The Tanzania Political Chaseboard: Tafsiri ya Mambo Mazito Kisiasa Tukielekea 2015

Huo utaku ni ukosefu wa uwezo wa kuona mbele zaidi juu ya sakata la mgomo wa Madaktari; eneo hili la Afya si eneo la kufanyia majaribio kama vile tulivyofanya kwa Walimu VODA FASTA

Jamani kwa maamuzi ya aina hiyo tutaua watu hivi vile vile hata nao madaktari wapya kuna siku watakuja na madai zaidi ya haya ya hivi leo.

Je tukija kujikuta katika hali ya ki-mgomo na hao madaktari wanaotazamiwa hivi sasa, uamuzi wetu tena utakuja kuwa ni wa kuendeleza huo mchezo wa kuajiri wengine?

Kuna habari kuwa serikali inatayarisha Tangazo la ajira kwa nafasi za Udaktari na udaktari bingwa haraka iwezekanavyo.

Je, hii inaweza kuwa long term solution ya matatizo ya mgomo wa madaktari.
 
Huo utaku ni ukosefu wa uwezo wa kuona mbele zaidi juu ya sakata la mgomo wa Madaktari; eneo hili la Afya si eneo la kufanyia majaribio kama vile tulivyofanya kwa Walimu VODA FASTA

Jamani kwa maamuzi ya aina hiyo tutaua watu hivi vile vile hata nao madaktari wapya kuna siku watakuja na madai zaidi ya haya ya hivi leo.

Je tukija kujikuta katika hali ya ki-mgomo na hao madaktari wanaotazamiwa hivi sasa, uamuzi wetu tena utakuja kuwa ni wa kuendeleza huo mchezo wa kuajiri wengine?

Kuna habari kuwa serikali inatayarisha Tangazo la ajira kwa nafasi za Udaktari na udaktari bingwa haraka iwezekanavyo.

Je, hii inaweza kuwa long term solution ya matatizo ya mgomo wa madaktari.
 
Kwa yeyote anayedhani kwamba CONSTRUCTIVE CRITICISMS tunazotoa kwa serikali yetu ni chukizo tupu, sasa angalieni hapo chini kwenye habari hiyo kwenye gazeti la Mwananchi kisha utagundua kwamba kweli wapo watu wenye AKILI na BUSARA huko serikalini ambao wanapata kugema mazuri yenye ukweli mtupu ambayo wengine tunayapinga huku mitaani na wao wanayafanyia kazi.

--------------------------------------------------------------------

JK: Polisi aliyetinga disko na SMG afutwe










Tuesday, 06 March 2012 20:54


Rehema Matowo, Moshi
Rais Jakaya Kikwete amesema matendo ya utovu wa nidhamu likiwamo la askari kuingia disko na bunduki,yasivumiliwe kwa sababu ni ya hatari na yanaweza kuondoa uhai wa watu wasiokuwa na hatia.Akizungumza katika mkutano wa kuboresha jeshi la polisi, uliofanyika jana katika chuo cha Polisi Moshi na kuhudhuriwa na maofisa waandamizi, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao kusimamia nidhamu ya askari wake.

Alisema askari asiyekuwa na nidhamu ndani ya jeshi hilo hafai kuwapo bali ni mamluki aliyeingia ndani ya jeshi.
Alisema sifa ya kwanza ya polisi ni kuwa na nidhamu na kwamba anapokosa hafai kuwa polisi.Kikwete alisema taarifa ya askari kuingia disko na bunduki aliisoma kwenye gazeti hili na kwamba kitendo hicho kimeonyesha dhahiri kuwa wapo askari ambao hawana nidhamu.

“Nimesoma kwenye gazeti, askari hapa Moshi ameacha lindo na kuingia disko na bunduki huyu mtasema ni askari wenu kweli, amelitia aibu jeshi la polisi na hafai kuwa polisi, wachunguzeni askari wenu mtabaini ni walevi, wala rushwa na muwaonye mara moja akirudia watoeni maana hawawafai,”alisema.

Rais Kikwete aliutaka uongozi wa polisi kuangalia upya utaratibu wa vijana wanaoomba nafasi za kujiunga na jeshi hilo kwani itafika mahali jeshi hilo litaonekana ni la wahuni na sio la ulinzi wa raia na mali zao.

Aliwataka kuwa na utaratibu wa ndani wa kuangalia tabia za askari wao ili wajue tabia zao na kuzirekebisha kabla hazijaleta madhara kwa wananchi .

“Mimi nimepata malalamiko mengi tu kwa wananchi wapo wanaolala baa ,walevi,wahuni,wala rushwa,wapo wanaoshirikiana na majambazi, wachunguzeni mkiwabaini waonyeni kwa mara ya kwanza wakirudia watoeni wapo vijana waaadilifu wanatafuta nafasi hizo hawajazipata, wanaochezea watoeni,”alisisitiza.

Alisema kwa kufanya hivyo itawasaidia kujenga imani kwa wananchi na kuondokana na lawama zinazotolewa kwa jeshi hilo mara kwa mara. Alitaka jeshi hilo kuweka utaratibu utakaowasaidia wananchi kutoa malalamiko yao kwa uhuru na bila hofu.

Alitaka jeshi hilo kutoa mafunzo ya ueledi kwa askari wake kwani mafunzo ya ueledi ni msingi wa jeshi hilo. "Kuvaa magwanda sio kuthibitisha kuwa huyu ni askari anayefaa,"alisema.

Alisema magwanda na vifaa vya kisasa havitamjenga askari kama hana mafunzo ya ueledi ambayo yatampa mbinu za kukabiliana na uhalifu katika kipindi hiki wahalifu wamekuwa wakitumia mbinu za sayansi na teknolojia kufanya maovu.

Mkuu mie pamoja na ugeni wangu kwenye hivi viwanja vya ma forums ya kimtandao na uwezo mdogo wa kupambanua mambo....SIJAKUELEWA.

Lengo ni vitisho?, habari, mkakati, pendekezo? Au?
 
Changamoto zitokanazo na mgomo wa Madaktari yasiposhughulikiwa na akili zilizotulia basi kuna makubwa ajabu yanatusubiri kama taifa wiki si nyingi sana toka sasa.

Remember, a fool's weakest spot in life is always an unreasoned DRIVE FOR REVANGE. Endapo tutaanguka katika mtego kama huu kwa suala la Madaktari basi tujue gharama yake huenda ikatushinda kubeba.

Hii ni tahadhari tu na tusipopendezwa nayo basi tukaitupe tu jalalani na mambo kuendelea.
 
Tunahitaji kuona mabadiliko makubwa juu ya taratibu zote kuhusu:

1. namna gani tunavyowapata watu wanaojiunga na jeshi letu la polisi nchini,

2. tunahitaji kuona taaluma zao zikibadilishwa kuweza kukubaliana na wakati,

3. tungependa kuona sheria na sera murua zinazoweka a working system in place yenye kuhakikisha kwamba kweli polisi watabakia WALINZI WA AMANI NA WATUMISHI WA UMMA wakati wote na kwa maana halisi ya maneno hayo.
 
Mhe Rais Kikwete,

Kwa mtaji wa ukali ulioonyesha na kuijia juu jeshi letu la polisi, kuamua kuwafuata mpaka kule kule jikoni CCP Moshi wanakototolewa na ukaamua kuwapasukia mwekundu huko huko kwamba HUTAJI UTANI JUU YA KUSIKIA TENA RAIA KUNYANYASWA AU KUUAUA NA POLISI, na kuhoji taaluma wanazofundishwa, uadilifu na nidhamu ya katika ujumla wake; Mzee hadi hapo KULA TANO Mkuu. Big Up sana!!!

Sisi wengine wakosoaji wa serikali yako tusiochoka wala kukata tamaa, ndio kama hivi tumeanza na mkondo mwingine wa ufuatiliaji kuona kama rai yako itaheshiwa kweli na sisi raia kuanza kupata ahueni zaidi au ilikua ni siasa tu za najukwa??????

Jeshi%288%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiwasili Chuo cha Polisi mjini Moshimkoani Kilimanjaro jana
kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi cha Polisi.


Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, amelitaka Jeshi la Polisi kukomesha vitendo vya mauaji, unyanyasaji dhidi ya raia na ukiukaji maadili miongoni mwa askari kwani vitendo hivyo vinalipaka matope jeshi hilo. Kadhalika amelitaka kuwaelimisha askari wake na kuingiza kwenye mitaala ya vyuo vya polisi nchini somo la haki za binadamu, kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa raia ya kuuawa na kufanyiwa vitendo vya kikatili wakiwa mikononi mwa polisi.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maboresho wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP). Alisema malalamiko ya raia juu ya vitendo vya kuuawa, kunyanyaswa, kubambikiwa kesi matumizi ya nguvu kubwa, kusababisha raia kujeruhiwa na kupoteza maisha pamoja na kuteshwa wakiwa chini ya mikono ya Polisi si vya kupuuzwa hata kidogo, hivyo Jeshi hilo linapaswa kujitizama kwa jicho pevu.
Alisema taarifa mbalimbali za Tume za Haki za Binadamu za ndani na nje zimekuwa zikiyaeleza hayo kuwa yanafanyika, hivyo ni vyema wakatumia mkutano huo kujadili kwa kina na kutoka na mazimio ya kukabiliana na hali hiyo, ili wananchi waendelee kuwa na imani na Jeshi hilo.

“Ipo haja ya kuwaelimisha askari kutumia elimu na akili zaidi kuliko nguvu kubwa, maneno yanayosemwa na raia si ya kupuuzwa yatageuka kuwa kero na kuwafanya mshindwe kufanya kazi zenu vizuri, kuweni na utaratibu mzuri wa kupokea kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi,” alisema na kuongeza: “Msiwapuuze, mkiwa karibu nao na kutunza siri watawapa taarifa nyingi na kuwa na imani nanyi, vinginevyo italeta matatizo sana, hawapati ushirikiano hadi wananitumia ujumbe mfupi wa simu nami namtumia IGP.”

Aliongeza kuwa Jeshi hilo linapaswa kujisafisha dhidi ya malalamiko ya rushwa, kwani utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utawala Bora umeonyesha kuwa linaongoza kwa maofisa na askari kuomba rushwa na kwamba taarifa hizo zisipuuzwe bali zifanyiwe kazi, ili kuwaondoa wale wote wanaosababisha Jeshi hilo kuanza kupoteza imani kwa raia. “Tumieni njia zenu kuwatambua wale ambao wanapokea rushwa, wawajibishwe kwa mujibu wa sheria zilizounda Jeshi la Polisi, kwani wanakwenda kinyume cha maadili na ndio wanaosaidiana na wahalifu na hivyo kulichafua Jeshi hilo na kulikwamisha katika utekelezaji wa majukumu yake,” alisema.

Aidha, Rais alilitaka Jeshi hilo kuweka utaratibu wa kuwafuatilia kwa karibu askari wake kama wanaishi kwa nidhamu inayotakiwa, kwani wapo ambao ni walevi kupindukia na utovu wa nidhamu mwingine, kiasi cha raia kuona kila anayevaa vazi la Polisi amechafuka kwa rushwa, utovu wa maadili na mambo mengine machafu. “Kuweni na utaratibu endelevu wa ndani kuwafuatilia askari wenu wakati wote, kuwatazama kabla ya kuwaingiza kazini, inapotokea askari anaonekana kuwa na mienendo yenye kutia aibu aitwe na kuonywa na akiendelea hatua ya kufukuzwa mara moja ifuate,” alisema na kuongeza: “Unakuta askari anakaa baa hadi usiku wa manane akiambiwa atoke ifungwe anajitapa yeye ni ofisa wa polisi hawezi kukamatwa, hili ni tatizo anachafua sifa nzuri mliyonayo, mfukuzeni.” Alisema nidhamu ni sifa ya msingi kwa askari, hivyo kwa wale ambao wameshindwa kufuata maadili ya kazi yao waondolewe mara moja, kwani haina maana polisi kuwa na mavazi mazuri, lakini tabia yake ni yenye kulichafua jeshi hilo.

MADEREVA WAKAIDI WAFUTIWE LESENI
Kuhusu kukithiri kwa ajali za barabarani, alilitaka Jeshi hilo kuwafutia leseni madereva wasiotaka kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, kwani ajali kwa sasa ni tishio kiasi cha kukaribia kuwa janga la taifa. “Ajali zimezidi zinaweza kuzuilika zisifikie kuwa janga la Taifa, fanyeni kila njia kupunguza, zamani chanzo kilitajwa ni ubovu wa barabara sasa barabara zetu ni nzuri na ajali ndio zinaongezeka, madereva wanalalamikia matuta, hatutayaondoa hadi hapo madereva watakapotaka kufuata sheria na kuendesha magari kwa nidhamu,” alisisistiza.

UHALIFU UDHIBITIWE
Kikwete alilitaka Jeshi hilo kuongeza mikakati na mbinu za kukabiliana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali zilizopo katika kutoa elimu kwa askari wao juu ya mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu kama wa fedha chafu na ugaidi.
Alisema matukio makubwa ya jinai yamepungua kutoka 94,390 mwaka 2010 hadi 76,052 mwaka 2011, na kwamba bado idadi hiyo ni kubwa na serikali itaendelea kuwasaidia kupata vifaa vya kisasa, magari na zana zote muhimu, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika mafunzo ambayo ndio msingi wa weledi wao. “Dunia ya sasa imebadilika na Tanzania imebadilika pia, mbinu za uhalifu zimebadilika, Polisi wanahitaji mafunzo yatakayoendana na dunia ya utandawazi, ambako kuna uhalifu unaofanywa kupitia mitandao na simu za kiganjani,” alisema Kikwete. Alisema serikali inaendelea na mpango wa kuboresha makazi ya askari na kwamba kwa sasa ipo kwenye majadiliano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili wapunguze riba ya mkopo ili waweze kukopa zaidi ya Sh. bilioni 100, ikiwa ni pamoja na kujadiliana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza kupunguza gharama za ujenzi.

KAULI YA WAZIRI NAHODHA
Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Naodha, alisema mkutano huo una lengo la kujadili, kutathmini mafanikio na changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, ambao unategemea weledi, umahiri, utii kwa maafisa wa jeshi hilo.
Alisema nguvu ya Jeshi la Polisi inategemea umahiri wa kazi na si wingi wa fedha wala nyezo na kwamba lina uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu hayo.

IGP: TUMEANZA KUJISAFISHA
Wakati Rais anaendelea na hotuba yake, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, alisema tayari hatua zinachukuliwa kwa askari ambao wanakwenda kinyume cha maadili ya kazi zao kwa kuwaondoa kazini baada ya kukutwa na makosa.
Mwema alisema mkutano huo utajadili wapi walipofanya vizuri na walipokosea kwa ajili ya kurekebisha kwa kupata mrejesho kutoka kwenye vituo, wilaya na mikoa ili kuboresha na kuidhinisha mikakati ya utekelezaji.


UONGOZI MZIMA WA HII WIZARA YA KI-POLISI HAKIKA WANANCHI HATUNA FURAHA TENA HATA CHEMBE NA UBABAISHAJI WENU KI-KAZI, KUKURUPUKA KILA LEO KAMA ZIMAMOTO HUKU WANANCHI TUKITEKETEA BILA HURUMA KATIKA MIKONO YA POLISI

Ni hatari sana raia polisi kuendelea kuua raia tena kinyama kila leo bila ya kuchukuliwa hatua zozote kisheria.

Kitendo cha hao polisi mwenzao kurudi kituoni kwenda kuwaita na kurudi nakuanza na shambulio kwa kijana Hassani na kisha kuendelea kumburuza chini wastani wa umbali wa kilometa 2, ni wazi kuwa mauaji haya yalikua ni mauaji ya KUDHAMIRI kwa kufuata mpango jinsi walivyojiwekea kabla ya kutoka kituoni.

Kwa jinsi hii si tu kwamba mahusiano kati ya polisi na umma utahama kuwa kama ule wa paka na chui tu bali sasa ni kwamba watu tunaanza kuhoji:

(1) Viwango vya uadilifi katika taratibu zote za kuwapata watu wanaojiunga na jeshi letu hili,

(2) aina na ubora wa mafunzo wanayopata kuwaandaa kweli kuwa WALINZI WA AMANI NA UTULIVU

(3) Mafunzo na uelewa wa polisi uhusiano wake na majukumu kwa raia , somo juu ya haki za binadamu na sheria za nchi

(4) Naam, hivi sasa tunatamani kuelewa hata viwango vya elimu kwa watu wanaojiunga na jeshi hili, viwango vya elimu vya wale wanaoitwa wakufunzi wa polisi pia,

(5) Kadiri matukio ya kustaajabisha yanavyoendelea kutokea nchini wananchi sasa tungependa pia tuelewe UBORA WA MAZINGIRA YA KAZI KWA POLISI kama vile aina ya ofisi wanazotumia, nyumba wnazoishi, mishahara na marupurupu wanayopata, na kadhalika

KWA UJUMLA WANANCHI HATUNA FURAHA HATA KIDOGO NA UONGOZI MZIMA WA VUAI NAHODHA, SAED MWEMA NA KATIBU MKUU WA HIYO WIZARA KWA JINSI WANANCHI TUNAVYOENDELEA KUUAUA KILA KONA YA NCHI KINYAMA NA POLISI NA WAO KUENDELEA KUONEKANA WAKO JUU YA SHERIA.
 
Tunahimiza serikali kushughulikia kwa haraka swala la mgomo wa madaktari nchi badala ya kubaki kwa kujifanya kams vile katikati yetu hivi sasa hatuna changamoto lolote linalohitaji kushughulikiwa kwa mtindo wa kuonyesha kujali uhai wa wananchi.

Kupiga biti media kutoshughulika na mgomo wa madaktari kwa maombi binafsi kwamba jambo hili litaisha tu lenyewe ki-hivo hivo tu ni sawa tu na mtu mzima kuamua kuficha kijinga cha moto kwe chupi ya nailoni.
 
Mtumishi wetu Mkuu mpya liyepata kazi majuzi tu, Balozi Ombeni, yuko wapi na kaama hawezi akaonyesha u-damu mpya wake katika kutatua mgogoro kati ya serikali na watumishi wake kwa maana ya Madaktari sasa kumbe majukumu yake kikazi tuseme ndio yepi hayo tena?
 
Hii nchi chini ya ccm hakuna la maana. Ona namna kiongozi au kada wa ccm akitoa hongo kugharimia uchaguzi inakuwa halali na takukuru hawawezi kumgusa, wapi zile kesi za kina mungai na yule aliyekuwa katibu wa tff?
 
Mabadiliko ya kisera yafanyike katika sekta ya afya nchini, tuache kuzunguka mbuyu kuhusu changamoto za mgomo wa madaktari.
 
Ni jambo zuri ijapokua kuna ka-harufu ya malengo ya ki-siasa iliofichama nyuma yake lakini kwa upande wa gharama kwa mlipa kodi ndio inanipa wasiwasi kidogo.

Swali langu ni kwamba je kama hii mipaka ya ki-utawala iliopo ndio imetushinda hata kuteua wakuu wa wilaya sasa fedha kuhudumia mikoa 31 ndio tutaweza?


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19


SERIKALI imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni:

1. Mkoa wa Geita -
Makao Makuu Geita,

a. Bukombe,
b. Chato,
c. Geita,
d. Mbongwe
e. Nyang’hwale.

2. Mkoa wa Katavi
- Makao Makuu
Mpanda,

a. Mlele
b. Mpanda


3. Mkoa wa Njombe - Makao Makuu Njombe,

a. Makete,
b. Njombe,
c. Ludewa
d. Wanging’ombe


4. Mkoa wa Simiyu - Makao Makuu Bariadi.

a. Bariadi,
b. Busega,
c. Maswa,
d. Meatu
e. Itilima.


Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.

Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni:

1. Buhigwe,
2. Busega,
3. Butiama,

4. Chemba,
5. Gairo,
6. Ikungi na

7. Itilima
8. Kakonko,
9. Kalambo,

10. Kaliua,
11. Kyerwa,
12. Mbogwe,

13. Mkalama
14. Mlele.
15. Momba,

16. Nyang’hwale,
17. Nyasa,
18. Uvinza

19. na Wanging’ombe.


Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).

Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang’hwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging’ombe wakati mkoa wa Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.


Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).

Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang’hwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging’ombe).

Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions),wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.


(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.

==================================================

My Yake: Je kuna umuhimu wa lazima kuwa na mikoa mipya?
 
Kuna mantiki gani Mkoa kuwa na Wilaya mbili au ndio kutoa asante kwa Nchimbi kwa kazi alioifanya uchaguzi wa 1995 hivo hivo hata kama mantiki inakataa ugawaji wa mipaka ya ki-utawala kihivi?

Tuliongozwa na misingi ipi kugawa mikoa no wilaya hata ifike mahala Mkoa moja uwe na wilaya 9 na nyingine ikabakia tu na wilaya 2. Waheshimiwa hebu tuelimishane hadi hapo.
 
Hivi ni kweli haka ka kauli ya 'TUMEJIANDAA VILIVYO KUPAMBANA' na madaktari katika mgomo wao huu ni kwali kasema Waziri Mkuu ambaye jalada la mazungumzo yenye lengo la kupata maridhiano kati ya serikali na madaktari iko mezani kwake hadi hivi sasa au amesingiziwa tu??

Na kama ni kweli kasema sasa atakubalika tena kweli baadaye kuongoza tena mazungumzo kama hayo akiwa kama mtendaji mkuu wa serikali? Na ikitokea kakataliwa huko mbele ya safari na hawa madaktari wetu, hilo litatoa taswira gani kwa umma wa Tanzania juu ya huyu kiongozi wetu?
 
CHADEMA KUMPA MTIHANI KAMANDA VICENT NYERERE ARUMERU MASHARIKI:
KIJANA SASA SIFA NADRA ZINAVYOZIDI KUJIDHIHIRISHA KWAKE KULE KWA KILA HATUA WATANZANIA TUJUE MWALIMU KAFUFUKA UPYA BUTIAMA KWA PICHA YA HUYU KIJANA NA JOHN MNYIKA WOTE WA CHADEMA


CHADEMA kwa uhakika Tanzania nzima imefurahishwa kwa namna mnavyompa uzoefu wa hali ya juu ki-uongozi kijana wetu mpendwa Vicent Nyerere.

Ni muda mrefu sana nimekua nikiwafuatilia kw karibu sana hawa vijana wenzetu wanne kwa maana ya Kamanda Tundu Lissu, Halima Mdee, John Mnyika na Vicent Nyerere - mbali na usomi wao hakika kuna tlanta mle ya kukat na shoka.

Lakini kwa leo darubini yangu imejikita zaidi kwake huyu ndugu Nyerere Junior. Mbali na nyinyi kumpa mtihani kule Arumeru Mashariki, hadi sasa tunachokiona kwake ni pamoja na:

1. Ubunifu wa hali ya juu namna gani kuwa Kampen Manager hodari,
2. Uwezo mkubwa wa kushirikiana na wenzie pamoja na wenyeji wa Arumeru,

3. Kucheza kama mwana-timu na wala katu hakimbii na mpira wa kisiasa uwanja mzima goli hadi goli kama Maradona enzi hizo,

4. Hajajiruhusu kuwa mfungwa wa kujiona mtu mwenye upekee wowote ule,
5. Kwake siasa za majungu na fitna katu,

6. Hupokea maelekezo na kufanya mara tatu ya ufanisi uliotarajiwa,

7. Hajitokezi sana kwenye vyombo vya habari na hupenda kuka 'viti vya nyuma' na wala si kujikweza,

8. Hashiriki siasa za sura-mbili na majungu kwa wakati mmoja ... yaani huyu kijana!!!

.... Wengine huku nje ya uwanja wa mchezo wa siasa kimya kimyaa tunaoendelea kumsoma huyu kijana mwenzetu hata bila ya yeye kujua lolote lile kama tunfanya hivo, lakini wenzenu kwa majibu ya tathmini hizi hakika wengi tunajihisi kama vile, mbali na uwepo wake Kamanda mwingine kwa jina la Mhe Makongoro Nyerere kule Mara na misimamo thabiti dhidi ya mdudu UFISADI nchini, laki kwake huyu kijana Vicent Nyerere kila leo tunazidi kumuona Baba wa Taifa Julius K. Nyerere kazaliwa upya katika nyumba yetu.

Kwa tathmini zangu hizi juu yake tena bila upendeleo wowote; wenzangu ngojeni mtaona huko mbele ya safari. Ndani ya CHADEMA kuna nyota ya mashariki na ishara zake zote.

Ndio, nasema hivi kijana huyu afundishwe kitu
UONGOZI WENYE UADILIFU uliotukuka maana hiyo ndio bidhaa kubwa ajabu iliokosekana Tanzania hadi leo hii na kufanya chama hiki pekee ndicho kibakie tumaini la MWISHO kwetu sisi wananchi tusiokua na kitu!!
 
TATHMINI ZA KITAKWIMU KUHUSU ZIAARA YA MHE MALIMA MKOANI MOROGORO NAAZMA YANGU KUPINGA NDOTO ZA 'URAIS WA NCHI HII KUPEWA VIJITOTO'

1. Hivi sasa ni Naibu tu wa Waziri -


a. Laptops 2
b. Mabegi 3
c. USD 4,000
d. Hela za Madafu Tshs infinity

2. Akija kutwaa U-Ngeleja -


a. Laptops 4
b. Mabegi 6 USD
c. 8,000
d. Muhuri wa Serikali pajani kusaini mikataba ya gesi na Uranium katika kichochoro chochote kile

3. Akija kutwaa U-Dk Bilal -


a. Laptops 8
b. Mabegi 12
c. USD 16,000
d. Kabeba shehena ya Dhahabu ya nchi kuwafuata nao 'Wawekezaji' kokote waliko.

4. Akija kutwaa U-Kikwete -

a. Laptops 16
b. Mabegi 24
c. USD 32,000
d. Na kuuza eneo zima la Kisarawe, Mbuga zetu, na meneo yote ya Madini na Uranium.


NB: Hadi hapa waheshimiwa sana Zitto Kabwe, Januari Makamba na Rais Kikwete, nasema SITAKI URAIS WA VIJITOTO kwa mtaji wa hii aibu ya mwaka ilitokea Morogoro.

Watu tucheke kidogo halafu turuhusu pia COMMON SENSE kufanya kazi kidogo. Kwa kuwa huyu Mheshimiwa anajulikana hana kiwanda Morogoro, machimbo wala biashaara yoyote ya kumuingizia kiasi kikubwa ajabu hivi ya fedha za kigeni wala yeye kuhitajika kuingizia fedha kwa sarafu hiyo, fedh hizi zote zilikua ni za malengo gani na kutoka mikono gni???

Je, ni kweli kwamba MheMalima alizilipwa hizi USD 4,000 pale Moro na 'Mtu' anyetaka gesi yetu, uranium, u-Dowans aau ni kweli Dr Kashillila siku hizi anawalipa kwa sarfu ya nci za nje????????

RAIS KIKWETE ANAPOMPIGA VITA MWALIMU JULIUS NYERERE KABURINI LEO HII KWA KUHIMIZA 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ALILOTUKATAZA WATANZANIA LICHA YA MADHARA MAKUBWA TUNAYOYAVUNA HIVI SASA KWAKE MWENYEWE HIVI SASA, YOTE NI KWA FAIDA YA NANI?

Rais Kikwete kamwe hawezi kurusiwa kwa mara ya tatu kufanyia majaribio ya kimaabara maisha ya WaTanzania kwa misingi ya kukamatishwa mawazo ya kiayawani barabarani kila kukicha huku taifaa likiendelea kuangamia kwa kiasi kikubwa kwa kila Jaribio la Kisiasa analolifnya ama ndani au nje ya chama chake.

By Candid Scope
ccccm.JPG


ccccm1.JPG

JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012


Mpaka hivi sasa, ni jambo lililo dhahiri kwa Watanzania waliowengi taifa limefikia hapa tulipofika kutokana na mambo matatu mazito ya kimajriobio hayo hayo.

Kwanza, madhara mazito yalioifikia taifa hili ilianza na jaribio la kwanza la kutumika dhna ya 'URAIS WA VIJITOTO' na matokeo yake tukampata Mhe Kikwete kuwa ndiye rais wa JMT licha ya Mwalimu Nyerere kuktalia jambo hili na kuonya kwa nguvu nyingi zaidi watu tusidhubuti kukumbatia jambo hili.

Kiukweli katika nchi hii hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kusahau mambo gani ambayo yametupata na yanyoendelea kutupata kutokana na mtaji wa dhambi ya kwenda kinyume na ushauri wa Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere, kwa kukumbatia 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ambayo hivi sasa tena imempata dalali mpya kwa jina la Rais Jakaya M. Kikwete.

Sote hatuna shaka kwamba uongozi wa nchi si sawa na uongozi wa jimbo wala kata hivyo mtu gani akachaguliwe kuongoza WaTanzania zaidi ya milioni 48 si swala la kuchezea chezea.

Inasikitisha mno jinsi ambavyo urais wa nchi hii unavyoendelea kukosa thamani na hata kuanza kurahisishwa kiasi hiki kwa namna mbavyo hata Rais Kikwete anafika mahala anakwenda kujibana mahali kujadilian jambo linalogusa mustakabali wa nchi na vijitoto kwenye mazungumzo binafsi na akina Zitto Kabwe na Januari Makamba kwenye mgahawa na kisha kesho yake kuonelea kuwa sasa hizo ndoto binafsi sasa ziwe ni Mambo ya Ki-Katiba ambayo kila Mtanzania ataswa kuyafuata. Katu hatudanganyiki na mawazo ya barabarani ya aina hiyo.

Hapa chini ni kijisehemu tu cha baadhi ya hatua za kimajaribio ya kimaabara ya Rais Kikwete kudiriki kucheza kamari na mchezo wa potea pata na maisha ya mamilioni y WaTanzania kwa namna isivyofaa hata tone:

1. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijitokeza naa kamari ya kwanza kabisa ya kutuletea kitu walichokiita DAMU CHANGA (kwa maana ya Ndg Jakaya Mrisho Kikwete) kugombea kiti cha urais wa taifa letu.

Sote hivi sasa ni mashahidi jinsi gani kila kitu ndani ya nchi kimepuputika na tumebakiwa tu na janga la taifa kwa kukubaliana na uamuzi huo huo kufanya uchaguzi chini ya DHANA HIYO HIYO POTOFU LA 'URAIS WA NCHI KUKABIDHIWA VIJITOTO' ambao hata kusimamia tu mambo yao ya kimapenzi tu na visichana vyao yenyewe bado ni mtihani.

Kwa nini watu turudie kosa eti kwa jina tu la kuchagua UDOGO WA UMRI kama kigezo ki-kuu mtu kuongoza nchi??

2. Kwa mara nyingine Rais Kikwete mwenyewe, kwa mtiririko ule ule uliojaa MAWAZO YA KUKOMOA MAADUI WAKE, akaja na DHANA POTOFU nyingine kwamba bunge letu ambalo ni mhimili muhimu mno kikatiba kwa kazi ya kutunga sheria za nchi sasa kiongozi wake kwa maana ya spika ili apatikane ni sharti KILA MMOJA WAO AMA AVUE SURUALI AU SKETI KUMTAMBUA JINSIA ALIVYOUMBWA halafu eti kwa kigezo hicho tu ikawa ni leseni kwa baadhi ya washindani kuwashinda wengine kwenye kinyang'anyiro na kuibuka kuwa MA-SPIKA UBWETE AMBAO KILA SIKU UFANYAJI WAKE KAZI NI MADUDU MATUPU NA KAZI NYINGINE NI KUDAI TU POSHO.

Sasa hivi nako chaguo letu kwa kuzingatia DHANA POTOFU LA JINSI nalo linatutokea puani mpaka kinamma wanaharakati kulazimika kuingia barabarani kupinga jinsi gani Spika Anne Makinda anavyowadhalilisha kwa maamuzi yake ya ki-shabiki hata kwa masuala mazito kwa mustakabali mzima wa nchi.

Kweli Rais Kikwete bado tu huoni jinsi gani ulivyotuuza hadi hapo na bunge kuonekana kupwaya ajabu kutokana na mojawapo misururu ya mi-dhana yako yanayopingana na katiba ulioapa kulinda?

3. Kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete amedhihirisha wazi kwa umma wa Tanzania kwamba yeye na MAFISADI nchini ni damdam, leo hii anapata wapi uhalali mbele ya uso wa jami na ujasiri uliomshinda kuwavua gamba mafisadi, eti kuja kuliambia taifa na wala si CCM yake kwamba Rais wa Tanzania ajaye atakua ni mtu wa aina hivi mara vile??

Mwenzetu huyu kwa jinsi alivyoongoza kwa KUKUMBATIA MAFISADI Tanzania na kutumia dola kuua wananchi kila kona ya taifa hili, moja kwa moja inamfanya awe ni mtu ambaye hana MORAL AUTHORITY kutuambia wananchi kwamba Rais ajaye atakua ni wa namna gani vile.

4. Isitoshe, masuala ya raia yupi mwenye umri gani ataweza KUWA NA HAKI YA KUZALIWA KUJITOKEZA KUCHAGUA AU KUCHAGULIWA kwa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya mipaka hii ni SUALA NYETI NA LA MSINGI KI-KATIBA ya JMT hivyo hakuna mtu yeyote au taasisi itakayojifurahisha na njozi zake mwenyewe kulivibadilishia vichochoroni huko Magogoni kwa malengo yasio na faida kwa Umma wa Tanzania.

Hivyo, mabadiliko makubwa kama haya eti kwa ajili tu ya HIVI VIJITOTO FISADI ni sharti kwanza tuletewe wananchi kwenye REFERENDUM ILI TUKAIPITISHE KWENYE TNURI LA KIDEMOKRASIA halisi.

5. CCM ikitaka a political showdown wa aina yoyote eti kwa ghiliba hizo hizo wanazozitumia hivi sasa kuzuia baadhi ya watu wenye hamu kubwa ya kugombea urais ndani ya chama chao, na sasa waanze kuvusha ghiliba hizo hizo kwenda kwa vyama vingine kwa kutaka URAIS WA HIVO VITOTO VIWILI VIWAKILISHI NA VINARA WA MAFISADI NCHINI, CHADEMA kipo katika nafasi zuri mara 50 zaidi ya hapo kugeuza ghilib hii mpya kurojeka zaidi ya uji na tena nda ya kipindi kifupi haijawahi kuonekana.


URAIS wa taifa hili kwa msururu wa dhana potofu kama vile JINSIA na au UMRI hauna nafasi hata kidogo kwa nchi hii mpaka mawazo ambayo ni HIGHLY CONTENCIOUS kama hayo yawe yamepitishwa kwenye KURA YA MAONI KITAIFA ikisimamiwa na Tume Huru ya uchaguzi ambalo si hili tume la huyu Jaji wa Mondo, Kondoa.

NOTE:
Na kama huu ndio mkondo mpya wa kutekeleza ile azma ya Rais Kikwete kwamba 'ninapoondoka madarakani uongozi wa nchi simuachii Mtanzania Mkristo ng'o' basi wenye mawazo haya mhesabu kula ya chuya kwa kuwa hamjafaulu bado katika hili la urais wa Januari Maakamba na na Zitto Kabwe!!!

 
Watanzania wenzangu,

Nyuma ya hii kashfa ya Mheshimiwa Malima, kwa Mungu kuamua kumuumbua vibaya mno kule mji karo bahari - Morogoro, sote tujue ya kwamba kashfa ilioko nyuma ya hiyo kashfa iliomkumba huko ndio nzito kuliko kawaida.

Hivyo sasa namhoji kiongozi wetu huyu kwamba Adam Malima twambie utakua umeuza mali gani ya sisi WaTanzania wenzako mpaka ukawa umevuna fungu kubwa kama hiyo kwa mkupuo tu hapa hapa mji mkavu wa Morogoro uliojaa wenye njaa tupu kama sisi huku??

Mhe Malipa, kuna UFISADI gani utakua umetendeka au unakaribia kutendeka kwa msikitiko yetu kitaifa ambao uliendea kujikingia manufaa binafsi Morogoro kiasi cha kugeuka CHUKIZO kwa 'JICHO LA TAIFA' mpaka wakaamua wakupokonye?

Je, pamoja na kujikuta kupoteza kila kitu hata kabla haijatulia mfukoni mwako hivi bado utaendelea kumtimizia huyo 'Mwekezaji' matakwa yake kinyume na sheria zetu ki-hivo hivo???

Tafakari sana tena sana juu ya maswali haya huku ukijua vema kwamba Taifa letu linabubujika machozi ya damu kwa kukamuliwa visivyo haki na kwamba siku zote kisicho haki hakiliwi!!!
 
Hivi Mbunge anapolala chumba shilingi laki nne Tsh 400,000/- kwa usiku mmoja tu, sawa na ada za wanafunzi 80 kwa mwaka wakiwa wamefuzu naakujiunga sekondari za serikali nchini, lazima watu tukajiulize baadhi ya maswali magumu hapa kama vile:

1. Je, huko kwa wenzetu Kisarawe hamna hata watoto yatima wanaohitaji misaada yatokanayo na hela za kumwaga kama hivi?

2. Je takwimu za vifo vya akina mama na watoto wachanga ikoje jimboni kwake?

3. Hivi huko Kisarawe nako kuna mwananchi yeyote anayepatwa na ugumu wa maisha jinsi tulivyo WaTanzania tulio wengi?

4. Je kwa mtaji wa wabunge wetu kuishi maisha ya anasa kiasi hiki katika taifa la watu tuliopigika kimaisha kwa hisani ya UFISADI uliokithiri, hivi kweli ni haki wao kulilia kitu posho tena hapa nchini wakati tumejionea wenyewe kwa huyu kijana mwenzetu?

5. Hicho kiasi ch fedha Malima kalipia hoteli kutoka mfukoni mwake binfsi au aakirudi Dar es Salaam atarudisha hizo risiti ili akachotewe kodi zetu kughramia anasa za aina hiyo?
 
Kimsingi Prof Lipumba alikua ni mtu wa kupewa makaribisho ya kitaifa na hotuba yake nayo ingefaa kufuata mkondo huo huo wa kuzungumzia masuala ya kiuchumi duniani na kuhusu taifa letu pia.

Lakini hivi sasa mambo yamekua triviolised na kufifishwa hadhi mpaka kubakia tu shughuli ya kisiasa tu chamani. Yetu macho kuona kati ya KAFU zote tatu nani hasa ndio mwenye ugeni wake uwanja wa ndege kesho; ni KAFU-CCM B, KAFU-Seif Sharrif Hamad au ile KAFU-ADC Hamad Rashid?

It will be so interesting to see how most jealous co-wives would be displaying their 'dirty linens in public' by each one fighting to get the first hug, kiss and a hold on briefcase as their LOVE HERO touches grounds from the aeroplane in Dar.

I just bet Massanja wa Ze Komedi Orijino naye atakuepo kushuhudia hako ka-songombingo, watu kutafuta VISIBILITY kwa nguvu hadi nguo kuchanika.
 
Mzee Mkapa,

Heshima zote mbeeele kama tai mkuu. Siku za hivi karibuni mzee wetu umepata kunisononesha sana tena sana moyoni kutokana na hisia ulizozitoa hivi karibuni Arumeru.

Kwa kweli kwa matusi yale kwa wapinzani hadharani tena mbele ya kandamnasi, mkuu kwa kweli wenzio HATUJAKUELEWA kitu hadi hapo.

Kwa jinsi tunavyokuchukulia siku zote katika jamii yetu hii, you are far better than those belittling utterances the most.
 
Back
Top Bottom