TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Sio siri ngoja niende kwenya mada moja kwa moja.

Huu mtandao una matatizo mengi sana kama yafuatayo:

1. Huduma ya T PESA
Aisee huu mtandao kama utatuma hela siku ya Ijumaa usiku ghafla litokee tatizo wallah utakuja kuhudumiwa siku ya Jumatatu.

Hili tatuzo limenipata juzi hapa Ijumaa tarehe 7 yaani nilitamani kulia wallah.

2. Vifurushi
Hawa majamaa ukitaka uende nao sawa kwenye masuala ya MBs nakushauri tafuta kitambulisho cha chuo.

Aisee yaani GB 5 kwa Tsh 5000 mwezi mzima.

3. Vocha
Asikwambie mtu, TTCL hawana vocha aisee. Jana nimeenda pale Makao Makuu niliulizia vocha ya 500 hakuna wanasema zipo za 1,000.

Aisee ukienda kuulizia madukani yaani muuzaji anaweza akashangaa maana hiyo vocha ya TTCL ndiyo kwanza anaisikia kwako.

Kilichonipata jana
Nilijiapiza nikaonane na Afisa Masoko pale Makao Makuu pale Posta ili nimshauri kitu kimoja tu. Yaani nikafika mapokezi nikaonane na bwana Kindamba lakini nikazuiliwa.

Yule mama wa mapokezi aliongea sana mpaka wakati naondoka nimeinamishwa kichwa chini kwa masikitiko. Maana shida yangu nilitaka kuonana na Afisa Masoko au CEO wao.


Nilitaka niwambie kama vocha mtaani ni ngumu basi katika option ya kununua bando mteja achague alipe upitia T PESA au salio la kawaida.
Kàribuni nyumbani
94138980_10158514837847884_190712722789236736_o.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku ya 6 leo kila nikituma SMS zinagoma kwenda.
Jamani kama Nyumbani Kumechoka mtuambie mapema ili tuhame twende kwenye mitandao mingine.
Hivi CEO wa TTCL huoni hili tatizo?
Waziri wa Mawasiliano nae yupo kimya.

Je kampuni inajukumiwa na wafanyakazi wa TTCL wenyewe?

Timua kazi kampuni nzima kisha fanyeni kuajiri watu wapya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ongea na Chati zaidi kwa gharama nafuu ukiwa na TTCL Corporation #RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1478257View attachment 1478258View attachment 1478259

Sent using Jamii Forums mobile app
Suala LA mbs tu nakubali. Mpo vizuri...kama kwa huduma za toboa na Bandika bandua...mpo vizuri.

Tatizo ni pale napo tuma sms kwenda mtandao mwingine...hapo ndo kimbembe...wakati mwingine naweza kuresend mpaka naamua kuachana na matumizi ya sms. Sijajua mnakwama wapi ttcl
 
Suala LA mbs tu nakubali. Mpo vizuri...kama kwa huduma za toboa na Bandika bandua...mpo vizuri.

Tatizo ni pale napo tuma sms kwenda mtandao mwingine...hapo ndo kimbembe...wakati mwingine naweza kuresend mpaka naamua kuachana na matumizi ya sms. Sijajua mnakwama wapi ttcl
Yani utaRESEND mpaka unajiuliza hivi nimejiunga MBs tupu au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom