoja chenye asilimia 80% bungeni, ama sivyo ni kutafuta ubias tu.
 
Anza na wewe kwanza kushiriki siasa Active, tunataka vijana wengi waende kuungana na wakina Mnyika na Zitto Kabwe pia

Zitto anaondoka Pengo lake litazibwa na Mwanakijiji kama atakubali.lakini hatujui kama Mwanakijiji ni kijana au Mzee.naamini anaweza kuziba pengo la Zitto Kabwe.

na Uenyekiti achukue Kitila Mkumbo kwani amewahi kuwa rais wa Daruso na pia mkuu wa Idara chuo kikuu cha Dar-es-salaam tunahitaji wanasiasa vijana kama Kitila sio wazee kama BAREGU au Ngaiza.
 
Chadema kuna Vijana wengi sana na sio hao tu, Kuna wengine ambao hawaonekani katika Jukwaa la Kisiasa na Kuna Samson Mgimba, Na watu wengine kibao
 
- CHADEMA chaweza kujipanga kuongoza taifa

Kinaweza endapo kitajipanga vizuri kuanzia ngazi ya shina hadi ubunge na hatimaye taifa.

- Ni mabadiliko gani ya kisera na falsafa ambayo yatasababisha Chadema kuonekana kujiandaa kuongoza?

Wajikite katika ‘Watu’ na ‘Haki’.

- Ni mabadiliko gani ya kiuongozi yataashiria mwanzo mpya kuelekea kuongoza taifa?

Uongozi wa juu wa Chama e.g. Mwenyekiti waachiwe Wazee, Vijana wawe Watendaji

- Je, ni nani ndani ya Chadema leo hii anaweza kuwa mgombea wao wa Urais na kwanini?

Mbowe anaweza kuwa Rais mzuri; Mzee Mwanakijiji, Dr. Slaa afaa kuwa Waziri Mkuu

Kuna ulazima wa wao kumsimamisha mgombea wa Urais?

Endapo watafanya tathmini ya kina na kuwa na uhakika wa ushindi wanaweza kusimamisha mgombea urais kwa mwaka 2010 vinginevyo wajikite kwenye Ubunge, Udiwani na nafasi za ngazi kata na mitaani.

- Kama Katiba haitabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa ikiongozwa na sheria ile ile je Chadema washiriki wakijua kuwa bado wako kwenye upande ambao ni vigumu kushinda kama taratibu hazitabadilishwa na kuwa za haki zaidi na usawa?

Kama uwezo wa kushiriki wanao, washiriki chaguzi zote, ili kuandika historia hata kama hawatatendewa haki.

- Je, kuna umuhimu wa kuungana na chama kingine chochote au Chadema ijizatiti kusimama peke yake?

Kama vyama vya CUF na NCCR watakuwa radhi kuungana kwa dhati na CHADEMA itakuwa changamoto ya kutosha kwa CCM. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

- Kwa vile wamepata nafasi nyingi za kuvutia watu na hali ya kisiasa imekuwa upande wao sana ni kwa sababu gani wameshindwa kuiangusha CCM kwenye majimbo kadhaa licha ya upepo wa kisiasa kuwa upande wao (chadema)? Je yawezekana ni dalili ya kutokuwa tayari kuongoza kitu ambacho kinatumiwa na CCM vizuri sana?

Kushindwa kuiangusha CCM kunatokana na contributing factors mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi wa vijijini kuhusu dhana nzima ya demokrasia na pia kutokana na ‘ujanja’ wa CCM wa kutumia udhaifu/unyonge wa wananchi wa vijijini. CHADEMA wakitumia nafasi mbalimbali na vyombo vya habari wazidi kuwaelimisha wananchi na kuwa karibu nao wakati wote.

- Ili waweze kukubalika kuliongoza taifa ndani ya mwaka mmoja na nusu hivi ni vitu gani vifanyike kwa Chadema au chama kingine cha kisiasa ambacho kitasababisha kuanguka na kuporomoka kwa utawala wa CCM?

Ushindi wa CCM unatokana zaidi na wananchi wa vijijini kuliko mijini. Kwa maana hiyo nguvu za chama chochote kinachotaka kuiangusha CCM lazima zielekezwe huko. Zibuniwe mbinu mpya, mbinu mbadala ambazo zinaweza kusaidia kuwafikia wananchi badala ya kutegemea hotuba za majukwaani tu. Wanachama wa CHADEMA ama vyama vingine vya upinzani na viongozi wao wajitahidi kupata wafuasi wa kweli ambao wako tayari kujitolea kutafuta wanachama ili kuongeza idadi ya ‘waumini’ wa mabadiliko watakaohubiri ulazima wa kuanguka kwa CCM.

Uovu wa CCM na ukiukwaji wa misingi bora ya uongozi ni sababu tosha ya kuweza kuiangusha CCM endapo wananchi wataeleweshwa wakaelewa.
 
Katika wote humo ndani wewe umejibu sahihi sana!! Asante sana kwa majibu mazuri na ya kisomi kama yako, Umeonesha kuwa unaelewa sana ndio tunataka kijana kama wewe maana unaweza kusaidi Taifa. Sina cha kuongezea asante sana
 
Chadema kuna Vijana wengi sana na sio hao tu, Kuna wengine ambao hawaonekani katika Jukwaa la Kisiasa na Kuna Samson Mgimba, Na watu wengine kibao

Mkuu na wewe ushajiunga na Chadema tayari? Wewe ni supporter mkubwa sana wa Chadema kwa ninavyo ona na they could use you more in their organization then here in JF.
 
Mimi ni Mchambuzi huru wenye mawazo huru na nimekulia katika mawazo huru, kwa hiyo sitaacha kusema ukweli, maana hata wewe unaujua ukweli huo maana sio kusema na kama leo Prof Othoman singekuwa Mkweli na kusema ukweli angekuwa wapi?? Mimi kama Kijana wa Kitanzania Msomi nina uwezo wa kujua, Hata hapa WanaJF wapo kwa ajili ya kuendeleza mijadala na uhuru wa kupata habari hata harakati za fikra mpya na uhuru wa kweli mzee wangu, Naijua CHADEMA sana,
 
Sawa mkuu lakini kama kijana hauoni wana kuhitaji kwenye chama chao. Hakuna anayekataa una mawazo huru au kwamba wewe ni msomi mkuu. Usipo jiunga wewe na chama unategemea nani ajiunge. Kama ulivyo sema wewe ni kijana so the best way both me and you can become part of the change is becoming part of the movement. JF is a start but it's not enough. The percentage of people we reach here is very small compared to the larger polulation. Pia most people in JF tayari wana party affiliations. Kuna wanachama wa vyama vingi hapa wanao promote sera ya vyama vyao so it is unlikely you are going to win any new votes here. Hapa JF we talk the talk but we also need to walk the walk. I myself am studying all the political parties very easy na kama kijana I will soon know where is the right place to make the biggest impact. Sawa tukutane JF mkuu but pia tukutane huko on the ground where the real change is needed. Where people don't have access to JF or any other source of information. Where the common mwananchi needs to be told the truth. Kuongea JF haitoshi, we need to go where we are mostly needed, where we can gain votes to benefit our country. Are you ready to walk the walk?
 
Umesema ukweli Ndugu yangu!! Tutaweza kuonana katika uwanja wa mapambano na katika hili tutaonana pindi muda mwafaka ukifika, Japo naweza nashiriki siasa za ndani sana , hata katika mawazo ya hapa na pale na pia katika hili tunaweza kabisa, I know that kuwa unaweza kuamua na kujiunga CHADEMA na Sio kingine maana ndio wameonekana kuwa wanaweza na kutoa changamoto halisi kwa CCM, Hivyo tutakuwa pamoja katika hili, Nimependa sana katika maandishi yako kwa kusema ukweli. Tunahitaji mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli. unajua kuwa leo ni maskini kwa sababu ya utawala wetu, so this is all about politics mzee wangu. Nakushauri jiunge CHADEMA na wengine wengi
 
Kama kweli wewe mzalendo na Taifa lako, utaanza na kuchukua hatua husika kwa ajili ya kulinda Taifa na vizazi vyetu na mali za Taifa
 
Tujiulize na sisi wenyewe humu ndani tunagombea nafasi zipi uchaguzi ujao na kwa vyama vipi au tunabaki kama tulivyo kutumia majina bandia, kuwatukana walioko madarakani na kutukanana sisi wenyewe, kuonyesha tuna uchungu na nchi yetu kwenye mitandao huku tukila kuku kwa mrija nje ya Nchi yetu,.....

kwani wanaokula kuku kwa mirija walioko ndani ya nchi wanafanya nini? Kutumia majina bandia wewe kunakuhusu nini kwanini usioneshe mfano wa kutumia jina lako halisi? Na nani humu anayetukana walioko madarakani? Na wale wanaojitukanisha wakiwa madarakani utamlaumu nani?

Hakuna CHAMA cha kuiondoa CCM madarakani au Bungeni kwa miaka kadhaa ijayo endapo vyombo vya DOLA havijaridhia. Tuvielimishe vyombo hivi kwanza hasa UwT na Polisi.

Hayo ni mawazo ya mtu anayejiona duni. Unafikiri hadi hivi sasa hatujavielimisha? Unafikiri yote unayoyasikia leo yanashuka toka Mbinguni?
 
chadema lazima kisimamishe mgombea wa urais 2010. lazima

kama chadema wasipo simamisha mgombea wa urais ni ujumbe gani wanatuma kwa wananchi wa TZ ambao wanamatumaini nao????

morali ni kitu muhimu sana kwenye siasa, chadema kutosimamisha rais kutashusha morali kwa wanachama wao

kama wasiposimamisha mgombea wa urais ni dhairi kabisa watakuwa wamewaambia wananchi wa TZ sisi atuwezi kushinda, wanachama itabidi watafute chama kinachojiamini
 
kwani wanaokula kuku kwa mirija walioko ndani ya nchi wanafanya nini? Kutumia majina bandia wewe kunakuhusu nini kwanini usioneshe mfano wa kutumia jina lako halisi? Na nani humu anayetukana walioko madarakani? Na wale wanaojitukanisha wakiwa madarakani utamlaumu nani?

Hayo ni mawazo ya mtu anayejiona duni. Unafikiri hadi hivi sasa hatujavielimisha? Unafikiri yote unayoyasikia leo yanashuka toka Mbinguni?
Hakuna chama cha kuoindoa ila WATANZANIA ndio mwenye uwezo wa kuwatoa CCM Madarakani na wengine, Lakini Kupitia CHADEMA Wanaweza kufanya haya yote
 
Sijui ni lini uchaguzi Mkuu wa Chadema utafanyika japo nakumbuka ulikuwa ufanyike katikati ya mwaka huu. Kwa vile muda uliobakia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ni kama mwaka mmoja na nusu tu, je:
- CHADEMA chaweza kujipanga kuongoza taifa
Nadhani CHADEMA kina nia ya kuleta mabadiliko ya kweli (NADHANI). Kinachotakiwa ni kupewa nguvu na watu wote wenye mapenzi mema ili kikuwe zaidi na kuongeza nguvu yake kimuundo. Ndio kinaweza kujipanga kuongoza Taifa vizuri tu.
- Ni mabadiliko gani ya kisera na falsafa ambayo yatasababisha Chadema kuonekana kujiandaa kuongoza?
Sera zinazotakiwa ni
1. zile ambazo zinajibu mahitaji ya Taifa kwa kipindi tulichopo na pia kuweka mwelekeo wa mipango ijayo katika kila sekta.
2. Sera zao ziwekwe katika maandishi ambayo yataweza kuelezeka kwa wananchi na kueleweka. Inatakiwa CHADEMA watafute consultant (ndani/nje ya chama) atakaeweza kusaidia kubainisha matatizo ya nchi na kutoa majibu yake kwa ufasaha na kwa lugha inayoshawishi kukubalika.
3. CHADEMA inatakiwa kuzungumza lugha ya wananchi walio wengi. Ni dhahiri kuwa wanaweza kuwafikia (kikauli) watu wengi wa mijini na kueleweka. Ila ili hiyo iweze kutoa tija kubwa, inabidi waweze kueleweka zaidi pia vijijini ambako kuna watu wengi zaidi na pia kuna majimbo mengi zaidi.
4. Mikakati ya kukisema chama fulani, ni kukijenga zaidi. CCM huwa wanasema vyama vya upinzani bila kutaja chama husika wakijua kuwa, wakikitaja watakuwa wanakijenga (ni ngumu kuelewa hili, lakini ndio ukweli wenyewe). Waizungumzie CCM kama chama tawala badala ya kukitaja kwa jina moja kwa moja.
5. Watafute wananchi wanaopendwa na kukubalika kwa wananchi kila sehemu (jimbo, Kata, mtaa) na wawashawishi kugombea nafasi za Ubunge, Udiwani na Uwenyekiti wa serikali za mitaa kupitia CHADEMA.
Ukweli ni kwamba, wananchi huchagua watu kabla ya chama. Hii itawasaidia kumnadi mgombea wao kwa urahisi zaidi
6. Wajue kura zao ziko wapi na ni ngapi. Wawe na takwimu halisi badala ya kuhisi ushindi bila kujua unapotokea. Mara nyingi hisia hizo huwa za plastic.

- Ni mabadiliko gani ya kiuongozi yataashiria mwanzo mpya kuelekea kuongoza taifa?
Sidhani kuwa uongozi wa ndani ya chama ni muhimu kwa ushindi wa uchaguzi mkuu. Labda kama uongozi huo una madhara ya moja kwa moja katika utafutaji kura, ulindaji wapiga kura wao au/na uteuzi wa wagombea n.k.
Nadhani CHADEMA ina uongozi mzuri tu, na hii inaweza kuwa moja ya sababu za mafanikio waliyonayo sasa. Wanachohitaji ni kuweka wazi jinsi wanavyopata uongozi, imani na maudhui ya chama na ushirikishwaji wa wanachama katika maamuzi ya kisera, kiuongozi n.k.

- Je, ni nani ndani ya Chadema leo hii anaweza kuwa mgombea wao wa Urais na kwanini? Kuna ulazima wa wao kumsimamisha mgombea wa Urais?
Swali hili ni gumu sana. Ila nitajaribu kulijibu kama ifuatavyo.
Mtu anaeweza kuwa mgombea mzuri wa CHADEMA ni lazima awe na sifa nzuri za kiuongozi. Sifa zinazojulikana na zinazoaminika bila makosa ya makusudi, tamaa, ubinfsi, wizi n.k. Sina jina la mtu huyo kwa sasa. Lakini kwa siasa za nchi yetu, mtu huyo anaweza kutoka popote (hata ndani ya CCM)

- Kama Katiba haitabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa ikiongozwa na sheria ile ile je Chadema washiriki wakijua kuwa bado wako kwenye upande ambao ni vigumu kushinda kama taratibu hazitabadilishwa na kuwa za haki zaidi na usawa?
- Je, kuna umuhimu wa kuungana na chama kingine chochote au Chadema ijizatiti kusimama peke yake?
Sidhani kuwa CHADEMA kwa jinsi inavyokuwa na kuendelea vizuri ina haja ya kuungana na chama chochote. Inachotakiwa ni kushawishi wananchama wa vyama vingine vyote (nguvu ya vyama hivyo) kuungana nao na kuutafuta ushindi katika uchaguzi.
Kuhusiana na Katiba. Ni kweli kuwa kwa Katiba ilivyo sasa, chama kingine chochote zaidi ya CCM hakina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wowote. Ila nina imani kuwa, madhara ya kukinyima chama kilichoshinda kihalali (hasa uchaguzi mkuu) ni makubwa na nchi nyingine zimetufundisha zaidi kuhusiana na hilo. Hivyo, si rahisi sana kwa chama cha upinzani kunyang'anywa ushindi kama kitashinda kwa kishindo.

- Kwa vile wamepata nafasi nyingi za kuvutia watu na hali ya kisiasa imekuwa upande wao sana ni kwa sababu gani wameshindwa kuiangusha CCM kwenye majimbo kadhaa licha ya upepo wa kisiasa kuwa upande wao (chadema)? Je yawezekana ni dalili ya kutokuwa tayari kuongoza kitu ambacho kinatumiwa na CCM vizuri sana?
Sidhani kuwa kushindwa kwa CHADEMA kunaashiria kutokuwa tayari kuongoza. Bali kunatokana na sababu nyingi, mojawapo ikiwa ni Katiba. Sababu nyingine chache ni zifuatazo;
1. Maandalizi ya kutafuta ushindi: Ushindi katika uchaguzi hutafutwa muda mrefu kabla ya kampeni na hatimaye uchaguzi wenyewe. Si rahisi sana kushinda uchaguzi kwa kufuatia Jimbo kuwa wazi na kuanza pilika wakati imetangazwa kuwa uchaguzi utafanyika siku fulani. Inatakiwa CHADEMA wajue kuwa majimbo yote yako wazi kuanzia tarehe fulani mwezi wa 10 mwakani na kura zianze kutafutwa sasa (kama wamechelewa kiasi hicho). Maana walitakiwa kuanza kuzitafuta mara tu baada ya uchaguzi uliopita. Bila hivyo, wanaoshikilia majimbo hayo au CCM watahakikisha kuwa wanarudi tena Bungeni. Na CCM huhakikisha hivyo mapema sana.
Kuanzia sasa kampeni zimeanza za wanaotaka kugombea Ubunge na Udiwani 2010 ndani ya CCM (kwa siri). Je, wapinzani wanafanya lolote? Maandalizi mazuri yanahitaji muda wa kutosha.

- Ili waweze kukubalika kuliongoza taifa ndani ya mwaka mmoja na nusu hivi ni vitu gani vifanyike kwa Chadema au chama kingine cha kisiasa ambacho kitasababisha kuanguka na kuporomoka kwa utawala wa CCM?

Wanachotakiwa kufanya ni yafuatayo;
1. Waanze sasa kupata wagombea, wawachuje kwa taratibu zao, wawape mipango ya kushinda na halafu wawatume waende kwenye sehemu wanazotaka kugombea kwa nia ya kutangaza nia, kufungua mashina/matawi na kuandaa mazingira (team) ya kampeni ifikapo mwaka 2010. Wajiandae kimuundo
2. Ni lazima sasa waandae kauli za kutumia kwenye kampeni ambazo zitawahakikishia ushindi. Waandae manifesto (ilani ya uchaguzi). Wasiogope kuiga baadhi ya mbinu za CCM kupata ushindi. Kama CCM wanazitumia na wanashinda kwanini wao wasiweze kuzitumia kutafuta ushindi huo huo?
3. Waweke nguvu nyingi kwenye kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu. Wawakilishi wao mitaani ndio watakaowekea mazingira mazuri kwao kushinda udiwani na ubunge mwakani. Msingi imara wa nyumba uko chini ya udongo. Wasidharau msingi maana nyumba haitajengeka, na ikijengeka haitakuwa imara.
4. Wahakikishe wanawafikia wananchi wengi iwezekanavyo. Waachane na malumbano ya kupoteza muda yanayofanywa na CCM, lengo lao ni kuwachelewesha kuchukua hatua na kushindwa kushinda uchaguzi mwakani. Wahakikishe kila dakika moja inazaa mafanikio yanayokusudiwa. Muda kwao lazima uwe ni mali isiyokubalika kupotea.
 
Mchango wako ni Muhimu sana katika Taifa Letu
 
Waachane na Urais, wajikite kwenye kuliteka Bunge kwanza, wakifanikiwa kuliteka hilo, watafanya mabadiliko yote ya sheria na katiba yatakayowarahisishia kuupata urais
CHADEMA au chama chochote kikidharau nafasi ya urais kitapunguza uwezekano wa kupata nafasi za Ubunge. Hili linaweza hata kusababisha wasipate wabunge kabisa.

Wananchi huchagua kwa kuamini kuwa Rais wa chama wanachokichagua akipata na Wabunge wake itasaidia kuharakisha maendeleo yao. Bila kuwa na mgombea wa URais, wananchi wengi hawatamchagua Mbunge wa chama hicho kwa kujua kuwa hataweza kufanya lolote kuwaletea maendeleo kwani chama kitakachoshinda kitapeleka maendeleo kule kilipopata kura za ubunge zaidi ya kule kilipokosa.

Kosa kubwa kabisa la kisiasa ambalo CHADEMA wanaweza kulifanya ni kutogombea uRais.
 
Siwezi kujua kwa sasa lakini sera za Chama Husika Huwa zinatolewa na Mgombea urais wkat wa Kampeni Sasa sisi kama wadau hatuwezi kukubali hali kama hiyo isitokee maana lazima CHADEMA wasimamishe mgombea
 
Sijui ni lini uchaguzi Mkuu wa Chadema utafanyika japo nakumbuka ulikuwa ufanyike katikati ya mwaka huu. Kwa vile muda uliobakia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ni kama mwaka mmoja na nusu tu, je:

- CHADEMA chaweza kujipanga kuongoza taifa
- Ni mabadiliko gani ya kisera na falsafa ambayo yatasababisha Chadema kuonekana kujiandaa kuongoza?
- Ni mabadiliko gani ya kiuongozi yataashiria mwanzo mpya kuelekea kuongoza taifa?
- Je, ni nani ndani ya Chadema leo hii anaweza kuwa mgombea wao wa Urais na kwanini? Kuna ulazima wa wao kumsimamisha mgombea wa Urais?
- Kama Katiba haitabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa ikiongozwa na sheria ile ile je Chadema washiriki wakijua kuwa bado wako kwenye upande ambao ni vigumu kushinda kama taratibu hazitabadilishwa na kuwa za haki zaidi na usawa?
- Je, kuna umuhimu wa kuungana na chama kingine chochote au Chadema ijizatiti kusimama peke yake?
- Kwa vile wamepata nafasi nyingi za kuvutia watu na hali ya kisiasa imekuwa upande wao sana ni kwa sababu gani wameshindwa kuiangusha CCM kwenye majimbo kadhaa licha ya upepo wa kisiasa kuwa upande wao (chadema)? Je yawezekana ni dalili ya kutokuwa tayari kuongoza kitu ambacho kinatumiwa na CCM vizuri sana?
- Ili waweze kukubalika kuliongoza taifa ndani ya mwaka mmoja na nusu hivi ni vitu gani vifanyike kwa Chadema au chama kingine cha kisiasa ambacho kitasababisha kuanguka na kuporomoka kwa utawala wa CCM?

Mzee Mwanakijiji,

Huu uchaguzi si ulikuwa ufanyike mwishoni mwa mwaka jana? nakumbuka wakati wa ugomvi na Wangwe, walisema hakuna haja ya kujaza pengo la nafasi ya makamu Mwenyekiti wakati uchaguzi utafanyika kama miezi sita ijayo.

Hivi uchaguzi unaendeshwa kwa katiba au mpaka mshika mkoba aamue?

Pamoja na madudu ya CCM lakini inajulikana lini uchaguzi husika utafanyika. Hili ni muhimu ili viongozi feki wasipitishe vipindi vyao kwa kuogopa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom