Tunahitaji chama kipya?

Kuanzisha chama sio solution...hata James Mapalala alianzisha Chama cha Wananchi CUF. Maalim na Prof wakakibinafsisha. Issue ni kuimarisha katiba za vyama vilivyopo kuzuia ubinafsishaji usijirudie.
 
Tunahitaji chama kitakachokuwa wazuri kutoka CDM na CCM; kwa kuwa neither of the two is good!
 
wana jamvi kiukweli nilikuwa naamini kuwa chadema ndicho chama kitakachoweza kutusemea,kututetea na kutujulisha mambo mbalimbali yanayoendelea TZ.lakini kutokana na maigizo yanayoendelea juu ya kesi ya Zito nimeamini hakuna mwanasiasa wala chama kitakachomkomboa Mtanzania wa chini sio chadema,ccm wala Cuf. Minashauri ni bora watanzania kuendelea na shughuli zetu za maendeleo kuliko kuwasikiliza waigizaji wanasiasa.
 
Wako watu wengi wamechoshwa na vyama vyao kwa sababu ya utendaji usiolenga maslahi ya Taifa hili. Tumaini la watanazia lilishahamia Chadema. Chadema inaonekana kutokuwa na adhabu mbadala zaidi ni kufukuza. Hii inawatia watu hofu na hasa wanaotaka kukua kisiasa. Kama kikianza chama cha Watanzania kinachoweza kurekebisha kasoro hizi katakuwa na nguvu sana. Watanzania tunataka kuona mikakati inayosimamiwa na watu waadilifu ili tuwapedhamana ya umma wawatanzania. Tunakikaribisha chama kipya. Referential option
 
Kila mmoja wetu humu anataka mabadiliko ya kweli katika nchi yetu, thus why wengine walihama ccm kwenda upinzani wakidhani tumaini lao la kutapa mabadiliko ya kweli.
Wengi sasa wamegundua hata hivyo vyama vya upinzani haviwezi kuleta hayo mapinduzi watu wanayo itaji!
Tatizo letu sisi watanzania ni kutaka mabadiliko kutoka juu kwenda chini, Hilo haliwezi kutokea hata hicho chama kitoke mbinguni, unataka mabadiliko yakweli anza na mjumbe wa nyumba kumi, then twende kwenye selikari Za mitaa then ndo tuangalie wabunge na raisi. Kwangu mm naamini mabadiliko ya kweli yanatoka chini
 
Tunakoelekea itakuwa issue siyo chama bali nani anaanzisha chama na ana malengo yapi? yale yale kama Kenya
 
Tatizo sio chama kipya, tuache kulalamikia vyama vilivyopo, na kuchukua hatua, mi nadhani imetosha sasa
 
Mzee Mwanakijiji naomba unipatie ufafanuzi,Hivi waanzilishi wa vyama vya siasa Tanzania wana nia ya dhati ya kumkomboa mtanzania kutoka katika hali aliyonayo ili apate ukombozi huru na wa kweli?Hivi kuna dhamira ya dhati kutoka kwenye hivi vyama ya kukiondoa chama tawala madarakani?Hivi miaka ile ilipoibuka NCCR na CUF kama kweli kulikuwa na ukombozi wa mtanzania walishindwa nini kuungana ili kutimiza dhamira yao?Hivi CDM kama wangeungana na vyama vingine na ukawepo mkakati wa kuwafikia watanzania wote leo si tungekuwa tunasubiri tu uchaguzi ili tuwatoe watawala?Binafsi nahisi kuna nia tofauti na sababu tofauti za kuanzisha hivi vyama,basi kama ndio hivyo tusianzishe vyama vipya,twendeni na fikra na mawazo mapya kwenye hivi vyama ili tufanye yale tuliyokusudia
 
Naaam MM UMEFIKA huko tena mkuu!!!Hao ndio watanzania wakenya wanawaita watz. Mkuu tatizo sio vyama tatizo ni MFUMO mkuu!!mfumo wetu unaitaji RESTRUCTURE, tena sio ya kubabaisha.Na atakae simamia hiyo naweza kutoka humo humo CCM, au CDM haitaji chama kingine.Kwa kuwa gharama ya ujenzi wa chama kingine njia ni zile zile alizopitia CDM kukua mpka hapo alipofika kinachotekea fikra za wanachama ndio zinaboreka.

Ndio maana sie wengine vyama tulimalizana navyo tukiwa A-level,hakika kwa mfumo wa Kitanzania siasa za vyama kwa malezi yale ya chama kushika hatamu,kunageneration fulani bado ina amini kuwa Taifa bila aina fulani ya mfumo wa kikundi/kijikundi fulani ndani ya chama kuendesha mambo katika kufanya maamuzi yote yaliyo ya msingi na yasiyo ya msingi kwa niaba ya umma bila kuwashirikisha wengine/umma na hao wengine/umma kuwa wao ni kundi la kupokea tuu kutoka kwa watoaji bila kuhoji ni gharama kwa umma na kwa kikundi pia katika siku za sasa na zijazo.

Aina hiyo ya mfumo wa kijikundi/[ningetumia jina zuri ''those who run the show''] limefikisha Taifa sehemu sote tunadapt.Na kwa kuwa umma wetu kihistoria una nasaba ya USWAHILI KITABIA [Jumla ya zao la tabia za nasaba za Uafrika , Uarabu na Uhindi] , basi nasaba hiyo ya Uswahili [Uafrika, Uarabu na Uhindi] imetufanya kuishi kwa mchanganyiko unaozalisha aina fulani ya tabia za ujanja ujanja, ujuaji, uelevu, uzushi, utapeli,uongo,na mengineyo yote yasiyo na hekima na hasa wengine kujiona ndio chama na hao hao ndio wenye dhamana ya Taifa kuliko raia wengine.

Ebu angalia hii MM, mtu ambae ujana wake hapo zamani alikuwa mnyanganyi, dhurumati, mwongo akatajirika kwa njia haramu na ovu, lakini baadae akahalalisha shughuri zake kwenye umma, baadae kwenye aina fulani ya utu uzima mtu huyo huyo anatumia nasaba ya Uswahili na kujishughulisha na siasa kwenye vyama mtu huyo huyo anapewa madaraka kwenye umma. hapa hivi ni aina gani ya mfumo utaishi?.

Matokeo ya aina hiyo ya nasaba ndiyo yaliyozalisha tabia ya watanzania na hasa familia zetu kushabikia watu wezi/ wadanganyifu waliopewa dhamana za umma/mashirika/makampuni au idara na kuzitumia dhamana hizo kuyaibia na kujineemesha na kwa wale ambao wanageuka na kuwa watendaji na viongozi waadilifu wenye kujali uadilifu [integrity] au unaminifu [honesty] wanageuzwa kuwa wajinga wa ovyo ambao hawakutumia nafasi zao vyema kujitajirisha na kuinua familia zao na marafiki zao.Na kwa kuwa Future security life ya watu haiko bayana hata kama alikuwa mwema na mwaminifu hatosita kuiba na kujifaidisha kwa kulimbikiza kwa niaba yake na familia yake kwa ujumla, kwa kuwa mfumo umeecha Umma kukumbatia tabia ya kusifia vile ambavyo havistahiki kusifiwa katika ulimwengu wa wastaarabu.

MM unajua dhahiri ulimwengu wa wastaarabu ni upi?Je nasaba zetu zinakidhi sie kuadapt yale tunayoweza kusema ni ustaarabu na kujiaminisha kwayo kwa ajili ya ujenzi wa vyama ambavyo tunavipa dhamana ya kuendesha Nchi.Kumbuka wapiga kura na wanachama wa vyama hivyo ndio wale wale wasifiaji wa wale watendayo yasiyostahiki kutendwa.

Mfumo umeruhusu vitu vingi ambavyo [Nikisema mfumo namaanisha waelevu] wenye kuona mbali wamekubali kuwa na aina fulani ya kuachia vijitabia na matendo yasiyo stahiki, kuanzia level za familia mpaka Taifa, na kuvipa ruksa ya kukua na kugeuka kuwa tabia tunazoziishi.

Binafsi mimi ni kijana, lakini sipendi na sitaki kwa kwa kuzingatia kizazi [generation] ya sasa ya wanaochipukia [teenagers-someone who is between thirteen and ninteen years old ] kumiliki simu akiwa maeneo ya Shule.Swala la mtoto kumilki simu akiwa Shule sio swala la mtoto na familia yake na kisha kuamia kwa mwalimu wake kumzuia asiingie shule na simu hiyo.Kimfumo swala ilo ilipaswa kuwa ni swala la maalufuku kwa mtoto yoyote ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania anayesoma kuanzia Primary school mpaka Secondary school kumiliki simu akiwa Shule. Onyo kali na adhabu kubwa itatolewa kwa muhusika wa tendo ilo, yote haya yangetendwa kwa kutumia ama sheria kubwa au sheria ndogo ndogo.Lengo kuu hapa ni Taifa kushape kizazi kwa faida ya wote kwenye aina fulani ya umri na sio swala la holelaholela tu, yani mzobe mzobe tu twende tutajua mbele kwa mbele.

Je waelevu wanaratibu future the generation kwa kuzuia kabla ya kutokea au wanaacha yaje yatokee ndio waratibu matokeo ya yasiyo ratibiwa.Nini matokeo ya kuratibu kitu ambacho hakikuratibiwa? Hivi leo aliyekuwa mwizi, jambazi, muongo, mlaghai, mnafiki, wapambe, wanaingia kwenye vyama na kupewa dhamana kesho utegemee matokeo gani, atakae tofautina nao katika mikakati au mipangilio yao ananafasi gani katika taasisi, idala au kampuni husika.

Najifunza nitaendelea kujifunza ila uwa naumia sana kwanini mfumo [system] inalea kibovu kikue na kuishi katika kizuri na daima kwa mfumo wetu kibovu kuonekana kukumbatiwa na mfumo na kuhakikisha kizuri kinakufa na kupotea kabisa.Kisha kibovu kikisha leta madhara ndio mfumo unaanza kuratibu na kutafuta kizuri kilipo na hatimae kukuta hata kizuri nacho baada ya kugundua kuwa uzuri wake hauthaminika unavunjika moyo na kukata tamaa na kuamua ama kugeuka na kufanana na kibovu au kupoteza maana ya uzuri wake.

Labda kwa hili la kunzisha vyama ushauri wangu kwako ebu twende navyo hivi hivi CDM vs CCM, kitaeleweka tu If you can defeat them join them!!Jibu lipo ila muda kwa kuwa mfumo unaenda unakumbana na changamoto!! Uliamini dogo angekosa busara na kutapika hayo aliyotapika kiasi kuwa mifumo ya pande zote mbili imepata majeraha si CDM wala si CCM wote Manche ga Nyanza.
 
Najiuliza kama kuna watu wameanza kuwa kama mimi; vyama vyote vya kisiasa vilivyopo nchini haviwezi kutupatia kile tunachohitaji kama taifa.

Siyo CCM, CHADEMA, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania.

Je, kuanzisha chama kingine ambacho kitatoka kwa wananchi na chenye ajenda ya mabadiliko ya kweli na kikiongozwa na watu wenye mwelekeo wa mabadiliko na wasioogopa political confrontation na ambacho hakitasita kufanya what is necessary to restore law and order and a constitutional rule kitaweza kuwa na nafasi.

Chama ambacho mrengo wake itakuwa ni kuhakikisha kuwa hakuna kurembuliana macho na mafisadi tena wala kuufafanua ufisadi bali kuushughulikia moja kwa moja.

Chama ambacho kitalenga kuleta mabadiliko ya kimfumo na kimuundo wa serikali yetu ndani ya miaka mitano ya kuingia madarakani kikibeba ajenda ya mabadiliko ya kweli (kikatiba, kisiasa, na kiutendaji) huku kikiwashughulikia kama simba mkali wale wote ambao wamelifikisha taifa letu hapa ikiwemo kutaifisha mali zao, kuwasweka jela na wale ambao ni vigogo wa ufisadi "kunyongwa" kama wanavyofanya huko China!

Chama ambacho hakitawabembeleza wawekezaji kama wakwe zetu!

Au ndiyo tubanane mumu kwa mumu huku tukiulizana "kajamba nani'!
MWANAKIJI,leo nimepata fursa kidogo.
Naamini swali la msingi ingekuwa "Kwa nini vyama vya upinzani vinapata misukosuko mingi na hatimaye kufa?"
Kwangu mimi ni kuwa tayari tlishakuwa na vyama ambavyo vingetusiadia sana kuendeleza demokrasi nchini lakini kwa kuwa na kwa maksudi vyombo vya ulinzi na usalama vimejiingiza kutetea chama dola na kubomoa vyama pinzani hata ungeanzisha kipya itakuwa hivyo hivyo.
 
Nilishasema juu ya chama Mbadala......!ila kina Mzee Mwanakiji hawatakiwi kuwa sehemu ya Uongozi
 
Last edited by a moderator:
naweza sema, leo wachangiaji mmenifurahisha sana, kila mtu amejaribu kuwa very serious..

mkuu mwanakijiji, soln ya tanzania iko mikononi mwa watz wenyewe, inabidi nchi itawaliwe na wananchi ili watawala (iwe CDM, CUF, CCM) wanapokuwa madarakani wawe na discipline ya uongozi.
Namaanisha kiongozi yoyote akifanya baya aadhibiwe na wananchi kama wale vibaka wa mitaani, akikatiza mitaani kwetu ni mawe tu (hili nipale watz wote tunapokuwa wazalendo) hii italeta uoga wa watawala kwa watawaliwa.

mwisho kabisa, tatizo la CUF=CCM=TLP=NCCR=CDM, matatizo yao yanafanana, inabidi wananchi tuchukue hatua wenyewe bila kuongozwa na mwanasiasa yoyote yule.
 
Watanzania wakibadilika kifikra basi vyama hivyo hivyo vilivyopo vya upinzani (vikiengezeka vizuri) vitafaa mradi vitakuwa disciplined na watu ambao wamebadilika kifikra.Kama vichwa vya Watanzania wengi vitaendelea kuamini kuwa CCM ndo nambari wani hata kama hakina jipya...basi tunaweza kuwa na vya zaidi ya 300 kama Congo kinshasa...na itakuwa Katibu wa Chama kimoja ni Mwenyekiti wa Chama kingine...

Watanzania wabadilike kifikra na kila kitu kitabadilika...Obama alipokuja na "Change Policy" aliwakuta Wamarekani tayari wameshabadilika kifikra na walikuwa tayari kwa chama au system nyengine ambayo itakwenda sambamba na fikra zao mbadala...hawakuhitaji chama kipya bali kile ambacho kitakua tayari kukubaliana na fikra zao...

Watanzania wabadilike...CCM ya jana si ya leo.
Tuendelee Kusupport hivi hivi vilivyopo.....hakuna haja ya kukata tama. Siku zote ukombozi ni mgumu sana. Najua kwamba kila mtanzania anahamu ya mabadiliko, hali iliyopo CHADEMA ni nzuri kwetu kwani itatusaidia kujua makosa yaliyopo na kuyarekebisha, TUTAVUKA TU HIKI KIHUNZI.
 
tukitaka kuichambua kasoro ya na udhaifu wa vyama na demokrasia yetu lazima tuangalie majirani zetu na nchi nyingine za Afrika haswa zile zinazosifiwa kua na demokrasia nzuri zimefikaje hapo au zina nini ambacho hatuna.

nchi zenye demokrasia nzuri Afrika (upinzani na ushindani wa kivyama vya siasa not necessarily strong democratic national institutions) ni Botswana, Ghana, Senegal, na Kenya na Zambia kwa kiasi fulani huku naidisqualify South Africa hapa kwa kua na strong democratic institutions kama tume huru ya uchaguzi, judiciary n.k huku wakipoteza upinzani wa kisiasa kupitia vyama vya siasa na weak civil society iliyofumbwa mdomo na ANC.

Botswana-nchi ndogo kiidadi ya watu na nchi ya kijadi zaidi ambapo kiongozi wake wa kwanza alikataa ufalme na kuweka misingi ya demokrasia toka uhuru wake tofauti na Swaziland au Lesotho(kwa kua hakukuwa na wasiwasi wa kupoteza himaya ya kisiasa na pili busara tu binafsi zilizochangiwa na kitu kinachoonekana kama uliberali wa kiongozi wa kwanza wa Botswana Bw Seretse Khama)..Tanzania Nyerere aliconsolidate power yote mikononi mwa TANU na baadae CCM kwa kuhofia kuipoteza kwa maadui wa ndani na nje na kuhofia kumegeka kwa umoja na kupoteza amani kwenye taifa kubwa la dini na makabila tofauti.

Ghana-kijamii haiko tofauti sana na Tz tofauti kubwa kijamii ni kwamba waghana wengi wamesoma tofauti na TZ. Kisiasa Ghana imekua na mapinduzi mengi ya kijeshi toka 1966-1986 na hivyo kutoipa nguvu chama chochote cha kisiasa hadi 1992 ambapo vyama vilikuja bila kua na dominant old party kama hapa nyumbani na hivyo kuweka uwiano fulani ambao hadi leo waghana wana vyama viwili vi3 vikubwa vinavyobadilishana madaraka

Senegal-demokrasia imekua baada ya Rais wa kwanza Senghor, kua na hekima ya kujenga utaifa kwa kushirikisha wapinzani wake kwenye serikali toka uhuru mazingira yaliyoruhusu ukuaji wa civil society bila kubanwa sana tofauti na Tz na baadae Senghor kuachia madaraka Abdou Diouf ambaye baadae na yeye alikubali kushindwa uchaguzi ( kitu kigumu sana Africa hii) mwaka 2000 kwa Wade kitu ambacho kilimfanye Wade nae akubali kushindwa kwa Sall ( political culture ilikua imewekwa toka Uhuru ya tolerance na ukubwa wa asisi za kiraia imeifanya senegal kua hivi ilivyo).

Kenya jirani zetu demokrasia yao kwa kifupi ni inatokana na ukabila uliopo miongoni mwa viongozi na wananchi wake, lakini hii haitoipa haki Kenya kwa kua kuna kundi kubwa la wasomi linalotumika kwenye kuleta changamoto demokrasia hii, na ukubwa wa civil society ya Kenya tofauti na Tz ambapo wasomi ni wapiga debe au waajiriwa wa chama tawala.

Zambia ni interesting story kwa sababu kihistoria Kaunda na Nyerere hawakua na tofauti kubwa kiongozi na kiushawishi ndani ya nchi zao.UNIP haikua na tofauti sana na TANU/CCM na mazingira yake kijamii na kiuchumi. Tofauti ilikuja wakati wa mageuzi miaka ya 80 mwishomi na 90 mwanzoni Zambia ilikua katika hali mbaya zaidi kiuchumi kuliko TZ ya miaka ya 90 mwanzoni kuelekea uchaguzi wa 95.
UNIP ikaanza kuondokewa na makada wake waliojiunga na MMD ya Chiluba na kumdhoofisha zaidi Kaunda. Kitu kilichokuja kuimarisha demorasia ya Zambia ni kukubali kwa Kaunda matokeo na kutoingilia serikali ya Chiluba kwa njia yeyote.. Tunaweza kusema wananchi wa Zambia labda labda hawakua tayari kwa mageuzi na kumtoa Kaunda na labda MMD na Chiluba kama walivyokuja kuprove baadae walikua ni opportunist na wababaishaji kama wapinzani hapa Kwetu, lakini uchumi mara nyingi ushawishi siasa na hiki kilileta mabadiliko Zambia na kuikuza demokrasia yake.

Hitimisho: Tanzania kama tulivyoona kwa wenzetu haina mambo mengi yaliyomo kwa wenzetu ili kuleta upinzani wa kweli wa kisiasa na kukuza demokrasia yetu. Miaka 51 ya TANU/CCM na sera ya ujamaa imedidimiza asasi za kiraia (civil society) ambazo ni muhimu sana kwa demokrasia kama tulivyoona Senegal, Kenya na kuufanya upinzani kupata wakati mgumu kuikosoa serikali bila kuonekana ni siasa tu na hivyo kuchangia kudumaza vyama.

Elimu ya watz nayo imechangia kutokua makini kwenye ukuaji wa demokrasia yetu kama ilivyo Kenya, Ghana. Kukosekana kwa ukabila Tz pamoja ni kitu kizuri, lakini kumevifanya vyama vipya kukosa "ready made" political base ya kuanzia na hivyo kuifanya kazi yao kua ngumu tofauti na nchi kama Kenya unaunda chama leo kesho kila mtu anahamia na chama kimekua tayari in a day.

Tz pamoja na kua na changanoto kubwa za kiuchumi bado hizi changamoto hazijafika hatua ya kuleta mapinduzi ya tabaka la utawala kama ilivyokua Zambia 91 na kuingausha UNIP bila wananchi kujali kama MMD ni mbadala mzuri wa UNIP au la.
Kwa kifupi kwa sasa Tz haina mazingira yeyote ya kijamii, kisiasa, kiuchumi ya kuleta upinzani mahiri utakaoipa changamoto CCM changuzi za 2015, 2020 na kuendelea.
 
haya yote yameifanya kambi ya Upinzani kua na sera nzuri kwenye makaratsi lakini kua dhaifu na kuchochea na kuhamasisha viongozi dhaifu pia wenye ubinafsi na tamaa tu ya ukubwa na madaraka bila ya umakini wa hali ya juu wa kukuza demokrasia zake za ndani ili kuvutia zaidi wasomi na watu wengine na kujenga matumaini na kujiamini kwa asasi za kijamii na zenyewe zisukume mbele gurudumu la mabadiliko.

mbowe leo anachukua pesa, zzk magari ya wale wanaowapinga kwa nguvu zote na kuwaita mafisadi na kuweka nguvu yao ya kimatinki ya filosofia ya uchaguzi kuwapinga hao watu na mfumo wao..

sasa utamshawishi vipi mtu kama Mharakati aache kazi zake ajitolee kuimarisha upinzani either kwenye asasi za kijamii, or direct kwenye chama chenyewe na viongozi shallow namna hii? Kila mtu bora abaki pale pale alipo hadi muda muafaka utakapofika, mabadiliko hayaletwi toka juu, ni kutoka chini na viongozi wa hayo mabadiliko watapatikana tu pindi yakianza.
 
Mzee Mwanakijiji,

Tatizo sio vyama bali ni watu, tatizo ni Watanzania ambao wengi ni wababaishaji, wezi, mafisadi.

Tunayoyasema hapa JF hatuyaamini kabisa.

Kama kuna watu wanataka kuleta mabadiliko, tayari tuna vyama vingi, ingieni kwenye hivyo vyama na anzeni mapambano kuanzia chini.
na hayo mapambano ukiyaanzisha ndiyo yanakupata ya liyowapata akina ZZK na wenzake
 
Back
Top Bottom