Uchaguzi Marekani

Mkuu Mag3
Katika hali ya kuzooeleka miaka ya karibuni, wagombea hufikia ''threshold' ya at least 30% ya kupata ugombea kabla ya kuelekea New York Primary. Kwamba front runner anaonekana wazi

Kama utakumbuka, tulisema uwezekano wa Republican kwenda convention ni inevitable
Wachambuzi wote wa siasa za ndani na nje waliona hilo wazi

Kilichosukuma hitimisho ni ukweli kuwa Trump alishinda chini ya 50% sehemu nyingi
Uwepo wa wagombea watatu, haukuweza kumpa mgombea yoyote 45-55%

Ushindi mfululizo wa Cruz na na kuchomoza kwa Kasich ilikuwa dhahiri RNC haiepukiki

Democrat;
Sanders kushinda majimbo 8/9 kulionyesha ni mapema kuhitimisha majaaliwa ya Clinton.

Uwezo wa kukusanya makundi ya watu na nguvu ya kampeni yake kwa kona zote, kuchangisha pesa, kushambulia, hoja n.k. ilikuwa ngumu kufikia hitimisho

Hesabu zote zilionyesha Clinton kuongoza, muda haukuwa na nafasi.
Michigan ili define mweleko wa uchaguzi ikimshtua Clinton na kumpa nguvu Sanders

Ilifahamika, ukubwa wa New York, Pennyslavania, Maryland, Connecticut ungetoa picha kubwa. Haikuwa makosa kufikiri hivyo.Picha imebadili mtazamokwa pande zote

Kilichobadilika:
NY iliwapa ushindi mnono Trump na Clinton na kubadili mwelekeo.
Matokeo ya jana yamehitisha matarajio yaliyokuwepo kuhusu wawili hao

Matarajio yamebadili sana uwezekano wa kwenda Convention kwa RNC.
Trump akiwa na wenzake wawili amewashinda kwa asilimia hadi 60.

Huko nyuma, ilibidi Trump ashinde kwa 58% majimbo yote ili kupata 1237.
Kwasasa inawezekana. Kashinda hadi 63 kwanini idhaniwehaitawezekana?

Clinton aliongoza kwa wajumbe kuanzia mwanzo, wawe pledge au super delegates.

Kasi ya Sanders ilionekana kumsimisha kwa muda. Naye kama Trump , NY, Pa, Md, Conn na delaware kumepanua pengo kati yake na Sanders.

Ili kumzuia, Sanders anahitaji 85% ya ushindi katika majimbo yote, jambo gumu sana

Trump na Clinton wanaelekea November kama hakutatokea miujiza mingine

Tusemzane
 
KWANINI NI TRUMP NA CLINTON?

Hoja zitajengwa kwa maneno au kauli, namba zitazjieleza kwa wawili hawa
1. Idadi ya kura 'popular vote'
2. Idadi ya Wajumbe
3. Idadi ya majimbo walioshinda
4. Ukubwa na uzito wa majimbo waliyoshinda

Kuwazuia itakuwa ni jambo gumu na litakalozua mtafaruku sana. Hata hivyo, jitihada zinaendelea kwa GOP na Dem kutumia njia za mkato ili kuwaengu wote wawili kinamna

Republican
The establishment wamegawanyika makundi mawili. Wenye nia ya kuendelea kwenda RNC na waliokata taama. Waliokata tamaa kutokana na namba ni wale waliotangaza kutoshiriki mkutano mkuu
Maana yake ni kutoidhinisha Trump kuwa mgombea au Cruz wasiyempenda

The establishment wanaoendelea ndio wameshawishi 'muungano'Cruz na Kasich
Lengo lao ni kuzuia hata kwa kura 50 tu Trump asifikie 1237 kuwa mgombea

Kwa muda huu wa saa 2 za hapa nchini, Ted Cruz ametangaza Carly Fiorina kuwa mgombe mwenza

Hili lina maana ya kuvuta akina mama si kushinda ugombea bali kukwaza kwanza Trump kufikia 1237. Fiorina anaonekana mbadala wa ''Clinton'' kisaikolojia

Democrat
Sanders anasema kila sauti isikike kwa maana uchaguzi ufike kila jimbo.
Anatambua hesabu ni ngumu lakini anataka kuendelea hadi June 7.

Kwa urahisi inaonekana hivyo, kinyume chake ana agenda kubwa sana.
Anachotaka ni kukabiliana na Clinton katika namba ya wajumbe wa kuchaguliwa

Atatumia hoja ya super delegates kama wajumbe wasiopaswa kumpa mgombea uhalali.

Katika mantiki , Clinton atakuwa na wajumbe pengine 50 au 100 short wa kuchaguliwa

Sanders atakwenda mkutano mkuu DNC kujenga hoja ya uchaguzi mwingine kule

Hoja yake ni kuwa wajumbe wa kuchaguliwa na super delegates wapewe nafasi sawa ndani ya DNC. Hiyo ndiyo hoja anayosimamia sasa hivi

Kimahesabu chaguzi zilizobaki zilipaswa kukamilisha ratiba, lakini kwa 'nia na dhamira' za walioshindwa uchaguzi utaendelea tena katika ushindani kwasababu tulizoeleza

Uchaguzi ujao ni katika jimbo la Indiana

Vionjo:
Hapa wale wa Indiana Pacers, Purdue na Notre dame wanapafahamu(Basketball)
Kwa wale wa mbio za magari, Indianapolis 500
Kwa NFL ndipo nyumbani kwa Colts
Na kwa wale wa muziki, Jackson street, Gary-Indiana alikokulia Michael Jackson

Tusemezane
 
Mkuu Mag3
Katika hali ya kuzooeleka miaka ya karibuni, wagombea hufikia ''threshold' ya at least 30% ya kupata ugombea kabla ya kuelekea New York Primary. Kwamba front runner anaonekana wazi

Kama utakumbuka, tulisema uwezekano wa Republican kwenda convention ni inevitable
Wachambuzi wote wa siasa za ndani na nje waliona hilo wazi

Kilichosukuma hitimisho ni ukweli kuwa Trump alishinda chini ya 50% sehemu nyingi
Uwepo wa wagombea watatu, haukuweza kumpa mgombea yoyote 45-55%

Ushindi mfululizo wa Cruz na na kuchomoza kwa Kasich ilikuwa dhahiri RNC haiepukiki

Kwa Democrat, Sanders kushinda caucus 7 mfululizo na majimbo 8 kati 9 kulionyesha ni mapema mno kuhitisha majaaliwa ya Bi. Clinton.

Uwezo wa kukusanya makundi ya watu na nguvu ya kampeni yake kwa kona zote, kuchangisha pesa, kushambulia, hoja n.k. ilikuwa ngumu kufikia hitimisho

Hesabu zote zilionyesha Clinton kuongoza, muda haukuwa na nafasi.
Michigan ili define mweleko wa uchaguzi ikimshtua Clinton na kumpa nguvu Sanders

Ilifahamika, ukubwa wa New York, Pennyslavania, Maryland, Connecticut ungetoa picha kubwa. Haikuwa makosa kufikiri hivyo.Picha imebadili mtazamokwa pande zote

Kilichobadilika:
NY iliwapa ushindi mnono Trump na Clinton na kubadili mwelekeo.
Matokeo ya jana yamehitisha matarajio yaliyokuwepo kuhusu wawili hao

Matarajio yamebadili sana uwezekano wa kwenda Convention kwa RNC.
Trump akiwa na wenzake wawili amewashinda kwa asilimia hadi 60.

Huko nyuma, ilibidi Trump ashinde kwa 58% majimbo yote ili kupata 1237.
Kwasasa inawezekana. Kashinda hadi 63 kwanini idhaniwehaitawezekana?

Clinton aliongoza kwa wajumbe kuanzia mwanzo, wawe pledge au super delegates.

Kasi ya Sanders ilionekana kumsimisha kwa muda. Naye kama Trump , NY, Pa, Md, Conn na delaware kumepanua pengo kati yake na Sanders.

Ili kumuzia, Sanders anahitaji 85% ya ushindi katika majimbo yote, jambo gumu sana

Trump na Clinton wanaelekea November kama hakutatokea miujiza mingine

Tusemzane
Kwa Sanders mbaya zaidi ni kwamba pamoja na kushinda Rhode Island kwa asilimia 56% dhidi ya Clinton 44%, katika jumla ya wajumbe 33, Clinton kazoa wajumbe 20 na Sanders 13 tu. Hii ni kutokana na uwiano unaojumuisha wajumbe wanaotambulika kama pledged delegates.
 
Ukiangalia hesabu, ushindi wa Sanders Washington state, Idaho, Utah na Wisconsin umefutwa na idadi ya wajumbe wa New York, na Penny

Clinton alikuwa na mkakati wa kuweka resources zake kwa big states
Sanders aliwekeza katika mlolongo wa ushindi bila kuangalia hesabu zinasomekaje

Hoja ya Sanders ni moja tu, kwamba sauti za kila jimbo zisikike. Super delegates sidhani kama watakubaliana na hoja zake za kwenda DNC, wakijua tayari keshatoa 'kitabu' atakachotumia Trump
 
TED CRUZ NA CARLY FIORINA
SANDERS KUPUNGUZA WAFANYAKAZI

Kila siku yanajitokeza mambo yanayoendana na zoezi la uchaguzi wa awali Marekani
Jumanne iliyopita,akiwashukuru wapiga kura,Trump alimzungumzia Hillary Clinton

Alisema endapo asingekuwa mwanamke hata 5% ya kura asingepata na kwamba wanawake hawampendi

Kauli hiyo imekuwa mazungumzo katika anga za kisiasa.
Bi Clinton alimjibu, ikiwa kusimamia haki za wanawake ni matumizi ya jinsia,na iwe hivyo

Clinton alitumia fursa hiyo kuwavuta akina mama kama mtetezi wao

Kura za maoni zinaonyesha Trump ana tatizo kubwa la kukubalika kwa wanawake

GOP wana hofu wakijua wanawake ni sehemu kubwa ya wapiga kura
Na sera za GOP nyingi zinaonekana kutowawapendeza akina mama

Republican wanazidi kuingiwa na hofu dhidi ya Trump katika hali tofauti

1. Position ya Trump kuhusu mambo ya kitaifa na kimataifa haijulikani
2. Kuendelea kuwagawa wapiga kura kunatoa nafasi kwa Democrat
3. Ugomvi na akina mama hausaidii chama ambacho tayari kinaangaliwa kwa jicho pembe

Kufuatia hali hiyo, 'the establishment' wakatumia karata si kumshinda Trump bali kumzuia

Kumbuka, Cruz na Kasich hawana nafasi katika uchaguzi, wanachotaka ni kuhakikisha uchaguzi unakwenda mkutano mkuu (RNC).Wanatumaini kubadilisha kibao dhidi ya Trump

Kwa mtazamo huo, Ted Cruz akamteua Carly Fiorina kuwa mgombea mwenza.
Katika mazingira ya kawaida mgombe mwenza hutangazwa mgombea akipatikana

Bi Fiorina alikuwa mgombea wa Urasi kabla ya kuachia ngazi. Aliamua kumuunga mkono Cruz katika jitihada za kukabliana na Trump.

Fiorina anajulikana kwa nafasi yake ya kazi kama CEO wa Hewlett & Parkard iliyonunua kampuni ya Compaq. Kuondoka kwake kulikuwa na utata baada ya kampuni kuyumba

Fiorina aligombea Useneta wa California na kushindwa na Bi Boxer.

Uteuzi wake ni kupeleka ujumbe kwa akina mama,Republican haipo kama Trump anavyoifanya ionekane. Ni kutaka kuungwa mkono katika hatua za mwisho kumzuia Trump asifikie 1237. Ni jitihada kama za kuungana na Kasich kuvuta muda

Swali,mkakati huu utafanikiwa? Fiorina atakuwa na impact katika hatua hizi za mwisho?

Kwa upande wa Trump, kauli zinamweka matatani kila siku.

Baada ya kugundua zogo katika vyombo vya habari, Trump alijaribu kutoa hotuba kuhusu mambo ya ulinzi na usalama kubadili mazungumzo.

Huko nako kazua maswali tena kuhusu uzoefu na weledi wa mambo ya usalama.
Tutajadili
 
SANDERS
Wakati timbwili la Trump likifunika anga za habari, Senata Sanders ametangaza kupunguza wafanyakazi wa kampeni yake.

Hili linazua maswali endapo Sanders sasa ameamua kuachia ngazi.
Akiwa Indiana Sanders amesisitiza bado anagombea kupata kuteuliwa

Pengine kwa kujua huenda asiwe mgombea,ameamua kupunguza wafanyakazi ambao
Ni ngumu kujua wapi anasimamia na nini lengo lake la mwisho
Haionekani kama amekata tamaa na kuna sababu za kuamini kipo anachokitafuta

Pengine uchaguzi wa Indiana utatoa jibu sahihi kuhusu kuendelea au kutoendelea na kampeni. Na pengine ni dalili za awali za kuondoka katika shindano. Haiujulikana kiuhalisia

HOTUBA YA TRUMP: MAMBO YA NJE , ULINZI NA USALAMA

Ulinzi na usalama imekuwa agenda kubwa kwa Republican kwa miaka mingi
Matarajio ya GOP ni mbeba bendera kuiendeleza sera hiyo kama ilivyo desturi

Dunia inabadilika kila uchao, changamoto nazo zinabadilika.
Ni makosa kudhani ulinzi na usalama unahitaji silaha tu.
Kuna suala la uchumi na washirika kwasababu vyote vinaambatana

Katika jitihada za kuua mjadala wa wanawake, Trump alitoa hotuba kwa kutumia teleprompter.Huko nyuma aliponda matumizi ya chombo hicho kama udhaifu wa kujieleza

Inaonekana alishauriwa kuhusu unyeti wa suala hilo na kwamba si la kuzungumza tu

Hotuba yake imepokelewa kwa hisia tofauti, wachunguzi na wataalamu wa siasa za nje wanaiona kama 'incoherent' inachanganya na haieleweki.

Inajichanganya kutoka sentesnsi moja hadi nyingine.
SenataLindsey Graham ambaye ni miongoni mwa Magwiji wa GOP ameiponda vilivyo.

Ndivyo alivyoichambua nguli wa habari za kimataifa Farid Zakharia

Kwa ufupi hotuba ya Trump haionyeshi weledi au ufahamu wa anachozungumzia.
Kibaya zaidi, hoja zake za siku za nyuma zinapingana na anachosema sasa

Hilo limemweka mahali pagumu hasa kwa GOP na ndiyo maana jitihada za 'kuzuia' asifikie 1237 zinaendelea kwa kasi.

Ikiwa, Republican watakwenda RNC, mzunguko wa kwanza ukashindwa kupata mgombea, Trump atakuwa katika wakati mgumu mzunguko wa pili au tatu

Tusemezane
 
Mkuu magode kwa idhini uliyotoa tutafafanua kuhusu hoja uliyoniuliza pembeni.
Magode anauliza mbona tunazungumzia sana Democrat kuliko Republican katika mabandiko?

Mkuu, tunaangalia pande zote sawa, kama ukifuatilia toka mwanzo

Hata hivyo, kuna sehemu ambazo kina cha mjadala wa Republican hakifikiwi kutokana na sababu mbali mbali

1. Hali ya Republican katika mijadala ni ya ukakasi.
Wagombea walijikita katika personal issues and attacks badala ya hoja.

Inakuwa si kwa public interest kujadili urefu wa vidole vya Trump au ufupi wa Marco Rubio. Tofauti na hivyo, Democrat wana afadhali hadi siku za karibuni

2. Kuna maeneo mengine yanachanganya kuhusu Republican na hivyo yanaelezwa kwa ufupi ili kuelewaeka kwa urahisi zaidi badala ya kuwachanganya wasomaji

Mfano, tangu mwanzo tumezungumzia namba 1237 kama mstari wa mwisho wa mshindi kuufikia. Lakini ndani ya 1237 kuna kanuni( formula) nyingi sana ambazo si rahisi kuzieleza kwa lugha nyepesi bila kuwachanganya wasomaji.

Ndio maana tulieleza maana ya winner take all, winner take most na mgawanyo wa congressional districts, state convention, Caucus n.k.

Mfano, juzi Pennyslavania , haikuwa rahisi kupata namba ya wajumbe kwasababu katika wajumbe 95 , wapo 54 wasiotengwa kwa mgombea yoyote.

Yapo majimbo mgombea anapata wajumbe kutokana na kura za Urais za 2012
Yapo majimbo anachaguliwa na state convention kwa mgawanyo maalumu n.k.

Kwa mifano hiyo, ni ngumu kupata namba za mwisho hadi zitakapotolewa na RNC

Tofauti kidogo ni Democrat mtiririko wao wa uwiano ni rahisi ukilinganisha na GOP

Kuhusu siasa napo kuna tofauti kubwa na hapo ndipo panapozua ukina wa eneo moja ukilinganisha na jingine

Tuseme kuwa tunazungumzia pande zote kwa usawa na hakika Republican wamechukua sehemu kubwa ya mjadala kutokana na hali ya mambo ilivyo
 
Update..hii hapa chini ndiyo idadi ya wajumbe wa kila mgombea hadi leo tarehe 29/4/2016;

GOP -
idadi inayotak.iwa kufikiwa...1237
  1. Donald Trump...994 - pungufu ya wajumbe...243
  2. Ted Cruz...........556 - pungufu ya wajumbe...671
DEM - idadi inayotakiwa kufikiwa...2383
  1. Hillary Clinton....2165 - pungufu ya wajumbe...218
  2. Bernie Sanders...1357 - pungufu ya wajumbe...1026
Kama inavyoonekana hapo juu uchaguzi wa Marekani safari hii imekuwa tofauti kidogo na za miaka ya nyuma. Ted Cruz na Bernie Sanders bado hawakubali ingawa kwa mahesabu namba zao hazitoi tumaini kabisa na wote wana imani kuwa Convention inaweza ikabadilisha mambo. Tofauti kati yao ni mbinu wanazotumia kujaribu kuwashawishi wajumbe wasiowaunga mkono ili waweze kubadilisha misimamo yao na kuwakubali. Nadhani Nguruvi3 kaeleza vizuri sana kuhusu hilo.
 
Mag3
Republican wana wakati mgumu kwasababu ya wimbi kubwa la wagombea lililoshindwa kuchuja kiuhalisia. Sasa hivi wanaangalia nyuma na kukumbuka alikuwepo Lindsey Graham, Marco Rubio, Mike HackBee, Kasich n.k.

Utakumbuka kuna bandiko tulisema ' Republican hawamtaki Trump kwasababu wanaona hana thamani za 'conservatism' na ni vulnerable katika uchaguzi mkuu'

Taratibu wanagundua hata weledi wake katika mambo ya siasa ni wa mashaka

GOP wanaona kufanikiwa kibiashara ni tofauti na uendeshaji wa siasa
Na ni wao ndio walio m-groom kwa kudhani ni Reagan wa nyakati hizi

Wakitafakari hali hiyo wanajikuta katika mbadala nje na uliotrarajiwa, Ted Cruz.

Republican hawampendi Ted Cruz kutokana na kuvurugana na wenzake iwe katika senate au masuala yanayoingiliana na congress

Hilo limetokea jana, Spika wa zamani John Boehner alitamka wazi, hawapendi wote na chaguo lake ni Spika wa sasa Ryan

Boehner kamwita Cruz 'Lucifer na kusema hatakuwa Rais over his dead body'

Kwa maana ya kumtumia Cruz wasiyempenda kuzuia Trump asifikishe 1237

Wakati huo huo wana agenda ya kumtosa Cruz kwa chaguo chungu Gavana Kasich.

Changamoto ni kuwa Kasich kashinda jimbo moja tu , ana wajumbe wachache kuliko Rubio aliyejitoa na wapiga kura wachache kuliko Trump

Ndio maana hakuna pressure ya kumtaka Kasich ajitoe kama walivyofanya kwa Jeb Bush au Marco Rubio, wakimuona kama karata ya mwisho(wild card)

Hilo nalo ni kosa, pressure dhidi ya Rubio haikuwa na maana. Pengine angekuwa mbadala bora kwa ubora wa wajumbe na kura ukilinganisha na Gavana Kasich

Kasich atachaguliwaje katika mantiki ya namba zake zilizo chini kwa kila kitu?

Spika Ryan amekataa kuingia kama karata ya mwisho ndani ya convention
Kwanini amekataa. tutajadili mbele

Magwiji hawataki kwenda Cleveland mkutano mkuu wakipinga kumuidhinisha Trump wasiyemtaka au kumkubali Cruz wasiyempenda au chaguo dhaifu Kasich
 
magode unaona jinsi gani mwenendo unavyobadili mjadala.
Mag3 kaweka namba na kuonyesha njia ngumu kwa Cruz na Sanders.
Hapa tayari kuna kujambo interesting limeingia, Sanders!

Aliposhinda New Hamshire, kauli mbiu dhidi ya mpinzani ilikuwa kura ya Iraq.
Aliposhinda Michagan kauli mbiu ikiwa 'mikataba ya biashara kama NAFTA'
Alipoelekea mgharibi kati na NY kauli mbiu ikawa wall street

Hakuwahi kusema lolote kuhusu mgawanyo wa wajumbe.

Aliposhinda majimbo 7 mfululizo kwa Caucus alibadili kauli na kuwataka super delegates waangalie nani anashinda kwa wingi wamuunge mkono

Kuelekea NY kauli ikabadilika akitaka super delegates wamuunge mkono kwavile anaingiza vijana na ''independents'' wengi

Baada ya kupoteza NY na kujua Penny, Connect, Maryland ni maji marefu akabadili kauli,uchaguzi wa Democrat uwe huru kwa yoyote.

Sanders,hajalaani caucus alizoshinda ambazo ni mbaya zaidi ya registered voters

Kwa mfano, waliopiga kura katika closed primary' inayowahusu Dem tu' Maryland ni malaki ukilinganisha na Utah, Idaho, Washington state na hata Wisconsin

Mbona hakulalamika vijana kuwa disfranchised katika caucus?

Sasa amebadili kauli, anasema hoja ni kubadili mfumo wa uchaguzi wa Marekani

Hapa kuna hoja, akiwa Seneta 'independent' hana rekodi ya kupeleka mswada wa jambo hilo. Alipoamua kugombea hakuhoji jambo hilo.

Aliposhinda hakuhoji , akishindwa anarudisha aliloshindwa kulisimamia toka mwanzo

Hii ina maana moja, Sanders anaendelee apate wajumbe wengi si kushinda bali kuleta pressure ndani ya convention. Pressure imelenga mambo mawili makubwa

1. Kujenga hoja anavuta watu na msisimko hivyo wajumbe wote wa kuchaguliwa na super delegates wachague upya ili kutoa 'haki'

2. Kuwashawishi wajumbe wa convention waweke pressure, Clinton amteue mgombea mwenza kuelekea DNC. Kwamba, atapkapokuwa na wajumbe wengi ni ngumu ku ignore kwasababu atakuwa na '' electoral college' ya wafuasi

Tukijuliza kwanini hana super delegates wengi, tayari mjadala unapanuka

Tutaendelea na hilo
 
SUPER DELEGATES (SD)
JE REPUBLICAN WANA SUPER DELEGATES KAMA DEMOCRAT?

Kabla hatujaeleza hoja ya kwanini Sanders ana super delegates wachache hadi sasa, kwa ufupi tuzungumzie namna SD wanavyopatikana.

Hili ni moja ya yale mkuu magode anayouliza, kwanini tunaongelea democrat Zaidi.

Kuna ukweli tumezungumzia idadi ya wajumbe wa Democrat tukihusisha SD kuliko Republican. Kuna sababu tutaeleza

Swali, je, Republican wana super delegates?
Na kwanini nguvu yao haionekani kama super deleagtes wa Democrat?

Kabla ya kujibu hoja hii, tuangalie kwa ufupi hawa super delegates ni akina nani?

Democrat
Super delegates(SD) ni wajumbe wa mkutano mkuu kwa nyadhifa bila kuchaguliwa

Hawa ni kama magavana, wabunge , marais wastaafu, makamu wa Rais, wenyeviti wa majimbo n.k. wanaotengeneza asilimia 15 ya wajumbe wote

SD wa Democrat wapo huru kumchagua yoyote na kubadili misimamo yao wakati wowote bila kufungwa na jambo lolote.

Hawalazimiki kupiga kura kutokana na matokeo yoyote ya uchaguzi
Nguvu yao kubwa ni uwezo wa kupiga kura ndani ya mkutano mkuu (DNC)

Inapotokea hali inayolazimu mkutano mkuu kupiga kura, SD wana nguvu ya kuamua
wenyewe wakisema 'tip the scale'

Hakuna kanuni ya SD kujifungamanisha na mgombea, bali uwezo wa mgombea kuwashawishi kwanini wamuunge mkono

REPUBLICAN
Wapo super delegates ingawa ni asilimia 7 ya wajumbe wa mkutano mkuu
Upatikanaji wao unahusisha formula ya wajumbe 3 wa Republican kutoka kila jimbo

Tofauti na Democrat ni kuwa, SD wa GOP wanalazimika kupiga kura kutokana na ushindi wa mgombea katika jimbo husika. Kwa mfano, SD wa NY watalazimika kumpigia kura Trump kama itabidi. Ndivyo ilivyo kwa Kasich Ohio au Cruz Texas

Ushawishi wa SD wa Democrat ni mkubwa na uhuru wake ni mpana.

Hili ndilo linamsukuma Bwana Sanders kusema, SD waondolewe ili kupata 2383 ya wajumbe wa kuchaguliwa.

Anafahamu katika mazingira ya sasa si yeye au Clinton anayeweza kufikia namba hiyo

Hili litamsaidia kujenga hoja ya kuelekea mkutano mkuu.
Kwavile SD wanaweza wa kubadili kibao, matumaini ni kuwashawishi wamuunge mkono.

Endapo ni hivyo, kwanini Sanders hakuwashawishi kabla ya kufikiria kura zao DNC?

Ndipo swali linapojibika kama tutakavyoona bandiko linalofuata
 
SANDERS NA SD
Tumeona jinsi gani wajumbe wanavyopatikana kwa upande wa Democrat.
Kwa mtazamo huo, tumwangalie Hillary Clinton kwa ufupi kabla ya kumwangalia Sanders

Clinton alikuwa first lady wa Arkansa ambapo mumewe walikuwa Gavana wa jimbo hilo.
Katika kampeni za Urais, Bill na Hillary walikuwa pamoja wakizunguka nchi yote kutafuta kura

Hillary Clinton alikuwa Seneta wa New York kwa miaka 8.
Akiwa ndani ya Seneti alishiriki mijadala na maseneta wenzake pamoja na wajumbe wa Congress

Hillary alikuwa First Lady, nafasi iliyomkutanisha na watu mbali mbali mashuhuri kama First Lady wa US
Hii ni pamoja na kushiriki conventions za Democrat mbili, pamoja na shughuli nyingine

Amekuwa secretary of states, nafasi iliyompa fursa za kukutana na Maseneta, congressmen and women, magavana n.k.

Bernie Sanders, ni Seneta wa kujitegemea akitokea jimbo dogo la Vemont. Zaidi ya maseneta wenzake na wabunge wa Congress, Seneta Sanders hana link kubwa zingine kama tulivyoona kwa Clinton

Hili tu linaeleza kuwa, mtandao wa Familia nzima ya Clinton ni mpana kuliko wa Sanders. Wapo wajumbe wanaomjua Hillary binafasi, wapo wenye mahusiano na mumewe na wapo wanaokubaliana naye hata kama hawakujuana

KWANINI MTANDAO NI MUHIMU
Mtandao wa Clinton ndio umemwezesha kupata ushindi kwa baadhi ya majimbo. Kwa mfano, NY , Bi Clinton alipata msaada mkubwa wa Gavana na wabunge wa Congress na Seneti. Ndivyo ilivyokuwa kule Florida

Lakini pia uhusiano wake na mtandao ni wa kutegemeana. Tunafahamu uchaguzi mkuu utakwenda sambamba na uchaguzi wa Maseneta na wabunge (baadhi). Wengi wanategemea kura za Democrat kaa political base yao

Ukifuatilia kwa makini kama tulivyoeleza mwanzo, Bi Clinton anashinda sana chaguzi zinazowahusisha registered Democrat. Bwana Sanders ameshinda zile zinazoruhusu watu wote bila kujali itikadi za vyama au utiifu wake

Super Delegates wanajua, pale ambapo Clinton ana nguvu na wakijua ni za registered democrat, ni ngumu kwao kwenda kinyume. Kumbuka hawa ni Maseneta na wabunge ambao baadhi yao watapigiwa kura mwezi wa kumi na moja

Pia ieleweke siyo SD wote wamemuunga mkono Hillary. Wapo 41 wanaomuunga mkono Sanders na takribani 200 wanotazama mwelekeo wa uchaguzi kabla ya kuunga mkono mgombea

Mwenendo wa uchaguzi una influence vipi super delegates kumuunga mkono mgombea au kubadili misimamo?

Inaendelea....
 
Mkuu magode kwa idhini uliyotoa tutafafanua kuhusu hoja uliyoniuliza pembeni.
Magode anauliza mbona tunazungumzia sana Democrat kuliko Republican katika mabandiko?

Mkuu, tunaangalia pande zote sawa, kama ukifuatilia toka mwanzo

Hata hivyo, kuna sehemu ambazo kina cha mjadala wa Republican hakifikiwi kutokana na sababu mbali mbali

1. Hali ya Republican katika mijadala ni ya ukakasi.
Wagombea walijikita katika personal issues and attacks badala ya hoja.

Inakuwa si kwa public interest kujadili urefu wa vidole vya Trump au ufupi wa Marco Rubio. Tofauti na hivyo, Democrat wana afadhali hadi siku za karibuni

2. Kuna maeneo mengine yanachanganya kuhusu Republican na hivyo yanaelezwa kwa ufupi ili kuelewaeka kwa urahisi zaidi badala ya kuwachanganya wasomaji

Mfano, tangu mwanzo tumezungumzia namba 1237 kama mstari wa mwisho wa mshindi kuufikia. Lakini ndani ya 1237 kuna kanuni( formula) nyingi sana ambazo si rahisi kuzieleza kwa lugha nyepesi bila kuwachanganya wasomaji.

Ndio maana tulieleza maana ya winner take all, winner take most na mgawanyo wa congressional districts, state convention, Caucus n.k.

Mfano, juzi Pennyslavania , haikuwa rahisi kupata namba ya wajumbe kwasababu katika wajumbe 95 , wapo 54 wasiotengwa kwa mgombea yoyote.

Yapo majimbo mgombea anapata wajumbe kutokana na kura za Urais za 2012
Yapo majimbo anachaguliwa na state convention kwa mgawanyo maalumu n.k.

Kwa mifano hiyo, ni ngumu kupata namba za mwisho hadi zitakapotolewa na RNC

Tofauti kidogo ni Democrat mtiririko wao wa uwiano ni rahisi ukilinganisha na GOP

Kuhusu siasa napo kuna tofauti kubwa na hapo ndipo panapozua ukina wa eneo moja ukilinganisha na jingine

Tuseme kuwa tunazungumzia pande zote kwa usawa na hakika Republican wamechukua sehemu kubwa ya mjadala kutokana na hali ya mambo ilivyo
Nakushukuru mkuu Nguruvi3 pamoja na kukuulizia pm lkn uliheshimu mawazo yangu na kunipa kile nilichotaka kufahamu. Ushauri wako pia niliuzingatia na kwa sasa tupo pamoja. Naendelea kukufuatilia ntarudi..!
 
MWENENDO WA UCHAGUZI NA MAAMUZI YA SUPER DELEGATES

Kuunga mgombea mkono kuna ambatana na mambo kadhaa mengine tumeyazungumzia
Hata hivyo, SD pia huangalia masilahi yao na uwezekano wa mgombea kuwawezesha kurudia nafasi zao za Useneta au ubunge kwa wale wanaoingia uchaguzi mwaka huu

Wanoingia uchaguzi mwaka huu tuna maana katika Congress na Senate, chaguzi hufanyika mara mbili kwa muhumula mmoja.

Uchaguzi unaofanyika katikati ya muhumula unaitwa midterm elections.
Hivyo, wapo watakaoenda katika uchaguzi mwaka 2016 Rais akiwa madarakani

Kuhusu SD, pia wanaangalia mgombea anayeweza kukiwezesha chama kupata ushindi

Kumbuka, uchaguzi wa marekani ni kutokana na idadi ya viti na si popular vote
Namba inayotakiwa ni 270 kati ya viti 538

Viti hugawanywa kwa utaratibu wa majimbo kwa vigezo vilivyowekwa
Angalia mgawanyo wa viti katika uchaguzi uliopita

Hii ni ramani ya uchaguzi mkuu, ikionyesha namna ambavyo mgombea anaweza kushinda majimbo lakini asifanikiwe kuwa Rais.

Angalia mfano huu, Seneta Sanders ameshinda Utah, Wyomin, Idaho, Wshington state, Michigan,Minesota, Vermont, New Hampshire kwa uchache. Hayo ni majimbo yenye viti

Hayo ni majimbo saba 'kwa mfano tu wa kujifunza' kama ingalikuwa ''uchaguzi mkuu'' kati ya Bernie na Hillary, Bernie angesginda. Idadi ya viti ni 80

Hillary ameshinda Florida, Ilinois, Ohio, New York sawa na majimbo 4 yenye viti 94
Fikiria, kuna aliyeshinda majimbo saba akapata viti 80, na aliyeshinda majimbo 4 viti 94

Hoja hii inaeleza SD wanaangalia nani anashinda wapi na si kushinda tu.
Wanaangalia nani anashinda Democrat states(blue states) na Swing states(zinazobadilika)

Haileti maana katika kuifikiri, ikiwa mgombea anashinda red states

Hizi ni baadhi ya sababu ambazo SD wanaziangalia kabla ya kubadili mwelekeo au kuamua kumuunga mkono mgombea.

Ni kwa msingi huo, Sanders hana SD wengi, na haionekani kama ataongeza kutokana na hesabu zilivyo. Anachokifanya sasa ni kutafuta njia ya kubadili mwelekeo wa uchaguzi ili ajenge hoja nyingine ambao ameitamka leo May 1 katika mkutano na waandishi

Seneta Sanders kasema nini leo hii kuhusu super delegates?

Inaendelea
 
SENETA SANDERS KASEMA NINI LEO?

Seneta Sanders amesema ' Suala la super delegates liangaliwe,kwamba wanapaswa kufuata matakwa ya wananchi. Kwa maana hiyo Bi Clinton hana namba ya wajumbe wa kuchaguliwa(2383) bila super delegates, na kwamba wakifuata matakwa ya wananchi, hatafaikia namba hiyo na jibu ni kwenda mkutano mkuu kwa contested convention ''

Haya ni maneno ya Sanders kama tulivyowahi kueleza mabandiko mengi ya nyuma.
Kwa ufupi anachosema Sanders tumekileza bandiko #122

Baada ya NY (Bandiko 103) tulisema hoja ya Sanders kushinda majimbo 7 tena yakiwa ya Caucus ndogo ililenga kubadilisha msimamo wa SD.
Alitamka wazi super delegates waanze kumuunga mkono.

Tukaeleza NY ita define mweleko, na ndivyo ilivyokuwa.

Ushindi wa point 15 NY wa Clinton ulizima kabisa uwezekano wa kuvuna wajumbe.

Mambo yalimwende kombo Sanders Pennsylvania, Maryland, Connecticut na Delare ambapo kwa usiku mmoja alipoteza majimbo makubwa 4 kwa pointi Zaidi ya wo.
Hesabu zikionyesha njia imefungwa kwa Sanders

Tulisema haja ya Sanders kubaki katika uchaguzi ni kutafuta njia za kupeleka uchaguzi mkuu kama kauli za kampeni meneja wake zilivyoashiria(Bandiko 10).

Mag3 akaonyesha hofu waliyo nayo Democrat kutokana na mwenendo wa Sanders (# 113).

Tuksema hali ilipofikia Democrat wana hofu yasije wakuta ya Republican (#111) n.k.

Kauli ya leo ya Bwana Sanders inaeleza umuhimu mkubwa kwa Clinton kampeni kuendelea na kasi ili kukabiliana naye.

Sanders ameshindwa kushawishi wapiga kura na super delegates kwa njia za kura na maoni kama ilivyo katika kanuni za uchaguzi za Democrat

Sanders anachofanya sasa hivi ni kile kile tulichosema

1. Kutaka super Delegates wasiwe sehemu ya mchakato ili Bi Clinton asipate 2383 na kulazimisha kwenda mkutano mkuu wa DNC Philadephia

2. Akifanikiwa hilo kwa maoni yake, atatumia formula ya Republican.

Rejea mabandiko matatu nyuma utaona Super Delegates wa Republican wanafungwa kumchagua mgombea kutokana na ushindi. Super Delegates wa Democrat wapo huru

Hapa Sanders anataka Democrat watumie formula ya Republican.
Kwamba SD wapige kura kutokana na matokeo ya majimboni.

Kwa maana mbili, atakuwa amezuia 2383 ya Clinton, na pili ataanza kampeni ndani ya mkutano mkuu na kuzua kizaa zaa ndani ya Democrat

Mpango wa Sanders una matatizo makuu mawili
1. Kwanza, itawalizimu Democrat wabadili kanuni ili kukidhi haja yake
2. Kutaendelea kugawa chama wakati wa uchaguzi mkuu

Kwanini Sanders hatafanikiwa kwa mpango wake?

Inafuata
 
Nguruvi3, tukiachana na swala la wajumbe, mpaka sasa, hizi ndizo idadi ya kura walizopata hawa wagombea kwenye caucuses na primaries katika majimbo yaliyokwisha kupiga kura;
  1. Hillary Clinton.....12,135,109
  2. Bernie Sanders..... 8,967,401
Mpaka hapo tu Clinton anamzidi Sanders kwa kura 3,167,708! Wakati huo huo Clinton anamzidi Sanders kwa wajumbe zaidi ya 800 pamoja na SD. Hali hii imewaacha Democrats njia panda wakijiuliza ni kitu gani anataka Sanders.

Hata hivyo wanasita kumtibua kwa wakati huu kwa sababu kwa kufanya hivyo chama kitayumbishwa wakati wanataka umoja udumishwe. Hata Clinton mwenyewe amejizuia kumshambulia Sanders kwa hofu hiyo hiyo ya kupoteza mashabiki na wapenzi wake.

Hata hivyo dalili zinaanza kujitokeza za uvumilivu kufikia mwisho kwani kila siku Sanders anazua jambo jipya na mengi ya matamshi yake hayasaidii chama. Matamshi ya wapenzi wake nayo yanazidi kukoleza mambo na hasa wale ambao wazi wazi wanasema hawatampa Clinton kura zao akiwa ndiye mgombea.

Hilo moja lakini la pili ni kwamba mgombea wa GOP anayeongoza, Donald Trump, anaonekana kuchangamkia hoja za Sanders na anapanga kutumia mashambulizi hayo hayo dhidi ya Clinton.
 
Mkuu hapa ndipo tunafika katika hoja ya 'kwanini Sanders hatafanikiwa'

1. Namba zinasomeka, Clinton ame 'hold' democrat base inayompa makali.
Hili SD wanaliangalia kwa ukaribu sana

2. Ukitazama majimbo, SD hawawezi kudharau ukweli wa ngome za Dem na swing states.
Florida, NY, Massach, Penny,Maryland, Ilinois.

3. SD wana hofu na similarity za sera za Trump na Sanders. Wapo on ''same page'' Mdahalo wa Brooklyn Sanders alitia hofu aliposhindwa kuji distance na Trump

NATO ni suala linalojadilika,Obama kaliongelea akiwa ulaya
Diplomatic language zaTrump na Sanders zina walakini

Sanders anapingana wazi wazi na 'Dem' katika mambo ya misingi ya Democrat.
Udhaifu ni pale anaposema hahitaji sheria kutenda anayofikiria!!!

Juzi katika dinner na waandishi, Obama alifanya 'utani' wenye ukweli.
Alisema 'Sanders ana ji distance na si sahihi kwa Comrades''
Comrades linaeleza mengi na ilikuwa kibao cha usoni

4. Trump anatumia kadi ya Sanders kuchochea mtafarauku akitaka agombee binafsi.
Hii ina maana atadhoofisha Democrat kwa kiasi fulani.Trump anatumia hoja za Sanders kumshambulia Clinton. SD na Democrat kwa ujumla hawana na raha na hali hiyo

5. SD wanajiuliza, kama Sanders analeta independents inakuwaje yupo nyuma kila eneo? Hofu ya Democrat ni kuwa Independents wanaokuja wanaweza kuwa independents kwa Trump. 'Dem core' ni loyal na ndio wa Clinton. Hilo litawaongoza pia

6.Democrat wanajua, chama kinapigiwa kura na watu wote.
Sanders kutoshinda katika maeneo ya watu wa rangi kunatia hofu kuliko faraja.

Kwa mfano maeneo ya weusi au Walatino nini itakuwa hatma ya Democrat?
Watu wa rangi ni 'electoral collage ya Democrat siku zote'

7. Sanders anaposhauri utumike utaratibu wa Republican , kwamba SD wafungwe kutokana na matokeo inawatibua Democrat.

Democrat wanajiuliza ikiwa Sanders alijua taratibu kuanzia mwanzo kwanini hakulalamika? Ilikuwaje alipokuwa anashinda haku raise concern?

Hapo nyuma tulisema,Clinton kampeni inajizuia kutoleta mtafaraku kwa wakati huu.

Si kwamba ni dhaifu, bali wanacheza karata kwa uangalifu.

Nimewasikia baadhi ya pundits wa Dem, inaelekea wamechoka na haya ya Sanders

Tusemezane
 
Nimewasikia baadhi ya pundits wa Dem, inaelekea wamechoka na haya ya Sanders
Hebu turudi nyuma kigodo hadi mwaka 2008 Hillary alipojitoa na kumuunga mkono Obama, je mambo yalikuwaje?

Tuanze kwa kuangalia idadi ya wajumbe wa kila mgombea wakati huo;
  1. Barack Obama...1764
  2. Hillary Clinton....1640
Tofauti ya wajumbe ...124

Sasa tulinganishe na idadi ya wajumbe wa kila mgombea mwaka huu;
  1. Hillary Clinton...2165
  2. Bernie Sanders..1357
Tofauti ya wajumbe...808

Hapa ndipo tatizo linakoanzia. Mwaka 2008, Hillary angeweza kabisa kuendelea hadi convention na nafasi ya kushinda ilikuwa kubwa kuliko nafasi aliyo nayo Sanders. Pundits wanamvutia pumzi Sanders wakijiuliza hasa malengo yake ni nini lakini wakati huo huo wako kazini na muda si mrefu watajua kilicho nyuma yake.

Wengine wameanza kumtupia lawama mke na mshauri mkuu wa Sanders, Jane O'meara Sanders, kama ndiye kisiki, u-first Lady umeshamwingia akilini...ameonja asali sasa anataka kuchonga mzinga. Nakumbuka mambo kama haya yamewahi kutukuta Watanzania katika nyakati tofauti tofauti. (Natanguliza samahani kwa hili).

Kimahesabu hata kama Sanders angepewa wajumbe wote anaodai na wote wa majimbo ambayo bado kupiga kura hawezi kumfikia Clinton, je lengo lake ni nini?

Huko Republican nako Donald Trump hakuna anayeweza kumfikia na inaaminika mpinzani wake mkuu Ted Cruz, kama atashindwa leo kuinyakua Indiana, mbio zake zitakuwa zimefikia mwisho. Lakini pia zipo dalili naye atajaribu kung'ang'ania kama Bernie Sanders ingawa kwa Republicans hali ni tofauti kidogo.

Anayelalamikia utaratibu wa uchaguzi GOP ni yule anayeongoza, Donald Trump, lakini kwa DEMs anayelalamikia utaratibu ni yule anayeshindwa. Hili swali limezua utata ambao haujawahi kushuhudiwa katika chaguzi mbali mbali Marekani. Kwamba anayeongoza upande wa GOP anakubaliana kwa hoja na anayeshindwa DEM...je kulikoni?
 
TRUMP ASHINDA INDIANA
SENETA TED CRUZ AACHIA NGAZI

Trump ameachia ngazi (suspended his campaign)
Democrat bado matokeo ya mwisho hata hvyo inaelekea Sanders atashinda

Tutaendelea na tahmini hasa tukiangalia nini kinafuata GOP ambako Trump sasa ni ''Mgombea' wa GOP
 
Namuona Trump akipenya aisee...

Ted Cruz Ame droup out rasmi....

Wahafidhina wa Republican naona wanaelekea kuzama kwenye tope!
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom