Uchaguzi Marekani

Nadhani kwa upande wa Republicans kama ilivyotabiriwa Trump kashinda Indiana na hivyo Ted Cruz kulazimika kubwaga manyanga. Na sasa macho yanaelekezwa kwa Democrats na msimamo wa wajumbe baada ya Sanders kushinda Indiana ni kama ifuatavyo;

Hillary Clinton...2201 (bado...182)
Bernie Sanders..1399 (bado...984)

Tayari Sanders kasema hatoki, anaendelea...
 
Update;
  1. Hillary Clinton...2202 (bado...181)
  2. Bernie Sanders..1400 (bado...983)
 
Nadhani kwa upande wa Republicans kama ilivyotabiriwa Trump kashinda Indiana na hivyo Ted Cruz kulazimika kubwaga manyanga. Na sasa macho yanaelekezwa kwa Democrats na msimamo wa wajumbe baada ya Sanders kushinda Indiana ni kama ifuatavyo;

Hillary Clinton...2201 (bado...182)
Bernie Sanders..1399 (bado...984)

Tayari Sanders kasema hatoki, anaendelea...
Sanders ameulizwa na CNN kwanini bado anaendelea. Kilichonishtua kidogo ni message yake kila baada ya muda
1. Anasema yupo ili watu wa majimbo yaliyobaki sauti zao zisikike.
Hapa kuna tatizo kidogo, Republican wameshamaliza licha ya wakati mgumu sana, sauti anazotaka Sanders zina mantiki gani?

2. Kabadili kauli na kusema analeta msisimko mkubwa na hilo ni jambo jema

3. Mwisho anasema uwezekano wa kushinda upo na super delegates waangalie majimbo yao yalivyopiga kura na wamuunge mkono

Tunaposoma kauli zake, kuna kitu ambacho Clinton kampeni haijakiona. Hatujui ni kipi, lakini lipo jambo. Na Clinton kampeni imefanya move ambayo haieleweki.

Clinton hakukampeni Indiana kwa bidii, mara alikuwa west Virginia.
Inaonekana wanajipanga kwa uchaguzi mkuu na kupambana na Trump.

Je, kwa haya ya Sanders yasiyoeleweka kirahisi, wana Imani ya'presumptive nominee'?

Sanders amekiri 'tough hill to climb, but not impossible to climb' Kwa maana ataendelea kuleta uharibifu mkubwa sana kwa Clinton hata kama hatafanikiwa kuwa mgombea

Tayari kama alivyozungumza leo,Trump anatumia hoja za Sanders kuanzia wakati huu

Ingawa Sanders anakana hilo kwa kusema 'Republican wanafanya research zao' kumhusu Clinton, hakuna shaka kwa upande wa Democrat, anaacha makovu makubwa

Makovu ni pamoja na lile la wafuasi wake kuendelea kuimba hawatampigia kura Clinton.

Katika hali ya 'frustrations' Sanders amewashambulia the Establishments kwamba ndio wanaotegeneza super delegates itakayomsaidia Clinton. Kauli yake inaweza kumgharimu

Kalenda http://www.nytimes.com/interactive/2016/us/elections/primary-calendar-and-results.html?_r=0
Tusemezane
 
Sanders ameulizwa na CNN kwanini bado anaendelea. Kilichonishtua kidogo ni message yake kila baada ya muda
1. Anasema yupo ili watu wa majimbo yaliyobaki sauti zao zisikike.
Hapa kuna tatizo kidogo, Republican wameshamaliza licha ya wakati mgumu sana, sauti anazotaka Sanders zina mantiki gani?

2. Kabadili kauli na kusema analeta msisimko mkubwa na hilo ni jambo jema

3. Mwisho anasema uwezekano wa kushinda upo na super delegates waangalie majimbo yao yalivyopiga kura na wamuunge mkono

Tunaposoma kauli zake, kuna kitu ambacho Clinton kampeni haijakiona. Hatujui ni kipi, lakini lipo jambo. Na Clinton kampeni imefanya move ambayo haieleweki.

Clinton hakukampeni Indiana kwa bidii, mara alikuwa west Virginia.
Inaonekana wanajipanga kwa uchaguzi mkuu na kupambana na Trump.
Lakini je, kwa haya ya Sanders ambayo hayaeleweki katika lugha nyepesi, bado wana Imani ya kuwa presumptive nominee?

Sanders amekiri 'tough hill to climb, but not impossible to climb' Kwa maana hii ataendelea kuleta uharibifu mkubwa sana kwa Clinton hata kama hatafanikiwa kuwa mgombea

Tayari kama alivyozungumza leo,Trump anatumia hoja za Sanders kuanzia wakati huu
Ingawa Sanders anakana hilo kwa kusema 'Republican wanafanya research zao' kumhusu Clinton, hakuna shaka kwa upande wa Democrat, anaacha makovu makubwa

Makovu hayo ni pamoja na lile la wafuasi wake kuendelea kuimba hawatampigia kura Clinton.

Katika hali ya 'frustrations' Sanders amewashambulia the Establishments kwamba ndio wanaotegeneza super delegates itakayomsaidia Clinton. Kauli yake inaweza kumgharimu
Sasa Clinton atakuwa na wapinzani wawili, Sanders na Trump, katika hoja zile zile. Kaazi kweli kweli!
 
Sasa Clinton atakuwa na wapinzani wawili, Sanders na Trump, katika hoja zile zile. Kaazi kweli kweli!
Hili ndilo linalowapa Democrat hofu kwasasa. Kwamba, mashambulizi kutoka pande zote yatamdhoofisha Clinton

Wapo wanaojiuliza Trump amewezaje kubadili mwelekeo kwa muda mfupi?
Zipo sababu nyingi

1. Kampeni ya Trump iliposhinda majimbo 5 wiki iliyopita ilikuwa pigo kwa Cruz na Kasich

2. Muungano wa Cruz-Kasich ulionekana ni kukata tamaa,wafuasi wao walivunjika moyo.
Washindani wawili wanapoungana dhidi ya mmoja, ni dalili za udhaifu na kukata tamaa

3. Cruz kumchagua Fiorina nalo liliongeza hali ya kukata tamaa.
Fiorina hana tatizo isipokuwa mazingira yake ya kuingia katika kinyang'anyiro yalikuwa na utata katika wakati wa majeruhi

4. Wafuasi wa Cruz na Kasich walikata tamaa na kumwacha Trump akipiga pigo la mwhisho kwa kishindo usiku wa jana

5. Reublican wengi hawakaupenda kwenda convention tofauti na the establishments. Wengi wanadhani convention ingeleta uharibifu Zaidi ya

Lakini pia kuna jambo zuri alilofanya Trump. Wakati kampeni yake ikisuasua wiki chache zilizopita wapinzani wake Cruz na Kasich waliomba wawe na mdahalo.

Trump aliona hatari ya midahalo kwani ilikuwa ina mu-expose katika mazingira magumu huku wapinzani wake wakiona bora. Kwa mfano, wengi walitambua kuwa Kasich ni mzuri sana dakika za mwisho wakati wamebaki 3. Hilo lilipelekea Trump kupoteza majimbo

Inaelekea washauri wake walimzuia, kwa maana mbili. Kwanza kutotoa nafasi kwa wapinzani wake ndani ya GOP kustawi, na pili, kutokuwa na rekodi inayoweza kumuumiza wakati wa uchaguzi mkuu.

Mfano wa hili ni kauli za kuondoa majeshi nchi za mashariki ya mbali ambalo kitaalamu na kwa siasa za Marekani halikukubalika kwa wataalam hawaafiki

Hata hivyol, pamoja na RNC kutoa tamko la Trump kuwa presumptive nominee, bado kuna mtifuano ndani ya Republican. Tutafafanua hili

Kwa Democrat, ipo sababu nyingine Sanders anaendelea kuwepo, akitegemea litatokea jambo nje ya uchaguzi dhidi ya Clinton na kuweza kujenga hoja. Tutaliangalia hili pia

John Kasich naye kabwaga manyanga na sasa Trump hana tena mpinzani ndani ya Republicans, sana sana wanapigana vikumbo kumpa sapoti isipokuwa bado watu kama Lindsey Graham. John Macain na wengineo. Gingrich tayari anaonekana kuchangamkia nafasi ya U-Vice President, duh!

Huko kwa Democrats mambo bado kabisa, Bernie Sanders ameamua liwalo na liwe, atapigana mpaka mwisho. Hali hii inamweka Clinton katika hali ya wasi wasi na sintofahamu ya kuamua aendeshe vipi kampeni bila ya kuwaudhi watu wa Sanders ambao wengine wameonesha kusita kumuunga mkono Clinton.

Update;
Kiujumla super delegates wako 712. Kati ya hawa 561 tayari wamechagua upande na 151 bado. Katika waliochagua upande 522 wako kwa Clinton na 39 wako kwa Sanders. Wakati huo delegates wa kuchaguliwa Clinton anao 1701 wakati Sanders anao 1411, hivyo kwa sasa hesabu kamili iko kama ifuatavyo;
  1. Hillary Clinton...1701+522 = 2223 (bado...160 kufikia 2383)
  2. Bernie Sanders..1411 + 39 = 1450 (bado...933)
Kimahesabu hakuna namna Sanders atamfikia Clinton; hata hivyo Sanders anadai anao ushawishi wa kutosha kuwabadilisha misimamo baadhi ya wajumbe kwenye Convention. Hii inatokana na baadhi ya polls kuonesha kuwa ni yeye anayeweza kumshinda mgombea wa Republican, Donald Trump, kwa mbali kuliko Clinton.

Clinton kwa upande wake ameamua kuelekeza mashambulizi yake zaidi dhidi ya Trump wa Republican badala ya mpinzani wake ndani ya chama, Sanders.
 
Poll za siku za karibuni zinaonyesha Clinton akimbwaga Trump kwa point 13

Hoja ya Sanders itabidi aijenge kwanini anadhani anaweza kumshinda Trump na si Clinton na tofauti ya point 13 na 19 inaweza kuelezwa vipi

Democrat wana wakati mgumu kidogo.
Sanders ana derail maandalizi dhidi ya Trump wakati Trump akimshambulia Clinton.

Hoja ya Sanders imebadilika sasa anasema ana uwezo wa kuwabadili super delegates

Suala ni kuwa ni kigezo gani atatumia ikiwa hana wajumbe wa kuchaguliwa wa kutosha, super delegates wa kutosha, ushindi katika majimbo tumaini na ana pungufu ya 2.5M kura kwa Clinton!

Hapa ina maana kuwa kushinda, Idaho, Utah na Vermont kwa mpigo ni sawa na ushindi wa electoral college moja ya Florida.

Na majimbo hayo ni red states, SD wataangalia ramani ambapo in favor Clinton.

Zipo habari zinazosemwa kichini chini kuwa Republican wanamhofia Clinton, na katika kuhakikisha wanaleta mtafaruku wataibua hoja ya email.

Hilo ni moja ya mambo yanayomweka Sanders katika kampeni, kwamba talaa ikionekana kuna tatizo awe mbadala. Tunakumbuka ametumia Benghaz sana hadi alipoona badala ya kumdhoofisha Clinton ilimpa Sympathy

Clinton alipata sympathy kwasababu hoja ile ipo 'orchestrated' na GOP, Democrat wanaona ilikuwa ni unfair akiwa kama secretary of state.

Tatizo ni kuwa hoja haijulikani kama imekufa,huenda GOP wanasubiri waitumie kwa Clinton wakati ukifika

Ikiwa ni hivyo, wanaweza kuitumia wakati huu Sanders akiwa mgombea ili kuleta mtafaruku ndani ya Democrat.

Kimahesabu Sanders hana nafasi, swali, kwanini bado ameshikilia msimamo?

Hofu ya Dem ni kuwa Trump ame prove kuwa lethal pamoja na mazonge zonge yake. Kumchukulia kwa wepesi ni kosa kubwa. Je, muda wa kumshughulikia wanao?

Tusemezane
 
Salama wakuu,

Naomba na mimi niweke senti zangu chache kwenye mada hii:

1. Baada ya Trump kushinda kwa upande wa Republican ni vigumu sana kuona ni jinsi gani mgombea yeyote kutoka Democrat ataweza kumshinda kwenye Uchaguzi Mkuu. Sasa hivi mtu wa kumvuruga Trump ni yeye mwenyewe.

2. Clinton pamoja na kubebwa sana na chama chake pamoja na Obama mwenyewe bado mvuto wake umepotea sana kiasi kwamba ni vigumu mno kuweza kushinda. Kwamba, mtu kama Sanders ambaye miaka michache tu nyuma (kama siyo miezi) Wamarekani wengi walikuwa hawamjua anampa shida itakuwaje kwa mtu ambaye ni maarufu, anajua kuchezea vyombo vya habari kama Trump?

3. Jambo ambalo tutashuhudia kwa miezi hii michache inayokuja ni mashambulizi makubwa sana ya vyombo vya habari dhidi ya Trump; kwa sababu kubwa mbili; kwanza anatishia mafanikio ya ajenda ya kiliberali ya Obama ambayo vyombo vya habari vya Marekani vingi vilikuwa vinaisapoti; na pili anatishia utengemano wa mwelekeo wa Mahakama Kuu ya Marekani (Supreme Court) hasa kama Jaji Garland hatapitishwa kuwa Jaji wa Tisa wa Mahakama hiyo kufuatia ubishi wa Seneti ya Marekani chini ya Republikani. Mashambulizi haya tumeyaona yamejaribiwa sana tangu alipotangaza na tumeona jinsi gani yamefeli mara zote. Sijui media wana mbinu gani nyingine chini ya mikono yao; lakini kama ni hizi za "Trump ni mbaguzi, mdhalilishaji wanawake, hana uwezo, na n.k n.k) so far hazijafanikiwa.

4. Kitu kimoja ambacho watu wengi hasa wanaomkosoa au wasiompenda Trump (na wasiokipenda chama cha Repablikani) wasichotaka kuamini ni kuwa Trump ana mvuto mkubwa kwa Wamarekani wengi hasa weupe. Nchi hii bado kwa kiasi kikubwa sana ni ya weupe na wengi wa hawa ni wahafidhina (conservatives). Wengi wameona jinsi gani taifa hili chini ya Obama limedhoofishwa hasa katika masuala ya ulinzi, usalama na masuala ya kifamilia ambayo wengi Wamarekani wanayaona ni tunu kubwa. Wanahofia kwa kiasi kikubwa kwamba Clinton akishinda utakuwa ni mwendelezo wa siasa za kiliberali za Obama.

Lakini zaidi pia mambo ambayo jamii hii ya Wamarekani wengi wanayajali wanaona yanawakilishwa vyema na Trump kuliko mtu mwingine yeyote - kupunguza kodi za mtu na za makampuni (corporate tax na income tax); kulijenga upya jeshi la Marekani, kupigana na ughaidi kwa ukali zaidi na kujenga heshima ya Marekani duniani - nikiyataja machache.

Ukishayaangalia haya yote unaweza kuona kuwa pasipo shaka kuwa bila kujali mgombea wa Demokrati Wamarekani wataganyikwa vizuri zaidi kiitikadi ni kimrengo kuliko uchaguzi wa 2008 ambapo weupe wengi waliamua kulipa lile ambalo wengine waliona ni deni lao - kuwa siyo wabaguzi wa rangi kwa kumchagua Rais mweusi. Deni hilo baada ya kulipwa sasa hivi tuhuma zozote dhidi ya ubaguzi wa rangi wa watu wengi hapa zinapuuzwa nao!
 
Salama wakuu,

Naomba na mimi niweke senti zangu chache kwenye mada hii:

1. Baada ya Trump kushinda kwa upande wa Republican ni vigumu sana kuona ni jinsi gani mgombea yeyote kutoka Democrat ataweza kumshinda kwenye Uchaguzi Mkuu. Sasa hivi mtu wa kumvuruga Trump ni yeye mwenyewe
Mkuu Nizipitiea hoja
Kuelekea uchaguzi mkuu Trump anakabiliwa na changamoto nyingi

(i)Ni hiyo uliyosema mwisho, Trump mwenyewe.
Kwa kumsikiliza dakika 5 hadi 10 Trump ni mzuri sana wa kuamsha hisia na shamra shamra. Katika muda mrefu, Trump ana tatizo la weledi na mawasiliano.

Kwa mfano; Suala la NATO linakubalika na wagombea wote. Tatizo ni Trump kulieleza katika hamasa badala ya mantiki.

Kusema tu Marekani ijitoe NATO si jambo linaloingia akilini kwa watu wenye weledi. Uwepo wa NATO ni muhimu kwa Marekani kuliko Austria au Moldova.

Marekani imeitumia NATO kwa agenda zake,imeitumia kwa kuwa karibu na mahasimu wao. Suala la gharama ni la kweli, tofauti na Trump au Sanders wanavyolieleza, kuokoa pesa na kujenga mashule kama France, Obama amelieleza kidiplomasia na kuonekana anawapa NATO jukumu wakati huo huo akilinda interest za Marekani ndani ya NATO

Mfano wa pili, Trump anataka kuondoa majeshi Korea na Japan kwasababu Marekani si polisi wa dunia. Well, uwepo wa majeshi hayo si kwa faida ya nchi hizo tu, sehemu kubwa ni kwa interest za Marekani.

Leo US ipo mlangoni mwa North Korea. China inataka kujipanua,Marekani yupo Mlangoni. Iran inakuja juu kama super power wa middle east, Marekani yupo mlangoni Saudia n.k.

Kamanda mmoja wa majeshi ya Marekani Korea amekaririwa akisema, kujilinda nyumbani ni ghali kuliko kuwepo Korea.

Hapa napo pana hoja, je ni muhimu kujifungia chumbani na zana nzito au kuangaza nje?

(ii) Trump anakabiliwa na upinzani wa ndani-Republican
Hata tukidhani umoja utarudi GOP hatuwezi kukataa ukweli kuwa mbinu zilizotumika wazi wazi na 'the establishment' kuzuia nafasi ya front runner haziwezi kudharaulika.

Bado kuna resentment kubwa sana dhidi yake, tutakachoikiona ni kujifanya tu

(iii)Kuna mpambano na Democrat ambao ni wa asili . Dem watabaki kama walivyo na Republicana kama walivyo. Ukiangalia electoral college kila chama kina namba za kuanzia.Tuna maana blue and red states zitabaki kama zilivyo

(iv) Ingawa suala la kauli za kibaguzi umelichukuliwa kwa wepesi, uhalisia ndilo lita tip the scale pale alipo na fursa. Tunaona Democrat, weupe wameshikana na Sanders. Clinton ana weupe na added advantage ya colored people, na tofauti ni hiyo ya wajumbe

Ukiangalia ramani ya electoral college, ukailinganisha na ya primaries za Democrat tofauti kubwa ya wajumbe kati ya Clinton na Sanders inatengenezwa na watu wa rangi

Uchaguzi wa November katika battle states na swing states, Trump atapata tatizo na watu wa rangi. Sasa wakiwa weupe wote wawili, watu wa rangi ndiyo factors

Kwasababu hizo chache, mwendo wake unakuwa na changamoto nyingi, zingine zikiwa za asili na nyingine zikiwa zimetengenezwa na Trump mwenyewe.
Kazi aliyo nayo si ndogo
 
2. Clinton pamoja na kubebwa sana na chama chake pamoja na Obama mwenyewe bado mvuto wake umepotea sana kiasi kwamba ni vigumu mno kuweza kushinda. Kwamba, mtu kama Sanders ambaye miaka michache tu nyuma (kama siyo miezi) Wamarekani wengi walikuwa hawamjua anampa shida itakuwaje kwa mtu ambaye ni maarufu, anajua kuchezea vyombo vya habari kama Trump? !
Mvuto wa Clinton unaathiriwa na mambo mengi.
Kwa kuanzia tu, tuseme kumlinganisha Sanders na Trump ni vitu tofauti

i) Clinton aliingia katika ugombea akiwa na point 25 hadi 30 kwa baadhi ya maeneo. Hakumchukulia Sanders serious akidhani itakuwa ni rahisi. Unaweza kuona tangu waazimie disqualify and defeat baada ya ushindi wa majimbo 7 mfululizo kwa Sanders, majibu yalikuwa mazito. Clinton kashinda majimbo 6 kati ya 7 mazito

ii) Clinton ana rekodi ndefu katika utumishi ukimlinganisha na Sanders.
Hivyo, hakuna wasichokijua au wasiyemjua. Ni yule yule first lady, secretary of sates na mgombea 2008. Hakuna anayejua rekodi ya Sanders, na hilo linampa advantage kama Clinton kwa kujulikana. Hata hivyo, Clinton ni vulnerable kwa rekodi tu kuwa wazi

ii) Sanders anasemekana kuleta independents. Ukitazama primaries majimbo 7 ya mwisho ni red sates. Hivyo independent katika open primairies wanaweza kutoka upande wowote.Ukizingatia Clinton alionekana tishio kwa Republican, hao independents hakuna anayejua ni for real au wana agenda gani.

iii) Kwa namba ni wazi Sanders keshashindwa si jana, bali siku nyingi.
The fact that bado yupo katika kinyang'anyiro haimaanisha analeta ushindani

iv)Kuelekea November, haitegemewi Clinton amchukulie Trump kirahisi.
Ikizingatiwa watu 17 wametupwa nje, Trump is a force to be reckoned with

Hivyo sidhani mfano wa Sanders tunaweza kuufanyia 'extrapolation' kwenda uchaguzi mkuu
 
Hii inaturudisha kule kule kwa swali, ni kitu gani kinamsukuma Sanders kung'ang'ania na kutokuwa tayari kumuunga mkono Clinton? Je wanaompigia kura Sanders ni watu wa aina gani na kwa nini wampe kura mgombea ambaye kimahesabu hana nafasi tena? Ukweli ulio wazi ni kwamba Sanders hata akiungwa mkono na super delegates wote 712 bado hawezi kufikia idadi inayotakiwa ya wajumbe 2383 kwa mujibu wa taratibu zilivyo miaka yote.

Republicans wanajua fika kuwa Democrats wakiwa wamoja, Trump hawezi kushinda na kuna uvumi kuwa Sanders anatumika bila kujua kuleta tafrani ndani ya DNC. Hizi zinazodaiwa kuwa ni polls zikionesha Clinton hawezi kumshinda Trump zinafuatiliwa kwa makini ili kubaini njama zilizo nyuma yake. Kama kuna mtu hawezi kuchaguliwa kuwa Rais Marekani ni mtu anayejiita Socialist na kwa sababu hiyo ni wazi Sanders hawezi kufua dafu mbele ya Trump.

Lililo wazi ni kuwa kuna mbinu sasa zinafanywa kumchafua Clinton kwa madai ya kutoaminika na pia kwamba ushindi anaopata ni za kupikwa. Kuna video zinatembea mtandaoni zikionesha kinachoweza kutafsiriwa kama wizi wa kura na lengo ni kuonesha kwamba Clinton hashindi kihalali. Zinaendelea kudai kuwa kura za Sanders zinafutwa na badala yake zinajazwa za Clinton. Ingawa ni dai la kipuuzi, wako wapenzi wengi wa Sanders wameaminishwa hivyo.

Mojawapo ya hizo video ni hii hapa;

4. Kitu kimoja ambacho watu wengi hasa wanaomkosoa au wasiompenda Trump (na wasiokipenda chama cha Repablikani) wasichotaka kuamini ni kuwa Trump ana mvuto mkubwa kwa Wamarekani wengi hasa weupe. Nchi hii bado kwa kiasi kikubwa sana ni ya weupe na wengi wa hawa ni wahafidhina (conservatives).

Wengi wameona jinsi gani taifa hili chini ya Obama limedhoofishwa hasa katika masuala ya ulinzi, usalama na masuala ya kifamilia ambayo wengi Wamarekani wanayaona ni tunu kubwa. Wanahofia kwa kiasi kikubwa kwamba Clinton akishinda utakuwa ni mwendelezo wa siasa za kiliberali za Obama.

Lakini zaidi pia mambo ambayo jamii hii ya Wamarekani wengi wanayajali wanaona yanawakilishwa vyema na Trump kuliko mtu mwingine yeyote - kupunguza kodi za mtu na za makampuni (corporate tax na income tax); kulijenga upya jeshi la Marekani, kupigana na ughaidi kwa ukali zaidi na kujenga heshima ya Marekani duniani - nikiyataja machache.
Kuhusu Trump kuungwa mkono na conservative, hapa ndipo atakabiliwa na tatizo kubwa. Hadi tunavyoandika kuna kundi la conservatives linataka mgombea mwingine (independent) ambaye ni conservative wakisema Trump siyo.

Ikifika wakati wa kuyaeleza kwa kina, na wakati umefika kwasabau watakuwa wawili, Trump atababaika zaidi na kuwagawa conservative.

Mfano, mwanzo aliunga mkono suala la 'abortion' akisema wanawake waamue hatma yao kama wanavyosema Waliberali.

Ilikuwa kutaka kuungwa mkono na akina mama. Kwa bahati mbaya lipo katika rekodi, na ndilo hasa akina Cruz walilitumia kuonyesha si conservative

Majuzi kaongelea Trans gender ya toilet akiwa na msimamo wa conservative.

Kuhusu Israel, Trump ana msimamo wa Democrat tofauti na ule wa GOP.
Ukimsikiliza Rubio na Cruz, misimamo yao ililenga kuwavuta conservatives.

Kuna flip flop za hapa na pale katika identity yake.

Kuhusu ulinzi na usalama, nani anaelewa agenda ya Trump?
Kuzuia Waislam wasiingie Marekani ita solve tatizo la Ugaidi?

Kuwatenga allies wa Uropa na middle east kutasaidia katika mapambano ya Ugaidi?

Kikubwa zaidi, Trump anapambana na gaidi yupi? Ukimsikiliza ana maanisha kwenda kuwatandika mabomu, swali wapo eneo gani?

Msimamo huo alikuwa nao Cruz kwa kusema atafanya 'blanket' kumaliza ugaidi.
Alipoulizwa eneo gani, hakuwa na jibu na si dhani Trump analo

Trump anaeleza mambo mengi yanayowagusa Wamerekani kama uhamiaji haramu, ugaidi, udhaifu wa uchumi n.k. katika 'sensational way''

Tatizo hakuna anayejua ana plan gani katika kukabiliana nayo
Mfano, anasema uchumi wa Marekani ni dhaifu ukishindwa na mataifa kama China.

Haraka haraka inaonekana kweli, kitakwimu si kweli.
Ni Taifa gani katika yale ya G20 lenye uchumi mzito zaidi ya Marekani kwa sasa?

Na je uchumi wa China ni mzuri kama Trump anavyosema?
Kwa miezi takribani 8 mfululizo namba za uchumi wa China zinaporomoka

Trump anawatisha watu kuhusu hali ilivyo mbaya, bila kuwaeleza ukweli.

''Atamaliza ISIS'' bila kueleza kwa mbinu gani ikijulikani siyo jeshi lenye eneo maalumu.

Wasi wasi wa baadhi ya Wamerekani ni jinsi ambavyo sera zake hazielezeki.

Utakumbuka katika primaries zote muda mwingi ametumia matusi, lugha chafu bila kueleza 'red meat' na hata aliojaribu alijikanganya sana

Kuhusu udhaifu wa jeshi la Marekani, hapa napo pana tatizo.
Ni kigezo gani kimetumika kubaini jeshi ni dhaifu?

Je, yale ya Bush kwenda kutandika nchi nyingine ndiyo uimara wa jeshi?
Na nani anajua jeshi la Marekani lina nini?

Walipobaki wawili, sera zitachambuliwa kwa undani kuliko wakati wa matusi

Democrat watafanya kosa wakienda mrengo wa matusi,Trump ni fundi hawatamweza.

Wakienda kwa sera, weledi wa Trump utaonekana na hapo pana tatizo kubwa
 
Mag3 #152
Sanders anatishia sana hali ya Democrat. Juzi katoa kamkana Trump kutokana na pressure inayoanza kujijenga ndani ya Democrat

Sanders ana madai mengi kuhusu uchaguzi. Kwanza, alidai closed election zina disfranchise vijana ambao ni wapiga kura wake.
Alipoulizwa mbona hajalalamika kuhusu caucus? Hoja ikafika ukomo

Anadai utaratibu wa Democrat si mzuri na ubadilishwe. Akiulizwa, alipojiunga na harakati za uchaguzi kitabu chenye blue print kilikuwepo,mbona hakuhoji hilo?

Kuhusu tuhuma za wizi wa kura, Sanders anafanya siasa za dhaifu sana.
Ukiangalia 'demography' na takwimu unapata majibu yote.

Clinton anakiri wapiga kura kati ya 18-30 hawampigii.
Mwanzoni namba zilionyesha wanawake wanampigia Sanders, Clinton alikiri ukweli

Clinton anashinda maeneo ya urban, sanders anashinda alikoshinda Clinton 2008. Clinton ana advantage,huko rural anashindana,mijini ana support (colored people).

Kundi la Clinton ni 'base ya democrat' ndiyo maana anashinda closed elections
Kundi la Sanders ni independents ndiyo maana anashinda caucus na open primaries

Ni wazi kwa kuangalia matokeo tunaweza kufanya forecast ya maeneo yajayo.

Sanders atashinda Oregon kwasababu 'electoral block' yake ni weupe.
Clinton ana nafasi kubwa California kwasababu ya colored people

Ukitazama ramani kwa undani, Sanders ameshinda red states kama Utah, Idaho n.k. kwasababu ya kile wanachosema ni independents.

Hawa si independents, ni Republican waliokuwa organized na Sanders team
Ndio maana uchaguzi wowote usiowahusisha Clinton anashinda tena sana

Chukulia mfano wa Connecticut vs Michigan. Utaona hayo tunayoeleza

Au Maryland, Pennyslavania, Florida Vs Wisconsin, washington, Utah, Idaho

Hoja za Sanders zinawapa GOP nguvu sana.
Ndio maana Trump ana sympathize na Sanders,hatendewi haki na Democrat.

Kila siku anachomeka hoja za kuamsha hisia ndani ya Democrat

Trump anajua Dem wakivurugana, wale conservative wanaoitwa independent wasiomtaka watagawanyika.Dem watagawanyika na hapo atakuwa na njia laini

Nadhani kwa upande wa GOP mchezo umeisha na vita inayomkabili presumptive nominee, Donald Trump, ni kukubalika kwake na mapokezi kwa baadhi ya viongozi wa Republicans. Leo Spika Paul Ryan amesita kumuunga mkono akisema anasubiri kuona jitihada zake katika kuleta umoja ndani ya chama. Viongozi walioapa kutomuunga mkono ni pamoja na Mitt Romney aliyeshindwa na Obama.

Kwa upande wa DEMS mambo pia bado magumu. Sanders ameapa kuendeleza mapambano ndani ya chama ingawa hesabu hazikubali. Mpaka sasa idadi ya wajumbe ambao bado wanaogombewa ni 1114 kutoka majimbo 15 ikiwa ni pamoja na California yenye wajumbe 546. Sanders anatakiwa apate angalau asilimia 87% ili afikie idadi inayotakiwa, kitu ambacho katu hakiwezekani kabisa.
 
Mkuu katika bandiko #150 (ii) tulisema Trump anakabiliwa na changamoto ya upinzani ndani ya chama.

Ukifuatilia chaguzi tatu zilizopita, muda kama huu mgombea wa Republican alikuwa anapata endorsement tu.

Leo high rank leader kama Ryan wanafikiria kama wamuunge mkono au la.
Inatia shaka na kumpa Trump changamoto kubwa sana.

Wapo wanaomuunga mkono si kwa sera bali nafsi zao

Katika bandiko# 150 na 152 tulisema kuwa sababu moja ya Sanders kuendelea na uchaguzi ni hoja ya email kama inavyonong'onwa na wachambuzi wa siasa

Kwamba alileta suala la Benghaz makusudi likaonekana kukosa mvuto Zaidi ya kumpa sympathy Clinton ikionekana ni mhanga wa kampeni za Republican

Well, leo kumevuja habari kuwa FBI wamewahoji wasaidizi wa Clinton, hata hivyo hadi sasa hakuna ushahidi kuwa alifanya jambo hilo kwa makusudi ya kukiuka sharia

Suala hilo halijafika mwisho, bado uchunguzi unaendelea na linaendelea kumweka Sanders katika kuzengea zengea kama lipo kubwa litakalotokea.

Tusemezane
 
Kuhusu Trump kuungwa mkono na conservative, hapa ndipo atakabiliwa na tatizo kubwa. Hadi tunavyoandika kuna kundi la conservatives linataka mgombea mwingine (independent) ambaye ni conservative wakisema Trump siyo.

Ikifika wakati wa kuyaeleza kwa kina, na wakati umefika kwasabau watakuwa wawili, Trump atababaika zaidi na kuwagawa conservative.

Mfano, mwanzo aliunga mkono suala la 'abortion' akisema wanawake waamue hatma yao kama wanavyosema Waliberali.

Ilikuwa kutaka kuungwa mkono na akina mama. Kwa bahati mbaya lipo katika rekodi, na ndilo hasa akina Cruz walilitumia kuonyesha si conservative

Majuzi kaongelea Trans gender ya toilet akiwa na msimamo wa conservative.

Kuhusu Israel, Trump ana msimamo wa Democrat tofauti na ule wa GOP.
Ukimsikiliza Rubio na Cruz, misimamo yao ililenga kuwavuta conservatives.

Kuna flip flop za hapa na pale katika identity yake.

Kuhusu ulinzi na usalama, nani anaelewa agenda ya Trump?
Kuzuia Waislam wasiingie Marekani ita solve tatizo la Ugaidi?

Kuwatenga allies wa Uropa na middle east kutasaidia katika mapambano ya Ugaidi?

Kikubwa zaidi, Trump anapambana na gaidi yupi? Ukimsikiliza ana maanisha kwenda kuwatandika mabomu, swali wapo eneo gani?

Msimamo huo alikuwa nao Cruz kwa kusema atafanya 'blanket' kumaliza ugaidi.
Alipoulizwa eneo gani, hakuwa na jibu na si dhani Trump analo

Trump anaeleza mambo mengi yanayowagusa Wamerekani kama uhamiaji haramu, ugaidi, udhaifu wa uchumi n.k. katika 'sensational way''

Tatizo hakuna anayejua ana plan gani katika kukabiliana nayo
Mfano, anasema uchumi wa Marekani ni dhaifu ukishindwa na mataifa kama China.

Haraka haraka inaonekana kweli, kitakwimu si kweli.
Ni Taifa gani katika yale ya G20 lenye uchumi mzito zaidi ya Marekani kwa sasa?

Na je uchumi wa China ni mzuri kama Trump anavyosema?
Kwa miezi takribani 8 mfululizo namba za uchumi wa China zinaporomoka

Trump anawatisha watu kuhusu hali ilivyo mbaya, bila kuwaeleza ukweli.

''Atamaliza ISIS'' bila kueleza kwa mbinu gani ikijulikani siyo jeshi lenye eneo maalumu.

Wasi wasi wa baadhi ya Wamerekani ni jinsi ambavyo sera zake hazielezeki.

Utakumbuka katika primaries zote muda mwingi ametumia matusi, lugha chafu bila kueleza 'red meat' na hata aliojaribu alijikanganya sana

Kuhusu udhaifu wa jeshi la Marekani, hapa napo pana tatizo.
Ni kigezo gani kimetumika kubaini jeshi ni dhaifu?

Je, yale ya Bush kwenda kutandika nchi nyingine ndiyo uimara wa jeshi?
Na nani anajua jeshi la Marekani lina nini?

Walipobaki wawili, sera zitachambuliwa kwa undani kuliko wakati wa matusi

Democrat watafanya kosa wakienda mrengo wa matusi,Trump ni fundi hawatamweza.

Wakienda kwa sera, weledi wa Trump utaonekana na hapo pana tatizo kubwa
Mkuu nadhani matatizo ya Trump unayoyataja ndiyo yale yale yaliyokuwa yanatajwa tangu mwanzo. Alichosema mwanakijiji ndiyo hali halisi. Kwamba vyombo vya habari vilijaribu sana kuyasema hayo kwa nguvu ili kumkwamisha trump lkn vimeshindwa,labda km watakuja na mbinu mpya ukiacha hizi zilizoshindwa.

Kwa maoni yangu na kwa wamarekani hawa walioteseka na ugaidi kipindi chote cha utawala wa obama,hakuna tena wa kumzuia Trump kuwa mrithi wa obama. Wamarekani hawatakubali kumrudisha Bill clinton ikulu kwa mara ya pili.
 
Nguruvi, utaona kuwa Trump hawagawi conservatives sana anawagawa Republicans; wale ambao wanaamini chama ni chao na kuwa huyu mgeni kaja na kakichukua. Republicans hawa (kina Paul Ryan, Mitt Romney, McCain na wengine) kwa kiwango kikubwa wanaona kuwa watu wao wote ambao wangewakilisha maslahi ya chama - kina Gov. Perry, Gov. Bush n.k hawakufanikiwa. Swali ni kwanini. Hawajajua bado mood ya Wamarekani wengi.

Conservatives wengi utawaona wanasimama nyuma ya Trump kwa sababu moja - wako tayari kumchukua 40% conservative kuliko 100% republican!
 
Exactly na hiki tumekiongelea sana kuanzia primairies na caucus zinaanza katika bandiko hili

Tulisema wapo 'the establishment' ambao umewaita Republican
Halafu kuna conservative wakiitwa kwa majina ya evangelical n.k.

Ndiyo maana tulionyesha huko nyuma kuwa Trump ana advantage moja, kwamba ana kundi lake loyal kabisa.

Kila chaguzi alishinda kwa asilimia 30-35, zimeongezeka baada ya wagombea wengi kuachia ngazi na baadhi ya Republican kuona mwendo wa convention utazua balaa.

Mfano watu walitambua Marco Rubio ni republican ikiwa too late. Walitambua anayeweza kusimama kati ya establishments na conservative ni Kasich, ilikuwa too late. Hilo lilimpa Trump fursa kwasababu 'kundi lake' lilibaki intact likimpa asilimia 30-38 wakati wengine wakigawana kura katika wingi wa watu 8-10

Tatizo la Trump ni kutaka kucheza karata zote mbili.
Hapo anajikuta anahangaika na katika misimamo.

Kuna nyakati anakwenda sambamba na hao conservative, kuna nyakati anakwenda sambamba na 'the establishment' na nyakati anaunga mkono independents kama Sanders na hata Democrat

Kwa msingi huo, anakuwa na turn on and turn off ya 'electoral block' yake
Hilo linamfanya aonekane hajui anafanya nini. Linawatia baadhi ya watu wasi wasi

Leo nani anajua Trump anasimama wapi kwa suala la Jaji wa mahakama kuu?
Nani anajua foreign Policy ya Trump japo kwa 'sketch diagram'
Nani anajua Trump anasimamia wapi katika masuala kama Abortion , LBGT
Nani anajua anasimamia wapi katika immigration
Nani anajua Policy ya Trump kuhusu Healthcare

Hili litakuwa tatizo sana mbele ya safari. Akiwa Republican atahitaji ku prove values zake, na Trump ameonyesha kuwa mtu wa kuvutwa na upepo kuliko msimamo

Kwa mfano, nguvu kubwa ya Republican ni ulinzi na usalama. Msimamo wa Trump unaonyesha kuwa madhubuti kwa haraka haraka. Ukiangalia plan yake, inashangaza

Atawezaje kuongelea ulinzi na usalama bila kuoanisha na uchumi na foreign policy?

Kwamba, Wamarekani wamekuwa wema sana kuweka majeshi Japan, Ujerumani, Korea n.k. na hivyo ni wakati wa kuondoa!! Lini US ilimpenda mtu bila masilahi?

Hapa sina maana yupo wrong, tyunachosema hawezi kutetea hoja hata kama zina mashiko. Yupo katika kuamsha hisia zaidi (ina work) kuliko kuzungumzia Plan

Kuelekea November itafika mahali ana tofautiana na kila kundi, isipokuwa lile linalomwamini kwasababu tu ni Trump. Je litatosha kumpa ushindi?

Ikifika mahali wapo wawili na details za Policy zao zinawekwa wazi, Trump atakuwa na wakati mgumu unaoweza kuwatisha baadhi ya wapiga kura
 
Hofu yangu ni kuwa Hillary anaweza kuwa indicted maana uchunguzi wa FBI unaonekana unazidi kumsogelea kwelii kweli... na hivyo inampa nafasi Trump ya kukosa mpinzani wa maana kwa kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom