Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

i1369_jimmycarter.jpg

Nyerere na Carter

i1370_fidelnyerere.jpg

Nyerere na Fidel​
 
lamba,naomba tusaidiane hapa,katika hiyo commitee ya watu 14,OKELLO yupo,na je,yeye ndio aliyoleta mapinduzi? maana frankly speaking historia ya mapinduzi,inatuchanganya,kuna versions nyingi,inasemekana historia ya mapinduzi imekuwa doctered sana-anyone out there who can give us a clear cut story.As neighbours,nimewahi kumuuliza NATEPE,but i got out none the wiser
 
Duh!! Babu mbona unataka kuvuruga thread ya watu? Ushaanza kukosa ustaarabu eh!!!

Yaani huoni kama hizi picha ni nuksi tupu ,hata ukitazama kwa kina utaona haziendani na hii Jamii forum inabidi ulete tambala lile lililokuwa linatumika na zile senema za bure akina Omo na Fakcho ,si mnazikumbuka ,wakituletea filamu kwenye viwanja vya mpira.
hawa ndio waliokuwa wakihimiza siasa za ujamaa na kujitegemea ,hebu angalia Madini ya Shinyanga yalianza kuchimbwa lini ,ni wakati huo huo wa siasa zao.

Kama kukumbukwa basi tukumbusheni mengi na ya kukumbuka sio picha hizi ambazo sasa zinaelekea kurithishana makampuni . Vizazi vya hawa ndivyo hivi hivi vinavyofanya biashala Ikulu ,watu hawa na siasa zao ni walemavu wa kuendeleza wananchi walio wengi ,hawa ni watu wa kusemwa na kupingwa kila kukicha ,mambo ya kuwakumbuka wayapeleke kwenye Chama chao ambacho kilitangaza kushika hatamu za Dola ,hivi wamejimilikisha kila kitu kwa faida ya nani kama sio yao yenye maslahi binafsi ila sasa tunaona akina Butiku wameanza kukana na kukanwa hii ni dalili mbaya sana.

Mwananchi anaekumbuka watu hawa bila ya shaka yeyote akiyapima maisha yake leo hii ataona ukweli kuwa hawa mnaoonyesha mapicha yao ndio walioidumaza Tanzania.

Tanzania ilipata uhuru ikiwa bado Bikira ,tofauti na akina Zimbwambwe,na wengineo ,hawa wangekuwa na uelewa maana ya kugombea Uhuru leo hii tungekuwepo mbali na maisha ya kutafutana na mlo wa siku.

Kila kukicha wanasifiwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani ,kumbe amani yenyewe ni moto unaowaka kwenye majivu ,wameitafuna Tanzania miaka 44 sasa yameanza kubaki mashimo ,wakati hao mnaowatazama wamishakufa na walio hai wanakimbiza vijisenti wanahama nchi na wengine ndio hao wanaenda kufia Ulaya na hazina na mahesabu yake hayajulikani yamepotea potea vipi ,wanasema eti fedha na mahesabu yapo katika hali ya kutatanisha toka Balali yupo hapa mpaka amepata ugonjwa mpaka wengine wanasema hajakufa na wengine amekufa ,mwisho serikali ya hawa mnaoonyesha picha zao ,haijui wafanye nini ? Hao ni CCM na waliopo ni CCM mnawakumbuka kwa misingi ipi ya uongozi na ufundishaji upi wa Uongozi tunao uona leo hii ,mwizi kusafishwa tena bungeni ,kama si aibu ni kitu gani kwao ?

Halafu mnaleta mapicha ya maiti eti tukumbuke ? hivi mkisikia kulogwa ,jamani si ndio huku ? baada ya kuzungumza mambu ya maana na maisha haya ambayo yanayokwenda na kupanda kwa kasi ya Kikwete ,mnaleta picha sasa niwaulize hivi mnafaidika na kitu gani na picha hizo wakati mpo kwenye ziki za kimaisha ? Au ndio mnajiliwaza ? Sasa kujiliwaza mngetafuta angalau mapicha mazuri yanayoburudisha moyo lakini si picha za waliotuzamisha ,mpo ?
Upinzani hauwezi kwenda mbele kwa kutazama picha za watawala au Chama cha walioko madarakani au waliokufa.
Tuna msemo wa kiswahili usemao samaki akioza mmoja ndio wameoza wote.CCM wameoza wote waliokufa na hawa waliokuwepo hai ndio usiseme ni harufu mbaya tupu.
 
Mwiba,
You are entitled to your opinion. Na sisi tuliosoma na kunufaika enzi za ujamaa ngoja na sisi tujikumbushe tumetoka wapi. Anayesahau historia yake hatajifunza hata kutokana na makosa ya historia hiyo. Kila binadamu ni mfu mtarajiwa. Nadhani tumeelewana.
 
Mtu anjikumbusha baada ya dhiki sio unajikumbusha wakati unaburuzwa kwenye dhiki angalau kumbukumbu zako ikiwa zitakusaidia kujinasua katika dhiki na kukupeleka katika maisha bora.matumaini ambayo yalijengwa katika harakati za hawa MaCCM ,...maisha bora kwa kila Mtanzania....ni miaka inakatika ,sasa wanatubabaisha kwa kutuletea makampuni ya simu ambayo yanakaribia kuweka simu bure kwa jinsi mirija yao inavyofanya kazi ,sifa za mashirika ya simu ya Tanzania hayapatikani duniani kokote kule isipokuwa hapa eti mnara umeanguka !
 
Kama mwenzangu uliona dhiki pole sana. Ndio maana nimesema you are entitled to your opinion. Na sisi wengine ambao hatukuona dhiki tuachie nafasi yetu ya kujikumbusha tulikotoka. It is that simple.
 
Kama mwenzangu uliona dhiki pole sana. Ndio maana nimesema you are entitled to your opinion. Na sisi wengine ambao hatukuona dhiki tuachie nafasi yetu ya kujikumbusha tulikotoka. It is that simple.

Sio hivyo,ikiwa wewe umetosheka na kuona wengine si lolote si chochote basi utakuwa hunatofauti na wao zaidi ni mbinafsi na hapo ndipo unapokuta unapata uongozi na kuzidi kuendeleza ubinfsi kwa maslahi yako binafsi,ndipo ikaambiwa haifai kuna kiongozi halafu ukajilimbikizia mimali na mivyeo ,wakati vyeo hivyo vingeweza kugaiwa kwa waTz wengine.
Mnaunda kamati , ajira hizi zingeweza kuenezwa kwa wasomi ambao wapo na shahada za kuifanya kazi hiyo tena kielimu kabisa ,lakini kwa vile kama ulivyosema mnajikumbusha ,kuwakumbuka hao ikiwa unafaidika na mambo yao la ikiwa huna faidai utakuwa sawa na wale wanaokaribia na kupiga kura kupeleka kura zao huko ,ukiwauliza wanakuja na jawabu kama lako, CCM ndio baba CCM ndio mama ,kasumba zimewajaa ,CCM ndio ilipeka watu kwenye mashamba na kuliwa na simba ,eti vijiji vya ujamaa kumbe ni mikakati ya kupunguza watu.
 
nyerere.jpg
Karume.jpg

Nyerere and Karume
Okello.jpg

Okello

Unification 1964

*United Republic of Tanzania formed 1964
*Julius Nyerere President
*Karume one of two vice presidents
*Zanzibar retained considerable autonomy, source of tensions in Tanzania in later years
 
Mkuu Icadon,

Heshima mbele bro, duh tuendelee kuweka vitu hapa maana so far tunakula elimu safi na ya bure, Ashante sana mkuu,

Mkuu Jasusi,

Please, acha kupoteza muda wako, maana ukiona bin-adam anapigana na picha zisizosema, basi utajua ni kwa nini tuna matatizo kwenye muungano! Sio kwamba hatujamuona na hiyo crying yake for attention, ila tumemdharau,

Najua kuwa unazo picha nyingi za kumbu kumbu, please weka picha hapa achana na kelele za mlango!

Mkuu Invisible,

Ahsante kwa marekebisho naomba uipitie hii topic mara kwa mara kurekebisha picha na maneno yasiyokuwa sawia kuambatana na hizi picha, za viongozi wetu mashuhuri waliotuwekea msingi wa taifa hili, ambalo some of us we are proud citizens wake.
 
Sio hivyo,ikiwa wewe umetosheka na kuona wengine si lolote si chochote basi utakuwa hunatofauti na wao zaidi ni mbinafsi na hapo ndipo unapokuta unapata uongozi na kuzidi kuendeleza ubinfsi kwa maslahi yako binafsi,ndipo ikaambiwa haifai kuna kiongozi halafu ukajilimbikizia mimali na mivyeo ,wakati vyeo hivyo vingeweza kugaiwa kwa waTz wengine.
Mnaunda kamati , ajira hizi zingeweza kuenezwa kwa wasomi ambao wapo na shahada za kuifanya kazi hiyo tena kielimu kabisa ,lakini kwa vile kama ulivyosema mnajikumbusha ,kuwakumbuka hao ikiwa unafaidika na mambo yao la ikiwa huna faidai utakuwa sawa na wale wanaokaribia na kupiga kura kupeleka kura zao huko ,ukiwauliza wanakuja na jawabu kama lako, CCM ndio baba CCM ndio mama ,kasumba zimewajaa ,CCM ndio ilipeka watu kwenye mashamba na kuliwa na simba ,eti vijiji vya ujamaa kumbe ni mikakati ya kupunguza watu.
Mwiba,
Naona hujanielewa ndugu yangu. Sijaifagilia CCM ya sasa hata kidogo. Nilichosema ni kwamba kukumbushana historia ya tulikotokea ni jambo muhimu na viongozi waliotutangulia. Mwalimu amefariki bila kujilimbikizia mali licha ya kwamba amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 24. Natamani viongozi wa sasa wa CCM wangeiga mfano wake lakini wanasema alishapitwa na wakati. Na hili la watu kuliwa na simba mashambani nimelisikia mara ya kwanza hapa JF lakini hakuna hata mmoja amewahi kuja na uthibitisho. Mimi ndugu zangu, wajomba zangu walihamia mashamba ya ujamaa. Kulikuwa na mazuri yake na mabaya pia. Ndio maana nimesema tukijivika baibui kuhusu historia yetu, mema na mabaya, tunaweza kujikuta tunarudia yale yale. Mimi siifagilii CCM hata kidogo. Ukiangalia mabandiko yangu utalitambua hilo. Niliacha kuwa memba wa CCM baada ya ndugu zangu wa leo kuwachana na itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Walipokwenda Zanzibar mimi nikaingia msituni.
 
LOL! Kumbe enzi hizo Malecela kuna wakati alikuwa anamshikia Mwalimu kifimbo chake? Imenifurahisha sana picha hiyo.

Mkuu Bubu,

Heshima mbele, fimbo ya Mwalimu ilikuwa fupi sio ndefu kama hii ya Malecela,

enzi hizo ilikuwa ni fashion na politically correct kwa kila mwanamapinduzi kiongozi wa Afrika, kushika Fimbo ikiwa ni alama ya kumuiga Nabii Musa na ile Fimbo aliyokuwa akiitumia kuchungia Kondoo, ambayo baadaye Mungu alimuelekeza kuitumia kuwaokoa wana wa Israel kutoka utumwani Misri.

Viongozi wote wa Afrika enzi hizo walikuwa na Fimbo, kuanzia kina Sekou-Toure, Kawawa, Kambona, Mobuttu, Mwalimu, Nasser, Kayibanda, Karekou, Kenyatta, Malecela, Banda, Kaunda (ambaye baadaye alibadili na kuanza kushika kitambaa cheupe), Nkurmah, Tafawa Balewa, Lummumba, Micombero, Nimeiri, Siad Barre, Bongo, Sengor, Ngwabi, hawa wote ni viongozi waliokuwa na hiyo tabia ya kushika Fimbo.

Ahsante Mkuu!
 
FMES,
Kenyatta hakuwa na fimbo peke yake. Alikuwa pia na ule mkia wa ng'ombe uliosukwa kwenye fimbo. Wenyewe wanaita whisk. Ningekuwa na hiyo picha nigeiweka hapa.
 
Mkuu Jasusi,

Hakuna wasi wasi mkuu, zipo picha nyingi sana zinakuja hapa, zote zitawekwa hapa, wakuu wengine leteni picha jamani pia natoa hongera za dhati kwa wakuu Kichuguu na hasa mkulu wangu Icadon, mkuu ubarikiwe tu maana naona picha safi sana hizi na ni ukumbosho mzuri sana kwa sisi wananchi,

Unajua inafika mahali as a nation mnakuwa hamuelewi mnakokwenda, kama sasa hivi tulivyo kwenye taifa letu, sio vibaya tukijikumbusha tulikotoka,

hotuba ya juzi ya Rais, binafsi imenihakikishia one thing kwamba sasa hivi we are not effective tena kama tulivyokuwa zamani, kumbuka huko nyuma hotuba zake zote muhimu kwa taifa alikuwa ni lazima alalmikie mtandao huu, kwa maneno ya ujanja ujanja ya ku-generelize ".......mambo yanayofanyika kwenye mitandao...." Hii ni mara ya kwanza ametuacha nje, ina maana hatuwakoseshi usingizi tena sasa hivi, sasa ni vyema kujaribu kutafuta mbinu mpya za kupigana ndani ya forum,

Hatutashindwa, tutashinda tu lakini sometimes ni vyema kukubali ukweli na kujiangalia na kujipanga upya!
 
Nyingine ambayo huwa naiangalia sana ni pale Nyerere alipotembea kwa mguu kutoka Butiama hadi Mwanza ati akiwa anaunga mkono Azimio la Arusha. Nadhani kuwa haya yalikuwa ni matumizi mabaya kabisa ya mali za umma.

azimio-jpg.2046
 
Attachments

  • azimio.jpg
    azimio.jpg
    34.6 KB · Views: 1,636
lamba,naomba tusaidiane hapa,katika hiyo commitee ya watu 14,OKELLO yupo,na je,yeye ndio aliyoleta mapinduzi? maana frankly speaking historia ya mapinduzi,inatuchanganya,kuna versions nyingi,inasemekana historia ya mapinduzi imekuwa doctered sana-anyone out there who can give us a clear cut story.As neighbours,nimewahi kumuuliza NATEPE,but i got out none the wiser

Son of Alaska,

Pamoja na kutoridhika na uchaguzi uliomweka Shamte madarakani baada ya Zanzibar kupata uhuru mwaka 1963, hakuweza kupatikana mtu huko kisiwani aliyekuwa na ubavu wa kuongoza mapinduzi. Wanaharakati kama Karume, Babu na wengineo ilibidi wakimbilie Tanganyika.

Huko Pemba alikuwepo kijana mkakamavu aliyeitwa John Okelo na aliweza kukusanya vijana na kwa pamoja wakaanza kufanya mikakati ya kuipindua hiyo serikali. Siku ya siku Okelo akiongza kundi hilo waliweza kuivamia Zanzibar na kupora silaha mbalimbali na kuteka sehemu nyeti za serikali ikiwa ni pamoja na kituo cha redio.

John Okelo kama mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi alitangaza hali ya hatari redioni na kumtaka Shamte achinje kwanza familia yake na watu wa karibu naye na kisha ajiue mwenyewe. Wakati wote huu Karume na wenzake walijificha Dar es Salaam, Tanganyika. Ni baada ya mapinduzi kufanikiwa ndipo walioikimbia Zanzibar waliweza kurudi wengi wao wakitumia mitumbwi na ngalawa. Ukweli ulio wazi ni kuwa bila Okelo mapinduzi ya Zanzibar yasingewekana kwa namna ile.

Hata hivyo viongozi wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mwl. Nyerere walipatwa na hofu hivyo kutafuta mbinu za kuhakikisha historia ya Okelo, ambaye hasa alikuwa raia wa Uganda, inafutwa. Alikumbana na mauti Uganda baada ya Idi Amin kutwaa madaraka na Okelo kujitokeza na kujigamba kwa kusema Ma "field marshal" sasa wako wawili nchini Uganda.

Kwa ufupi aliyeitangazia dunia kuwa serikali ya Zanzibar imepinduliwa mwaka 1964 ni Field Marshal John Okelo, Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Zanzibar.
 
Mkuu Icadon,

Nahisi hii ni picha ya Kanali Nyirenda, akiweka Mwenge wa Uhuru Mlima Kilimanjaro, au?

Naikumbuka sana hii picha kutoka Primary School, enzi zile tunapewa mafuta ya kula kwenye kopo kubwa sana na Bulga ya uji, kutoka kwa Mkulu JFK wa USA.
 
Back
Top Bottom