Uchaguzi Marekani

DEMOCRAT NY

Matokeo yakiwa 94% ya kura, Bi Clinton ameshinda kwa 57.5 hadi sasa, Bw Sanders 42.5%
Kwa hali yoyote Bi Clinton atakuwa ameshinda kwa point Zaidi ya 10 kama kura za maoni zilivyoeleza kabla ya uchaguzi

Ushindi wa Clinton ulikuwa muhimu na alionekana kufarajika sana akieleza furaha yake ya kushinda NY alikokuwa Seneta. Ushindi ni mkubwa ikizingatiwa idadi ya wajumbe

Dem ni uwiano hata hivyo uwiano huo hutegemea jimbo na jimba NY ikiwa na taratibu zake.
Ushindi wa leo umemuongozea morali na kuondoa hofu aliyokuwa nayo kwa wiki kadhaa

Kwa upande wa Sander, kushindwa NY kuna atahari zifuatazo
1. Nyumbani alikozaliwa, ilitarajiwa kuwepo na ushindani. Kushindwa kwa point 15 ni tatizo

2. Alitakiwa ashinde ili kuonguza gap kati yake na Bi Clinton, kinyume chake kwa utaratibu wa Dem na NY Clinto atakuwa na wajumbe takribani 50 Zaidi ya Sanders na hivyo kufukia mashimo ya chaguzi ziizopita

3. Kunazidi kupunguza uwezekano wa kushinda katika majimbo yenye watu wa rangi

4. Imeonyesha katika state ambazo uchaguzi ni closed kwa Dem Sanders hana nguvu

5. Inatia shaka kama wafuasi katika mikutano yake ni wafuasi wa Dem

Inaendelea
 
DEMOCRAT NY

Matokeo yakiwa 94% ya kura, Bi Clinton ameshinda kwa 57.5 hadi sasa, Bw Sanders 42.5%
Kwa hali yoyote Bi Clinton atakuwa ameshinda kwa point Zaidi ya 10 kama kura za maoni zilivyoeleza kabla ya uchaguzi

Ushindi wa Clinton ulikuwa muhimu na alionekana kufarajika sana akieleza furaha yake ya kushinda NY alikokuwa Seneta. Ushindi ni mkubwa ikizingatiwa idadi ya wajumbe

Dem ni uwiano hata hivyo uwiano huo hutegemea jimbo na jimba NY ikiwa na taratibu zake.
Ushindi wa leo umemuongozea morali na kuondoa hofu aliyokuwa nayo kwa wiki kadhaa

Kwa upande wa Sander, kushindwa NY kuna atahari zifuatazo
1. Nyumbani alikozaliwa, ilitarajiwa kuwepo na ushindani. Kushindwa kwa point 15 ni tatizo

2. Alitakiwa ashinde ili kuonguza gap kati yake na Bi Clinton, kinyume chake kwa utaratibu wa Dem na NY Clinto atakuwa na wajumbe takribani 50 Zaidi ya Sanders na hivyo kufukia mashimo ya chaguzi ziizopita

3. Kunazidi kupunguza uwezekano wa kushinda katika majimbo yenye watu wa rangi

4. Imeonyesha katika state ambazo uchaguzi ni closed kwa Dem Sanders hana nguvu

5. Inatia shaka kama wafuasi katika mikutano yake na ufuasi wa 'wajumbe'

Inaendelea
Baada ya New York, idadi ya wajumbe hadi sasa ni kama ifuatavyo;

Republicans
  1. Donald Trump... 844
  2. Ted Cruz........... 559
Democrats
  1. Hillary Clinton...1885
  2. Bernie Sanders..1190
 
YALIYOJIRI KUTOKANA NA UCHAGUZI WA NY
Republican
Trump ameonyesha uwezo wa kushinda 60%,jimbo la nyumbani kwake,halielezi uhalisia h

Aliyepoteza NY ni Seneta Cruz kwa 14% hawezi kupata mjumbe hata mmoja

Democrat
NY imenyanyua morali ya Bi Clinton, ikimnyong'onyeza Bw Sanders
Sanders alifahamu ushindi NY ulikuwa mgumu. Alichotaka ni kukaribia matokeo

Kushindwa kwa 15 points kumemuumiza.
Clinton amepata wajumbe wa kufidia cacucus mbili au tatu alizoshinda Sanders

Bw Sanders aliwekeza sana NY angalau matokeo yawe katika 51 kwa 49%
Alitumia milioni 7 kwa matangazo ,Bi Clinton milioni 3.7

Sababu zilizoplekea kushindwa kwa Sanders ukiacha za kampeni ni hizi

1. Clinton amegombea Useneta(2)anaijua NY vizuri, na ni Dem state kwa ukamilifu
2. Clinton ana network aliyoitumia kufikia wapiga kura kirahisi
3.Kuna watu wa rangi ambao Clinton anashinda hasa mijini
4. Alimbana Sanders kule vijijini kwa weupe kiasi cha kupunguza tofauti ya kura
5.Uchaguzi wa NY ni closed, Clinton alishaandikisha wapiga. Sanders hakufanya mapema

Kisaikolojia Sanders ametikisika kiasi cha kurudi Vermont kushauriana na timu yake namna ya kwenda mbele katika new reality. Namba zinazidi kuwa ngumu.

Uchaguzi unaofuata ni wa majimbo haya (Jumanne ijayo)
Pennsylvanian (Pa), Connecticut, Delaware, Maryland, Rhode Island

Pa. ndiyo ina wajumbe takribani 197.

Chaguzi ni closed primary ingawa kuna tofauti kati ya jimbo na jimbo
Rhode Island uchaguzi ni mixed

Hapa penye closed primary kuna 'trick' sana. Mfano, NY ni closed tangu tarahe ya mwisho ya kujiandikisha. Kwa wasiojiandikisha hawakupiga kura.

Hili Sanders analia nao akisema vijana wamenyimwa fursa.
Hata hivyo, alitakiwa afahamu hilo akiwa mgombea kuanzia mwanzo

Tuangalie hali itakuwa vipi tarehe 26 katika jumanne ya majimbo minne kwa mpigo

Je, Sanders atahitimisha safari au atapata momentum?

Tusemezane
 
JUMANNE 26
Kitim tim kitakuwa pande zote ingawa kwa Democrat utatoa mwelekeo mwingine
NY imebadilisha ramani hasa ushindi wa point 15 kwa Bi Clinton

Kabla ya Jumanne iliyopita, majimbo yaliyobaki na idadi kubwa ya wajumbe ni NY, California, Maryland, Pennyslavania, New Jersey

Kupoteza NY kwa point 15 ni pigo. Alichotaka ni kupunguza gap kati yake na Bi Clinton

Katika mjimbo yaliyobaki chaguzi nyingi ni primary tena zikiwa closed.

Closed kwa maana ni dem waliojiandikisha .
Mfano, Delaware inapiga kura jumanne inataka mtu ajiandikishie siku 21 kabla

Lakini pia katika closed elections,yapo majimbo yanayoruhusu kujiandikisha muda mfupi kabla ya kura, mengine yakitoa fursa za wapiga kura kubadili vyama muda mfupi

Kwa ufupi sheria za majimbo zinabadilika kutoka moja hadi jingine tunasema ni 'tricky'.

Bw Sanders ameshinda Caucus ambazo hazina control na wachache wanapiga kura

Sanders ameshinda wajumbe 150 katika caucus na majimbo takribani 7

Katika Primary, ana tatizo ingawa kwa zile za(open) kama Michagan amevuta makundi na kushinda. Hili ndilo lilikuwa tatizo la Sander NY(closed elections)

Sanders ameshinda kwa 'white' na kutegemewa kushinda Rhode Island Jumanne ijayo.

Clinton anashinda katika majimbo ambayo ni likely kuwa democrat

Kuelekea Maryland, Penn., Connecticut, Delaware, Rhode Island chaguzi ni closed

kwamba baadhi ya majimbo uandikishaji umeshafungwa. Ni Rhode Island tu yenye maxed

Kura za maoni, Bi.Clinton akiwa mbele point 8-15 kutoka jimbo moja hadi jingine

Ukisoma aya ya pili ya bandiko, utaona NY tayari na Sanders kapoteza sana.

Hivyo anatakiwa ashinde Penn na Maryland kwa kishindo ili kufidia uharibifu uliotokea NY

Inaendelea...
 
PENNYSLAVANIA
Penny state ni jimbo lenye wajumbe wengi 197 katika uchaguzi wa Jumanne

Mtifuano utakuwa mkali nyumbani kwa Penn state univ yenye timu ya basketball NCCA,
76ers kwa wale wa NBA, Phillies kwa NFL na Pit Penguin kwa NHL
Mji mashuhuri ni Philladephia.

Bw Sanders amelalamikia chaguzi (closed) za kujiandikisha mshiriki apige kura.

Kampeni yake ina 'independents' ambao hawakujiandikisha hali inayomtia wasi was na kusema ipo 'disfranchise'

Mikutano yake NY ilijaza watu, kwa bahati mbaya hawakujiandikisha na kutokuwa msaada
Kwa kutokuwa na uhakika wa kampeni, hakushawishi wapiga kura wajiandikishe

Hata hivyo, malalamiko ya Sanders yanakosa mashiko kwa njia hizi

1. litakiwa atambue utaratibu huo na kujiandaa kwa kuandikisha wapiga kura mapema

2. Kupitia utaratibu wa Caucus unao disfranchise, Sanders alishinda wajumbe 150

3. Chaguzi za wazi 'open' zinazoshirikisha wote Sanders ameshinda 16 Clinton 21

4. ni ngumu kubadili sharia za mchezo katikati, DNC haiwezi kukubaliana naye

Hofu ya Sanders ni kuwa chaguzi zote 4 zinazokuja ikiwemo Penn. ni closed.

Swali, ilipofika March 28 Sanders aliandikisha wapiga kura?
Inaonekana wanaojiandikisha ni Dem-establishment,wengi wanaegemea kwa Clinton

Kura za maoni zinampa nafasi ya pili kila jimbo isipokuwa Rhode Island

Sanders ana kampeni kubwa na ya nguvu na wakati wowote anaweza kuziba pengo.
Ukitazama kura za maoni kuna 7% inayosemwa undecided inaweza kwenda upande wake

Advantage ya Bi Clinton ni kuongoza maeneo ya jumanne kwa asilimia kubwa.
Hata ikitokea akapoteza,uwezekano wa kupoteza 59% anazohitaji Sanders unapungua.

Anachohitaji Bi Clinton ni kumzuia katika wastani wa 51 hadi 55

Kwa Sanders, Penn na Maryland ni must win tena kwa ushindi mkubwa.
Changamoto, ni closed elections,haijulikani independents wanaomuunga mkono itakuwaje

Tatizo jingine kwa Sanders,wakati anapigania NY, Bi Clinton alishaanza kampeni Penn na kwingineko. Katika uchaguzi wa majimbo 5, nafasi ya Sanders kuwafikiwa wapiga ili kupata ushindi mnono ni ngumu kidogo.

Hata hivyo, pesa anazo, ameajiri watu 6000 katika grass root. Hilo laweza msaidia sana
Pia majimbo hayo yana 'white' wengi hasa vijijini .

Je, Clinton atambana huko vijijini kama alivyofanya NY.


Hali ipo vipi Connecticut, Maryland na Kentucky?

Tusemezane
 
KUELEKEA JUMANNE APRIL 26

REPUBLICAN
Matokeo ya Jummane kwa GOP hayawezi kubadili sana hali ya msimamo wa wagombe

Ni matokeo yanayoweza kubadili picha kwa jicho la kisiasa.
Baada ya NY Trump ana momentum, Sen.Cruz akipoteza na Kasich akiwa power broker

Hali ya Republican inatia shaka, wimbi la magwiji kususia mkutano mkuu (RNC) linaongeza. Mgombea wa Rais 2008 J. McCain ameonyesha kususia, akiungana na J.Bush na maseneta wengine.

Zipo taarifa RNC wanakaa kikao kubadili taratibu zilingane na mazingira ambapo uwezekano wa kwenda uchaguzi mkuu ni 50/50. Tutaendelea kuwajuza kinachojiri

DEMOCRAT
Baada ya ushindi wa NY , kampeni ya Bi Clinton inashika kasi.
NY ilimchanganya Bw Sanders.

Kampeni ilitambua haiwezi kushinda, lakini si kupoteza kwa asilimia takribani 15

Kura za maoni za taasisi zote zinaonyesha Bi Clinton akiongoza Connecticut, Maryland na Pennyslavania. Hakuna kura za maoni za taasisi kwa Rhode Island na Delaware

Taasisi ya Quinnipiac katika kura za maoni za Jumatano inaonyesha Bi Clinton akiongoza Connecticut kwa 51% kwa 24%. Idadi ya wajumbe wa inayoitwa constitutional state ni

Macho yapo Keystone state (Pennsylvania) yenye delegates na super delegate takribani 210 na Old line state (Maryland) wajumbe takribani 118

Kwa wale wa NBA Washington Wizard walianzia Maryland kabla ya kuhamia DC
Connecticut ndipo aliposomea Hasim Thabiiti kabla ya draft ya kuingia NBA

Majuzi kura zinaonyesha ifuatavyo; Clinton 50% kwa 38% Pen, nyingine 50% kwa 44%. Ni wazi, matokeo yatakaribiana pengine 50 kwa 48 au 49.
Kwa hali yoyote hayo yatakuwa matokeo mazuri kwa Bi Clinton ikitokea

Bw Sanders akishinda Pennyslavania itampa nguvu ya kuendelea na kampeni California. Kampeni ya Sanders inasema California ni wajumbe takribani 540 wanaoweza kuziba pengo la tofauti yake na Bi Clinton.

Matumaini ya Sanders ni kuwa California ni 'open primary' na hivyo kuweza kuvuta ' independents'. Pamoja na matumaini hayo lipo suala moja, la proportionality. Tutajadili

Kwa upande wa Maryland nako hali si nzuri kwa Bw kufuatana na kura za maoni
Hadi juzi ilikuwa 58 % kwa 36% . 'Old line state ' ina wajumbe takribani 118

Delaware na Rhode Island hakuna kura za maoni. Wachambuzi wanasema, upigaji kura wa Pennsylvania na Maryland uta influence Delaware nyumbani kwa makamu wa Rais Joe Biden. Rhode Island inabaki kama ilivyo kwamba inaweza kwenda popote

Hivyo matokeo ya Rhode Island, Delaware na Connecticut hayana impact kwa wagombea kama yale ya Baltimore au Philadelphia kutokana na idadi ya wajumbe, hivyo macho yapo Pennsylvania na Maryland Zaidi

Tuangalie kwanini California haina umuhimu ukilinganisha na Pennyslavania na Maryland kwa Bw Sanders kwa sasa.

Inaendelea
 
CALIFORNIA
Tuongelee California kutokana na idadi ya wajumbe kwa Democrat takribani 540
pengo la wajumbe wa kuchaguliwa 'pledged delegates' kati ya Clinton na Sander inafikia 240

Lengo la Sanders kule NY lilikuwa kubaki na pengo lililokuwepo na ali kampeni sana NY

Matarajio yalikuwa ni matokeo ya 48 kwa 50,wagawane wajumbe na kumzuia Clinton kuongeza idadi ili kuelekea Penn, Maryland, Connect, Rhod, Delaware ili Sanders azibe pengo

Hesabau zilivurugika na kwa mtazamo wa Jumanne hazimpi nafasi kubwa kufanya vizuri

Sanders ana uwezo sana wa kampeni na anaweza kushinda baadhi ya majimbo Jumanne
Hata hivyo, lazima ashinde katika asilimia 85 ili kuweza kuziba pengo kati yake na Clinton

Hilo haionekani kutokea japo kwa kusema. Akiwa nyuma ya kura za maoni, ushindi wa asilimia 85 ni jambo gumu.

Ikitokea,ushindi wa 85% utamhakikishia wajumbe wote, kwani sheria za Democrat zinasema, ili mgombea asipate wajumbe ni lazima ashindwe chini ya asilimia 15

Kwa maana hiyo Sanders akishinda Penn na Maryland kwa 85% Clinton hatakuwa na wajumbe(zero), hivyo wajumbe wote 240+ 118 sawa na 258 watamwezesha kumfikia Bi Clinton. Hii ni nadharia ya kihesabu, uhalisia haupo karibu na hapo kwa asilimia 99.99.

Bi Clinton hawezi kupoteza Penn au Maryland kwa asilimia chini ya 15.
Kumbuka, Clinton alimshinda Obama na kujenga hoja kuelekea California ikiwa too late

Hivyo, Sanders ana matumaini ya kukaribiana matokeo aendelee kujenga hoja ya kuelekea California. Hesabu hazimpi nafasi California. Kwanini?

Uchaguzi wa Democrat si kama Republican. Tumeeleza, Republican kuna winner take all, au winner take most, au state convention allocation au Caucus

Kwa Democrat iwe iwavyo, wajumbe wanagawanywa kwa 'proportion' ya ushindi yaani uwiano wa mgombea na ushindi kwa asilimia ilimradi avuke 15% ya kura

Kinadharia, Sanders akishinda asilimia 70 California, 30 %ya Clinton itampa wajumbe wengi kati ya takribani 540. Pengo litapngua lakini halitazibika.

Hesabu za uwiano zinazingatia mambo mengi ikiwa ni pamoja na popular vote, eneo la ushindi, ukubwa wa vitongoji na miji n.k.

Kumbuka tulisema awali, hesabu za kugawa wajumbe kwa vyama vyote zinazingatia vigezo vingi na ndio maana namba tunazoweka hubadilika kila baada ya matokeo

Kwa Jumanne ijayo, matokeo yataamua kama Sanders anaendelea au ndiyo safari imefika mwisho. Namba ndizo zitakazo eleza ukweli, na hilo linampa Bi Clinton nguvu kwa sasa

Tusemezane
 
KUELEKEA JUMANNE APRIL 26

REPUBLICAN
Matokeo ya Jummane kwa GOP hayawezi kubadili sana hali ya msimamo wa wagombe

Ni matokeo yanayoweza kubadili picha kwa jicho la kisiasa.
Baada ya NY Trump ana momentum, Sen.Cruz akipoteza na Kasich akiwa power broker

Hali ya Republican inatia shaka, wimbi la magwiji kususia mkutano mkuu (RNC) linaongeza. Mgombea wa Rais 2008 J. McCain ameonyesha kususia, akiungana na J.Bush na maseneta wengine.

Zipo taarifa RNC wanakaa kikao kubadili taratibu zilingane na mazingira ambapo uwezekano wa kwenda uchaguzi mkuu ni 50/50. Tutaendelea kuwajuza kinachojiri

DEMOCRAT
Baada ya ushindi wa NY , kampeni ya Bi Clinton inashika kasi.
NY ilimchanganya Bw Sanders.

Kampeni ilitambua haiwezi kushinda, lakini si kupoteza kwa asilimia takribani 15

Kura za maoni za taasisi zote zinaonyesha Bi Clinton akiongoza Connecticut, Maryland na Pennyslavania. Hakuna kura za maoni za taasisi kwa Rhode Island na Delaware

Taasisi ya Quinnipiac katika kura za maoni za Jumatano inaonyesha Bi Clinton akiongoza Connecticut kwa 51% kwa 24%. Idadi ya wajumbe wa inayoitwa constitutional state ni

Macho yapo Keystone state (Pennsylvania) yenye delegates na super delegate takribani 210 na Old line state (Maryland) wajumbe takribani 118

Kwa wale wa NBA Washington Wizard walianzia Maryland kabla ya kuhamia DC
Connecticut ndipo aliposomea Hasim Thabiiti kabla ya draft ya kuingia NBA

Majuzi kura zinaonyesha ifuatavyo; Clinton 50% kwa 38% Pen, nyingine 50% kwa 44%. Ni wazi, matokeo yatakaribiana pengine 50 kwa 48 au 49.
Kwa hali yoyote hayo yatakuwa matokeo mazuri kwa Bi Clinton ikitokea

Bw Sanders akishinda Pennyslavania itampa nguvu ya kuendelea na kampeni California. Kampeni ya Sanders inasema California ni wajumbe takribani 540 wanaoweza kuziba pengo la tofauti yake na Bi Clinton.

Matumaini ya Sanders ni kuwa California ni 'open primary' na hivyo kuweza kuvuta ' independents'. Pamoja na matumaini hayo lipo suala moja, la proportionality. Tutajadili

Kwa upande wa Maryland nako hali si nzuri kwa Bw kufuatana na kura za maoni
Hadi juzi ilikuwa 58 % kwa 36% . 'Old line state ' ina wajumbe takribani 118

Delaware na Rhode Island hakuna kura za maoni. Wachambuzi wanasema, upigaji kura wa Pennsylvania na Maryland uta influence Delaware nyumbani kwa makamu wa Rais Joe Biden. Rhode Island inabaki kama ilivyo kwamba inaweza kwenda popote

Hivyo matokeo ya Rhode Island, Delaware na Connecticut hayana impact kwa wagombea kama yale ya Baltimore au Philadelphia kutokana na idadi ya wajumbe, hivyo macho yapo Pennsylvania na Maryland Zaidi

Tuangalie kwanini California haina umuhimu ukilinganisha na Pennyslavania na Maryland kwa Bw Sanders kwa sasa.

Inaendelea
Nguruvi3, kuna wanaofikiria kwamba msimamo wa Meneja wa Kampeni, Jeff Weaver, huenda yameathiri ushindi wa Sanders kwa kiwango kikubwa. Matamshi yake yametafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kwamba yameelekezwa zaidi katika kukidhoofisha chama hicho na kuinufaisha GOP.

1024x1024.jpg


Jeff Weaver, Meneja wa Kampeni wa Bernie Sanders.

Aina ya kampeni iliyoelekezwa kwa Bi Clinton ya kumshambulia kwa maswala binafsi ambayo mengi hayana msingi, imeonekana kuathiri ushindi wa Bernie. Kinachoshangaza zaidi ni ukimya wa Bernie bila kukekemea, jambo linalotafsiriwa kama kubariki matamshi ya meneja wake huyo.

Baada ya kuona nafasi ya ushindi kwa bosi wake tangu mwaka 1986 unazidi kuwa finyu, Jeff Weaver, inaonekana ameaua liwalo na liwe na heri wakose wote. Watu wanaanza kujiuliza kwa nini katika matamshi yake yote hajawahi hata mara moja kuwashambulia wagombea wa GOP! Nini malengo yake.
 
Mkuu Mag3 kilichokuwa kinafuata ni kuhusu suala uliloongelea, na nashukuru sana sana umelileta mapema.

Baada ya kuzungumzia Jumanne ijayo kwa ufupi na California na ugumu wa hesabu, nilitaka kuuliza kulikuwa na ulazima wa Sanders kuendelea na kampeni?
Na hiyo ina faida ya hasara gani?

Msikilize Sanders hapa chini

Sanders Returns: "It's Not Just About Me," Clinton Will Have To Change Her Platform To Earn My Support

SANDERS NA KAMPENI ZINAZOITIA DEMOCRAT HOFU
Democrat tangu mwanzo walijadili issues za wananchi tofauti na person attack

Kama kawaida ya kampeni, mshindani hutumia udhaifu wa mwenzake kutafuta kura

Sanders alitumia hoja ya Bi Clinton kuhusu judgement ya kura ya Iraq.
Hoja aliyoona inampatia nafasi kule New Hampshire.

Hoja hiyo haikuwa na mashiko ya muda mrefu, akahamia katika suala la biashara na mikataba yake. Hoja ikampa ushindi wa Michaigan ambao ulichagizwa na ''Independents'

Kisha akahamia hoja ya Benghaz, ambayo ilimpa Clinton nguvu na sympathy kutoka Democrat. Benghaz ni silaha ya Republican, Dem hawakukubaliana nayo. Akaiacha

Akashinda caucus 7 ambazo kihesabu hazikuwa na impact Zaidi ya kauli mbiu.
Sanders akapoteza majimbo makubwa kama Florida kwa asilimia 60 kwa 40

Ndipo akaanza kucheza karata ya wall street kuelekea New York.
Karata hiyo haionekani kumsaidia na NY ilikuwa pigo kubwa.

Kwanza, amezaliwa na kukulia Brooklyn, pili, ni karibu na Vermont anakowakilisha na tatu idadi ya wajumbe aliopoteza ilifunika caucus Zaidi ya 2 alizoshinda

Kampeni ya Sanders ameijenga katika vijana, kwa maana anatumia baadhi ya vijana

Katika midahalo kama wa Brooklyn,vijana wake wakimzomea Clinton katika mazingira yasio na ulazima, wakazusha maandamo kule California kupinga akina George Clooney kuchangisha pesa kwa ajili ya kampeni za Clinton

Frustrations zilikuwa kubwa baada ya NY na hapo ndipo akina Weaver walipoanza rafu

KAMPENI ZA RAFU

Inaendelea....
 
KAMPENI ZA RAFU

Kwa sehemu kubwa, kampeni ya Clinton haitumii rafu isipokuwa hoja na udhaifu wa mpinzani
Hapa tusisitize, udhafu wa mgombea ni katika hoja , huo ni fair kutumika wenye wakisema 'drw the distinctions between..)

Kampeni ya Bw Sana kutokana na frustrations za hali ilivyo , inawatumia vijana kuzua sintofahamu. Vijana kama black lives matter, California na kwingineko wamevuka mipaka

Imefikia wakati kampeni ya Sanders wakimwita Bi Clinton 'kahaba' au Hoe
Hayo yakitokea Bw Sanders yupo kimya ikionyesha kurudhishwa nayo

Katika mdahalo wa Brooklyn,Bw Sanders alimsifia Clinton katika dhihaka akisema , Clinton ameshinda majimbo ya 'deep south'

Kauli hiyo iliwaudhi viongozi wa DNC akiwemo Donna Brazil ambaye ni mzaliwa wa Luisiana na aliyeiongelea kuonyesha kutoridhishwa nayo

Na hivi karibuni kama alivyoonyesha Mag3 kampeni meneja ameongea 'bila kujali nini kitatokea, uchaguzi lazima uende mkutano mkuu'

Hapo juu, bw Sanders amerudia kauli hiyo akisema 'si suala la yeye bali la watu' na kwamba ili amuunge mkono Clinton ni lazima achukue sehemu ya mawazo yake

Bwana Sanders anasema kama wataendelea kushinda basi kwenda mkutano mkuu ni lazima

Kiongozi mmoja wa DNC akizungumza CCM alisema ''Sanders ana wajibu wa kuhakikisha ndege inatua salama na si kuangukia katika nyumba'' akimaanisha kutoleta uharibifu

Kwasasa, DNC ina wasi wasi sana na mwenendo wa Bw Sanders na kampeni zake
Inaonekana anatoa silaha Zaidi kwa Republican badala ya kuponya makovu

Kuna kila sababu za DNC kuamini kuwa Sanders yupo tayari kwa lolote hata kama ni kushindwa kwa Democrat.

Hoja gani anazoisimama nazo Sanders ili kuelelekea mkutano mkuu? Tutaziangalia

Tusemazane
 
DEMOCRAT NA HOFU YA SANDERS

Kauli za karibuni za Bw Sanders zimeanza kuwatia hofu viongozi wa DNC
Ni kana kwamba, Sanders ameamua liwalo na liwe.

Sanders anarusha 'madongo' kwa mpinzani wake bila kujali athari za siku za baadaye

Bw Sanders amesisitiza ataendelea na kampeni hadi mkutano mkuu.
Kinachowatia hofu DNC ni matatizo yanayoweza kutokea ikiwa hali hiyo itajitokeza.

DNC wanakumbuka mtifuano wa Ted Kennedy na Jimmy Carter siku za nyuma

Uwezekano wa Sanders kushinda ndani ya mkutano mkuu ni ndogo. Super delegates wataangalia wajumbe wa kuchaguliwa,idadi ya wapiga kura, ushindi katika primaries

Inavyoelekea Bi Clinton atakuwa na wajumbe wengi wa kuchaguliwa, ana idadi kubwa ya kura (popular vote) na ameshinda majimbo makubwa yakiwemo ya blue(Democrat)
Itawezekanaje kumwacha kama mgombea?

Hoja ya Bw Sanders ni kuleta 'independents' ambao ni vijana. Hoja hii ina shaka.
Je, hao independents ni kweli wana azma njema au ni kwa msimu tu wa uchaguzi?

Vipi ikiwa ni Republican wanaotaka kumzuia Clinton kama tishio?

Na iweje popular vote ziwe ndogo? Nafasi ya Democrat wanaompigia itakuwa wapi?

Kwa viongozi wa DNC kauli kama ile ya 'deep south'zinaashiria hali kutokuwa njema.
Tayari wameanza kuonyesha wasi wasi wa Sanders kugawa chama.

Swali ni kwanini Sanders anataka kumwaga mboga na ugali?

Majibu ya swali ni mengi lakini kwa mtazamo wa haraka ni kama ifuatavyo

1. Hesabu hazimpi nafasi kwa sasa, na bado anaona ndiye alipaswa kuwa mgombea
2. Umri wa Sanders ni miaka 79, na hakuna tumaini tena la kugombea baada ya hapa
3. Kubwa Zaidi ni kauli hii Sanders Returns: "It's Not Just About Me," Clinton Will Have To Change Her Platform To Earn My Support

Hapa ndipo hoja ya Sanders ilipo. Anasema Clinton abadili 'sera' zake ili amuunge mkono
Anachotaka kukifanya ni shinikizo ili Clinton imfikirie na hivyo kumshirikisha

Ushiriki anaoutaka ni kuwa mgombea mwenza au makamu wa Rais.

Hilo ni sehemu ya shinikizo analotaka likubalike kwasababu 1 na 2 tulizoeleza hapo juu

Kwanini Bi Clinton anaonekana kuwa kimya licha ya mashambulizi ya Bw Sanders?

Tutajadili sehemu ijayo
 
UKIMYA WA Bi CLINTON

Kwa kiasi kikubwa Clinton amekuwa kimya kana kwamba hana majibu 'provocations'

Timu ya Bi Clinton ingawa haioenekani wazi, ni ile iliyompeleka Billy Clinton white house.

Wapo akina Paul Bagala,James Carvile na wengine.
Timu hiyo ndiyo ilipambana na Obama 2008, tunakumbuka jinsi ilivyocheza rafu

Inatosha kusema, kikosi chake kinaweza kukabiliana na Timu ya Sanders.

Kinachowazuia ni ukweli kuwa Hillary Clinton kuanzia mwanzo alionekana atakuwa mgombea wa Democrat. Ingawa bado chaguzi zinaendelea mwelekeo unaonyesha hivyo

Mbele ya safari timu ya Clinton itahitaji wafuasi wa Sanders kuelekea uchaguzi mkuu.

Hivyo,wanachojaribu ni kuhakikisha wanacheza 'salama' ili muda ukifika wafuasi wa Sanders wamuunge mkono ikizingatiwa wengi ni rika la chini na sehemu ya wanawake

Mbinu watumiazo ni kumshambulia Trump kama vile ndiye mgombea
Hata isipotokea, kampeni inawatumia Republic kuepuka malumbano na Sanders

Pili, kutomzungumzia Sanders ni kumpa athari za kisaiokolojia, kwamba tayari wameshaachana na kampeni zake na sasa wana focus uchaguzi mkuu(ignore)

Hili linamuathiri Sanders kisaikolojia na wafuasi kuvunjika moyo wa kupiga kura

Tayari kuelekea Jumanne, Sanders amepunguza mashambulizi dhidi ya Bi. Clinton
Sasa anaongelea hoja kama ilivyoripotiwa na jarida maarufu la Wall street asubuhi hii

Kama Clinton atashinda majimbo ya Pennsylvanian, Connecticut na Marylanda au Delaware na rhode Island, kufuatana na kura za maoni, atamaliza tambo za Sanders

Hata hivyo, Sanders amekuja na hoja nyingine. Kwamba, kura za maoni kitaifa zinaonyesha akimshinda Trump kwa point nyingi kuliko Hillary (electability)

Tatizo la hoja hii ni kuwa, wajumbe au DNC wataangalia vigezo mbali mbali

1. Idadi ya wajumbe 'pledged delegates' hata kabla ya super delegates. Sanders yupo nyuma
2. Kitaifa, Bi Clinton ana kura nyingi 'popular vote' kuliko wagombea wote wa vyama
3. Bi Clinton ameshinda majimbo au kiasili ngome ya Democrat
4. Na ameshinda majimbo mengi kuliko Sanders yenye wajumbe wengi 'electoral college'

Je, Jumanne itakuja na majibu gani kuhusu mweleko wa Democrat?

Tusemezane
 
Kuna wakati nilimpenda Bernie Sanders lakini taratibu naanza kuwa na wasi wasi na malengo yake na wale walio karibu yake kwani inaonekana kama vile ama ni yeye la sivyo heri Republicans washinde kuliko Hillary Clinton. Huu msimamo hata baadhi ya wafuasi wake wanao, wako tayari kumpa kura mgombea wa GOP Donald Trump kuliko kumpigia kura mgombea wa Democrats.
America blog said:
Bernie Sanders’ campaign manager, Jeff Weaver, suggested this past week that Sanders will contest the Democratic nomination at the convention in July even if Hillary wins the nomination before that date.


Talking to CNN, Weaver suggested that if Hillary doesn’t win the nomination with pledged delegates alone — the delegates you win in the state primaries and caucuses — Sanders will effectively declare a civil war at the Democrat convention this summer.
Hali hii imezua mtafaruku mkubwa ndani ya kambi ya Democratic Party na hivi sasa wanatafuta namna ya kukabiliana na tishio hilo la Bernie Sanders. Wanaona kama anahatarisha umoja ndani ya chama na kisheria hakuna namna ya kumzuia. Mambo aliyoongea Meneja wa Kampeni wa Sanders akiongea na CCN yaliwaacha wapenzi na wanachama katika hali ya mshangao mkubwa!
 
Kuna wakati nilimpenda Bernie Sanders lakini taratibu naanza kuwa na wasi wasi na malengo yake na wale walio karibu yake kwani inaonekana kama vile ama ni yeye la sivyo heri Republicans washinde kuliko Hillary Clinton. Huu msimamo hata baadhi ya wafuasi wake wanao, wako tayari kumpa kura mgombea wa GOP Donald Trump kuliko kumpigia kura mgombea wa Democrats.

Hali hii imezua mtafaruku mkubwa ndani ya kambi ya Democratic Party na hivi sasa wanatafuta namna ya kukabiliana na tishio hilo la Bernie Sanders. Wanaona kama anahatarisha umoja ndani ya chama na kisheria hakuna namna ya kumzuia. Mambo aliyoongea Meneja wa Kampeni wa Sanders akiongea na CCN yaliwaacha wapenzi na wanachama katika hali ya mshangao mkubwa!
Democrat wameshaanza kuwa na wasi wasi kwasababu ya vijana wa Sanders, tayari amewachagiza washinikize kuwa kama si yeye watapigia Republican kura. Sanders ndiye anaweka shinikizo kupitia mtandao wake wa vijana

Hoja zote za Sanders zipo katika vitabu vya Dem.
Kwamba, utaratibu uliotumika upo katika maandishi kama anavyosema Donna Brazil, kiongozi wa DNC

Sanders ameleta msisimko ndani ya Democrat, lakini sasa anaonekana kutaka kuwapeleka Democrat katika mzozo kama uliopo Republican.

Kwasasa viongozi magwiji wa Republican wametangaza kususia mkutano mkuu wa chama Cleveland

Hili ndilo lile tulilojadili wiki mbili zilizopita kuwa Republican hawamtaki Trump lakini hawamepndi Cruz na Kasich hana njia. Hivyo Magwiji wanaanza kujitoa ili kutotoa uhalali wa mchakato mzima

RNC walikuwa na mkutano Florida kuhusu kubadili sheria za RNC convention. Hilo limegoma

Walitaka kufuata rule 40b kwamba anayekwenda katika contested convention lazima ashinde majimbo si chini ya 8. Hapa mwenye fursa hiyo hadi sasa ni Trump, swali watamzuiaje kwa kigezo hicho ikiwa wanamtaka Cruz kwa shingo upande na Kasich kwa shingo ndefu akiwa hana urefu wa shingo wanayoitaka?

Jumanne itaamua njia ya Democrat. Ikiwa Clinton atashinda Pennsylvanian na Maryland, magwiji wataanza kujitokeza kuweka shinikizo Sanders aachie ngazi. Ndivyo ilivyoanza taratibu NY lakini sasa itapata nguvu

Hoja kubwa kwa DNC ni kuwa Sanders anaonekana kujenga mazingira ya kugawa chama badala ya kukijenga na kuna uwezekano wa kuzua mtafaruku mkubwa.

Uchaguzi ukienda DNC convention hapo wanachama wanagawnayika na hivyo Dem watakuwa na kazi mbili
1. Kuunganisha chama kilichovurugana ndani ya DNC
2. Kufikiria namna ya kushinda November
 
KUELEKEA JUMANNE YA 26
MAJIMBO MATANO NDANI YA SANDUKU LA KURA

Panapo majaaliwa tutawaeletea matokeo ya uchaguzi kesho kadri yatakavyowajia

Yapo yanayojitokeza kwa uchache, likiwemo swali moja lililoulizwa na ndugu X
Ndugu yetu anasema, nini hatma ya wajumbe ambao wagombea wao walijitoa?

Hapa anaongelea Republican ambapo akina Rubio walijitoa wakiwa na idadi ya wajumbe (169)Dr Carson (8) Jeb Bush (4) Fiorina (1) n.k. Watakwenda kwa nani?

Ni kweli wajumbe ni wengi wanaoweza kumvusha au kumnyanyua mgombea
Taratibu za uchaguzi zina vitu vingi sana na si rahisi kuwa na jibu la moja kwa moja

Kwa mfano, Jimbo la Pennyslavania lina wajumbe 95 katika kinyang'anyiro cha kesho
Miongoni mwao 54 wapo huru na watampigia mgombea ndani ya mkutano mkuu
Hivyo uchaguzi wa leo wagombea wataibuka na wajumbe wachache sana

Kila jimbo lina utaratibu wake katika chaguzi.
Kuna wanaofanya Caucus, convention, winner take all, winner take most na mixed

Hivyo , wajumbe wa waliojitoa wataongozwa na sheria za jimbo husika.

Yapo majimbo ambayo aliyejitoa lazima abaki na mtu wake hadi convetion ifanye mzunguko wa kwanza. Yapo majimbo wajumbe wanagawanywa kwa vitongoji. n.k.

Jibu la hoja, wajumbe wataongozwa na miongozo ya majimbo na RNC.

Isijedhaniwa wajumbe hao hawana msaada, kinyume chake wana msaada mkubwa wakati wa mzunguko wa pili wa convention ambapo 55% ya wajumbe inakuwa huru.

KASICH NA CRUZ WAUNGANA

Wameungana si katika sera bali kuachiana majimbo. Baada ya kubaini Trump anachanja mbuga, njia ya kumzuia kuelekea 1237 ni kutengeneza ushirika wa kutogawana kura.

Hii maana yake ni kuwa Cruz na Kasich wana matumaini makubwa na RNC , kwamba Trump atachinjiliwa mbali. Wajiuliz,e kwanini magwiji wa Republicana hawana furaha?

Hali ya ushirika inazidi kumuongezea Trump umaarufu.Ni wazi hawezi kufikia 1237, akikaribia namba kwa pungufu ya wajumbe 100 , itakuwa ngumu sana kumzuia.

KWA UPANDE WA DEMOCRAT

Kuelekea April 26 hali si nzuri, wachambuzi wengi wakimlaumu Sanders kwa kushindwa kudhibiti wafuasi na wapambe wake 'surrogates'

Leo Bi Rosario Dawson, amemshambulia Hillary Clinton kwa kashfa ya Monica Lewensky

Shambulio limemweka pabaya Sanders,wengi hawangependa kampeni iende huko.
Waandishi wamembana Sanders kujibu tuhuma kutokana na maneno ya kashfa

Huko kwenye twitter hali si nzuri, kurushiana maneno huku kampeni ya Sanders ikishambulia sana. Hali inazidi kuwatia DNC wasi wasi na hatma ya kampeni

Tusemezane
 
MATOKEO YA CHAGUZI ZA AWALI
Pennsylvania, Connecticut , Maryland, Delaware na Rohode Island

Republican
Donald ameshinda kwa kishindo (landslide)majimbo yote matano . Asilimia alizoshinda tunazisema ni 'decisive victory''

Democrat
Hillary Clinton ameshinda Pennsylvania , Maryland na Delaware
Bernie Sanders ameshinda Rhode Island
Connecticut bado ni 'neck to neck' tutawaletea muda mfupi ujao

Kwa ufupi, Trump amepeleka message kali sana kwa wapinzani wake
Clinton ameshinda majimbo 3 hadi sasa akiwa na usiku mzuri

Update
Clinton kashinda Connecticut

Tathmini itafuata
 
MATOKEO YANATUELEZA NINI?

Matokeo ya majimbo matano ni kama ifuatavyo
Donald Trump 5/5
Hillary Clinton 4/5
Bernie Sanders 1/5

Ushindi wa Trump wa Republican ulikuwa mzito
Pennsylvania 56.8%
Connecticut 57.7%
Maryland 55.5%
Delaware 60.8%
Rhode Island 63.9%

Ushindi wa Hillary Clinton na Democrat
Pennsylvania 55.6%
Maryland 63%
Connecticut 51.6%
Delaware 59.8%
Rhode Island

Ushindi wa Bernie Sanders na Democrat
Rhode Island 55.0%

Kura za maoni zilikuwa sahihi kwa kiasi kikubwa sana kwa pande zote mbili GOP na DEM

Njia ya nomination kwa Trump inapanuka kutokana na asilimia za ushindi

Ili kufikia 1237 atahitaji ushindi katika asilimia 50 kwa majimbo yaliyobaki
Kutokana na ushindi wa leo, uwezekano upo ingawa ni mgumu kwa mtazamo mwingine

Kwa upande wa Ted Cruz, matokeo ya leo yamekatisha tamaa 'the establishment' Inaonekana hawezi kushindana na Trump wala Kasich.

Muungano wa kuachina majimbo na Kasich hatawapa namba japo karibu na 1237. Hivyo, kwenda mbele kazi yao ni kumzuia Trump kuelekea mkutano mkuu

Kwa upande wa Democrat, Bernie Sanders yupo katika wakati mgumu
Kama tulivyowahi kujadili, Bi Clinton alimsubiri NY,PA, MD ambako kuna idadi kubwa ya wajumbe. Pamoja na hayo, Clinton ameshinda Connecticut uchaguzi wa wazi 'open''

Njia ya Sanders kupata ushindi ni kama imefungwa. Kwa utaratibu wa uwiano wa wajumbe ni ngumu Sanders kushinda majimbo yaliyobaki kwa asilimia 85.

Pamoja na kupoteza majimbo makubwa matatu, Pa, MD na Delaware uchaguzi umeonyesha udhaifu kwa Sanders.

Ushindi wa Rhode Island unaonyesha jinsi Bi. Clinton anapomkaba kwa weupe hali ilivyo.

Sanders ameshindwa maeneo ya watu wa rangi,chaguzi closed na 'open' kama Connecticut. Hata hivyo, Sanders amesema ataendelea na uchaguzi hadi kura ya mwisho.

Hili linafaida moja ya ushindani wa kumwandaa mgombe November.
Lakini lina matatizo ambayo sasa yanaonekana kwa Democrat

Tutafafanua kwa kuangalia hotuba za Clinton, Sanders na Trump ambapo tayari uharibifu unaanza kujitokeza na hasa upande wa Demo

Inaendelea
 
KAMPENI NA HOTUBA ZA LEO
Kwa wiki nzima Sanders ameendeleza mashambulizi dhidi ya Bi. Clinton

Katika hotuba yake leo, Sanders ameonekana kugahfilikiwa akisema mpambano utaendele hadi kura ya mwisho kuhesabiwa akimaanisha June 2016 kule California

Hoja ya Bw Sanders kushinda majimbo 7 mfululizo imekwama. Katika chaguzi 6 Hillary Clinton ameshinda 5.Tatizo kwa Sanders ni kuwa haya ni majimbo yenye umuhimu wa aina yake kuelekea November

Hoja ya pili ya kuwataka super delegates wabadili msimamo nayo imekwama.
Kwa matokeo ya NY hadi leo, ni ngumu kushawishi super delegates wamuunge mkono.

Hoja ya kura za maoni kumpa nafasi 'electability' nayo inakumbana na idadi ya kura alizo nazo Bi Clinton ambazo ni Zaidi ya milioni 2.5 dhidi yake

Hoja liyobaki ni kutaka Clinton ashirikishe sera zake katika platform yake.
Hapa pana ugumu, ikiwa zimekataliwa(kutoshinda) kwanini ashinikize?

Sanders ana mahesabu yake, anachotaka ni kumkwamisha Clinton asifikie namba 2383

Hili litawezekana kama atakuwa na wajumbe' wa kura' kumkaribia Cinton, hivyo kutumia hoja hiyo kupeeka mchakato ndani ya mkutano mkuu

CLINTON
Katika hotuba yake alimsifia Sanders katika hali ya 'kumweleza' imefika mwisho

Alifanya hivyo kuleta Democrat pamoja akisema yapo mengi yanayowaunganisha na Sanders kuliko kuwatofautisha.Ni ktik kuponya makovu ingawa iliwashambulia Republican

TRUMP
Hotuba yake ilionekana kumshambulia Clinton kwa kutumia kitabu cha Sanders

Trump ameziongelea hoja zote anazotumia Sanders katika mashambulizi kwa Clinton
Kaongelea
NAFTA
Benghazi
Wall street

Na pia kumshambulia Clinton kijinsia kuwa asingalikuwa mwanamke 5% asingefika
Trump amejenga 'fitna' kwamba Democrat hawajamtendea haki Sanders, agombee kama mtu binafsi. Ukimsikiliza kwa umakini, kitabu anachotumia sasa hivi dhidi ya Clinton mtunzi na mwandishi ni Sanders.

Ndio maana tuliwahi sema hapa jamvini, Sanders anaiweka Dem pabaya! Ni kwanini?

Itaendelea
 
Nadhani mambo yalipofikia ni salama kabisa kusema wagombea wa hivi vyama viwili wamepatikana nao ni Hillary Clinton upande wa Democrats na Donald Trump upande wa Republicans. Ingawa bado wapo watu wanaamini maajabu yanaweza kutokea lakini kulingana na hali halisi, ukweli wa hao wagombea wawili kupeta hauwezi kupuuzwa hata na wenye roho ngumu kama wapenzi wa Bernie Sanders (DNC) au wa Ted Cruz (GOP).

Huu ndio msimamo kamili baada ya chaguzi za Aprili 26 na idadi ya wajumbe kwa kila mgombea;

GOP (Idadi inayotakiwa...1237)
  1. Donald Trump...954 (bado...283)
  2. Ted Cruz............562

DNC (Idadi inayotakiwa...2383)
  1. Hillary Clinton....2154 (bado...229)
  2. Bernie Sanders...1338
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom