Tunahitaji chama kipya?

in CDM we trust... chama kina nguvu, mvuto, pendwa na kipo tayar kuwapigania watz. chama kimeibua maovu mengi ndani ya serikali yako, watz wengi wamepevuka kifikra na hawapo tayar kuendelea kuburuzwa na maccccm.

CDM ni chama sahihi kama unataka anzisha chako anzisha tu wote mliovuliwa magamba na wasaliti ndo mtakuwa member
 
mabadiliko hayataletwa na vyama au mtu mmoja mmoja, bali yataletwa na wananchi masikini ambao wamenyonywa kwa muda mrefu, wakiungana, na kutambua hali duni inasababishwa na chama dhalimu. Mabadiliko yanaweza kuja hata nje ya chama cha siasa. Wananchi wakiamua. itakuwa.
 
Mtu yeyote anayeweza kuilinganidha CCM iliyokaa madarakani miaka 52 sasa na vyama vingine vya upinzani( Chadema ikiwamo), kama sio MWENDAWAZIMU basi atakuwa ni KICHAA au bac atakuwa MwanaCCM anayetafuta huruma kutoka kwa watanzania kwa chama chake kwa kuchafua vyama vingine!

Mwanakijiji ni wazi ana wivu na hatua waliyopiga Chadema,kwa hiyo ameona ni bora "Tukose wote!"

Kwani mwanakijiji mwanasiasa? kwani mwanakijiji ni mdau wa CCM hata aone bora wakose wote? mbona ni wazito sana kukubali kusikia tusichokipenda? kwa tabia hii ya ushabiki wa kijahilia ndio maana chadema inafanana na ccm,,,na kwa hivyo kuna haja ya kuzaliwa chama chengine.
 
Tatizo kuu la mwenendo usiotia matumaini ndani ya vyama hivi likowapi hasa? Je, tiba itakayoleta ahueni kwa raia wa Tanzania ni ipi? Hapa ndipo inapoanzaia njia panda baina yashule ya mawazo yangu na ya marafiki zangu.

Tofauti yangu na wengine haijajengwa juuya tofauti ya kimtazamo juu ya taswiratunayoiona ndani ya CHADEMA bali ni juuya namna sahihi ya kushughuliki ugojwa wenyewe. Tofauti ya shule zetu za mawazobaina yangu na watanzania wengine wenye fikra za kimapinduzi ni juu ya tiba stahiki. Baadhi ya wachambuzi mahili akiwemo Dr Kitilla wanatoa suluhisho latatizo la kimfumo kwa kuunda aina nyingine ya chama kiteule ndani ya jamiiileile iliyolewa kwa mvinyo wa kimfumo.


Wnatoa tiba ya kuwa nachama mbadala ndani ya mfumo unaorutubishwa na kurutubika kutokana na Elimuisiyohandisi raia wavumilivu ndani ya mawimbi ya fikra kinzani. Mfumo wenye raia wepesi kustahimili dhoruba namikiki-mikiki ya hoja mbadala. Naam, wanaofura kama vifutu pale maono yaoyanapotupwa jalalani mithili ya takataka kwamba ni ya ovyo au yana mashiko.Katika hili, Wao anataka tuaminikuwa iwapo tutanunua viriba kipya, kwa maana ya chama kipya, na kisha kutiamvinyo uleule wa zamani uliochacha, kiriba hicho kitaweza kujifanyia muujiza wakugeuza mvinyo ulioharibika na kuwa divai mpya! Tiba hiyo ni ya kimuujizaZaidi. Tiba inayohitaji kiasi fulani cha uwendawazimu kuweza kuisapoti kwakuipigia makofi, vifijo na nderemo!

Wakati taswira ya kisiasa ndani ya CHADEMAinaaksi mfumo unaotamalaki kitaifa. Mfumo wa ubinafsi na kutovumilia mawazombadala, hali ambayo hata Dr kitilla na wachambuzi wengine amekiri wazi kwamba chimbuko lake ni mfumowetu wa Elimu butu, usiojali uwekevu wa maono mapevu, Kitila anatoa suluhishombadala lenye ukweli na upogo kwa mbali; Wanapendekeza ianzishwe midahalomashuleni ili kusaidia kuhandisi jamii ya watanzania wenye kushindana kwa nguvuza hoja. Sipingani na hoja hiyo. Hata hivyo naomba wabatizwe ndani ya ukweli huuwa ziada ili kushibisha hoja yao. Tatizo kubwa la wapinzani wa fikra za mabadiliko chaya ni la kimaadiliZaidi kwa maana ya kusukumwa na tabia ya ubinafsi.

Midahalo, kwa sehemu kubwa, inawapa wasomiuwezo wa kujenga na kupangua hoja.Midahalo haiwezi kufanikisha zoezi lakufinyanga jamii ya watu waadilifu hata kama watapewa fursa ya kudahalika tanguasubuhi hadi jioni. Katika hili, Dr Kitilla anapaswa kusimama kizimbani ili kujibu maswaliyaliyostawishwa kwa mboji ya ushawishi wake wenye naksi ya uhalisia wa mambo. Je,kwa vile gonjwa la CHADEMA na vyama vingine chimbuko lake ni la kimaadili kwa maana yakuhandisiwa kimfumo, ni mikakati gani itatumika, ili kupata krimu ya wanachama wa sampuli isiyona virusi vya mfumo uliowahandisi? Je, chama hicho cha kufikirika kitaanzishaviwanda vya kuhandisi sampuli hiyo wapi? Je, ni mwezini kusikofikiwa na virusi hivi vya kimfumo? Bahati mbayahuko hakuna wanadamu! Je, ni kinga gani itakizuia kisikabiliwe na mkwamo wakiburi cha mafanikio kama ilivyo kwa vyama hivi viwili? Tuseme, na hata kamakingefanikisha mpango huo, bado chama hicho kitapaswa kufanya kazi ndani yajamii ileile, iliyonajisika kimfumo.

Kwa vile tatizo ni la kimfumo,Je, ipi ni njia ndefu na yenye gharama kubwa kuliko nyingine kati ya hizimbili. Njia ya kwanza: Kuendelea na mapambano dhidi ya virusi vya kimfumo ndaniya CHADEMA na pembezoni mwake. Njia ya pili: Kuanzisha Chama kipya ndani yajamii ileile yenye mfumo butu. Wakati tathimini ya haraka ya Kitilla ni kwambaili kulifikia lengo kusudiwa njia ya pili inaweza kutumia miaka ishirini Je, haoni kuwa iwapo watanzania watapewa Elimustahiki, njia ya pili inaweza kuchukua muda michache Zaidi?

Kwa maoni yangu,naliona tatizo la itifaki ya ujenzi wa hoja za Dr kitilla juu ya tiba ya tatizola vyama hivi viwili vya siasa. Akiwa kama mjenzi wa hoja za kisomi, muktadhawa makala zake umeibua wazolinalikinzana na kile anachokijengeaulinzi kwa wigo wa dhahabu, yaani ujenzi wa jamii yenye nidhamu na fikra huru.Tiba ya matatizo ya kimfumo yapaswa kufanyika ndani ya mfumo huohuo na sio nje.Chumvi bora yapaswa kuwekwa ndani ya chakula na wala sio pembezoni. Wapambanaji wa kweliwasiishiwe pumzi. Waendelee kuuelimisha umma wa watanzania ili wajue kufanyamaamuzi stahiki na wala si kuwashawishi kuanzisha utitiri wa vyama. Tafakari.

Joshua Lawrence niMchambuzi wa masuala ya kitheolojia na kijamii, na mtafiti wa tiba mbadala na mwanachama wa jukwaa la jamii, mawasiliano drjoshualawrence.blogspot.com
 
uko sahihi,,,kunahitajika chama.
Yes yes tunahitaji Chama kipya Kama anayoandika Dr kitila katika gazeti la Raia Mwema.


Hicho Chama mwenyekiti wake awe ZITTO, Makamu awe Rashid HAMADA, Katibu MKUU awe KITILA, naibu Katibu mkuu awe KAFULILA, kitakuwa SUPA Maana wataridhika na KUtuletea maisha BORA, VIVAAA mafisadi!!!!!!
 
Yes MM tunahitaji chama kipya tatizo ni kwamba vyama vipya vinavyopatikana vinaongozwa na masalia yaleyale kutoka vyama tusivyovitaka
 
Ishu sio chama kipya,ishu ni watu waliodhamiria,mi bado ninaamini katika chadema,haifanyi vibaya sana,inapita katika magumu ambayo ni kawaida katika maisha ya kiumbe hai au hata jumuia yoyote ile.leo tunawasifu wamarekani,ila hatujui shida walizopata mpaka kufika hapo leo. Magumu humfanya mtu ajifunze na kuimarika
 
Nasubiri kwa hamu kusoma mawazo ya Mkumbo;
Nionavyo mimi tatizo si chama; tatizo ni watu - watu ambao ni matokeo ya jamii iliyowatengeneza hao watu
SIAMINI kabisa kwamba kikundi kidogo cha watu kinaweza kuyumbisha jamii nzima (kama ilivyo sasa) bila jamii yenyewe kukubali kuyumbishwa (kwa kujua au kutokujua / hiari au kulazimishwa).
Kuna mdau aligusia kuhusu "kusubiri tu hadi watu wachoke"... Nadhani watu washachoka siku nyingi tu! Tatizo ni ukweli kwamba - BADO TUNA mtizamo hasi wa KUTEGEMEA mtu au watu wengine kututafutia na kutupatia ufumbuzi wa matatizo yetu! WaTz tulio wengi, tunapenda - na imekuwa ni tabia sasa; kujiona kama hatuna uwezo wa kujitatulia matatizo - hadi msaada utoke nje ya sisi wenyewe. Utegemezi huu (dependency); umejikita ndani sana ya chembechembe za jamii yetu kiasi tumefika mahali hata hatuwezi tena (na wala tulio wengi hatujui tena namna ya "kufikiria" namna ya kutatua matatizo yetu.
NI katika mazingira haya ambapo viongozi "Muflisi wa mawazo chanya" wanapo chukua nafasi na kutuburuza wanavyotaka - na kisha kikiuma sana tunalalamika!
Tunahitaji chama kipya? ... Nadhani tunachohitaji ni "Udhihirisho" watu wenye mawazo, mtizamo na utendaji mpya! Ninaamini kabisa; Watu hawa wapo! Lakini sina uhakika kama wanaweza kudhihirika katika mazingira tuliyonayo sasa!
Natamani sana iwapo jamii yetu ingetoa nafasi kwa watu hawa kusikika! - Hawawezi kusikika kwenye mfumo wa vyama uliopo! waliopo huko WATAHAKIKISHA watu hawa hawasikiki! Watapigwa vita na kupachikwa majina mabaya mabaya... mradi tu waonekane wabaya kwenye macho ya jamii!
Ili tupone kama taifa; ni lazima jamii yenyewe ifike mahali IKATAE kudanganywa na wajanja wachache walioshika mipini kwenye vyama vya siasa! Ni lazima jamii iamue kuwatambua, kuwalea na kuwalinda "wachache" wanaodhihirisha "UZALENDO" wa kweli! Wachache ambao wamedhihirisha kutetea ZAIDI maslahi yetu kama TAIFA /Jamii, kuliko maslahi yao wenyewe. Wachache ambao hawajali sana kuvuliwa cheo katika chama - kuliko kuona hoja yenye faida kwa taifa na jamii nzima inatekwa na kubadilishwa "rangi" na wahuni wachache wanaotafuta kulinda maslahi binafsi na ya kikundi chao.
TUnaa nza je kufanya hili?
1. Tuanze kwa kutambua ukweli na uhalisia wa tulipo sasa! - HATUPO mahali pazuri! Tulipo sasa kama jamii SIO PETU! TUmefikishwa hapa na wahuni wachache - ambao wanafanya kila linalowezekana tuendelee kukubali kuwepo hapa tulipo (hata kama ni kwa kudanganyiwa pipi na kashata)!
2. Tukubali ukweli kwamba HATUWEZI kutoka hapa tulipo kwa msaada wa mtu YEYOTE zaidi ya SISI WENYEWE kutaka na kuchukua hatua kuleta mabadiliko tunayoyataka - kwa njia zinazokubalika kwenye jamii yetu!
3. Tutambue ukweli kwamba kila mmoja wetu ana KILA SABABU, ana Uwezo, na inampasa kuonyesha wazi NIA ya dhati katika kudai na kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii yetu!

Mabadiliko ya kweli yanaanza na mtu binafsi...na wala mwanzo wa mabadiliko hayo hautegemei wingi wa wanaokuunga mkono! - tukilijua na kuamini hilo; tutakuwa tumeanza kuchukua hatua!

Cheers
 
  • Mkumbo amekuwa katika siasa za upinzani zaidi ya miaka 10 lakini ameshindwa kueneza chama wilaya ya Iramba achilia mbali mkoa wa Singida!
  • Zitto amekuwa kwenye siasa tangu akiwa na miaka 16 kama anavyosema yeye lakini ameshindwa kusimika chama chake mkoani Kigoma!

Leo wanakuja na ngojera za kuanzisha chama, huu ni upuuzi na kiwango cha mwisho cha usaliti! Wamewauliza waliojaribu kuanzisha CCJ, CCK na ADC?

Mwisho tutakuja kujua hizi fedha za kuchezea wanazitoa wapi? Lakini anayewapa hizo fedha naye ana akili timamu? Au ni zile tunazoambiwa za pembe za ndovu?
 
mkuu wana haki kikatiba, ila inatakiwa tu watimize mashariti... halafu unapotoa maada ujaribu kupunguza jazba...na chuki binafsi...kwa sababu kwa katiba ya nchi hata wewe una haki ya kuanzisha chama haihitaji uwe na hela...
 
CHADEMA INAKUFA, By Dr Kitila Mkumbo
Katika Makala Alioipost Jana Yenye Kichwa cha Habari'CCM is Stabilising, Chadema is Shrinking and CUF is Disappearing, Dr Kitila Mkumbo (Hon and Senior Lecture UDSM) Amesema Licha ya Chadema Kukubalika sana Mitaani na Kuwa na Mashabiki wengi LAKINI Chadema Haipati Kura za Kutosha Katika Chaguzi Kwa Sababu Kuu Nne:

1. Chadema Imeonekana Sio Mbadala Sahihi wa CCM (Chadema is not Credible Alternative of CCM).Licha ya Kwamba Chadema Imefanikiwa Kuweka wazi MABAYA ya CCM kwa Watanzania Lakini Imeshindwa Kuwashawishi Watu ya Kwamba wao ni Mbadala wa CCM.Dr Kitila Akaenda Mbali na Kusema ni Heri Kutawaliwa na Wakoloni Weusi (CCM) Kuliko Wakoloni WEKUNDU (Chadema) Maana hawa ni Zaidi ya Kudandia Meli ya Kigiriki.

2. Viongozi wa Chadema ni MAFISADI,Waroho wa Pesa na Viongozi Wenye Njaa Kali Kuliko Viongoozi wa CCM.Dr Kitila Amesema Viongozi wa Chadema Wanapenda Sana Posho Kuliko Viongozi wa CCM,Wanapenda Kutembelea Magari ya Kifahari sana Kuliko Viongozi wa CCM, Wanapenda Sana Safari za nje ya Nchi Ndio Maana Kila Siku Utasikia Freeman Mbowe na Mke wake Wameenda Kutalii Marekan,Dubai..kwa Pesa za Serikali.Kwa sababu hizo imekuwa ngumu kutofautisha Viongozi wa Chadema na wa CCM…

3. Chadema Hawataki KUKOSOLEWA na wala hawataki KUJILEKEBISHA:Dr Kitila Amesema,Ukiikosoa Chadema Hata Kama Unachokisema ni Kweli,Hawachelewi Kukuita wew ni MSALITI,Pandikizi la CCM,Umetumwa……na Mambo mengine ya Kiuchonganishi ili Wakuchafue Kisiasa.Hii ni Hatari sana kwa Chama Kichanga chenye Dhamila ya Kushika Dolla

4. Mpasuko ndani ya Chadema:Dr Kitila Anasema,Viongozi wa Chadema Wametumia Muda mwingi wa kampeni kumchafua Zitto Kabwe na sio kuwanadi wagombea wao.Dr Kitila Amesema,Kitendo cha Chadema Kumtangaza Zitto Kabwe kama Muhaini wa Chadema na ili Hali wananchi wanajua Mchango wa Zitto katika mafanikio ya Chadema,Wananchi wamepoteza Imani kabisa na Chadema na Hawakitaki tena.

Dr Kitila Ameongezea kwamba:
Ni Bora Tuendelee Kutawaliwa na CCM Ambao Wanang'ata na Kupuliza Kuliko Hawa Viongozi wa Chadema Ambao wananjaa ya Kufa Mnyama.Hawa Wanaweza Kuiba Mpaka Tukaingia kwenye Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe.
Dr Kitila Amemalizia kwa Kusem'Chama cha Upinzani Imara Bado Hakijazaliwa (A credible and Serious Opposition might be in the Offing) Hivyo Watanzania tuendelee kuwa na Subira na Vijana Tuache Kushabikia Chadema kwani Hakuna Chochote cha Ujenzi wa Taifa ndani ya Chadema Zaidi ya UOZO na WIZI....
CHADEMA INAKUFA......Dr Kitila Mkumbo
See Translation
My verdict of the 27 ward by-election results: CCM is stabilising, CHADEMA is shrinking and CUF is disappearing

Dr Kitila Mkumbo
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom