Elections 2010 Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza?

chadema haiwezi kuanza kufikiria kuongoza taifa wakati viti vya ubunge hata 10 hawana! ..
wajipange kwanza kuanza kujuulikana vijijini ambapo ndio kuna wapiga kura wengi zaidi.

Gaijin, Mimi niko tofauti na wewe kidogo. CHADEMA imeanza kuwa vizuri zaidi kwa kipindi hiki cha miaka mitatu iliyopita, sasa swala la kuwa na wabunge wengi litegemewe kwenye next election 2010. Kutokana na CHADEMA kuonyesha upinzani mkali kwenye chaguzi ndogo hadi kusababisha UONGOZI mzima wa CCM kwenda ku-support wagombea wao inaonyesha wazi kuwa CCM watakwamwa kwenye uchaguzi mkuu kwa sababu majimbo yote yatakuwa yanagombewa kwa pamoja. Sioni uwezekanao wowote ule wa VUONGOZI wakuu wa CCM kuzunguka nchi nzima.

Kwa hiyo wana JF ambao tunahitaji mabadiliko tunatakiwa kutafuta na namna ya kufanya uhamasishaji ili kuing'ona CCM kwa kuhakikisha Wapinzani wanapata idadi kubwa ya viti vya ubunge.

TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ndugu yangu Augustine Moshi hivi Mzee Slaa unamjua vizuri? Au na wewe umeingia kichwa kichwa kwenye ushabiki wa kutaka Slaa agombee Urais? Si kila king'aacho ni dhahabu!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Tukiendelea na VIPIMO hivyo vya zamani badala ya kumuangalia mtu jinsi alivyo sasa na anayoyasimamia hatutapata viongozi tunaowataka. Dr Slaa akiwa Padre na hata alipokuwa CCM sio huyu wa sasa. Hata Obama alivuta Bangi ujanani.
 
TAARIFA mpya za uchunguzi wa kifo cha msanii Michael Jackson zimeonyesha matokeo ambayo yanashangaza kwa kiasi kikubwa.

Vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni vimefichua kuwa msanii huyo alikuwa amedhoofika kiasi cha kutisha na kubakia mifupa kutokana na kutokula na kisha kutumia kiasi kikubwa cha vidonge.

Uchunguzi huo umeonyesha kuwa baada ya kifo chake mabaki ya baadhi ya vidonge hivyo yamekutwa tumboni mwake.

Mwili wake, uchunguzi huo umebaini kuwa ulikuwa umedhoofu kiasi kwamba kiuno, mapaja na mabega yake yalikuwa na matundo ya vidonda vingi vya sindano, vinavyodhaniwa kuwa ni vya sindano za kutuliza na kuondoa maumivu ambazo alichomwa mara tatu kutwa, tena kwa miaka mngi.

Pia, amekutwa na makovu mengi yaliyotokana na upasuaji wa mara 13 ailiofanyiwa kwa ajili ya kubadili sura yake.

Wataalam hao wamegundua uchunguzi wa kusikitisha wenye kuonyesha kuwa msanii huyo, Wacko Jacko hali yake ilikuwa imedhoofu wakati mauti yakimkuta wiki iliyopita mjini Los Angeles.

Uchunguzi huo umeonyesha kuwa licha ya kuwa na urefu wa futi tano na inchi 10, lakini msanii huyo alikuwa amepungua uzito na kubakia na kilo chache ambazo hazilingani na urefu wake.

Wataalam hao wanaeleza kuwa alikuwa akila mlo mmoja kutwa, kiasi kwamba wakati akifariki tumbo lake lilikuwa tupu, mabaki ya vidonge vilivyoanza kusagika ambavyo alitumia na sindano ambazo hatimaye zilisababisha moyo wake kusimama. Sampuli zaidi zimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kichwani, Wacko Jacko alikuwa amepoteza nywele karibu zote. Mfalme huyo wa pop, uchunguzi umeonyesha kuwa alikuwa akivaa nywele bandia, ambazo wachunguzi hawakuwa na kazi ya kuziondoa kwa ajili ya uchunguzi wao.

Kichwani mwake, upande wa sikio la kushoto, alikuwa na jeraha kubwa ambalo liliacha upara kutokana na ajali ya mwaka 1984 wakati alipoungua moto akipiga picha ya filamu ya tangazo la Kampuni ya Pepso.

Mwili mwake, wachunguzi hao wamebaini kuwa alikuwa amevunjika mbavu kadhaa, ikiaminika kuwa zilitokana na juhudi za kujaribu kuokoa maisha yake baada ya kuzimia. Matundu manne ya sindano yamegundulika karibu na moyo wa msanii huyo.

Uchunguzi huo umeonyesha kuwa harakati za kumwokoa ndizo zilizomsababishia madhara hayo yakiwamo ya sindano tatu zilizochomwa na kupenya ukuta wa moyo wake, kumsababisha madhara.

Katika uchunguzi huo, imeonekana kuwa magoti ya Jackson na sehemu ya mbele ya ugoko wake zilikuwa na majeraha kama ilivyokuwa mgongoni mwake.

Daktari wake binafsi, Conrad Murray, ambaye alikuwa karibu na msanii huyo amekamatwa na kuhojiwa huku familia ya msanii huyo ikieleza kuwa inataka uchunguzi zaidi unatakiwa kufanyika.

Dk Murray, ndiye anayeaminika kumpiga sindano msanii huyo kabla ya umauti kumkuta, akiaminika kumpa dawa iitwayo Demerol, jambo ambalo limemwingiza katika mzozo wa kitibabu.

Rafiki wa karibu wa familia, Mchungaji Jesse Jackson alieleza wasiwasi kuhusu chanzo cha kifo cha msanii huyo na kutaka uchunguzi zaidi na mtaalam, Dk Murray ambaye alikodiwa na Kampuni ya AEG Live , ambayo ilikuwa na jukumu la kuandaa matamasha 50 ya msanii huyo, katika ukumbi wa O2 Arena, London mwezi ujao, achunguzwe zaidi.
 
kama jf mmekata tamaa kiasi hicho, watanzania wa kawaida watakuwa vipi. mi nafikiri kila kitu kinawezekana. bahati mbaya tumejenga jamii ya wabeuzi, hakuna jema tunalolitarajia katika siasa. tubadirike, ikiwezekana tuwe mfano. chadema wanaweza kushika hatamu ya uongozi wa nchi hii.
 
Lukundo, mbona unatuchanganyia madesa. Hili swala la Michael sio mahala pake hapa.
 
Mkuu tunavilimishaje? Hebu tupe njia ambazo wewe ungezi tumia kuvielimisha hivi vyombo vya dola. Maana mimi naona tatizo la vyombo vya dola vina tokana na mamo makuu mawili:
1.Kuna nafasi nyingi sana ambazo mtu huteuliwa na raisi na anaweza kuondolewa muda wowote raisi atakapo amua. Hivi nafasi ni pamoja na msajili wa vyama, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, mkurugenzi wa UwT, mkurugenzi wa Takukuru nk. Sasa watu hawa unategemea uwaminifu wao utakuwa wapi kama siyo kwa raisi? Na tunajuaje kama wenyewe hawapewi hizo nafasi on the basis of being loyal members of CCM?

2.By default watu huogopa aliye juu yake. Kwa hiyo unakuta mtu anafanya yale yanayo mpendezea CCM bila kujijua kwa maana mtu anataka kumridhisha boss.

Mimi ushauri wangu ni kwamba tuangalie vizuri hizi nafasi zinazo teuliwa na raisi zina madhara gani. Kama mtu kula yake ina tegemea furaha ya raisi hata uumpe somo vipi hata kuelewa. Leo hii hata wewe Wilcard kama unamtegemea mtu kwa ajili ya maisha yako hata nikueleze vipi hafai huto nisikiliza and that is human nature.
MwanaFalsaFa1,
Teuzi za Rais hazipaswi kuwa kikwazo hapa. Kule UwT anayeteuliwa na Rais ni mmoja tu vivyo hivyo na kule Polisi. Tuwape elimu ya kutosha hawa wadogo. Sidhani kama hawaioni hali tuliofikishwa na CCM ambamo wao pia inawaumiza.
Teuzi za Rais ni kwa mujibu wa KATIBA yetu ya sasa ambayo kwa kweli ndio ya kupigiwa kelele ibadilishwe. Na hapa kwa maoni yangu ndio pa kuanzia badala kufikiria CHADEMA ijipange upya kwani hata kuchukua Busanda tu wameshindwa na hawatachukua Biharamulo pia.
 
Mimi nakwambia mkuu, Mwakani CCM wajiandae labda wafanye mambo ya ajabu sana na kwa kuwa wanajua washindani wao ni CHADEMA, wanawapangia mikakati ya Kishetani ili washinde, Utashuhudia mengi sana mwakani na kujua hali ya mambo ikoje maana Tazama tu chaguzi ndogo jinsi CCM wanavyoweza kuhangahika sana jinsi ya kushinda hata kutumia njia za panya ili kufanikisha mwizi huo
 
Bad logic. Kabla ya TANU kuanza kujipanga kuongoza Tanganyika ilikuwa na viti vingapi?

CHADEMA iongoze maandamano ya kudai mazungumzo ya kubadili katiba. Lazima kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwanza. Kwa sasa CCM inazunguka ikitishia kuwafukuza kazi viongozi wa Tume ya Uchaguzi. Hilo litabadilika kama Tume ya Uchaguzi itachaguliwa na vyama vyote, na kuajibika kwa Bunge na sio kwa Rais.

Dr. Slaa is Presidential material. Akisimama atakumbatiwa na wananchi. He has name recognition and is charismatic. Na ni sumu ya CCM.

challanging person stay aside to challenge. lets find a strong foundation . kiujumla kujipanga muhimu lakini slaa hatafaa kuwa presdaa anatakiwa awe upande wa changamoto .
 
Kuna watu wengi sana ila bado kujitokeza maana, kuna watu wengi sana ila wakati mwingine CCM wanatumia wanatumia mianya kama hiyo kwa ajili ya kusema bado but it is so enough man
 
1.Chadema wananafasi nzuri sana ya kushika nchi maoni yangu ni kuwa 2010 wasimsimamishe Mbowe kuna mtu wao msomi sana ambaye nafahamu wantaka kumsimamisha huyo ili akina mbowe wagombee majimbo.
2.Sasa hivi wembe ule ule ili mradi viongozi wa kimila,kidini,kijamii,vijana na wasomi wanawakubali sana watumie mtaji huo wakushawishi na kuwa na wanachama hai ambao watashiriki katika chaguzi za majimbo yote hata pale wakiona hawana nguvu wao waweke tuu ili mradi kutandaza mtandao.

3.Waangalie swala la uchaguzi wa mwezi wa kumi wa serikali za mitaa mwaka huu baada ya bunge kampeni yao ya Sangara ikite zaidi vijijini
4.Waelewe kabisa kwamba wanajijenga ili kuwa chama chenye nguvu na vilevile chama kikuu cha upinzani wanaweza kushirikiana na cuf kwa upande wa zanzibar kwa sababu sasa sheria imeruhusu vyama kuungana wakati wa uchaguzi
5.waangalie sana kuwahamasisha akina mama ambao ndio wengi nchini idara yao ya wanawake,vijana,na wazee waziimarishe kwa nguvu zote
baada yaho nataka kujua
Josh thread zako zote ni chadema vipi mkuu unawania ubunge jimbo fulani nini hebu tupashe.
 
Bad logic. Kabla ya TANU kuanza kujipanga kuongoza Tanganyika ilikuwa na viti vingapi?

CHADEMA iongoze maandamano ya kudai mazungumzo ya kubadili katiba. Lazima kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwanza. Kwa sasa CCM inazunguka ikitishia kuwafukuza kazi viongozi wa Tume ya Uchaguzi. Hilo litabadilika kama Tume ya Uchaguzi itachaguliwa na vyama vyote, na kuajibika kwa Bunge na sio kwa Rais.

Dr. Slaa is Presidential material. Akisimama atakumbatiwa na wananchi. He has name recognition and is charismatic. Na ni sumu ya CCM.
Ya ukweli hii Dr. huyu ni material ya kweli ya urais kwa Tz
 
NAweza kufanya hivyo lakini kuna Hoja ya Msingi hapa, Wale wote walipata kura kama laki tano ya urais wame wamepata ubunge moja kwa moja na kufanya bunge letu liwe na watu makini sana hata kutumia uwezo wao
 
Ndugu yangu Augustine Moshi hivi Mzee Slaa unamjua vizuri? Au na wewe umeingia kichwa kichwa kwenye ushabiki wa kutaka Slaa agombee Urais? Si kila king'aacho ni dhahabu!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bishanga kwani jk mlipompa nchi mlikuwa mnamfahamu? Infact kwa Tanzania the way mambo ninavyoyaona unlike enzi za mwalimu, kwa sasa mtu yeyote anaweza kuwa rais au waziri. Otherwise tungekuwa serious kuhusu hilo hao wanaotuongoza wasingekuwa hapo walipo. By the way, huyo aliyeko madarakani cha mno nini anachokifanya ambacho hata wewe hukiwezi?
 
Hapana shaka Ametoa mchango mkubwa sana Bungeni na tena aliweza hata kufanya kile wale wakina Selelii wanafanya leo kwa kuiga nao wapo kwenye mfumo mbovu, ila
 
Lishayasema haya Katika Makala yangu kuhusu CHADEMA, Kuna tumaini Jipya kwa Kizazi hiki na pia watu ndio wafahamishwe tu, Hakuna nichoshindikana
 
kwa mtazamo wangu naona kuna vitu kadhaa vinatakiwa kufanyika kabla chadema[au chama kingine]kishinde uchaguzi.kwanza kabisa ni ngumu sana kushinda uchaguzi kwa kutegemea mashabiki wa wakati wa uchaguzi,NI LAZIMA KUWA NA MTANDAO WA WANACHAMA.chukulia mfano wa chaguzi ndogo hizi zilizopita kwa mfano wa busanda,chadema walikuwa na mashabiki wengi sana waliokuwa wanahudhuria mikutano yao,lakini sio wananchama,nguvu ya shabiki wa chama ni kama nguvu ya soda,lakini nguvu ya wanachama ndio hasa nguvu ya uhakika kwa uhai wa chama na kujihakikishia kushinda uchaguzi.
vyama vingi vya siasa vimebaki kuwa na mashabiki,tena wa muda tu,wakati wa chaguzi mbalimbali,baada ya uchaguzi kwisha wanarudi likizo.operesheni sangara ilikuwa ni mradi mzuri mzuri sana wa wa chadema kujihakikishia na kujitambua kiasi gani inakubalika kwa wanachi katika maeneo husika,ili inapofika wakati wa uchaguzi wanajua kabisa eneo flani tuna wanachama kadhaa,kwahiyo tutahitaji nguvu kiasi flani kuwashawishi hao wasio wanachama,na pia wanachama wa eneo husika wanaweza kushiriki kwa kiasi kikubwa kushawishi wananchi wenzao ambao sio wanachama wao kukipigia chama chao kura[kitu ambacho hakiwezi kufanywa na shabiki]
kwahiyo mapendekezo yangu kwa vyama vya upinzani viache kusubiri chaguzi mbalimbali ndipo viamke na kwenda kwa wanachi,wakati ambako kunakuwa hakuna uchaguzi ndio wakati mzuri zaidi wa kujitangaza na kutafuta kuungwa mkono na wananchi kuliko wakati wa uchaguzi ambako chama kinakuwa kwenye presure za kutafuta kura na kinaweza ku-over look jukumu la kutafuta wanachama,kosa ambalo si rahisi kulifanya kukiwa hakuna uchaguzi.
pili vyama viaze kujijenga hadi vijijini[kwa kutumia wanachama vinaowapata huko]kwa kufungua ofisi hadi vijijini,kitu ambacho kinaweza kusaidia kurahisisha ushindi hasa kuazia chini kwenye ngazi za serikali za mitaa,na kuendelea hadi uchaguzi mkuu.ni vyama cichache sana vyenye angalau ofisi hata kwenye kata tu,achilia mbali vijijini.

ni mtazamo tu,
 
Wewe umesema ukweli kabisa na ndio maana tunasema kuwa sisi kama Taifa tumechoka na tunataka Chama Mbadala
 
CHADEMA kwanza wanatakiwa kuacha kuiga ''siasa'' za CCM. CCM imeundwa kwa misingi tofauti na CHADEMA na kuiiga CCM inakuwa ni sawa na jinsi Afrika inavyoendelea kuwa masikini kwa sababu ya kuhangaika kuiiga Ulaya ( ambayo historia yake imeiweka hapa ilipo).
CHADEMA wanapaswa kufocus kwenye kuwadhihirishia wananchi kuwa CHADEMA ni waaminifu. Imani ya watanzania kwa vyama vya siasa, NGOs, Serikali na Viongozi haipo tena. Ukweli ndio huu. Mtu, watu au chama kitakachoweza kurudisha imani kwa wananchi watakuwa na mafanikio makubwa kisiasa.
CHADEMA sasa hivi nayo inajiingiza kwa kasi kubwa sana kwenye siasa za hila, vurugu, malumbano etc. Hii inafanya CHADEMA ionekane haina tofauti na CCM. Ukienda Dodoma leo hii, huwezi kuona tofauti kati ya mbunge wa CHADEMA na yule wa CCM. Unadhani wananchi wataamini vipi kwamba CHADEMA ni tofauti iwapo wote wanatafuna kwa mtindo huohuo?
CHADEMA pia wanatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Siasa za uchuuzi hazina manufaa yoyote. Mfano, Mbowe alipata ubunge. Kulikuwa na kila sababu ya Mbowe kutokuliachia lile jimbo lirudi kwa CCM. Sasa hivi tunaona Zitto naye anasurrender jimbo. Hii inadhihirisha kuwa CHADEMA kila mtu ana agenda yake na hakuna agenda ya chama. Kwa mtindo kama huu watakuwa wananusa na kuachia na hawatafika popote.Urais ni rahisi kuutamka lakini kama huna wabunge usitegemee kupata uraiskwa jinsi siasa za Tanzania zilivyo.
CHADEMA inapaswa kuonyesha usafi wa hali ya juu ili iaminiwe. Chaguzi zao za ndani tu zimejawa na mizengwe. Matumizi ya ruzuku yamejawa na mizengwe. Katika hali kama hii hata ukipiga makelele vipi unaonekana another mlaji tu.
 
yeah ni kweli huu ni wakati wa Chadema...lakini inabidi kazi ya ziada sana ifanyike bila na kuwa na tamaa kubwa ya kuingia ikulu...kwanza wajipange kisera...wahakikishe wanachukua majimbo mengi 2010 ili idadi yao iwe kubwa bungeni...huu ni wakati wa kujiandaa na kuandaa timu yao...wapeleke watu majimboni, vijijini, watafute watu wanaokubarika katika maeneo yao ili wawasimamishe kwenye uchaguzi ujao wa ubunge.
chadema ina advantage nyingi, moja ni kwamba wamepata recognition nzuri na pili safari hii CCM imeboronga sana na kila mwenye akili ameona...ila wasipojipanga...ikiwa ni kujua kwamba kula anakoachia Zitto wamemuandaa nani?? je hakuna uwezako wa kumshawishi Zito kuendelea???
 
Back
Top Bottom