Uchaguzi Marekani

HOFU YA REPUBLICAN
DEMOCRAT NAO WATAMANI CONVENTION

Hofu ya GOP kuelekea RNC inajengeka katika hali hizi
1. Trump ana wajumbe na kura nyingi akiwa front runner.
Mizengwe haitawezekana wakijua ana kundi kubwa la Republican nyuma yake?

2. Round ya kwanza isipotoa mshindi, itabidi round ya pili ifanyike.
Sehemu ya wajumbe watakuwa free kumchagua wantakaye.

Kasich akishida, Trump na Cruz watapuuzwaje wakiwa karibu 3/4 ya wapiga kura?

3. Ikiwa Cruz atashinda mzunguko wa pili au wa tatu(75% ya wajumbe wapo free)
nini hatma ya GOP, Trump akigombea kama mtu binafsi?

Tusisitize mkutano mkuu una sheria zake zinazobadilika kutokana na mazingira.

Tutafafanu katika mabandiko yajayo baadhi na sehemu kidogo tu ya sheria za RNC

DEMOCRAT
Hali si njema kama inavyodhaniwa. Stara inapotea na tutasikia mazito kulekea NY.
Clinton kampeni wanasema, wamechoshwa upotoshaji wa Sanders sasa ni 'Brawl'

Hesabu ni ngumu kwa Sanders katika taratibu wa kugawana wajumbe kwa uwiano

Tofauti ya wajumbe 200+ na punguzo la wajumbe 10 kwa wastani , litahitaji majimbo 20 katika ushindi wa 60% kumfikia Clinton(assumptions)

Jana kampeni ya Sanders imegusia super delegates na uamuzi wa kumuunga mkono.

Anasema uchaguzi uende DNC maamuzi yafayike huko.Unaweza kuona hata wao wana uhakika hesabu haziwapi nafasi ya kushinda bali ya kumfikia Bi Clinton tena kwa taabu

Hoja ya Sanders kwa sasa ni kuwa ameshinda majimbo 7 kati ya 8.
Hata hivyo, Sanders amepoteza majimbo 5 kwa usiku mmoja huko nyuma

Sanders anadai ameweza kuvuta watu wengi na hilo ni jambo jema.
Hapa kuna hoja, Sanders anashinda chaguzi wanazoweza kupiga vyama vyote.

Je,wanaokuja wana lengo la kumuunga mkono au ni kumdhoofisha Clinton?

Sanders anasema, kura za maoni zinaonyesha kushinda Republican tofauti na Clinton

Clinton kampeni wanasema, kura walizopata ni 2.5M zaidi ya wagombe wote DEM au GOP

Kuelekea NY kuna mitihani ifuatayo kwa wagombea wa Dem

Tutafafanua
 
KUELEKEA NY

DEMOCRAT WAANZA KUTIBUANA

Bandiko la juu tulisema kuelekea NY Bi.Clinton anakwenda 'brawl'

Sanders anaonekana 'kumshambulia' mwenzake si kwa hoja tu , bali kukaa kimya wafuasi wake wanapovuka mipaka. Hiyo ndiyo hoja ya Clinton kampeni

Tangu juzi hali inaonekana kuwa mbaya kwa Dem. Mdahalo unaokuja utakuwa mkali

Kuna shule mbili za fikra. Kwanza, Dem kwa uchache wao hawana haja ya kufumushana. Iwe Sanders au Clinton, kila mmoja atamhitaji mwenzake mbele ya safari.

Fikra ya pili , Clinton anaongoza anayepoteza katika malumbano ni yeye.
Kwamba, aendelea na hoja za kushambulia Republican badala malumbano na Sanders

Kuelekea NY kuna changamoto kwa pande zote

Clinton: Kushinda jimbo alilokuwa ni seneta ni lazima, kinyume chake itamuathiri kisaikokolojia. Kushinda jimbo kubwa ni muhimu kujenga imani kwa super delegates.

Na ni muhimu adhihirishe kuwa anashinda katika 'diverse' population

Changamoto; ni kuwarudisha akina mama kundini, kushinda nyoyo za vijana 20-29

Sanders
Changamoto: Ni endapo atashinda katika ''diverse population'
Amekuwa na tatizo kwa weusi na Latino, amepoteza majimbo mengi kusini na kati

Pili, athibitishe, watu wanaokuja kupiga kura (independents) si wenye lengo la kubadili sura ya Democrat bali kuvutwa na hoja zake. NY wanapiga kura registered Dem tu

Athibitishe anashinda majimbo makubwa. So far ukiacha michigan, Sanders anashinda majimbo ambayo si makubwa. Hii ni nafasi yake kuthibitisha uwezo wake

Hayo machache yana umuhimu kwa kutazama super delegates wenye uwezo wa kubadili mwelekeo kutokana na ufanisi wa mgombea.

Upande wa GOP hali ni ngumu kwa Cruz pale NY ingawa haibadili hesabu

Itandelea


Tusemzane
 
'UWANJA WA VITA NY'

Mr Trump yupo eneo lake akiongoza kura za maoni. Uwezekano wa kushinda ni mkubwa Cruz pamoja na the establishment wanaomuunga mkono kukubalika imekuwa tatizo

Cruz aliwahi kutumia kauli ya 'New York values' katika hali ya 'semantics' sasa inamwinda. Trump ameikomalia na watu wa NY hasa City wanaojivunia U-NY inawakera

DEMOCRAT
Kama tulivyosema hali ya kurushiana maneno imeshika moto.
Hii ni baada ya Clinton kampeni kuamua 'kumuondolea ' uvivu Sanders

Huko nyuma Bi Clinton alizungumzia hoja bila kuleta 'kejeli' au habari za Sanders.
Sanders alitumia nafasi hiyo kuzungumzia rekodi ya Bi Clintion jambo lililoumuudhi

Clinton kampeni ikaanzisha kilichosemwa ' Disqualify Bernie, defeat him and unify the party' kauli aliyoinukuu Sanders/CNN

Kwa idadi ya kura/Wajumbe Sanders yupo nyuma ya Bi Clinton
Kauli mbiu anayoitumia ni ile tuliyosema 'ameshinda chaguzi 7 kati ya 8' zilizopita.

Hili linaumiza Clinton, lina demoralize base yake huku sanders akipata momentum. Katika kukabiliana na hali hiyo Clinton kampeni imeamua kumwendea ''nuclear''

Sanders kampeni wameeleza lengo ni kukaribiana na Clinton uchguzi uende mkutano mkuu (DNC) na hivyo wanafanya lolote liwezekanalo .

Tatizo linalojitokeza ni malumbano yatakayokiweka chama katika wakati mgumu
Uongozi wa Democrat unaonekana kuwa na wasi wasi ya Republican yasije hamia kwako

MBINU WANAZOTUMIA ZINA HATARI NA FAIDA ZAKE

Clinton katika kutekeleza disqualify, defeat and unity the party, ametupa kombora kwa Bernie akieleza yeye ni democrat siku dahari.
Maana yake, Bernie (independent) amejiunga kuelekea uchaguzi

Sanders akaguswa na kutoka kwa ukali bila kujua ni Kamba ametupiwa.
Amemjibu Bi Clinton kiasi cha kuonekana yeye ni mkorofi na anataka kukigawa chama

Inaendelea...
 
MBINU WANAZOTUMIA.....
Sanders anatumia mbinu ya kuhusisha Bi. Clinton na pesa za walstreet.
Katika kufanya hivyo, ameshambulia kampuni ya GE.

GE inatengeneza vitu vingi kama mashine za ndege, mionzi , vifaa vya nyumbani n.k.

Hatari ya hili ni kuingia katika mpambano na watu wenye uwezo.
Je, anajua super delegates wanaofaidika na uwepo wa kampuni hizo au wall street?

Hoja inajibiwa na Bi. Clinton aliyesema,Obama alichukua pesa za Wall street, haikumzuia kupitisha sheria kali inayowabana Wall street Dodd-Frank act.

Kumetokea malumbano kati ya Bill Clinton na '' black lives matters' kundi la weusi
Majibishano yakipunguza nguvu za Bi.Clinton kuhusu mahusiano na watu wa rangi
Bw Clinton ameomba radhi kutokana na malumbano, kuonyesha utata uliozuka

Kuelekea NY kwenye watu wa rangi, tukio halikuwa zuri kwa Bi. Clinton kampeni

Swali la kujiuliza, inakuwaje Bill aliitwa 'first black president' ashambuliwe na weusi?
Kilichotokea ni kuwa Sanders ametumia mbinu za kuchochea.

Anafahamu hoja za kuvuta watu wa rangi, hatashinda Bi.Clinton
Kuelekea NY ni mwendo mgumu, na kwa kuangalia 'diversity na idadi ya wajumbe

Majimbo yote aliyoshinda ni ya weupe kwa wingi ikwemo caucus ya Wyomin leo hii
Ana wakati mgumu ku-connect na watu wa rangi,njia nzuri ni kutumbukiza ufarakano

Mbinu inaweza kuwa nzuri ikifanikiwa.itakapogeuka kuwa suala la rangi, hoja ya Sanders kushinda kwa watu weupe itamsumbua kuelekea NY, NJ, CA

Bi Clinton ameshikilia hoja ya 'kwamba Sanders amesema Clinton hana sifa(qualify) kuwa Rais Hii ipo katika mkakati wa 'disqualify, defeat and unite the party'

Hatari ya hoja hii ni kurudisha rekodi ya Bi.Clinton katika masikio ya watu.
Hoja ya kupiga kura ya Iraq akiwa seneta, Benghazi akiwa secretary of states n.k

Urahisi wa Bi.Clinton,rekodi yake ipo wazi na inajadiliwa.

Itakapofika kwa Bw Sanders rekodi yake kuhusu video za Cuba, kura kuhusu wahamiaji, na umiliki wa silaha zitaingia katika mzunguko wa mjadiliano

Hatari kubwa kwa Bw Sanders,atakapoijadili hoja anaweza kutafriwa kama ni suala la jinsia 'sex' Anaweza kupoteza uungwaji mkono na wanwake asipokuwa mwangalifu

Ndio maana Bi.Clinton ameishikia bango hoja hii ili kumvuta Bw Sanders
Mjadala wa NY utaeleza kwa uhakika hali ilivyo, utakuwa ni mkali na wenye hisia.

Tusemezane
 
KUELEKEA NY

Wiki iliyopita kulikuwa na chaguzi mbili, Colarado na Wyoming kwa Democrat
Colarado uchaguzi wao kwa Republican ulikuwa tofauti.
Haikuwa primary wala caucus balli kitu kati kati ya hivyo

Walifanya Republican state convention ambako wagombea walipigiwa kura kwa uwiano

Mshindi ni Seneta Cruz aliyondoka na wajumbe zaidi ya 21 kati ya wajumbe takribani 35
Matokeo yalimuongeze idadi ya wajumbe kumkaribia Trump anayeongoza hadi sasa

Kuelekea NY kwenye, Bw Trump anaongoza kura za maoni kwa 'double digit'

Katika wastani wa asilimia 56, Trump amewaacha mbali wapinzani wake.
NY kwa GOP mshindi anachukua wajumbe wote(winner take all)

Cruz anashika nafasi ya tatu jambo linalozidisha utata.

Hakuna anayeweza kuvuka namba 1,237 licha ya ushindi wa Cruz Colarado na matarajio ya Trump NY. Hili linaeleza jambo moja, kwamba safari ya mkutano mkuu ni wazi

Gav Kasich anaelew, ingawa ana nafasi ya pili NY matokeo hayawezi kubadilisha hali yake

Siku za karibuni amejenga hoja, kadri watu wanavyomtambua ndivyo anakubalika
Hilo linaleta matumaini kwake kuwa mkutano mkuu utaweza kumuuunga mkono.

Hata hivyo, ana changamoto kubwa anayokabiliana nayo.
Licha ya kushiriki chaguzi nyingi kuliko Marco Rubio, gavana Kasich ana wajumbe takribani 140 na Marco Rubio aliyejitoa 165.

Baadhi ya wachambuziwanasema,kwenda mkutano mkuu, jina la Rubio lirudishwe ana wajumbe wengi kuliko Kasich

La sivyo, Kasich ajitoe ili kuacha nafasi kwa Trump na Cruz, hasa wakilenga Cruz.

Hili halina maana kuwa Trump au Cruz watavuka mstari wa mwisho, maana yake ni kumpa Cruz wajumbe wengi ili ajenge hoja ndani ya RNC(Mkutano mkuu)

Kutokana na hoja hiyo, Trump anapiga kampeni za kushinda ili aongeze wajumbe.

Anafahamu kwa namba 1,237 anatakiwa ashinde majimbo yaliyobaki kwa wastani wa asilimia 56 , jambo gumu

Hata hivyo, anataka kuwa na wajumbe wa kutosha ili akienda RNC ajenge hoja, inawezekanaje mtu anayeungwa mkono na wapiga kura kataliwe na mkutano mkuu!

Hiyo ndiyo hoja anayosimama nayo sasa

Tutafafanua changamoto za mkutano mkuu kwa kuangalia advantage kwa Trump na Cruz au uwezekano wa mgombea nje ya hao.

Kwasasa turudi Democrat kwenye mtifuano mkali unaoendelea..

Inaendelea...
 
DEMOCRAT
Bw Sanders ameshinda caucus ya Wyoming na kupata wajumbe 14 kati ya 18.
Ushindi haukuwa juu ya wajumbe, ni kujenga hoja, chaguzi 9 ameshinda 8 mfululizo.

Tulisema, lengo lake ni kubadili mwelekeo wa super delegates iwamuunge mkono

Hiyo ni kauli yake, kwamba ukubwa wa ushindi si hoja, bali anashinda majimbo mengi

Bw Sanders aliongea kuwashukuru watu wa Wyoming akiwa NY.
Haaikuonekana kuwa na shamra shamra kutokana na mazonge ya wiki yaliyoharibu mtiririko wake wa ujumbe. Lakini pia ukweli unaokuja mbele

Kuelekea NY, Bi. Clinton anaongoza kura za maoni kwa point 15 kama Pennyslavania

Majimbo hayo mawili tu kati ya mengi yanawajumbe zaidi ya 400.

Kitendawili kinabaki kama Sandes ataweza kushinda katika asilimia 60 na zaidi ukizingatia magawanyo wa population wa maeneo kama NY

Bi Clinton kuongoza kura za maoni haielezi kama ni ushindi.
Huko nyuma aliwahi kuongoza na Bw Sanders kufuta na kubadili matokeo kama ilivyokuwa Michigan, karibu sana Illinoi na hivi karibuni Wisconsin.

Na majimbo yote yana watu wanaomuunga mkono Sanders ambao ni weupe
Hivyo kuna matumaini bado kwa Bw Sanders kubadilisha matokeo na hiyo itadhihirisha kuwa wanaopmpigia kura wengi ni registered Dem tofauti na chaguzi za wazi anazoshinda( wapiga wowote wanaruhusiwa)

Katika mkakati huo, Sanders amelazimisha mjadala kule Brooklyn siku ya Alhamisi.

Mjadala huo utakuwa mkali na atakayebofoa itaeleza zaidi katika kura.

Kutokana na mkizano uliopo 'tension' alhamisi inaweza kuwa siku ya kubadili mwelekeo wa kura za maoni, ima Sanders kuziba pengo au Clinton kuongeza

Inaendelea Democrat
 
....Inaendelea

Bado Sanders anakabiliwa na wakati mgumu kwa maana moja.

Iikitokea kashinda NY kwa 55 kwa 45(nadharia) na Pennyslavani katika 55 kwa 45, pengine Connecticut 55 kwa 45, idadi ya wajumbe bado itakuwa chache.

Democrat wanafanya uwiano, na hiyo itaamaanisha haya

1. Sanders ataziba pengo la wajumbe kati yake na Clinton.
Ataweza kujenga hoja ya nguvu kwenda mkutano mkuu

2. Wakati huo Bi. Clinton ataongeza wajumbe na kukaribia 2383

Tufafanue kuhusu hili la pili.

Kwasasa Bi Clinton ana wajumbe kwa ujumla wao 1736. Bw Sanders 1068

NY ina wajumbe takribani 250 kwa hesabu za karibu , katika ushindi wa 55 kwa 45 in favor of Sanders, ataongeza wajumbe karibia na 130 na Bi Clinton 120.

Ukiongeza kwa idadi kuu waliyo nayo, utaona Clinton anakaribia 2383 kuliko Sanders

Sanders ana nafasi ya kusema, hana wajumbe wengi lakini ameshinda majimbo mengi.
Hilo litabadili super delegates na kupelekea kwenda mkutano mkuu.

Pia atasema, kura za maoni zinaonyesha akiwashinda wagombe wote wa Republican

Advantage ya Bi Clinton ,atasema ana kura nyingi kuliko mgombea wowote wa 2016

Ana wajumbe wengi kukiko mpinzani wake,kura za maoni anamshinda Trump na Cruz

Tumaini lake ni kama Kasich ataachia ngazi, kura za maoni zinaonyesha akimshinda Bi Clinton.

Democrat bado hali si laini kama inavyoonekana ingawa hesabu ni ngumu kwa Sanders

Tusemezane
 
THE ESTABLISHMENT'
HAWAMTAKI TRUMP, HAWAMPENDI CRUZ

Magwiji wa Republican wanapiga kwa kila hali kumsimamisha Trump
Wao husema hawamtaki Trump, hawmpendi Cruz!

Magwiji hawamtaki Trump anakinzana na 'values' zao na huenda GOP ikashindwa

Hizo ndizo hisia zao kuwa Trump hawezi kusimama na mgombea wa Dem kwasababu zao ziwe za kisera au za kichama. Hawamtaki

'The establishment' hawampendi Senta Cruz kutoka na mitifuano katika seneti na vikao vingine. Cruz haendani sambamba na 'wazee' wa Washington wakimwita Jeuri

Swali, kama ni hivyo inakuwaje huko nyuma tulisema 'the establishment' wanamuunga mkono Cruz?

Inaonekana kama kuchanganya masuala, la hasha.
Magwiji wanamtumia Cruz katika kumzuia Trump kufikia wajumbe 1,237

Hilo Magwiji wamefanikiwa kwasababu hesabu hazimpi nafasi ya kufikia 1,237.

Wisconsin tuliona akina J.Bush, Fiorina, Scott Walker na wengineo wakimpigia kampeni ya kufa mtu.

Si kwamba wanampenda,wanajua Cruz hawezi kufikia namba 1,237 isipokuwa ni msaada mkubwa kumsimamisha Trump kabla ya kuelekea mkutano mkuu

MKUTANO MKUU (RNC)
Tukiri wazi sheria zinazotumika na Republican au Democrat ndani ya mkutano mkuu, ni nyingi ,zinachanganya na zina formula na takwimu ngumu.

Kuzieleza kwa ukamilifu itahitaji muda sana , na pengine hazitaeleweka

Tunachokifanya ni kueleza picha nzima itakavyokuwa na jinsi mikakati na mbinu mbali mbali za ushindi zinavyotumika.

Hivyo,ni picha ya juu kupata mwanga nini kinaendelea

Mkutano mkuu (RNC) utapiga kura ya kumpata mgombea ikiwa hatapatikana katika uchaguzi unaoendelea.

Utaratibu ni kuwa na mizunguko mitatu ya kura. Kila mzunguko una namna zake

Mzunguko wa kwanza, wajumbe wa mgombea kumpigia kura kwa lazima bila kujali katika jimbo hilo mjumbe alimuunga mkono nani.

Mfano, Trump akienda na wajumbe 700 wote watalazimika kumpigia kura kama ilivyo kwa Cruz na Kasich au ''mwingine''

Mzunguko wa kwanza hautegemewi kutoa matokeo tofauti na sasa.
Ulazima wa kumpigia kura mgombe husika unafunga wajumbe

Mzunguko wa pili, wajumbe asilimia 55 watakuwa huru kumpigia wamtakaye.
Ikitokea hakuna anayefikia namba husika, mzungo wa tatu utalazimika kuingia

Mzunguko wa tatu wajumbe watakuwa huru kwa asilimia 85. Hii maana yake, hadi hapo robo tatu ya wajumbe watakuwa huru kumpigia kura wamtakaye

Hapo ndipo hesabu za magwiji zilipo, kwamba kazi ya kumsimamisha Trump wasiyemtaka itakuwa imekamilika na kupelekea kwenda mkutano mkuu.

Kukamilika kwa kazi kutafungua mlango wa kumuondoa Cruz ''wasiyempenda''

Hapo ndipo hesabu za gavana Kasich zilipo, kwamba atakuwa mbadala wa wawili

Hata hivyo Cruz ana matumaini kwamba si magwiji wote wasiompenda na kwamba kwa wenye hofu na Trump yeye ndiye chaguo. Kuna ukweli?

Trump hana furaha akijua mzunguko wa pili utawaacha huru wenye misimamo inayoyumba dhidi yake.

Anahisi kuwa vulnerable mzunguko wa tatu na ndipo hofu yake ilipojijenga leo hii

Tutaendelea ....
 
GAVANA KASICH NI 'FACTOR'

Katika hali ya kawaida, Republican wangeweka shinikizo kwa Gav Kasich kuaachi ngazi

Licha ya ushindi wa Ohio, hajashinda popote, ana wajumbe wachache kuliko Marco Rubio. Bado hakuna shinikizo la yeye kujitoa

Magwiji wa Republican wanamuona kama msaidizi mzuri katika jitihada za kumzuia Trump

Trump amesikika mara nyingi akilalamikia uwepo wa Kasich kama kikwazo cha ushindi

The establishment wamemuacha,anasaidiana na Seneta Cruz kuweka ngumu kwa Trump.
Wanamwangalia kama mbadala kwa wanaoamini 'hawamtaki Trump na hawampendi Cruz'

Kasich msimamo wake ni kwenda mkutano mkuu ''MM'' au RNC.

Cruz anatambua, licha ya usaidizi wa Kasich kumdhibiti Trump mbele ya safari ni tatizo

Trump anasema Kasich anapunguza kura zake,Cruz ana hofu ndani ya RNC kuwa mbadala

Kwa pamoja wanatoa shinikizo Kascih aachie ngazi.Magwiji( siri moyoni) wapo pembeni

Gavana Kasich anasema ndani ya RNC uchaguzi uwe 'open na si closed'

Open maana yake yoyote anaweza kushiriki. Spika wa Congress Paul Ryan anatarajiwa kukataa jina lake lisiingie mkutano mkuu.

Kwa open convention Kasich anataka kukwepa Rule (40)b

Rule 40b inasema, ili mtu aingie katika mkutano mkuu, lazima ashinde majimbo nane katika uchaguzi. Kasich ana jimbo moja tu.

Cruz ana hofu, kwamba open convention atatokea mwingine,kwavile hapendwi ''ana maadui wengi'' upendeleo dhidi ya Trump utatokweka.
Pili, anataka kumzuia Kasich kwa 40b kwasababu tulizoeleza, hana majimbo 8

Cruz anataka 'closed convention' Kasich anataka 'open convention'

Trump anataka 'closed convention' ingawa kwenda RNC ni chaguzo asilolitaka kabisa

Trump angependa Kasich aende RNC ili agawane kura za wajumbe na Cruz

Lakini pia anataka Kasich aachie ngazi ili ashinde majimbo yaliyobaki aende RNC akiwa na hoja ya wajumbe wengi.

Kwa mtazamo huo, gavana Kasich ni factor. Ni msumeno unaokata mbele na nyuma
Ni sime yenye ncha na pande mbili kali, kuibeba inahitaji uangalifu sana

Tusemezane
 
MDAHALO WA DEMOCRAT 13/04/2016
REPUBLICAN : MATARAJIO YA MKUTANO MKUU

Wiki hii waombea wa GOP walikuwa na midahalo iliyohisisha maisha yao nje ya kisiasa yakiambatana na shughuli za kisiasa

Gavana Kasich alisisitiza ushiriki kuelekea mkutano mkuu akisisitiza kadri anavyoeleweka ana nafasi ya kushinda ndani ya mkutano mkuu

Bw Trump amekuwa katika malumbano na viongozi wa RNC akisisitizau chaguzi hasa wa Colorado 'umeibiwa' kumnyima fursa' . Hoja ya Trump niwananchi kutoshirikishwa

Tufafanue, Colorado haikupiga kura kama jimbo bali mkutano mkuu wa jimbo ulichagua idadi ya wajumbe. Cruz alishinda, jambo ambalo Trump anaoliona kama hujuma

Hoja ya viongozi wa RNC ni kuwa mwongozo upo miaka yote, Trump hana sababu za kulalamika kwa 'sheria' za Repunblican zinazotumika miaka dahari na alizozikuta

Hofi kubwa ya Trump ni kuelekea mkutano mkuu ambako ndoto yake inaweza zimwa

Seneta Cruz, matumaini ni mzunguko wa pili utampa wajumbe wa kutosha
Hapa tusema , mzunguko wa kwanza hautazaa matokeo tofauti kwani wajumbe lazima wapige kura kama maamuzi ya kura za wananchi yalivyosema

Maana yake,mzunguko wa kwanza utakuwa na idadi watakayokuwa nao wakati wakiingia mkutano mkuu. Kwamba, aliyeshinda jimbo, wajumbe wanalazimika kumpigia kura kutokana na 'popular vote' iliyompa ushindi

Matumaini ya Cruz yana namna mbili. Yanaweza kuwa kweli kwani wajumbe 55 watakapokuwa huru katika mzunguko wa pili, wanaweza kumuongezea kura.
Na kwavile 'the establishments' wapo nyuma yake ana matumaini

Kwa upande wa pili, matumaini yanaweza yasiwe kweli.
Wajumbe huru wanaweza kumpigia kura Trump au Kasich.

Lakini pia dalili zinaonyesha the establishment wameanza kukacha mkutano mkuu.
Jeff Bush na Senata mwingine wametangaza kutohudhuria. Nguvu ya the establishment ikipungua, nguvu ya Cruz ipo matatani

Kumbuka, hawamtaki Trump kuwa mgombe lakini hawampendi Cruz.

Hii inakuwa katika advantage ya Kasich na mzunguko ukifikia wa tatu, mambo yatabadilika kabisa. Asilimia 85 ya wajumbe wakiwa huru, picha itakuwa tofauti

Hayo yakiendelea kwa Rep. kizaizai kipo Democrat siku ya leo
Mdahalo utakaoamua mwelekeo wa kura za April 19 kule NY na ku set new tone

Inaendelea
 
MDAHALO WA DEMOCRAT

Mjadala haukuwepo katika kalenda za midahalo. Seneta Sanders aliomba ufanyike Brooklyn NY akitegemea ni eneo alilozaliwa na anaweza kubadili mwelekeo.
Hoja kubwa ni kuwafikia watu wengi na fursa hiyo kupambana na Bi Clinton

Bi Clinton hakupendelea mara ya kwanza. Kutokana na umuhimu wa NY na kwavile mjadala uliombwa Brooklyn kwenye support nyingi, hakuchukua risk akakubali

Alikubali akijua utafanyaika siku chache kabla ya Jumanne na hivyo kuto toa nafasi ya Sanders kubadili upepo ikitoke vinginevyo.

Ni uamuzi wenye 'risk' kwasababu baadhi ya kura za maoni zinaonyesha akiongoza kwa point 8 hadi 13. Mdahalo ungeweza kumjenga au kumboma. Akakubali

Mdahalo ulitegemewa kuwa mkali kwa Sanders kubadilisha hali ya kura katika jimbo analohitaji sana. Bi Clinton anataka kumaliza mlolongo wa majimbo aliyepoteza na kwamba, New York ni nyumbani kwake akiwa Seneta

Mjadala ulitawaliwa na mambo ya ndani , uchumi na nje.
Ulikuwa juu ya issues tofauti ingawa kwa nyakati 'makonde' yalivurumishwa

MBINU
Sanders alitumia mbinu ya kumhusisha Bi Clinton na pesa za 'wall street na Super PAC'. Huko nyuma tumeongelea nini maana ya super PAC.

Mara zote alimhusisha akitarajia litajenga chuki na watu hasa walioathrika na mdodoro wa uchumi ulioanza na matatizo 'wall street'

Mbinu ya pili ni kumbana Clinton kuhusu kura yake kuhusu vita ya Iraq

Na pia alitumia uzoefu wa Bi Clinton kama secretary of state kuonyesha matatizo yanayotokea Libya yameanza wakati wake

Kuhusu siasa za nje Sanders ameungana na Trump kuhusu gharama za US katika umoja huo. Msimamo wake ni sawa na wa Trump

Bi CLINTON
Alitumia mbinu ya kujifungamanisha na maamuzi 'mazuri' ya Obama.
Alitumia uzoefu wake katika siasa za kimataifa
Alilinda rekodi yake akiwa seneta wa New York na aliyoyafanya
Aliegemea katika constituents akiwafikia watu wa rangi na jinsia tofauti

inaendelea..
 
Katika mambo yaliyojitokeza na kumsumbua Bi Clinton ni suala la hotuba aliyoitoa wall street ambayo Bw Sanders angependa itolewe hadharani.

Kwa Sanders suala la kodi (tax file)limemsumbua sana hadi kuahidi kutoa kesho

Bi Clinton alionekana kujiandaa na mtulivu kuliko Sanders.
Hoja alizorushiwa aliweza kuzigeuza na kuwa mwiba kwa Sanders.

Kwa mfano, suala la hotuba, Clinton alimgeuza kibao kwa Sanders ili naye aweke rekodi zake wazi

Bwana Sanders hakuongelea suala la Benghazi Libya kama alivyozoea.
Ilionekana kiuchambuzi, kadri alivyoliongelea ndivyo lilivyompa Clinton umaarufu

Katika siasa za kimataifa, Bi Clinton alionyesha kuwa na utambuzi wa suala la uchumi na usalama na aliweza kulihusisha vema na ushiriki wa NATO.

Bwana Sanders amechukua nafasi ya Trump katika suala la NATO, mbele ya safari awe mgombea au la litamsumbua.

Hakuliongelea kama sehemu ya ulinzi na usalama

Kuhusu afya, msimamo wa Bi Clinton ni kuendelea na Obamacare pale alipoachia.
Bwana Sanders anasema atatengeneza mfumo tofauti.

Kwa eneo kama NY kauli ya Sanders itamsumbua. Suala la afya ni maarufu kwa baadhi ya watu hasa wa rangi. Ingawa si wote lakini sehemu kubwa italiangalia suala hilo kama tishio la kufutwa kwa Obamacare

Bwana Sanders alisifia rekodi yake ya kumshinda Trump kwa kura za maoni kuliko Clinton, na ushindi wake mfululizo wa majimbo 7.

Hoja hii ilikutana na ya Bi Clinton aliyejibu kuwa ana wapiga kura milioni 2.5 Zaidi ya Sanders na 1.5m Zaidi ya Trump na alivyoshinda kusini, kaskazini, mashriki n.k

Hoja hiyo ilionekana kumaliza tambo za Sanders. Hata hivyo, Sanders amesifia rekodi yake ya kuleta vijana wadogo katika siasa na independent.

Hili ni jambo lililomfanya aonekane ana nguvu na msisimko kisiasa kuliko Bi Clinton

Yapo mengi ya kuzungumzia tutaendelea kudonoa donoa hadi Jumanne tutakapokuwa NY katika kitim timu

Tusemezane
 
MDAHALO WA DEM
Baadhi ya yaliyojitokeza ni wagombea kucheza na 'political base' zao. Bi Hillary hakusita kusema kuna 'systemic racism' akiwanyooshea vidole weupe. Sanders aliendelea na hoja ya wall street na livyosimama kuilaumu Israel kwa kutumia nguvu nyingi kule gaza

Sanders alilenga jamii ya watu wa mashariki ya kati akijua mji wa NY una mchanganyiko

Alichotaka ni kura popote hasa kwa kuzingatia kura za maoni hazimpi nafasi kushinda

Sanders alikwenda kwenye mkutano Vatican uliohusu mambo ya utawala na umasikini

Pamoja na hayo alikutana na Pope Francis. Ziara hii ilikuwa ni ku boost siasa za nje

Ni ziara iliyolenga kuwavuta baadhi ya watu wenye misimamo ya kidini 'evangelical'
Tatizo ni kuwa values anazosimamia zinatofautiana na zile za kanisa Catholic
Na kwamba yeye ni Myahudi jambo linaloleta maswali Zaidi

Lengo lake hasa ni kuvuta evangelical kuelekea majimbo yanayofuata Aril 26

Majimbo hayo ni primaries tofauti na caucus na hadi sasa inaonekana Clinton ametambua njia za kumbana katika maeneo ya weupe

Na hili la uyahudi linaenda mbali. Bw Snaders anasimama kulaumu Israel, wakati huo huo akisema yeye ni pro-Israel na akiwa Myahudi .

Kwa kiasi fulani haliingii vema masikioni mwa walengwa hasa wa mashariki ya kati. Anaonekana kama kucheza na siasa na si uhalisia

Bi Clinton alitumia suala la udhibiti wa silaha kumbana vema bwana Sanders.

Clinton alionekana ku connect vema matukio ya silaha na hali ilivyo kwa kumsukumia lawama bw Sander kwa kura alizopiga kuhusu suala la gun control

Vermont anakotoka Sanders kama Senata hawana udhibiti wa silaha.

Bi Clinton alitumia hilo kuonyesha tatizo la kuzagaa silaha NY.

Hata hivyo, kidogo angeingia kwenye matata kwa kutokuwa na takwimu za kuthbitisha ingawa ki mantiki inaweza kuwa hivyo

Haionekani kama kura za maoni zimebadilika sana NY baada ya mdahalo kufanyika. Bado Bi Clinton anatarajia kushinda

Ushindi wa Clinton utauwa na maana tatu
1. Kuzuia Sanders kuendeleza kauli za ushindi mfululizo na momentum ili kulinda super delegates. Hadi sasa Sander ameongeza 11 na kufikia 46

2. NY ni jimbo alilokuwa seneta kwa miaka 8.
Kushindwa katika jimbo hili iamuathiri sana kisaikolojia na hasa timu aliyo nayo.

3. Ushindi wa point 10 unaweza kumsaidia kufukia idadi ya wajumbe waliopeteza katika majimbo yaliyopita tukijua NY ina wajumbe Zaidi ya 250 na tofauti ya asilimia 5-10 ina impact kubwa katika idadi ya wajumbe

Hali ikoje hadi sasa kwa Dem na GOP?

Inaendelea
 
Mkuu nlikua naomba kama utaeka majimbo yote na kura walizopata coz kuna majimbo mengine sijaona matokeo kwa mfano yale ya april 5
 
Mkuu nlikua naomba kama utaeka majimbo yote na kura walizopata coz kuna majimbo mengine sijaona matokeo kwa mfano yale ya april 5
Pamoja na kwamba umemuomba Nguruvi3, ngoja nimsaidie katika hili;

Kwa upande wa Democrats wajumbe wanaoitwa super delegates ambao ni 500, mpaka sasa Hillary Clinton tayari anao 469 na Sanders 31 tu.

Katika kura zilizopigwa hadi leo kwa kila jimbo mambo ni kama ifuatavyo;

us-elections-jpg.339703

Mpaka sasa kwa matokeo hayo hapo juu;
Clinton ana wajumbe 1289 + 569 = 1758
Sanders ana wajumbe 1045 + 31 = 1076

Pia zipo teritories kama Guam, Puerto Rico, Virgin Islands n.k.​
 
Thanx sana mag3 na kule GOP cipi odd zao zipoje mpaka sasa
Kwa Republicans kuna mkanganyiko kidogo ila ni vizuri tu kusema mpaka sasa Trump anao delegates 743, Cruz 559 na Kasich 144. Tatizo lao ni kwamba wagombea bado ni wengi na pamoja na kura kupigwa pia bado kuna kunyang'anyana wajumbe. Ziko sehemu ambako mshindi anaweza kuishia kuambulia wajumbe wachache na ziko sehemu ambapo mshindi anazoa wajumbe wote...Idadi inayotakiwa kufikiwa ni wajumbe 1237 tu.

Mengine ni kama alivyoelezea Nguruvi3
 
Mkuu Shark kama alivyoonyesha namba Mkuu Mag3 hiyo ndiyo hali ilivyo

Niongezee kidogo kuhusu mchanganuo wa hizo namba na jinsi unavyotueleza

Republican
Namba inyotakiwa kwa mgombea kubeba bendera ya chama ni 1237

Trump ndiye mwenye wajumbe wengi hadi sasa na hivyo kuwa mfano mzuri wa hesabu

Idadi ya wajumbe wa Trump ni 743 kukiwa na tofauti ya 494 kuifikia magic number 1237

Wajumbe waliobaki katika majimbo yaliyo salia ni 838.

Idadi ya wajumbe anaotakiwa apate kutoka 838 ni 494 ili kufikia 1237 sawa na asilimia 58.9

Hii ina maana, kwa majimbo yaliyobaki Trump lazima ashinde kwa asilimia 58.9 kila moja

Tatizo linakuja katika hali zifuatazo

1. Hadi sasa Trump hajaweza kushinda jimbo lolote kwa asilimia 58

2. Wapo wagombea 3, katika asilimia 100 mmoja wao akipata asilimia 10 katika jimbo na wawili kugawana zilizobaki itakuwa 45% kwa 45% (Hii ni nadharia tu) hapo front runner Trump hataweza kupata ile 58% hata kama ni jimbo moja tu. Hivyo ile nafasi ya kufikia 1237 inapungua

3. Uchaguzi wa Republican ni ule wa winner take all ambapo uwezekano wa Trump kupoteza jimbo moja upo katika majimbo yaliyobaki. Hivyo atakuwa amepoteza 58% ya jimbo ambalo atashindwa.

Asilimia ya kufikia 1237 itakuwa zaidi ya 60 na kufanya ugumu.
Akipoteza majimbo 3 tu katika yaliyobaki namba 1237 haitawezekana

Pili, uchaguzi wa Republican kuna baadhi ya majimbo ni winner take most. Kwamba watagawana wajumbe kutokana na ushindi katika district congressional. Hapo uwezekano wa kupata asilimia 58 anayohitaji ni mdogo sana

Hili linatueleza jambo moja, kwamba kwa Republican uwezekano wa mmoja wao kupata 1237 ni kama haupo.

Kinachowezekana ni kukaribia katika 1237 pengine kukiwa na upungufu wa wajumbe 100 au 200

Katika mazingira hayo lazima uchaguzi uende RNC (mkutano mkuu)

Huko nako mzunguko wa kwanza hautazaa tofauti. Taratibu ni kuwa wajumbe alio nao mgombe watampigia kura watake wasitake. Hivyo, Trump anaweza kuwa na wajumbe 1200 hao watampigia kura kama Cruz na Kasich kwa wajumbe wao

Mzunguko wa pili, asilimia 55 ya wajumbe itakuwa huru kumpigia yoyote. Inawezekana Trump akapata 1237 au la

Mzunguko wa tatu asilimia 85 itakuwa huru kumpigia mgombea, hapa ndipo tutarajie mgombea kupatikana

Hili la mkutano mkuu si rahisi. Kwa mfano, inajenga picha gani Trump mwenye wajumbe (mfano) 1200 akiachwa mzunguko wa tatu na Kasich mwenye wajumbe 160(mfano) kwa wakati huo?

Tumeeleza haya kutoa picha, na tunakiri sheria zinazohusiana na RNC ni ngumu kueleweka.
Mathalani kuna majimbo yana taratibu zake, ndani ya RNC wajumbe watagawanywa kufuatana na takwimu za matokeo ya uchaguzi mkuu 2012 n.k

Tutaangalia Democrat nako hali ikoje kutokana na namba hizo hizo alizoweka Mag3
 
UCHAGUZI NY
Kura zinaendelea kupigwa kwa pande zote GOP na Dem
Matarajio ya awali ni Trump kushinda kwa upande wa Republican na Clinton-Dem

Hata hivyo, kura za maoni zimekuwa zikionyesha matokeo tofauti na uhalisia

Kwa upande wa Dem,kura za maoni Clinton aliongoza Michigan kwa point zaidi ya 10 huku matokeo yakimpa ushindi Bw Sanders

Bw Sanders amekuwa na mikusanyiko mikubwa. Kampeni yake imechagiza vijana si kupiga kura tu bali kuleta 'sintofahamu' kama ilivyotokea California na katika midahalo

Bw Sanders analaumiwa kwa kukaa kimya hata pale wafuasi wake wanapovuka mipaka

Kwa NY Bw Sanders ana changamoto moja kubwa, kwamba siyo uchaguzi wa wazi unaoweza kuvuta watu wote kupiga kura.

Ni uchaguzi wa Democrat waliojiandikisha
Inategemea aliwezaje kushawishi watu wake kujiandikisha siku za nyuma

Makundi yanayoonekana katika mikutano yake yanaweza kuwa hayakujiandikisha

Kwa upande mwingine,ushindi wa NY utampa morali ya kuendelea na uchaguzi.

Kwa hali ilivyo hata kama atashinda kwa mfano wa Michigan (51%) bado hatapunguza pengo la wajumbe, lakini atakuwa na momentum na hoja kama tulivyoeleza siku za nyuma

Pamoja na hayo atakuwa na hoja kwamba ameuvuta makundi ikiwemo watu wa rangi. Tatizo la watu wa rangi ni kubwa kwake, ameshinda kwa weupe katika caucus na chaguzi za 'open' kama Michigan

Kwa Bi Clinton, ana mzigo mzito. Kilicho mbele yake ni kushinda, akishindwa katika jimbo alilokuwa seneta kwa miaka 8 itajenga hofu kwa super delegates kuhusu uwezo wake, lakini kubwa itamuathiri sana kisaikolojia

Tutaendelea kuwahabarisha kadri masaa yanavyosonga mbele
 
MATOKEO NY

Bw Trump kashinda upande wa Republican
Bi Clinton kashinda upande wa Democrat

Namba zinakuja, na tutawaletea matokeo ya mwisho muda si mrefu

MATOKEO YA NY

REPUBLICAN

Matokeo yakiwa 83% Trump anaongoza kwa 59.9% akifuatiwa kwa mbali na Gavana Kasich 25.3% na Senata Cruz 14.9%

Ni wazi, Trump atashinda si chini ya asilimia 58, ushindi utakaompa wajumbe wengi
Hilo halimfanyi akaribie namba 1237, bali linamjenga kisiasa zaid baada ya kupoteza momentum kwa muda sasa

Jambo moja lililojitokeza leo, akiwashukuru wapiga kura wake Trump alitoa hotuba fupi isiyo na majigambo wala kashfa dhidi ya wenzake. Ni kama ameshauriwa kuongea vitu vya maana ili kupunguza 'controversies' zinazotokana na kauli zake

Ushindi wa Trump dhidi ya wapinzani wake upo katika 35% Zaidi kinyume na kura za maoni zilivyoonyesha, kwamba amekwenda mbali ya ilivyotarajiwa

Namba za mwisho za wajumbe 95 zikipatikana tutaendelea kuwaletea mchanganuo na hali ilivyo mbele ya safari

Tuangalie Democrat
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom