Elections 2010 Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza?

Kuhusu presidential candidate, mi nadhani mwanasheria Tundu Lissu anafaa kama atapendekezwa na chama.[/QUOTE]

Wakimsimamisha LIssu watakuwa wamecheza kweli,Jamaa anajiweza kweli,l na wanachi wanamwamini sana akini waanze sasa kuangalia watu wanaoonyesha kutaka kugombea majimbo ili waanze kuimarisha maeneo ya majimbo ya uchaguzi
 
Wakati ukifika tutasema nani ni Bora zaidi kuliko wote kati yao maana kila mtu ataweza kusema kuwa anafaa kuliko mwingine kati yao
 
Wanabodi,
Maoni yangu kwa chama Chadema yataendelea kuwa yaleyale kuwataka waungane na vyama vingine nikiwa na maana vichwa vya watu toka pande zote wajipange pamoja kugombea uchaguzi mwaka 2010. Kama ilivyokwisha tokea, ikiwa vyama vingine havitaki kujiunga basi wale viongozi na wananchama wanaotaka Muungano wajiunge na Chadema kwa sababu nafasi yetu kujiunga ipo wazi kabisa..
Kifupi ktk mbinu za kujiandaa hata ikibidi kuwafuata na kuwaomba wajumuike na Chadema ktk kugombea mwaka 2010 basi jambo hilo lifanyike kwa nia njema ya kujali maslahi ya Taifa letu.

Pili, wazo la kiti cha Urais ni gumu sana kwa sababu wananchi huchagua jina la mtu na umaarufu wake. Ni lazima Chadema au Upinzani kama wataungana kusimamisha jina litakalo weza kuuzika kwa wananchi..Kama ingekuwa amri yangu Dr. Slaa pekee ndiye anasimama mbele ya Mbowe kwa umaarufu sasa hivi.
Na sidhani kama kuna ubaya kama akifuatwa mtu kama Salim.A Salim na kurubuniwa nafasi hiyo maadam tu Chadema ipate kupita mtihani huu wa kwanza. Nasema salim kwa sababu sii dhambi kabisa kuhama chama kwa sababu ya maslahi ya Taifa..
Kikwete ambaye ni rais wetu alitishia kukihama chama CCM ikiwa asingechaguliwa kusimama uongozi wa CCM..Hivyo basi kama kuna dhambi au makosa nadhani Kikwete alifanya kwa herufi kubwa..
Nionavyo mimi Salim A. salim anaweza kusimama na Kikwete na akashinda bila kutegemea ni sera zipi anakuja nazo kwani NDIVYO TULIVYO..
Na mwisho ni lazima Chadema wafahamu, waelewe na kuzingatia kwamba Wadanganyika wote - NDIVYO TULIVYO. Mbinu ,ahadi na maandalizi yote yafanyike kwa kufikira WATU na MAZINGIRA tunayoishi na siii Siasa nyingi za sera na mrengo wakati wananchi wenye njaa wanataka kuona ugali mezani..

Haya ni maoni yangu tu kutokana na jinsi nilivyowasoma wadanganyika..
 
Wanabodi,
Maoni yangu kwa chama Chadema yataendelea kuwa yaleyale kuwataka waungane na vyama vingine nikiwa na maana vichwa vya watu toka pande zote wajipange pamoja kugombea uchaguzi mwaka 2010. Kama ilivyokwisha tokea, ikiwa vyama vingine havitaki kujiunga wbasi wale viongozi na wananchama wanaotaka Muungano wajiunge na Chadema kwa sababu nafasi yetu kujiunga ipo wazi kabisa..
Nifupi ktk mbinu za kujiandaa hata ikibidi kuwafuata na kuwaomba wajumuike na Chadema ktk kugombea mwaka 2010 basi jambo hilo lifanyike..

Pili, wazo la kiti cha Urais ni gumu sana kwa sababu wananchi huchagua jina la mtu na umaarufu wake. Ni lazima Chadema au Upinzani kama wataungana kusimamisha jina litakalo weza kuuzika kwa wananchi..Kama ingekuwa amri yangu Dr. Slaa pekee ndiye anasimama mbele ya Mbowe kwa umaarufu sasa hivi.
Na sidhani kama kuna ubaya kama akifuatwa mtu kama Salim.A Salim na kurubuniwa nafasi hiyo maadam tu Chadema ipate kupita mtihani huu wa kwanza. Nasema salim kwa sababu sii dhambi kabisa kuhama chama kwa sababu ya maslahi ya Taifa..
Kikwete ambaye ni rais wetu alitishia kukihama chama CCM ikiwa asingechaguliwa kusimama uongozi wa CCM..Hivyo basi kama kuna dhambi au makosa nadhani Kikwete alifanya kwa herufi kubwa..
Nionavyo mimi Salim A. salim anaweza kusimama na Kikwete na akashinda bila kutegemea ni sera zipi anakuja nazo kwani NDIVYO TULIVYO..
Na mwisho ni lazima Chadema wafahamu, waelewe na kuzingatia kwamba Wadanganyika wote - NDIVYO TULIVYO. Mbinu ,ahadi na maandalizi yote yafanyike kwa kufikira WATU na MAZINGIRA tunayoishi na siii Siasa nyingi za sera na mrengo wakati wananchi wenye njaa wanataka kuona ugali mezani..

Haya ni maoni yangu tu kutokana na jinsi nilivyowasoma wadanganyika..

Kuunganisha vyama kwa kweli mimi napinga sana napenda sana ninavyoona kuwa chadema inainuka kama chama chenya nguvu na kinachokua kwa nguvu ya ajabu,ningelipenda sana tuwe na chama kimoja kikubwa cha upinzani kitakachochuana na CCM

uzoefu umeonyesha wakiungna wanatumia muda mwingi kulumbana na kukashifiana kwa hiyo kwangu mimi ruksa kuwa na chama kimoja chenye nguvu
Wanaweza kushirikiana na vyama vyote vya upinzani kwenye maslahi ya nchi kama kubadili katiba,kupambana na mafsadi,usalama wa taifa n.k.
kama wana JF tunaweza kuorodhesha majina hapa kutoka miongoni mwa wanajamii ambao tunaona wanaweza kusimamishwa kwa ngazi ya uraisi itakuwa changamoto yetu pia kuwajadili kwa kina tukitoa sababu kwa vipi atakuwa changamoto kwa JK ambaye anatakiwa aachie ngazi 2010 kabla hajaipeleka nchi pabaya zaidi amba[po itakuwa shida kurudi
Chadema waelekeze nguvu zao zote sehemu zote mijini na vijijini na walenge makundi yote kwa nguvu zote
 
Kaka yangu Mkandara, Mimi sijapenda kuunganisha vyama na maneno yako umeyasema kweli kabisa na kufanya kuwa na watu makini, anaweza kuwa Salim A. Salim maana anaweza kufanya kuwa na msingi imara wa Demokrasia na hatimaye kufanya yale wakachuana nao. Sasa unasema juu ya kumpata huyu mzee na kukubali kugombea
 
Kuunganisha vyama kwa kweli mimi napinga sana napenda sana ninavyoona kuwa chadema inainuka kama chama chenya nguvu na kinachokua kwa nguvu ya ajabu,ningelipenda sana tuwe na chama kimoja kikubwa cha upinzani kitakachochuana na CCM

uzoefu umeonyesha wakiungna wanatumia muda mwingi kulumbana na kukashifiana kwa hiyo kwangu mimi ruksa kuwa na chama kimoja chenye nguvu
Wanaweza kushirikiana na vyama vyote vya upinzani kwenye maslahi ya nchi kama kubadili katiba,kupambana na mafsadi,usalama wa taifa n.k.
kama wana JF tunaweza kuorodhesha majina hapa kutoka miongoni mwa wanajamii ambao tunaona wanaweza kusimamishwa kwa ngazi ya uraisi itakuwa changamoto yetu pia kuwajadili kwa kina tukitoa sababu kwa vipi atakuwa changamoto kwa JK ambaye anatakiwa aachie ngazi 2010 kabla hajaipeleka nchi pabaya zaidi amba[po itakuwa shida kurudi
Chadema waelekeze nguvu zao zote sehemu zote mijini na vijijini na walenge makundi yote kwa nguvu zote

Mkuu ni uzoefu gani huo?.. mimi nachofahamu vyama hivi havikukusudia kabisa kuungana toka mwanzo pamoja na kwamba Chadema walikuwa tayari na nadhani TLP ndiye mwanzilishi wa hoja hiyo. Tatizo limekuja baada ya vyama vingine kukataa kuunda chama kimoja na sababu kubwa ni Uongozi wa juu na hizi ruzuku..Kwa sababu kila mmoja wao anafikiria anayo shot to being elected akiwaweza kusimama kama mgombea..

Chadema kinaweza kuwa chama mbadala kwa kipimo gani?.. kumbuka hata asilimia 20 kwa Wabongo ni chama mbadala maadam chama tawala kina popularity ya zaidi ya asilimia 70. Hivyo kipimo halisi cha Mbadala, uwezo wa kupambana na CCM ni pale chama kinapoweza kufikia asilimia 40 ya umaarufu na hasa kwa viongozi wake kwani Tanzania hadi leo umaarufu wa chama unatokana na kiongozi. Sidhani kama Chadema wamefika huko hata kidogo lakini kama wataunganisha nguvu zao wanaweza kufikia asilimia 40.. mchezo ukabakia ktk kura za wale wasiokuwa na mrengo...

Kikwete kashuka Umaarufu na yawezekana imefikia asilimia 60 au hata 50 lakini tatizo ni replacement. Watu wengine wote walibakia hawana umaarufu kabisa na sioni ndani ya CCM kama kuna mtu mwenye Popularity sasa hivi..Mwandosya jina kubwa lakini halina mvuto kwa wakulima hivyo wanaochukua nafasi wengi wapo Upinzani lakini pia hawana nguvu kubwa kuweza kufikia asilimia 40, labda huyo Dr. Slaa na Salim kutokana na sifa walokwisha jenga.. Tukumbuke tu kwamba wapiga kura wengi nchi zote duniani ni wazee, vijana wengi huwa ktk mihangaiko ya kutafuta riziki hata siku ya upigaji kura..

Mwisho kuungana nakozungumzia mimi ni kwa watu, vichwa vya watu viungane badala ya vyama kwani jambo hilo limeshindikana. Wale wote wenye nia nzuri kwa taifa, warubuniwe wafuatwe na kupewa nafasi ktk uchaguzi mkuu kwani kinachotakiwa sasa hivi ni kuitoa CCM ktk Uongozi kisha baada ya hapo itajulikana mbele ya safari.. kama Kenya walipoweza kumsimamisha Mwai Kibaki (popular) against Moi na Mtoto wa Kenyatta. Wakachukua ushindi kuiondoa KANU ktk kiti cha IKulu, halafu wakaja tengana baada ya kutofikia muafaka wa kisera..Leo hii Kibaki na Raila (upinzani) ndio wanaongoza vyama vinavyopingana Kenya.. Kanu haina nafasi tena.
 
kweli kabisa lakini mapinduzi ya kifikra yanaweza kufanywa sasa hivi mpaka mwakani kwamba jamii nzima ihamisishwe kutambua kwamba nchi ni yetu wote jwa hiyo wale wanaoonekana ni wapambanaji kwa namna fulani,kugombea haki za wanachi kwa namna yeyote washawishiwe kujiingiza kwenye siasa za kuiangusha CCM miaka 48 mzee tuko palepale inasikitisha.nakubaliana nawe tuungane kifikra
 
Mkuu ni uzoefu gani huo?.. mimi nachofahamu vyama hivi havikukusudia kabisa kuungana toka mwanzo pamoja na kwamba Chadema walikuwa tayari na nadhani TLP ndiye mwanzilishi wa hoja hiyo. Tatizo limekuja baada ya vyama vingine kukataa kuunda chama kimoja na sababu kubwa ni Uongozi wa juu na hizi ruzuku..Kwa sababu kila mmoja wao anafikiria anayo shot to being elected akiwaweza kusimama kama mgombea..

Chadema kinaweza kuwa chama mbadala kwa kipimo gani?.. kumbuka hata asilimia 20 kwa Wabongo ni chama mbadala maadam chama tawala kina popularity ya zaidi ya asilimia 70. Hivyo kipimo halisi cha Mbadala, uwezo wa kupambana na CCM ni pale chama kinapoweza kufikia asilimia 40 ya umaarufu na hasa kwa viongozi wake kwani Tanzania hadi leo umaarufu wa chama unatokana na kiongozi. Sidhani kama Chadema wamefika huko hata kidogo lakini kama wataunganisha nguvu zao wanaweza kufikia asilimia 40.. mchezo ukabakia ktk kura za wale wasiokuwa na mrengo...

Kikwete kashuka Umaarufu na yawezekana imefikia asilimia 60 au hata 50 lakini tatizo ni replacement. Watu wengine wote walibakia hawana umaarufu kabisa na sioni ndani ya CCM kama kuna mtu mwenye Popularity sasa hivi..Mwandosya jina kubwa lakini halina mvuto kwa wakulima hivyo wanaochukua nafasi wengi wapo Upinzani lakini pia hawana nguvu kubwa kuweza kufikia asilimia 40, labda huyo Dr. Slaa na Salim kutokana na sifa walokwisha jenga.. Tukumbuke tu kwamba wapiga kura wengi nchi zote duniani ni wazee, vijana wengi huwa ktk mihangaiko ya kutafuta riziki hata siku ya upigaji kura..

Mwisho kuungana nakozungumzia mimi ni kwa watu, vichwa vya watu viungane badala ya vyama kwani jambo hilo limeshindikana. Wale wote wenye nia nzuri kwa taifa, warubuniwe wafuatwe na kupewa nafasi ktk uchaguzi mkuu kwani kinachotakiwa sasa hivi ni kuitoa CCM ktk Uongozi kisha baada ya hapo itajulikana mbele ya safari.. kama Kenya walipoweza kumsimamisha Mwai Kibaki (popular) against Moi na Mtoto wa Kenyatta. Wakachukua ushindi kuiondoa KANU ktk kiti cha IKulu, halafu wakaja tengana baada ya kutofikia muafaka wa kisera..Leo hii Kibaki na Raila (upinzani) ndio wanaongoza vyama vinavyopingana Kenya.. Kanu haina nafasi tena.
Ukweli kabisa ila ni kupewa muda CHADEMA, wanaweza na kuna uwezekano kuwa kura za mwaka 2010 Jk atapata zaidi ya asilimia 60 hivi na ndio maana huwa nasema kuwa kuna ulazima wa kuunganisha nguvu ya chama
 
Mr Mkandara huwa napenda sana kusoma maandiko yako na comments zako pia, upo huru sana katika kutoa mawazo
 
Hatuna haja ya kuuliza Cardinal Pengo au Askofu Kilaini kama Dr Slaa alifanya nini mpaka ikafikia aache au aachishwe upadre. Tunajua baada ya upadre alioa kama most of JF Members. Tunajua Slaa ni layman kama sisi, na kwamba ni mtu mwadilifu sana.

Pia tunajua Dk Slaa aliendelea kuwa mtumishi wa watu akiongoza Taasisi inayohudumia walemavu. Tunajua pia kwamba baada ya kuingia Bungeni, amekuwa shupavu na jasiri kufichua maovu ya mafisadi lukuki katika nchi yetu. Amejitolea, bila kujali usalama wake binafsi, kutaja wakubwa waliokwapua fedha za umma na kujitajirisha binafsi bila aibu.

Tunajua kwamba ktk Jimbo lake la Karatu ameleta maendeleo ya haraka, sio tu kwa kushirikiana na serikali kuboresha miundombinu kwa kutumia fedha zinazolipwa kama kodi na wananchi, bali pia kwa kuwasiliana na wafadhili wa nje moja kwa moja kuongezea juhudi za Tanzania. Dr Slaa ni mfano wa kuiga kwa Wabunge wote, wa Chadema na wa ccm. Karatu ni Wilaya iliyopiga hatua za mbele na za haraka tangu Slaa achaguliwe mbunge wao.

Hata hivyo, Chadema ina viongozi wengi wazalendo, jasiri, waadilifu na wenye uwezo. Juu ya yote, Chadema ni chama kinachoamini, kudhamini na kuheshimu demokrasia. Chadema kimeonyesha ktk historia yake tangia 1992 kwamba viongozi wake sio wang'ang'anizi wa madaraka au vyeo. Naamini kitaweza kutupatia mgombea mzuri atakayeweza kuongoza nchi. Kama ilivyodokezwa hapo nyuma, siyo lazima chama kiwe na uzoefu, na TANU haikuwa na uzoefu Waingereza walipowaachia Nyerere na wenzake.

Ningeshauri kwamba kwa sasa, wale viongozi wa kitaifa na wa kimkoa katika vyama vya siasa vya upinzani, wajifunze toka kwa Wifred Lwakatare na waungane na Chadema kuimarisha chama ambacho kimedhihirisha kwamba ndicho kitakachoweza kutoa changamoto kamilifu na ya kweli kwa ccm. Naamini ni kwa kutoa real challenge kwa ccm, ndipo nchi hii itaweza kupata demokrasia ya kweli na maendeleo ya kuridhisha wengi.

Nakubaliana kwamba kwa sasa juhudi lazima zifanywe ili Katiba ibadilishwe kuleta usawa ktk malumbano ya kisiasa. Tume ya Uchaguzi ni lazima ibadilike iwe ni Tume huru isiyopendelea Chama tawala.

Haya ni mambo yatakayofanyiwa kazi ktk kipindi hiki kabla ya Uchaguzi Mkuu, na yatafanikiwa zaidi endapo viongozi wa vyama vya upinzani watakiri sasa kwamba Chadema ndicho chama cha kuingia ili wafikie malengo. Nina hakika viongozi ndani ya Chadema sasa wataweza kuwa-accomodate wote watakaojiunga nao kuwaimarisha.
 
Last edited:
kama wachangiaji wengine walivyo kwisha sema, mimi pia nadhani chadema waanze sasa kueleza ni nini watafanya tofauti na ccm pindi wakiingia madarakani. Mfano,

1. Wanaweza kuweka issues kwamba hawatakuwa na wakuu wa wilaya wa kuteuliwa isipokuwa watachaguliwa na wananchi na cheo cha mkuu wa mkoa kitafutwa.

2. Elimu ya msingi bure,
3. Elimu ya sekondari ni lazima kwa kila mtoto hadi form 4 na serikali itagharamia nusu ya ada ya watoto wote ktk sekondari za serikali.
4. Mishahara ya wafanyakazi itapanda kila mwaka kwa flat rate
5. N.k.

Kuhusu presidential candidate, mi nadhani mwanasheria tundu lissu anafaa kama atapendekezwa na chama.
tundu lissu ni mtupu mbele ya kitila mkumbo.apewe nafasi hiyo kitila mkumbo kama kweli ni chama makini.
 
Masikini,wenzetu wanajenga mifumo ya vyama toka vijijini,ati hapa kwetu vyama vyetu vinazunguka na helkopta siku mbili na kuchukua majimbo matatu vinadai vinataka kuchukua nchi uchaguzi ujao,kweli?
Mimi ni chadema lakini kwa mwenendo huu hatutafika, bado kuna matatizo mengi-5 kati ya wabunge 6 wa kuteuliwa wanatoka moshi.
Mbowe bado ndiye mungu mtu ndani ya chadema(nyote mnajua).
Busanda mengi ametoa mamia ya mamilioni kufadhili kampeni zetu,mnajidai hamjui.
Mengi huyohuyo anafadhili CCM nyote mnajua.
Jimbo la Kigoma Kaskazini linarudi CCM,nyote mnajua.
Jimbo la Tarime Mwera ameshawachokoza wakurya,mnajidai hamuoni.
Tuwashauri chadema vizuri vinginevyo tukikaa kuleta sifa hapa tutastuka 2010 ndio kwanza majimbo yanapungua badala ya kuongezeka.
Tusitegemee umaarufu wa Zitto na Slaa kuendesha Chama,tutakipoteza chama chetu.
 
Bila kuchukua hatua muhimu za kuonesha kujiandaa kuongoza, Chadema itaweza kuongoza? Uongozi ni maandalizi, asiyejiandaa kuongoza ataongoza bila kujiandaa! Matokeo yake ni kuburuzana.
 
Bila kuchukua hatua muhimu za kuonesha kujiandaa kuongoza, Chadema itaweza kuongoza? Uongozi ni maandalizi, asiyejiandaa kuongoza ataongoza bila kujiandaa! Matokeo yake ni kuburuzana.

Logically CHADEMA haiwezi kitu, haihitaji mwarobaini kulibaini hilo CHADEMA kuipa uongozi ni sawa na kununua mkate dukani harafu na kwenda nao sehemu wanakookea mikate.
 
Logically CHADEMA haiwezi kitu, haihitaji mwarobaini kulibaini hilo CHADEMA kuipa uongozi ni sawa na kununua mkate dukani harafu na kwenda nao sehemu wanakookea mikate.

simile hii haingii akilini. Labda uifafanue.
 
Back
Top Bottom