Tuliosoma Shule ya Sekondari Tosamaganga tukutane hapa

Hivi muungano ndio linaitwa mandela?......oooh nimekumbuka,tulibadilisha jina wakati mkuu alipotoka lupango! umenikumbusha mbali sana!
Hiyo mitaa ni muhimu sana,ndiyo mkwawa alipomuua mwanajeshi Zelewisky wa manazi,kwa mikono yake.
 
Tosa bana miaka ile ya 90 nawavulia kofia hawa jamaa, nakumbuka umiseta mlikuwa mnapiga boli hakuna hasa mkikutana na highlands dahhh eeh kuna huyo jamaa miaka ile wakimuita MARADONA alikuwa sooo, alitupiga bao nikiwa Ruaha Sec O level wakati ule halafu anawaambia poleni jamani hahahahha Tosaaa walitukanyaga mbao nne si mchezo

Unamkumbuka na John Vicent? Nilikuwa Kiungo mshabuliaji kama unakumbuka niliumia kwenye mechi na Lugalo
 
Ulimnofu wela! kwi kwi kwi

Hata bila kusema hivo mimi nilihisi kitu kama hicho ulichokisema hapo juu, kitu kingine ni hiyo avata yako yani kama tule tuzee twa mafinga sasa hakana koti alafu ni mwezi wa sita, Heshima kwako kaka, Makasi bwana!
 
Naona mnaongelea mambo ya Msiwasi Footbal Ground si mchezo bonge la uwanja si ndio? ila ole wako uchelewe kurudi pale Banavanu usiku noma, teh teh teh
 
Eee bwana eeeh Rados yuko wapi? Kuna siku alikuwa hafungiki....Lipuli enzi hizo walimtaka
Mara ya mwisho nilionana naye Dar,alikuwa India nadhani wakapigana kwenye mechi akaambiwa arudi bongo,
Nilikuwa SUA na kina sempeho,crispus madeje......
 
Mara ya mwisho nilionana naye Dar,alikuwa India nadhani wakapigana kwenye mechi akaambiwa arudi bongo,
Nilikuwa SUA na kina sempeho,crispus madeje......

Sifa kubwa ya hao jamaa ni ulevi na uzinzi!
 
Tosamaganga [todza maganga] kweli ni academic hill. Mtu anaweza soma boarding toka chekechea hadi form six akicheza hapo hapo kilimani. Chekechea hadi la saba, anasoma Lyalamo P/S. Form I-VI, Tosa Sec aka Tosa boys aka Iringa boys.

Mchungaji wewe uliishi bweni gani?
 
Inanikumbusha mbali sana, wadau mliopitia hapo mpooooo!

View attachment 31724

Duh!! Mkuu, yaani unatukumbusha mbali sana. Tosa hill!!!

Kwa karibu napaona East London, halafu kuna paa za jengo la masista, na kwa mbali paa ya bweni la Mandela na la PCM block.

For us to forget Tosa is lthe same as Okwonko to forget Umuofia.
 
Aisee mmenikumbusha mbali sana,enzi za dudu aka mpogole,alipotimuliwa alikuja headmaster msukuma aitwaye Mbanga.
Second master Mwavika sijui yuko wapi siku hizi?
Enzi za half mile na quota mile.Duh enzi zile
 
Hivi muungano ndio linaitwa mandela?......oooh nimekumbuka,tulibadilisha jina wakati mkuu alipotoka lupango! umenikumbusha mbali sana!
Hiyo mitaa ni muhimu sana,ndiyo mkwawa alipomuua mwanajeshi Zelewisky wa manazi,kwa mikono yake.

Acha kudanganya watu hapo penye nyekundu.

Kwanza Mkwawa hakumuua Zelewisky aka Nyundo kwa mikono yake, bali aliuliwa na majeshi ya Mkwawa.

Pili, Nyundo aliuliwa eneo la Lundamatwe karibu Ilula (mpaka leo mnara wa kaburi lake upo just about 20 mts away from Moro-Irg road). Lundamatwe kuna umbali mkubwa sana hadi Tosa.

Tatu, mapigano yaliyohusisha mlima huo (kabla haujaitwa Tosamaganga) kati ya Mkwawa na wajerumani siyo zamu hiyo aliyokuwepo Nyundo.

Naweka sawa tu, tuendelee na mada.
 
shule yetu tosa, maganga ipo kilimani mazingira bora wapi mzee malata nice skuli hasa kipindi cha migomo
 
Tosa boys sio wapiga gitaa kama wa Pugu na Minaki.

Tosa huwezi kuifaidi kama
~hujaenda shambani na bustanini Idete
~hujatembea kwa mguu toka Tosa hill hadi Junction kwa miguu
~hujaenda kwa masista kununua "bans"
~hujaenda Msiwasi ground
~hujaenda half mile, the most luxurious place ever in the hill
~hujaenda power station hadi Ipamba

Kakuruvi, hebu ongezea ktk list.
 
Du nimejaribu kujikaza Kimbunju wapi Bwana.

Na mimi ni Alumina wa Tosamaganga miaka 26 iliyopita.

Bweni langu Muungano, Cabin yetu iko pale juu kabisa kulia.


Enzi zetu ni zile akina Mawe Matatu Naibu Waziri Charles Kitwanga alikuwa Kilanja mkuu lakini usiku kwenye kuchoma mahindi tuliyomwibia Dudu tulikuwa wote. Hii hiii hiiiiii!

Form one Mahindi mmetoa wapi??

Wewe kula usilete Unyoka hapa! Hiiii Hiii! hiii1
 
Mi nimetoka pale 2004 nilikaa mandela 86 nafurahi kuonana na kaka zngu humi. Mnakumbuka mabanzi ya kwa masista makubwa ukipiga na piriton aka uji full usingizi, kaka ametaja lyalamo ps lakini ipo home boys kwa watoto wa kiume wako chini ya mabrother. Vyuo vya ufundi kibao kama scim bros nice to remember nilipiga pcb,
 
Du nimejaribu kujikaza Kimbunju wapi Bwana.Na mimi ni Alumina wa Tosamaganga miaka 26 iliyopita.Bweni langu Muungano, Cabin yetu iko pale juu kabisa kulia.Enzi zetu ni zile akina Mawe Matatu Naibu Waziri Charles Kitwanga alikuwa Kilanja mkuu lakini usiku kwenye kuchoma mahindi tuliyomwibia Dudu tulikuwa wote. Hii hiii hiiiiii!Form one Mahindi mmetoa wapi??Wewe kula usilete Unyoka hapa! Hiiii Hiii! hiii1
Mkuu, unakumbuka zama za kuchemsha mahindi kwa heater ambayo ni vijiko? Utafikiri unafanya electrolysis process. Wakati mtambo unaunguruma, mnamweka mlinzi kupiga chabo kama kuna noma. Mkiambiwa kuna Mwalimu,within a min, mtambo unapandishwa darini,ndoo, sufuria na ninyi wenye kwa dari. Uko darini kuna vumbi, ila marufuku kukohoa wala kupiga chafya. Kama mapaka shume mnatulia.
 
Kwa picha bora za Tosamaganga Hill, shukrani nyingi sana zimwendee Mwl Mlwale. Kakuruvi, unamkumbuka huyu teacher also photographer?

Palikuwa na teacher mmoja wa Bios anaitwa Mrisho, chapombe huyo. Mnamtoa kilabuni anakuja darasani kufundisha yuko mwake. Anaegemea ubao, mkono mmoja anachaki, mzee anamwagashule. Mkitaka ahudhurie mara nyingi basi msisahau kumwandalia gongo aka moshi.
 
Mkuu Kakaruvi,

Asante kwa Kunikumbusha juu ya Tosa Hill, binafsi nakumbuka yafuatayo:

* Nilikuwa pale toka 1988 hadi 1990,
* Nilikuwa nachukua PCM, darasa langu lilikuwa PCM 3,
* Nilishawahi kutembea mara nyingi sana toka njia panda lami (Tanangozi) hadi Tosamaganga,
* Nakumbuka Dansi lililopigwa pale Iringa Girls (Feb-1990) kwaajili ya kukusanya fedha za kujenga madarasa ya F5 na F6, duu ilikuwa balaa kwani TANCUT Almasi, ndo walitumbuiza pale!
* Nakumbuka Mwl. Pimbi(nick name) huyu alikuwa Mwl wa O-level, na alikuwa mnoko mno hasa kwa A-level,
* Nakumbuka pia CONSTANT (fimbo sita), ulikuwa ukiambiwa constant basi ujue ni bakora sita!
* Mwisho, nakumbuka Quarter Mile na Half Mile.
* Headmaster Dudu Mpogole(RIP), alitisha kama Ukoma!!
 
Back
Top Bottom