Elections 2010 Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza?

Hakuna chama cha kuoindoa ila WATANZANIA ndio mwenye uwezo wa kuwatoa CCM Madarakani na wengine, Lakini Kupitia CHADEMA Wanaweza kufanya haya yote

Michael kwanza inabidi uwe na chama kama Taasisi sio chombo cha watu wachache.chama chako bado kina mapungufu mengi Ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.

kwanza unatakiwa upate Mwenyekiti kwa maana ya Mwenyekiti sio mtu wa kuruka na helkopta ndio iwe sifa ya uenyekiti. ndio nikapendekeza kuwa pamoja na yaliyomkuta Kitila na Mfanyakazi wake wa ndani bado KITILA ni ASSET kwa Chadema,Mbowe ana mambo mengi ambayo yanawazuia watu kujiunga na Chadema. kina Morgan au Zumma wamepita kwenye movements ambazo zimewajenga kisiasa.

Mbowe si mtoto wa Masikini,baba yake na familia yake zimenufaika sana na serikali ya Nyerere,elimu duni ya Mwenyekiti n.k ni mambo ya Chadema kuyafanyia kazi,lakini kama Katiba haifuatwi uchaguzi ulikuwa ufanyike toka Mwaka jana hakuna kilichofanyika au hadi wanachama waandamane kwa msajili wa vyama ndio uchaguzi ufanyike? kama ni Wangwe amekwishakufa mnaogopa nini kufanya chaguzi?

Upendeleo wa wazi kuteua wabunge wa viti maalum ni ushahidi kuwa Chadema kina safari kubwa ya kuwa chama kama Taasisi ni si kundi la watu wachache wenye nasaba za kifamilia.hawezekani Ndesamburo aseme "Mwanangu Lucy Owenya awe mbunge kwa tiketi ya Chadema" na hakuna kura wala taratibu iliyopitisha kwenye chama kumpa wadhifa huo.

KOMMU nae akasema mke wake ANNA KOMU awe mbunge na akawa. yaani Chadema hawana baraza au jumuiya ya kina mama au wanawake ambako ungefanywa uchaguzi kuwapata wabunge wa viti Maalum?
 
Mzee Mwanakijiji,

Huu uchaguzi si ulikuwa ufanyike mwishoni mwa mwaka jana? nakumbuka wakati wa ugomvi na Wangwe, walisema hakuna haja ya kujaza pengo la nafasi ya makamu Mwenyekiti wakati uchaguzi utafanyika kama miezi sita ijayo.

Hivi uchaguzi unaendeshwa kwa katiba au mpaka mshika mkoba aamue?

Pamoja na madudu ya CCM lakini inajulikana lini uchaguzi husika utafanyika. Hili ni muhimu ili viongozi feki wasipitishe vipindi vyao kwa kuogopa uchaguzi.

Unamuonea Mwanakijiji haliwezi hilo na katika duru za JF hakuna hata Kitila hana jibu lake.
 
Mwanakijiji, WHY CHADEMA of all parties? What makes THEM so special to be given the right to lead this country? Please answer that one.
 
ndani ya baraza la mawaziri wanaoana na kufanya dating...itakuwa vyama...no more comment..ila WANAUME WENGI WENYE VIGOGO WAMEJEUKA ENGNEER KAZIBWE!!!
 
Mzee Mwanakijiji,

Huu uchaguzi si ulikuwa ufanyike mwishoni mwa mwaka jana? nakumbuka wakati wa ugomvi na Wangwe, walisema hakuna haja ya kujaza pengo la nafasi ya makamu Mwenyekiti wakati uchaguzi utafanyika kama miezi sita ijayo.

Ndio maana nimeuliza. Kwa jinsi ninavyoelewa uchaguzi utakuwa katikati ya mwaka huu na mwezi Juni ndio umetoka huo hivyo labda baada ya uchaguziwa Biharamulo. Hata hivyo sioni sababu ya kugandisha Katiba kwa ajili ya uchaguzi. Ishara mojawapo ya chama kukomaa ni kuweza kufuata Katiba yake no matter what.

Na ukimya wa kutotoa taarifa ili watu wajue inafungua mwanya wa watu kudhania na kushuku.

Hivi uchaguzi unaendeshwa kwa katiba au mpaka mshika mkoba aamue?

Inategemea Katiba inasemaje; kama Katiba inasema uchaguzi hadi mshika mkoba aamue, basi ndiyo Katiba hiyo. So, hadi sasa sijaona kama kuna hoja ya Katiba kutofuatwa.


Pamoja na madudu ya CCM lakini inajulikana lini uchaguzi husika utafanyika. Hili ni muhimu ili viongozi feki wasipitishe vipindi vyao kwa kuogopa uchaguzi.

Inategemea na Katiba yao. Na sheria ya vyama vya siasa inasemaje. Siamini kama kuna sheria imevunjwa. Naamini tatizo ni mawasiliano. Ni vizuri kama viongozi kutoa taarifa ili wananchi na hasa wanachama wao wajue nini kinaendelea. Vinginevyo ni kukaribisha minong'ono isiyo ya lazima.
 
Mwanakijiji, WHY CHADEMA of all parties? What makes THEM so special to be given the right to lead this country? Please answer that one.

where did I mention the so called "the right to lead" this country? Show me and I'll answer ur question.
 
Ina maana chadema hawajui wataifanyia nini nchi mpaka mtumie JF kujadili?

Kwani yote tunayojadili kuhusu CCM ina maana CCM wao hawayajui?
a) Bado sana!! waclare kwanza issue ya ukabila?

mara ngapi ndio utaridhika? Na ukabila ni nini hasa?

b) Wadeclare financial scandals ambayo alianza kudodosa wangwe?

Umewahi kuulizia financial statements zao ukakataliwa? Umetafuta ripoti za ukaguzi ukaona kuna tatizo?


c) Watafute candidate mzuri (zanzibar) vinginevyo hakuna kitu imekaa kibara zaidi?

Maana yake nini?
 
Mtaji mkubwa wa sisiem ni ujinga(ignorance ) na umaskini wa watanzania hususan waliopo vijijini. Nguvu za ziada zinahitajika kuleta mabadiliko ya kweli. Innovations za hali ya juu zinahitajika kuingoa sisem madarakani. Moja ya mbinu ni kwa kutumia nyimbo, mashairi, riwaya n.k. Wote twafahamu role ya nyimbo propaganda zilivyotumika kum-demonise idd amin, kupamba vikra za mwali na kujenga uzalendo. Kwa kutumia wasanii makini wanaoweza kutunga kazi za kina na elimishi. We can get somewhere.
 
Penye nia pana njia.Vyama vya upinzani kwa sasa,hawana nia ya dhati ya KUTOA RAIS ATAKAYE ONGOZA TANZANIA HII bali wanataka kuongoza kwa remote control.
Nasema hivyo kwa sababu hakuna hata kiongozi mmoja au chama ambacho kimesema kitafanya nini na vp kama kikipewa dhamana bali wanasema CCM imeshindwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi.
Na wanawaelekeza CCM nini cha kufanya.
 
Hata mimi nashangaa kuona hilo maana wana kila hali ya kufanya hivyo na kushinda uchaguzi
 
Ndugu yangu Augustine Moshi hivi Mzee Slaa unamjua vizuri? Au na wewe umeingia kichwa kichwa kwenye ushabiki wa kutaka Slaa agombee Urais? Si kila king'aacho ni dhahabu!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Acha vitisho hata wewe humjui anayemjua ni mke wake tu!!
 
Ni kweli kabisa mzee wangu kwa kipindi hiki,ni chama kizuri sana na hata watu wake wako makini sana
 
Sijui ni lini uchaguzi Mkuu wa Chadema utafanyika japo nakumbuka ulikuwa ufanyike katikati ya mwaka huu. Kwa vile muda uliobakia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ni kama mwaka mmoja na nusu tu, je:

- CHADEMA chaweza kujipanga kuongoza taifa
- Ni mabadiliko gani ya kisera na falsafa ambayo yatasababisha Chadema kuonekana kujiandaa kuongoza?
- Ni mabadiliko gani ya kiuongozi yataashiria mwanzo mpya kuelekea kuongoza taifa?
- Je, ni nani ndani ya Chadema leo hii anaweza kuwa mgombea wao wa Urais na kwanini? Kuna ulazima wa wao kumsimamisha mgombea wa Urais?
- Kama Katiba haitabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa ikiongozwa na sheria ile ile je Chadema washiriki wakijua kuwa bado wako kwenye upande ambao ni vigumu kushinda kama taratibu hazitabadilishwa na kuwa za haki zaidi na usawa?
- Je, kuna umuhimu wa kuungana na chama kingine chochote au Chadema ijizatiti kusimama peke yake?
- Kwa vile wamepata nafasi nyingi za kuvutia watu na hali ya kisiasa imekuwa upande wao sana ni kwa sababu gani wameshindwa kuiangusha CCM kwenye majimbo kadhaa licha ya upepo wa kisiasa kuwa upande wao (chadema)? Je yawezekana ni dalili ya kutokuwa tayari kuongoza kitu ambacho kinatumiwa na CCM vizuri sana?
- Ili waweze kukubalika kuliongoza taifa ndani ya mwaka mmoja na nusu hivi ni vitu gani vifanyike kwa Chadema au chama kingine cha kisiasa ambacho kitasababisha kuanguka na kuporomoka kwa utawala wa CCM?

Kama wachangiaji wengine walivyo kwisha sema, mimi pia nadhani CHADEMA waanze sasa kueleza ni nini watafanya tofauti na CCM pindi wakiingia madarakani. Mfano,

1. wanaweza kuweka issues kwamba hawatakuwa na wakuu wa wilaya wa kuteuliwa isipokuwa watachaguliwa na wananchi na cheo cha mkuu wa mkoa kitafutwa.

2. elimu ya msingi bure,
3. elimu ya sekondari ni lazima kwa kila mtoto hadi form 4 na serikali itagharamia nusu ya ada ya watoto wote ktk sekondari za serikali.
4. mishahara ya wafanyakazi itapanda kila mwaka kwa flat rate
5. n.k.

Kuhusu presidential candidate, mi nadhani mwanasheria Tundu Lissu anafaa kama atapendekezwa na chama.
 
I told you guys, kuwa CHADEMA kuna watu wengi sana wenye uwezo wa kuongoza na pia hata wapo fit kisiasa. ngoja usubiri uone mambo yako vipi
 
Mwanafalsafa,with due respect kwa uhuru wa kulonga ndani ya JF kwa hili mimi naomba Kanisa Katoliki likitaka ndo liongee,nisamehe ndugu yangu.

Ushauri wa bure kwako Bishanga,

1.Acha kabisa kuamsha kiu usiyoweza kuikidhi.JF si mahala pake.
2.Ukishindwa,rejea kanuni namba moja hapo juu.
 
Back
Top Bottom